natureIjumaa hii,tarehe 20 March 2009 msanii Juma Nature au Sir Nature kama ambavyo mashabiki wake hupenda kumuita anazindua albamu yake ambayo ameipa jina Tugawane Umaskini.Uzinduzi unatarajiwa kufanyikia ndani ya Ukumbi wa Diamond Jubilee uliopo maeneo ya Upanga jijini Dar-es-salaam.

Inasemekana kwamba Juma Nature ndiye msanii ambaye anashikilia rekodi ya watu wengi zaidi kuhudhuria takribani kila uzinduzi wa albamu zake.Kama mwaka huu ataendeleza rekodi hiyo au la ni jambo la kusubiri kuona ama kusikia. 

Akiteta nami Nature amesema albamu hii ya Tugawane  Umaskini amerejea “nyumbani” kwa maana kwamba amerejea katika kuelezea hali halisi ya maisha ya mtanzania hususani yule ambaye anaishi “uswahilini”. Anasema kule ndipo alipotokea na kimsingi ndipo walipo mashabiki wake wengi.

Uzinduzi wa Tugawane Umaskini unategemewa kuwa wa aina yake kwa sababu msanii mwingine,Ferouz,….yes Ferouz yule yule aliyeanzia Daz Nundaz naye atakuwa akizindua albamu yake iitwayo Sauti na Vyombo.

natureb11

Juma Nature na Ferouz walipokuwa wakiongea na waandishi wa habari hivi karibuni kuhusiana na uzinduzi wa albam zao Ijumaa hii pale Diamond.

Kwa maana hiyo wahudhuriaji katika uzinduzi huo ambao umepangwa kuwa na kiingilio cha Tshs 5000 tu kwa kichwa,wataua ndege wawili kwa jiwe moja.Kila la kheri Sir Nature na Ferouz

Feedback / Comments

24 Responses to “TUGAWANE UMASKINI-JUMA NATURE”

  1. Comment by cley on March 17th, 2009 12:07 pm

    mzuka mwingi kaka mi bonge la fan wake kama vp akitoa hii asande gemu maana watu wanabana sana kipndi hk

  2. Comment by MAKULILO Jr on March 17th, 2009 3:22 pm

    HONGERA JUMA NATURE

    Napenda kukupa pongezi wewe binafsi kwanza halafu kwa kundi zima.Nature wewe ni msanii wa kuigwa ktk mambo ya kimuziki Tanzania.Ni msanii ambaye kwanza kila mwaka unatoa album yako, na pia mwaka mzima unakua hewani kupitia colabo (featuring) na wasanii wenzako.Hii inakufanya unakuwepo ktk anga ya muziki kwa mwaka mzima, hupotei.Chukulia mfano huyo Feruzi, yeye hafanyi colabo na msanii yoyote yule, na album sio gurantee kila mwaka kutoa, sasa anapotea kitambo, kurudi unakuta anatumia nguvu kubwa sana kutafuta mashabiki sana.Hata hapo kufanya uzinduzi na Nature ni njia ya kurudi katika ramani kwa haraka, ni kubebwa huko.Wewe unadhani angekuwa anasikika mwaka mzima kama Nature, AY, Mwana FA, Fid Q na wengineo angeanza kuhangaika hivyo??

    Kitu kingine kwa Nature ambacho ni cha msingi, ni moyo kwa wenzake.Ukiangalia kwa kuwa msanii mkubwa kama yeye unapomkuta na wasanii undergraound hakuna mashauzi kama wengineo.Kitendo cha kuwa msanii mkubwa tayari then unakuwa na kundi na hujikuzi kushikilia kundi kama wewe ndio wewe, ni suala la kupewa pongezi.Angalia mfano watu pori, kundi linakuwa mfukoni kwa Afande Sele: Angalia East Coast Team, kundi mfukoni mwa GK, nk.Kawasaida wengi sana kimziki kwa featuring na kwa kuwa nao ktk kundi moja pia.Najua kila binadamu ana udhaifu wake, ila kwenye credit lazima tumpe pale pafaapo wandugu.

    Suala lingine ambalo ni bora kwa Nature, sauti yake ni bomba mno.Anajua kuimba, kuweka sauti kulingana na tukio.Mfano akiimba mambo ya shari, vurugu kweli vurugu, si unakumbuka kwenye ile ngoma ya BOSI ya Feruzi alivyofanya kweli?Anapoimba mambo ya huzuni kweli huzuni, na sauti inaleta huzuni, akiwa furahani kweli furaha nk.Msanii inatakiwa uwe na uwezo wa kuwa na mabadiliko kama haya.Ukimsikiliza Feruzi kwa makini, hana uwezo wa kuimba nyimbo za furaha, nyingi ni huzuni ndio kutoka kwake.Ukisikiliza wimbo wa JIRUSHE ule wa Feruzi utasikia ile sauti Jirushe inatoka lakini bado kuna kasauti flani ka majonzi na sio Full Kujirusha.Ni tofauti na Jay Mo akmiimba mambo ya kujirusha au Ngwea, na wengine.

    Tuzo za bongo na Nature. Binafsi nashawishika kusema tuzo nyingi za bongo hutolewa kwa kupendelea au makmubaliano na msanii fulani.Hainiingii akilini tangu Nature aanze kuimba hajawahi kupewa tuzo hata moja Tanzania, na wakati huo huo tuzo za kimataifa anashinda vizuri.Tumeona ameshinda Channel O, na aliingia MTV.Je huu kweli ni uungwana??Tutafakari hili jamani.Sio kwa Nature tu, bali kwa wasanii wengi wakali wanabaniwa tuzo.Inafika kipindi Besta anapewa tuzo bora ya Reggae, Besta anaimba Reggae gani??Bob Marley ngoja awasikie nyie.Au kile kioja cha kutoa tuzo kwa Bushoke wakati wimbo sio wa Bushoke, Bushoke namshukuru aliikataa ile tuzo kwa kusema yeye alipiga featuring tu.Sasa hawa wanaotoa tuzo wanatumia vigezo gani vya msingi, yaani hadi mwenye wimbo humjui.Hainiingii akilini.TMK wanaume family, ile ya akina Chege na hata hii TMK Halisi haijawahi kushinda Tuzo, kwanini wakati ni makundi bora Tanzania??

    Nawatakia uzinduzi mwema.Jitahidi uvunje rekodi uliyojiwekea hapo Diomond Jubilee kwani ni wewe msanii pekee wa bongoflava uliowahi kujaza ukumbi huo, sasa hakikisha watu wanajaa hadi pomoni.

    MAKULILO Jr,
    http://www.makulilo.blogspot.com

  3. Comment by binti-mzuri on March 17th, 2009 10:22 pm

    kha! alishatoka jela?

  4. Comment by amimi on March 18th, 2009 1:16 am

    Juma nature ni msanii wa Kitanzania, ni msanii wa kipekee pia kwa kuwa na ufahamu mkubwa wa lugha ya kiswahili, si ya mtaani tu, ila maneno anavyoyapanga, anatakiwa afanye kolabo na washairi, Juma nature mimi namuweka katika kundi la kina ‘mjomba’ kwani haoni uvivu kufikira namna ya kupamba lugha, nashangaa hajawahi kuitwa kuitwa kwenye vipindi vya kiswahili.
    Ukisikiliza wimbo wake lazima ufikirie mara kadhaa, ujumbe mzito, na sio toka kwa mzee bali kijana!!!

    Hongera nature,
    keep it up, mcheza kwao hutunzwa, wewe uko peke yako kwenye hilo anga la kupamba kiwahili, kwenye bongo fleva
    mfano ‘tugawane umasikini’ ‘ubinadamu kazi’

  5. Comment by Mzee wa ££££ za kutosha on March 18th, 2009 5:51 am

    Ebwana big up Kiblah uko juu sana chalii angu,unakimbiza kama mwewe au kale kausafiri cha juu kwa juu..uko unique sana mashairi yako..

    Ila kama vipi check maujanja mengine maana apo bongo hautaendelea chalii angu apo ni mna tumika tu, mida ndo inaenda ivyo,mwenzenu mad Ice anauza tune zake kwenye Itune kwa ma £ (paundi) chalii angu, haya ndo maujanja yakufuata..izo buku buku za show achana nazo…Fanya mambo utoke man wewe kichwa long time nakukubali sana..
    Kam vipi tuwasiliane man…nikupe maujanja ujimuvutishe Utaborani, 2po uku wanao wakumwaga…na 2na maujanja ya kutosha sana tu…mhhhh imetulia
    Ebwana hii albam kama sikosei ya 4 kaka na mambo bado ndo ivyo ya kuunga unga sasa, mida inaendaa@ chalii angu

  6. Comment by mzinguaji on March 18th, 2009 9:46 am

    Mzee wa ££££ una-bore! Aliyekwambia wasanii wa bongo hawaijui sanaa kwa njia ya internet ni nani!? Acha ujinga! Vijana wanafanya mambo bongo wewe ukilemaa na box bila kufumbua macho, wazungu watakuvuna na utaambulia ushololo tuu!

  7. Comment by Mzee wa ££££ za kutosha on March 18th, 2009 3:55 pm

    Oya wewe unayejiita mzinguaji, changia mada…acha kutupotezea…Mad Ice peke yake katika wasanii toka bongo ndo anaye uza kwenye Itune kataa kuubali, na hadi masnii kuuza kwenye Itune ujue ni kiwango si wote wanaoweza mambo hayo….au na wewe mbongoflavour nini?

    Naona unalizimia ili boks la uku Utaborani, kama vipi njoo tukupe kazi, kazi zipo za kumwaga chalii angu…

  8. Comment by charonaire on March 18th, 2009 4:24 pm

    Ebana nina imani utawajaza kama kawaida yako,mi nakufeel kwa ki2 kimoko hauna ubinafsi japo kuwa ni wa zamani sana kwenye hii gemu tofauti na wasanii wa juzijuzi wenye mashauzi wanaojiona wamefika

  9. Comment by AS on March 19th, 2009 12:37 am

    mkubwa nature/kiroboto nakubari sana mashairi yako yanatukonga mashabiki ili nyimbo la tugawane umasikini ni noma,kimsingi ni msanii unaekubarika na watu wengi zaidi ndio maana unaongoza kwa kujaza mashabiki kwenye show.big up sana mkubwa

  10. Comment by mzinguaji on March 19th, 2009 8:28 am

    Mzee wa ££££ nenda zako wewe! Wewe ndio usiyejua mambo. Unalala walipoamkia wenzako. Usiingilie kupitia mlango wa kutokea. Watu hawaoni kuishi nje ya nchi ni deal siku hizi. Utabebea box wazungu hadi uote kibyongo! Wapo wasanii bongo wamesimama zaidi ya wewe mbeba box!

  11. Comment by watubwana on March 19th, 2009 4:50 pm

    siri ya mtungi aijuaye kata,hongera Juma Nature kwa kazi nzuri unazozifanya.
    jama msipende sana kuwasema wabeba BOX,kwani kubeba box ni kazi kama kazi nyingine,na inatulipa vilevile,wapo watu kibao wanafanya kazi za kijinga na wanahela chafu vile vile.tunasoma,tunakula,tunalisha familia na tunasaidia ndugu,wazazi wetu waliopo huko TANZANIA.kwani leo nikibeba box nikimaliza shule nikiondoka nikija bongo na elimu yangu utajua mi nilikuwa nabeba box??utaniju kama mi mbeba box???kazi ni kazi,JITUME KIJANA.na sio watu wote tuliopo huku tunabeba box tu,huku kunakazi nyingi sana shwa..ni.kumshauri NATURE aje huku si lazima aje kuishi huku,anaweza kuwa anakuja kufanya show na kuondoka zake,kama wafanyavyo wasanii wengine wanaokuja huku kutoka TANZANIA,NATURE njoo upige show za maana upate mshiko wa maana ufanye mambo makubwa na ya maana,hizo buku buku ndugu hazikupeleki kokote bro,mcheki FA,AY,JIDE,KIBA,BLUE waulize wanafaidika nini????hata kutembea tu na kubadili mazingira kupumzisha mind,kukutana na watu wanaideas tofauti tofauti inasaidia,sio kila siku watu hao hao tu unaokutana nao.tembea uone.twende kazi kaka,ni mtazamo wangu tu

  12. Comment by Bob Sambeke on March 19th, 2009 8:54 pm

    Hi

    BC!

    Hakuna Kitu wizi mtupu! Juma Nature alikuwepo Zamani! kipindi Hicho

    1.Wababe click(Kingsepeto,Bicco)-Kighetogheto
    2.Zigzag Crew – watu Bwana
    3.Mabaga Fresh – Mtulize
    4.Joint Mobb – Mtani Jirani

    Hapo Ndo alikuwepo Juma Nature lakini sasa

    Hamna Kitu! Promo Nyingi tu ndo zinamuweka

    kwenye chati kwa sababu ya kutoa ankara kwa

    ma Djs!

  13. Comment by Bob Sambeke on March 19th, 2009 8:58 pm

    Hi

    Ushawai kusikia wapi watu wanagawana umasikini! Hivi Clouds wamejaa wapumbavu wa kutoweza kujua uo usemi upo wrong!

    Umasikini – Ni hali ya kukosa kitu! Then

    Juma Nature kaja na Philosophy ya kugawana

    vitu ambavyo auna sasa ndo utagawa vp?

    PulekePuleko twentyscarie Tamakawega Hajii

  14. Comment by binti-mzuri on March 19th, 2009 9:44 pm

    hhahhaha bob sambeke

  15. Comment by Don shushu on March 20th, 2009 6:26 am

    yap yap ushafungulia nyuki big up sir Nature tunakusubiri kwa hamu Tanga huku uje tugawane umaskini

  16. Comment by halima on March 20th, 2009 8:07 am

    Mijitu mingine bwana ovyoooo sasa ulitaka aseme tugawane utajiri? wakati nchi yenyewe inanuka umaskini.

    Nature kama kawaida yako lazima wakubali tu hata kama watabana.

  17. Comment by big D on March 20th, 2009 10:27 pm

    Ile case yake ya kubaka imeishia wapi??

  18. Comment by OGOPASANA on March 23rd, 2009 4:38 pm

    muziki ni sanaa,na msanii anaweza kutumia title yoyote aipendayo kubeba ujumbe wa kazi ya sanaa yake kwa anavyoelewa yeye na alivyokusudia yeye,natumai kwa waliofuatilia mahojiano ya Nature mwenyewe juu ya album yake wanaweza kumuelewa anachokifanya mtanzania mwenzetu,jamaa ana ubongo na akili za ajabu tofauti na wanavyomfikiria juu juu watu wengine.

  19. Comment by mark on March 26th, 2009 5:56 pm

    iam, not haters but nature aka kiroboto style zenu wototo wa tmk sizielewi labda mimi mtu wazamani ila nulikuwa nawazimia sana G.W.M mulla vipi tunakutegemea uwe kiongozi tmk ,kama utasoma hapa nikuomba urudie style yako yazamani pleseeeeeeeeees shabiki no1 kama nyimbo mguu nje mguu ndani,mazimwi, utakubali vipi uwe namba mbili big up kulwa ,i ride wit u allday my homie.

  20. Comment by allen fenya on April 3rd, 2009 5:18 am

    ebwana nature ni zaidi ya wasanii, namkubali kinoma kwani jamaa hana malingo ukizingatia cash ipo, bado superstar na anakubarika. Ila nataka nature nikushauri kitu mkubwa, rudi na enzi za nini chanzo.Zaidi ya hapo hakuna noma mkubwa .Kira la heri naumaskinitumegawana sio viungo vya maalbino. From ur fan ALLEN A. town

  21. Comment by vedasto.malima on April 5th, 2009 9:59 am

    hongera kaka juma nature,kaza buti watu wajua kama wewe ni mkali,ila ile kesi yako ya kubaka imeishia wapi.

  22. Comment by vedasto.malima on April 5th, 2009 10:01 am

    hongera kaka,kaza buti si unajua underground wanavyokuja kwa kasi.

  23. Comment by mgunda,serengeti on October 4th, 2009 2:54 am

    kaka big up sana,kamanda wako hapa mgunda serengeti,kitu chakokipya cha africa no,one kimetulia,chamsingi kinachotakiwa kioneka,bila pasipo uwerevu aidha kuona ubunifu tunaweza kupotelea kizani,ubunifu unao kaka komaa nao hivyo hivyo.

  24. Comment by Lightness Mollel on March 12th, 2010 4:20 am

    uko poa sana naaminia mistari yako

Leave a Reply