
Viongozi wa nchi za SADC wanakutana huko katika jumba la kifalme la Lozitha huko nchini Swaziland,kusini mwa bara la Afrika.Rais wetu,Jakaya Mrisho Kikwete(kama anavyoonekana pichani) ni miongoni mwa viongozi wanaohudhuria.
Mojawapo ya mambo muhimu yaliyopo juu kabisa kwenye ajenda ni suala la kujaribu kuisaidia Zimbabwe ambayo uchumi wake umeyumba kupita kiasi na pia kuzungumzia hatua za kuichukulia nchi ya Madagascar ambayo hivi karibuni imepitia “mapinduzi”.
Pamoja na hayo,mijadala kadhaa imezuka mtandaoni kuhusiana na “fashion statement’ ya Mfalme wa Swaziland.Wengine wanasema alistahili kuvaa suti kama wenzake ili aonekane kuwa “serious” na mambo kama hayo.Wewe unasemaje?Ni kweli kwamba kuvaa suti ndio kunafanya mtu aonekane “serious”?
Na je hivi ukitokea mwaliko unaoamuru kwamba kila kiongozi avae vazi lake la Taifa(vazi la Mfalme Mswati ni la kitaifa kwa Mfalme) wa kwetu atavaa nini au ungemshauri avae nini?
Feedback / Comments
27 Responses to “SADC AND FASHION STATEMENT”
Leave a Reply


sending...
he he he !!….hiki ni kitendawili.
…miye hata sielewi Rais wetu atavaa nini…!!
…Labda avae la kabila lao (sijui ni Mzaramo vile…)…hivi vazi la kizaramo la wanaume ni nini atii??….can remember seeing a zaramo man in a native costume…lol
….
…au la kitanzania…hii nayo inachanganya…hebu nisaidieani hapa kaka zangu wa hapa BC….hata sielewi napo.
…ila nahisi mwanamke wa Ki-Tz anaweza kuvaa vazi la khanga in its varied tastes and styles…
Wapambe wa Rais jakwanya hapa wamekwenda mchomo ingekuwa jambo la busara kama wangemvalisha vazi la kimasai ili kuzidi kuinadi TANZANIA
Alichokifanya King Mswati ni kuwaumbua wenzake barabara wote wanaonekana kam mkoloni alivyowacha miaka ya sitini bila Cultural identity ya namna yoyote..Suti Vazi la Mzungu. ktk vikao vya kiafrika basi shurti viongozi wa bara hilo kujitoa kiafrika… aniwei badala ya kudiscuss DJ pale Madagasca nadhani wangejadili kumuondoa Mugabe hapo Zim
huyo mwanamama huko nyuma kabisa nae ni rais? kama ni rais basi wanaume wa kiafrika wamekosa sana heshima kwa kinamama kwani alipaswa asimame mstari wa mbele kabisa.
vazi la suti si kama la heshima kuzidi vazi la kimila tusipende kujizarau sisi wenyewe, unapokwenda njee tujitaahidi kuvaa mavazi ya taifa letu, kutangaza utamaduni wetu, watanzani saizi tupo juu.
acha watu wenye culture zao wazi-express, let the rest keep on up-rising the whites.
swali ndugu yangu ndio uafrika huo wanawake nyuma huko wala msionekane upo hapo?? si ndio mila jamani sasa wewe wategemea wanaume wafanyeje?? hapa issue za gender zimeachwa majumbani hapa
well…anyways….to be honest sijawahi kumuona our President in one of them cutltural attires…(I stand to be corected here)….sana sana gear ya kidini ya kanzu na barakshia anapopenda kubadili
….wapambe wake wake chini wafikirie hili….pia H.E. JK mwenyewe aridhie….once in a while kuachana na hizo suti….lol
Represents his country why not……?
mafisadi wamekutana!
Hivi King Mswati mwaka huu ameshao au bado??
Mzinguaji umeongea pointi MAFISADI WAMEKUTANA:..wengine wanajitia kupenda kuvaa kitamaduni na wengine WAMEVAA Kizungu.. mwisho wa siku wote tabia zao ni ufisadi na Afrika inazidi kudidimia..mimi binafsi wamenikera sana hamna kitu hapo…
machoni kama watu,moyoni hawana utu,imani imetoweka mabaya yanaongezeka.
muangalie MUGABE sura kama x@xx@x nyooo,watu wako wanakufa na njaa huko,hali inazidi kuwa mbaya utaki kuachia madaraka shwa@xx@ni weee.huyo mswati nae kila kukicha kuoa,jamani mila zingine sio kabisaa yani ,zinadidimiza nchi yetu na kuzid kuleta UMASKINI.
Chizi ndungu yaani umeongea point ya maana..huyu Mugabe anakera jamani..nadhani two weeks ago alikuwa na Birthday eti nikamuona kwenye TV hupo na watoto (sijui ndio wajukuu) na keki kubwa eti ana celebrate birthday yake ambayo ilimkost kama 200,000 US Dollar. Jamani ana akili huyo??..wananchi wake wanakufa kwa kipindupindu eti yeye yupo busy na Birthday Party sh…zi kabisa hana maana kabisa. Hawa viongozi wetu wa Africa kwa kweli mie mwezenu wala siwafagilii kabisa..huyo mswati huko kwa watu asilimia 40 % wanakufa kwa ukimwi yeye hata kuwasaidia hataki anaakili kweli huyo sh…zi type kabisa
Nyie mnaosema tradition attire imependeza ect nimewashangaa sana..hawa viongozi wa afrika badala ya kuleta maendeleo ndio wanajifanya very Traditional ili wazidi kutugandamiza..mie wala siwapendi..waliovaa situ au huyo Mswati mbona wote ni sawa tu..hawatuletei maendeleo so for me it really doesnt matter FISADI kama AMEVAA SUTI YA KIZUNGU AU TRADITIONAL wear WOTE TU NI MAFISADI TU na hawana maana yoyote mimi binafsi nitawasifia endepo siku wataleta maendeleo Africa…
TOBA mkutano wa mafisadi wa kiafrika hamna jambo la msingi wanaongelilea hapa..kazi kula per diem tu..
Na hao wanaojitia kuvaa Traditional wear ndio wabaya kupita hao waliovaa suti za kizungu..kwa ujumla wote ni FAKE hamna jipya hapo, bibi yangu kule kijijini hana BASIC NEEDS sasa eti mimi niwashangilie Maraisi waliovaa TRADIONAL WEAR au eti Kikwete handsome oh TO HELL WITH THEM ALL…siwafagilii kabisa tena naomba hii picha muitoe kabisa humu ndani mie inanitia kichefuchefu..na kwa mwendo huu wa viongozi wetu wa Afrika, kamwe hatuwezi kupata maendeleo
Mie mwezenu na huyo Kabila ndio ananiboa huko kwake kutwa vita, watoto hawana chakula na wakufa, watoto wengine wanakuwa wanajeshi ect sasa mimi ndio eti nikae hapa nisema ohh Kabila ni handsome au Kibala avae Traditional wear BULL SHIT siwezi fanya hivyo jamani Afrika inaungua moto jamani na sisi tupo hapa busy kwa kuwasifia viogozi ambao wamevaa Traditional wear..
SADC na AU ni uozo mtupu hamna jipya..viongozi Afrika bado hawajazaliwa..
eti traditional wear ya Mswati imependeza..mhhh Mswati ni mnafiki hamna jipya arudi kwake akaoe tena maana ndio kazi ambayo anayoweza kufanya..na siku hizi huko Swazi wazazi wa watoto wanao olewa hawapendi kabisa wana resist sana na wanataka watoto wao waende shule..kila kitu kina mwisho wake..na Human Rights activitist kutwa wapo huko Swazi
BC watoe hapa haraka sana hata sitaki kuwasikia hao viongozi wetu, mimi nitamsifia kiongozi ambae ataleta maendeleo maana sasa hvi nasikia huko TZ kuna mgao tena wa umeme jamani mbona kazi..sasa ndio tuwasifie hawa viongozi wetu no WAY mimi siwezi maana ukiwa nchi za watu na unaona vitu ambavyo vinawezekana jamani roho inauma, ukijua huko nyumbani inawezekana ila kuna watu fulani hawataki kufanya kazi yao basi unabaki kuwa na hasira tu..
TUMKENI JAMANI WAAFRIKA,TUPENDANE NA KUWAJALI WENZETU,HUKU TUNAKOELEKEA SIKO
I have no say but I am very much dissapointed and confused in general I don’t know what to say. Anyway I cannot go without giving my input King Mswati was suppose to wear like is fellow men. Unless otherwise if one can tell me that the interest of taking that photo and wearing such outfit with bright colour was to attract people to concetrate looking at him without paying atention to the rest then I will understand. Although there is a say that what you wear might not represent how you behave, talk, walk etc etc…. but someone was soppuse to tell him that its not a modeling neither fashion show time but it was a time for discussing serious issues concerning problems faced by SADC. If he had no suit he could have put on a simple shirt/tshirt + a jeans or formal trouse just simple like that it could be better.
Anyway that is my perspective
FLORA WAPE HAO..maana hapa watu waliaza oh uafrika oh oh tutafute vazi la kiafrika ect hamna lolote kama mdau alivyosema hapo juu sisi bwana tunahitaji maendeleo hapa..na viongozi wakienda kwenye mikutano waongee vitu vya msingi na sio eti kuvaa traditional wear au oh huyo kavaa kizungu sana..Mimi i really dont care about what they wear what i care about ni watu wa kawaida ambao wanapata shida sana huko nyumbani..na vile vile NIMESIKIA MGAO WA UMEME UMeaNZA TENA; jamani hivi kwanini miaka ya hivi karibuni kila mwaka lazima kuwe na mgao wa umeme??
CHIZI viongozi kama wanaboa jamani mapenzi yatatoka wapi?? maana naona unaongelea oh watanzani tupendane..mapenzi hapa tupende viongozi hata kama hawaleti maendeleo NO WAY hemu usitutanie hapa
sister TZ hujanipata sijasema tupende viongozi wetu NO,tupendane nikimaanisha tuwe na moyo wa upendo kwa wengine,kabla ya kufanya baya kwa mwenzio 1st ujiangalie je ukitendewa wewe utafurahi?so tukiwa na upendo inamaana tutapata viongozi wanaojali utu na kuwajali wengine,sasa we fikiria MUGABE hanahata chembe ya upendo moyoni mwake,wananchi wanakufa kwa njaa ye anasherekea bathdei kwa mapesa kibao,mswati nae wananchi wake umeshasikia wanapukutika kwa UKIMWA TZ haiingii ndani,ye wala ndio kwanza anendeleza MILA kuzidisha kuoa wake wengi,ye anapata vibya bado BIKIRA.KABILA kila kukicha kuuwana,TANZANIA si hatuna vita tunayakwetu hapa nikilist hayatoisha ila kuna mfumo ambao upo unaoitwa CHUKUA CHAKO MAPEMA USINGOJE KUPEWA,hii yote ni sababu kila mtu anajiangalia mwenyewe na si je nikifanya hivi wangapi watakao kuwa na shida,ama ataumiza watu wangapi?yeye anachojali ni maslahi yake ndio maana viongozi wetu wanaishia KUJILIMBIKIZIA MALI,KUWAPA SEHEMU NYETI WATOTO WAO,KUFUNGUA ACCOUNT NJE ZA NCHI NA KUWEKA MABILION YA PESA NA KUANDIKA MAJINA YA WATOTO WAO NA SI YAKWAO,KUWAKABIDHI WATOTO WAO MIGODI.HEHEHEHEH UMENIPATA hapo,WITHOUT LOVE UR NOTHING BUT AN ANUS.
nyie mnaoropoka hapo juu sijui na nyie kama mnavaa mashuka ya kabila lenu.eti wengine wanasema wangemvesha kikwete kama mmasai,yaani kaazi kweli kweli