yanga12bc

Tuende mbele turudi nyuma,ukipata nafasi ya kuchezea Yanga au Simba basi suala la umaarufu au u-celebrity halina mjadala sana.Wapo watu lukuki ambao watalijua jina lako,wataitambua sura yako na ukiwa mitaani watapenda kupiga japo stori kidogo na wewe.Ndio maana zinapokuja habari kwamba ama Yanga au Simba wametwaa ubingwa nchini,basi hiyo huwa ni habari kubwa iwe mtaani au kwenye vyombo vya habari.Mpaka hivi leo mchezo wa Yanga na Simba huwa ni gumzo kubwa mtaani.

Kwa bahati nzuri au mbaya,safari hii ni Yanga tena.Yanga wameutwaa ubingwa wa ligi ya soka nchini Tanzania kabla hata ya ligi hiyo kumalizika.Kwa maana hiyo wanastahili pongezi.

Lakini ubingwa wa soka nchini Tanzania,umaarufu,pesa nk vinakuwa na raha yake kama angalau vitakumbuka walipolala na kuamkia mashabiki wao.Tumekuwa tukiona jinsi ambavyo wanamichezo katika nchi zilizoendelea wanajitolea kwa namna mbalimbali ili kuboresha jamii zilizowazunguka na pia mashabiki wao.Wengi wanajitolea kwa namna mbalimbali kama vile kujitolea muda wao,pesa zao,ujuzi wao .Kama sio hivyo, basi wamekuwa wakijitolea katika aidha kuhamasisha michango ya hiari,kujitegemea,kujiamini miongoni mwa vijana nk.

Nchini Marekani kuna kitu kinaitwa NBA Gives Back.Hawa ni wachezaji wa ligi ya mpira wa kikapu ya Marekani ya Kaskazini waki-toa chochote wanachoweza au walichopata kwa jamii zao,kwa mashabiki wao.Wachezaji wenye majina nchini Tanzania,wanaweza kuiga hili.Wadhamini wa ligi hiyo,Vodacom,wanaweza kuhamasisha hili kwa kuwatumia wachezaji wa ligi ya soka Tanzania.Shirikisho la Soka nchini linaweza kusimamia au kuongoza harakati kama hizo.

Tusiishie kwenye kufurahia tu Ubingwa bila kukumbuka walikolalia au kuamkia mamilioni ya mashabiki wa soka nchini.Lakini mbali ya yote,BC inatoa Hongera kwa Yanga!

Feedback / Comments

One Response to “HONGERA YANGA KWA UBINGWA!Lakini…”

  1. Comment by mwenyewe!!! on March 27th, 2009 12:07 pm

    Ni mawazo mazuri uliyo nayo kiongozi lakini unashangaza unapowalinganisha “wavuja jasho” wa Bongo walio Simba na Yanga..pengine hujui hata mishahara yao..nambie unawafahamu wangapi waliokuwepo S&Y hivi karibuni say 5 yrs ago na wana maisha mazuri ambayo unaweza kuyatolea mfano ili tuamini kuwa hawa vijana wa Jangwani na Msimbazi wanachezea hela..make hata hatuoni kinachofanyika mitaani zaidi ya kwamba wana maisha ya kawaida pengine mabaya tu ila zaidi “UMAARUFU” wa kuandikwa magazetini..hebu tafakari vizuri..cjakuBAli hili la kuwalinganisha hawa vijana na wachezaji wa USA..otherwise unamaanisha hawa WAKENYA, NIGERIA na Wageni WENGINE..C WASWAHILI..

Leave a Reply