
Kampuni ya bia nchini Tanzania(TBL) kupitia kinywaji chake cha Kilimanjaro Premium Lager, leo imetangaza majina ya wasanii na wanamuziki waliopendekezwa kuwania tuzo za muziki za Tanzania 2009 maarufu kama Kili Music Awards.
Akitangaza majina ya waliopendekezwa, Meneja wa bia hiyo ya Kilimanjaro,Oscar Shelukindo, amesema kwamba wanachotakiwa kufanya watanzania hivi sasa ni kuwachagua wanamuziki na wasanii wanaowavutia kwa kuwapigia kura kupitia namna kadhaa ikiwa ni pamoja na njia ya ujumbe mfupi wa maneno yaani (SMS),kuponi za magazetini na pia kupitia tovuti ya www.kilitimetz.com na pia kwa njia ya barua pepe(e-mail) kwenda: nominate@kilitimetz.com.
Sherehe za kuwatunza washindi zitafanyika mapema mwezi wa April mwaka huu(2009).Baada ya hapo kutakuwa na ziara maalumu ya washindi wa tuzo hizo katika miji mbalimbali ya Tanzania.
Je ni kina nani wamependekezwa kuwania tuzo za mwaka huu?Je unakubaliana na uteuzi? Haya hapa majina ya waliopendekezwa na categories walizomo;
MWIMBAJI BORA WA KIKE
a) Vumilia
b) Lady Jaydee
c) Mwasiti
d) Keisha
e) Isha Ramadhani
MWIMBAJI BORA WA KIUME
a) Matonya
b) Makamua
c) M.B.Dogg
d) Hammer Q
e) Q.Jay
ALBAMU BORA YA TAARAB
a) V.I.P- Jahazi Modern Taarab
b) WHY-T.O.T
c) MWANAMKE HULKA- East Africa Melody
d) KITU MAPENZI- Dar Modern Taarab
WIMBO BORA WA TAARAB
a) V.I.P- Jahazi Modern Taarab
b) WHY- T.O.T
c) MWANAMKE HULKA- East African Melody
d) MWANAMKE MVUTO- New Zanzibar Taarab
e) YA WENZENU MIDOMONI- Jahazi Modern Taarab
WIMBO WA MWAKA
a) Tabasamu – Mr.Blue ft Steve
b) Anita- Matonya ft Lady Jaydee
c) Dar Mpaka Moro- TMK Family
d) V.I.P- Jahazi Modern Taarab
e) Nzela- Banana Zorro & B-Band
WIMBO BORA WA KISWAHILI(Bendi)
a) Sumu ya Mapenzi- African Stars
b) Heshima kwa Mwanamke- FM Academia
c) Supu Umeitia Nazi- DDC Mlimani Park
d) Safari Sio Kifo- Akudo Impact
e) Mkono Shavuni- Vibration Sound
ALBAMU BORA YA KISWAHILI (Bendi)
a) Pekecha Pekecha- Akudo Impact
b) Nyumba ya Urithi- Double M.Sound
c) Ulimwengu- JKT Band
WIMBO BORA WA R ‘n’ B
a) Natamani- MB Dogg
b) Neila- Tundaman
c) Zamu Yangu-Sarah
d) Natamani- Q.Jay na Makamua ft Joslin
e) Usiniache- Spark ft Chid Benz
WIMBO BORA WA ASILI YA KITANZANIA
a) Dela Dela- Che Mundugwao & Mbeya Arts
b) Kataa Unyanywaswaji wa Kijinsia- Maringo Group
c) Kwetu Serema Ukerewe- Maringo Group
d) Kazi ya Dukani- Dogo Mfaume
ALBAMU BORA YA ASILI YA KITANZANIA
a) Dela Dela- Che Mundugwao & Mbega Arts
WIMBO BORA WA HIP HOP
a) Bado Nipo Nipo- Mwana F.A
b) Nipe Deal- Mangwair ft Dark Master
c) Ngoma Itambae- Chid Benz
d) Sintomsahau- Kingwema ft Marlaw
e) Nakuita Njoo- Prof.Jay ft Nyashinsky
WIMBO BORA WA REGGAE/RAGGA
a) Tutaonana Wabaya- Q-Chief
b) Mama Neema- 20%
c) Ripoti- Tunda Man
d) Dude la Kimataifa- Chege
e) Taxi Bubu- Matonya
MSANII BORA WA HIP HOP
a) Mangwea
b) Fid Q
c) Chidi Benz
d) Mwana F.A
e) Witness
WIMBO BORA WA AFRIKA MASHARIKI
a) Sweet Love- Wahu(Kenya)
b)Ti-Chi- Ken Raz(Kenya)
c) Zuwena- Wezzre(Uganda)
d) Sirimba- Ngoni ft Lady Jaydee(Uganda)
e) Salary- Nameless(Kenya)
MTUNZI BORA WA MUZIKI
a) Mzee Yusuph
b) Karama Legesu
c) MB Dogg
d) Lady Jaydee
e) Matonya
MTAYARISHAJI BORA WA NYIMBO
a) Ambross a.k.a Dunga
b) Lamar
c) Marco Chali
d) Hamie B
e) Man Walter
MWANDIKAJI BORA WA NYIMBO
a) Professor Jay
b) Matonya
c) Mwana FA
d) Lady JayDee
WIMBO BORA WA ZOUK
a) Naomba Umwambie- Kalunde Band
b) Awena- Kassim
c) Nalivua Pendo- Mwasiti
d)Karim- Ally Kiba
e) Lonely- Q.Jay
MTAYARISHAJI BORA WA VIDEO
a) Visual Lab
b) Kallaghe Production
c) Maujanja Supplier
d) Empty Souls
e) Outcome Production
WIMBO BORA WA KUSHIRIKIANA
a) Goodbye- Chege ft Q-Chief
b) Anita- Matonya ft Lady Jaydee
c) Natamani- Q.Jay,Makamua ft Joslin
d) Sintomsahau- Kigwema ft Marlaw
e) Nakuita Njoo- Prof.Jay ft Nyashinsky
BC inawakatika kila la kheri wote waliopendekezwa.
Pichani juu ni Meneja wa Kilimanjaro Premium Lager,Oscar Shelukindo(katikati),DJ JD(kulia) na Mzee Luhala(kushoto) kutoka baraza la sanaa.Hii ilikuwa wakati wa kutangazwa kwa majina ya walipendekezwa na pia kuonyesha zawadi watakazoshinda washindi.Picha na Issa Michuzi
Feedback / Comments
21 Responses to “KILI MUSIC AWARDS:AND THE NOMINEES ARE…”
Leave a Reply


sending...
makubwa haya taxi bubu nao ni reggae/ragga? duh!! mnamuweka matonya hapo halafu bushoke (rain on me) mnauacha! mnayeyusha bwana sometime na nyie!!!!!!!
KIZUNGUMKUTI KTK TUZO ZA KILI CHAANZA
Nataka kujua kitu kimoja hapo khs ALBUM BORA YA ASILI YA KITANZANIA. Iweje mgomaniaji awe mmoja??Au ndio kizungumkuti hicho kimeshaanza, mambo yale ya upendeleo?Ina maana hakuna mtu bongo nzima mwenye album ya mziki wa kiasili Tanzania??
Kama Dogo Mfaume, mfano ana Album yake, na nyimbo zote ni za kiasili, na ndio maana hata ktk kutafuta wimbo bora wa kiasili Dogo mfaume yumo na wimbo wake.Kwanini album yake isiwekwe hapo?Kuna ushindani gani kama mtu ni mmoja na pekee?
Hivi nyimbo za Taaraba, mambo ya mwambao nao si ni mziki wa asili ya Kitanzania?Au wasemapo huo mziki mpaka awepo mtu mmoja tu inakuaje hapo?Mfano kule Kigoma kuna watu kama vile MAPIGO SABA, Ukienda Dodoma kuna vikundi vingi vina album za nyimbo za asili.Hivi Wanne Star inakuaje hapo kweli hafai?
KILI hizi kasoro muwe nazo makini, hata kama hamna nia mbaya, mnaleta walakini jamani.Haituingii akilini kusema ni mtu au kikundi kimoja Tanzania nzima ndio kina album ya mziki wa asili.
Fanyieni kazi kasoro hizi mapema.Sio mje kuaibika kama mwaka jana mlipotoa zawadi kwa Bushoke kumbe wimbo sio wake, yeye alifanya colabo tu na mkenya, ikaonesha waandaaji ni wazushi, yaani hata hamjui mwenye wimbo ni nani.Kuweni makini, ombeni ushauri kwa watu mbalimbali kwanza kabla ya kuweka mambo hadharani.Fanya mambo ki-Preofessional jamani.
MAKULILO Jr,
http://www.makulilo.blogspot.com
West Virginia, Marekani
Ebwana apo kwenye list ya wasanii na hizo nyimbo mi naona kuna mapungufu makubwa Taxi bubu toka lini ikawa reggae jamani?????????
Na vile vile hizi tunzo wanapewaga wengine ambao ata hawastahili…kuna wasanii wengi ambao wako unique sana, na mashairi yao yanabamba vilivyo, sasa apo sijui inakuwaje! Au labda tuulize ni vigezo gani vinavyotumika kuwapata washirikishwaji?
hivi nyie manjua maana ya music industry? kwanini msihusishe wataalamu wa music industry? Mbona mmedharau na kusahau kwamba kuna GOSPEL Music? Duniani kote tuzo zinatolewa kwa kila aina ya music, oneni South Africa nk, kina Rebeca Malope, Lundi.
Tunataka kuona hambagui aina ya music. Gospel music si ulokole ni music kama music mwingine wa aina yoyote katika music industry tofauti tu ni message.
Kuweni open minded ninyi watu wa Kili Awards.
A. UK
nadhan lazma kuwe na watu wenye ujuzi na uzoefu wa kuandaa hizi tuzo na sio ubabaishaji huu kufanya vitu kiwa kubahatisha!
mwenzenu labda sifahamu muziki!!!!!!!!!!!hivi mwimbo wa taxi bubu wa matonya uko kwenye maadhi ya reggae kweli?
At least mmeimprove, but still kuna mapungufu mengi, nadhani kuna ka ubaguzi flani au hizi tuzo zipo kisiasa/kujuana zaidi au kili haina wataalam wazuri, coz kuna wasanii ambao ni waandishi wazuri wa musics but huwa hatuwaoni mfano afande sele! duh! mazee hii imekaaje. Hebu jaribuni kucheki wenzenu BET awards jinsi wanavyofanya hadi raha but nyie mi naona mnatangaza tu bia yenu.
jamani tusifanye vitu kwa kuiga alafu tunaiga vibaya,hizo category mbona ni chache,mbona hakuna msanii chipukizi,video nzuri..unajua hivi vitu vinawapa motisha hata wasanii wenyewe kiukweli kamati ya maandalizi bado haija kaa vyema kabisa badilikeni ili tuone vya maana ata hizo mlizo zichagua haziko sawa kabisa..ningewaashauri ata muingie mitaani mpate kujua mashabiki wanayapi yakusema kuliko kuulizana wenyewe..
kwanza nimejikuta leo nakuwa mjinga wa kutojua muziki wadau nisaidieni matonya tax bubu ni reggae kweli. hainingii akilini jinsi hawa kili wnavyopanga izi category zao. na wasiwasi kama kazi hii inafnywa as team work au ni mtu mmoja mwenye kilaptop chake anakkaa na kuanza kupanga. naomba watayarishaji wanishawishi kukubali kuwa tax bubu ni reggae kwasbabu sitaki kuamini kama mdau wa muziki anaweza kusema taxbubu ni reggae
nawakubali katika category ya waimbaji bora wa kike but wangeweka wazi katika mahadhi yapi
msipendelee masela
Jamani mbona hao ya mwasiti na chidi haikuingizwa na imefanya vizuri mwaka jana
eEEBWANA mmekosea ki2 kimoko yan na hioo nyimbo ya matonya ni rege du yan ata jhiko man am muon jaman au ndoo……. alaf ivii uyuu joh makin mna asila gan nae mbona yupo juu sana au ndo “wanatuzwa na wanao fagilia bia” ndi kinacho waboa aaaah achen asila
ME NATAKA KUJUA NYIMBO YA MWASITI NA CHIDI BENZ MBONA HAIJAINGIA? MNAANGALIA VIGEZO GANI? MBONA ILITINGISHA SANA MWAKA JANA.
INAMAANA HUYU 20% NYIMBO YAKE YA NINGEKUASEHEME HAINA VIGEZO MPAKA MMEAMUA KUIWEKA YA MAMA NEEMA MBONA IMEPITWA NA WAKATI.
MBONA KUNA NYIMBO NYIMBO NYINGI ZIMETOKA KABLA TABASAMU NA HAMJAZIWEKA?
KWANINI NYIE WATOA TUZO HAMPENDI KUWEKA NYIMBO ZA DULLY SKES,KIKOSI CHA MIZINGA NA WALE NDUGU ZETU WA ARUSHA AKINA JOE MAKINI?
Hi. hii ni kwa wataarishaji wa hizi awards,hivi hizi comments zinazotumwa na wadau wa muziki mnazifanyia marekebisho au ndo mmeweka hii “Leave a reply” kiushahidi tu. nasema hivi kwasababu tokea mmeanza kuandaa tuzo hizi makosa ndo yanazidi kuwa makubwa plus makubwa. hey pliz wahusika kuweni kama mmesoma na mnajua nini ya kitu mnachokifanya( try to be dynamic not static). sio mnatuletea aibu kila mwaka. kwa ambao tupo/wapo nje ya nchi ni aibu kujisifia kama na sisi watanzaina huwa tuna awards halafu ukiangalia grouping ya categories ni msiba matakatifu. badilikeni bwana mnazinguaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!1
mimi nashangaa sana ujue kuna wasanii wapo ila awajapata bahati ya air time ,kwa mfano ukisikiliza nyimbo za kikosi cha mizinga ,kama nyimbo tosha au pata potea hiphop bila madawa ,masikini akicheka utaona kuna ujumbe kwy jamii yetu hata hayati mwalimu nyerere angesema hivyo ila ndio wahabiki hawapati kusikiliza, ushauri wa bure ingia google/kikosi cha mzinga utasikiliza mapumbu yakutosha kukubadilisha mtazamo,thanks
ndio kaka Mark tell `em.
Hi
BC
Kweli Ukisikiliza nyimboza kikosi cha mizinga
Zina ujumbe sana lakini hazipo kwenye list,lakini wadau Tatizo nini? Tatizo ni Promo,Tatizo ni Promo! Hazipati Airtime sana ndo maana aziweki kwenye Kinyang’anyiro!
Ebu check Tracks hizi
1.Mstali wa mbele
2.Umoja ni nguvu
3.Dira
4.Asiekubari kushindwa si mshindani
5.Uwezo
6.Hip Hop Bila Madawa
Poa Hongera DJ JD nakouna Kwa Pembeni Hapo!
Ni Hayo Wana BC!
YOOH………….
Ilibidi kuwe na kategori za hiphop ya kigumu na nominees wawe watu kama WATENGWA,KIKOSI CHA MIZINGA,KIMBUNGA,MANSU LI,SAIGON,SALU T na ma mc wengine kibao
sasa huyo kallage’s picture amefanya nini cha maana au zaidi ya visual lab. HIVI KWELI MNAFIKIRIA NYIE….. aU MME MPA KWA ajili ya kuwaweka wasichana wa watu uchi….. fikirieni na uhalisia jamani…
kilimanjaro has paved a way 2 our artistz this showz hw we r grateful 2 their work