kilangobc

Hivi karibuni,Marekani,kupitia ubalozi wake nchini Tanzania,ulimtunukia Mheshimiwa Anne Kilango,tuzo ya Mwanamke Jasiri kwa mwaka wa 2009.Tuzo hiyo ambayo hutolewa kwa wanawake ambao wameonyesha ujasiri na uimara katika uongozi,imemwangukia Mheshimiwa Anne Kilango kutokana na juhudi zake za kupinga ufisadi na kukabiliana nao bila uoga.

Mheshimiwa Kilango ambaye ni mke wa aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania,Mheshimiwa John Samwel Malecela, ni Mbunge wa Same Mashariki mkoani Kilimanjaro kupitia chama tawala cha CCM.

Pichani ni Mheshimiwa Anne Kilango akipokea tuzo hiyo kutoka kwa Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania,Larry Andre. Pembeni ya Anne Kilango ni mumewe,Ex-PM,John Malecela.

Tunampongeza Mheshimiwa Anne Kilango.Hongera,unastahili.

Feedback / Comments

7 Responses to “ANNE KILANGO:MWANAMKE JASIRI 2009”

  1. Comment by Mwanamke wa Shoka (UK) on March 31st, 2009 1:27 am

    hmmmm…!!

    sasa itabidi Mama Anne ahamie Dodoma tuu…halafu aniachie hapo Same Mashariki mnamo 2010….lol…

    ….amependeza….na hongera Mama Anne…kaza buti hao mafisadi ni ama zao ama zako….lol
    …tumewachoka mafisadi maana wanatuletea shida tupu hapo Bongo…

  2. Comment by Mattylda on March 31st, 2009 3:13 am

    yes we can mama much respect!!!!!!!!!!!big up!

  3. Comment by john on March 31st, 2009 3:37 am

    kufuchua mafisadi bungeni sio ujasili,ndio wajibu wako kama mbunge.

    mimi sielewi hiyo tuzo aliyopewa ni ya nini.

  4. Comment by Ras on March 31st, 2009 6:57 am

    Nimekuikubali hii tuzo na mtunukiwa pia. Ni heshima na funzo kwa wanawake wote wajifunze kujiamini.

  5. Comment by Bingo on April 1st, 2009 6:25 am

    i have soooo much love for you Anne, even though i dont know you in person. But the fact that you have been the voice of the voiceless and the kind of values you stand for, that alone makes not anly me but the wider tanzanians most well thinking persons stand by you and support you. Everything hapens for for a reason, i believe since you were born God himself had already equiped you with every tool you need to bring about change we all want in this country. You deserve the award and i think you deserve more than that; “our respect and support”. we the peaple assure you that your fight against corruption is not a waste. we are praying for you and may God protect you from all the evils. I salute!

  6. Comment by Hassan Makongoro on April 6th, 2009 6:32 am

    Mama yetu nimekubali juhudi zako!!!!!tunahitaji tanzania wakinamama kama wewe hongera sana na mungu akuongoze na kukulinda pia.

  7. Comment by kyokwete on January 13th, 2010 2:54 am

    its all for thinking youngs to make critical reflections on these commited leaders Anne! i dont think you are strugling for these awards, but achieving them, for i know you still deserve others, shows how people recognise what you are doing…and it is recognition that matters! hongera sana mama.

Leave a Reply