MY TANZANIA   |   PLACES TO GO   |   MEDIA   |   ONLINE ENTERTAINMENT    

dar-explosionImekuwa ni wiki ngumu kwa watanzania hususani waishio jijini Dar-es-salaam na zaidi waishio maeneo ya Mbagala. Milipuko kadhaa ilitetemesha jiji.Hofu ikatanda. Ikawa mshikemshike Mbagala kwenyewe mpaka katikati ya jiji na maeneo mengine. Wengine wakajua vita nyingine labda ndio imeshawadia.Penye wengi pana mambo mengi. Maneno mitaani nayo yakazidi. Hofu ikawa hofu.

Wananchi kadhaa ambao walikuwa katika siku yao ya kawaida,ya mihangaiko ya kawaida ya maisha wakapoteza maisha. Ama kweli kifo kikija hakipigi hodi! Ndio maana tunaambiwa kila siku kwamba tujiandae. Wengi wengine wakajeruhiwa. Wengi bado wapo mahospitalini.

Vifo vinapotokea au maafa ya namna hii, huwa ni wakati wa simanzi kubwa. Kifo ni kitu cha mwisho ambacho binadamu yeyote anataka kukabiliana nacho.Kinaogopesha. Lakini kifo ni sehemu inayokwenda sambamba kabisa na maisha. Ni sehemu ya maisha na sote tutapitia njia hiyo hiyo.Tunachoweza kufanya ni kutoa pole tu kwa wote walioondokewa na wapendwa wao. Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi! Pole nyingi pia ziwaendee wote waliojeruhiwa.Ni matumaini yetu kwamba Mwenyezi Mungu atawaponya na kukupeni tena afya njema.

Nini kilitokea? Ni ajali au uzembe tu wa mtu au watu fulani? Kama ni uzembe je walioathirika aidha kwa kuumia au kupoteza ndugu,jamaa na marafiki watafidiwa? Je tunavyo vitendea kazi na watendaji wa kutosha kutupatia majibu ya maswali hayo? Hayo ni baadhi ya maswali ambayo serikali ni lazima iyapatie majibu yanayoeleweka,ya wazi bila kificho. Tusipofanya hivyo,kesho bado ni tete. Yanaweza kutokea tena na tena matukio kama hili la wiki hii. Kama hali ile ilitokana na uzembe wa mtu au watu,basi hatua kali zichukuliwe. Ni wakati mwingine muafaka kwa serikali kuonyesha jinsi “inavyowajibika” kwa wapiga kura,walipa kodi na wananchi wake kwa ujumla.

Naam,kwa sababu leo ni Ijumaa na kawaida ni kwamba huwa tunaburudika na zilipendwa na kutokana na hali ya majonzi tuliyonayo,kibao cha Dr.Remmy Ongala cha Kifo ndicho ambacho nadhani ni muafaka. Kimsingi kibao hiki sio cha kuburudisha bali kutusaidia kuungana na wenzetu waliopoteza ndugu,jamaa na marafiki katika maombolezo.

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Leo pia ni Mei Mosi. Ni sikukuu ya Wafanyakazi katika sehemu nyingi za ulimwenguni ikiwemo Tanzania yetu. Nachukua nafasi hii kukutakia wewe mfanyakazi na watanzania wote kwa ujumla sikukuu njema.

Share and Enjoy:
  • Digg
  • Sphinn
  • del.icio.us
  • Facebook
  • Mixx
  • Google Bookmarks
  • email
  • LinkedIn
  • Live
  • Spurl
  • Technorati
  • Yahoo! Buzz
  • YahooMyWeb

chokinyotabc

Yupo mwanamuziki mmoja wa zamani kidogo aliwahi kuimba kwamba “wivu katika mapenzi ni lazima….japo kidooogo”. Alimaanisha kwamba wivu ni sehemu ya mapenzi ingawa pia aliashiria kwamba ukizidi unaweza kuwa kero na wakati mwingine kuleta balaa kabisa. Si ushasikia mtu kamchinja mwenzake kisa wivu?

Swali la kujiuliza ni je nini husababisha wivu? Ni kutojiamini,kupenda kumiliki kitu mwenyewe au ni kweli kwamba mapenzi ndio husababisha wivu?Na kama jibu ni ndio je hayo huwa mapenzi ya dhati au ndio tulivyo tu sisi wanadamu?

Huo ni upande mmoja.Upande wa pili ni kuhusu “mpenzi wa zamani”. Hivi watu wakishaachana bado huwa wanaachana kweli au huwa wanapeana nafasi? Na inakuwaje unapoona mpenzi wako wa sasa anaendeleza sana mawasiliano na mpenzi wake wa zamani? Ni sababu tosha ya kuwa na wivu?

Ali Choki akishirikiana na msanii Nyota Ndogo anayetokea nchini Kenya maeneo ya Mombasa(Naamini unamkumbuka kutoka katika kibao chake Watu na Viatu) wanaimba kuhusu mambo ya wapenzi wa zamani na “wivu”. Mmoja anakuwa haelewi,wivu unamtatiza.Mwenzake anamwambia tulia,usiwe na papara wala wasi,hakuna kitu. Mwenzake anamsihi kwamba asimfiche na ndio maana wimbo unaitwa Usinifiche. Mimi najiuliza;akiambiwa ukweli ataweza kuhimili? Can he handle the truth? Usikilize wimbo Usinifiche kwa kubonyeza player hapo chini.

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Share and Enjoy:
  • Digg
  • Sphinn
  • del.icio.us
  • Facebook
  • Mixx
  • Google Bookmarks
  • email
  • LinkedIn
  • Live
  • Spurl
  • Technorati
  • Yahoo! Buzz
  • YahooMyWeb

president-obamabc

Barack Hussein Obama ametimiza siku 100 leo tangu aapishwe kuwa Rais wa Marekani. Wamarekani wana utaratibu wao wa kijadi wa kupima uwezo wa kiuongozi wa viongozi wao wakianza na siku 100 za kwanza. Ni utaratibu wa kihistoria ambao kwa mujibu wao,huwa unaonyesha dalili za jinsi uongozi wa Rais mpya utakavyokuwa. Misingi,misimamo na hulka ya kiongozi wao huonekana ndani ya siku 100! Obama anazidi kujijengea umaarufu na pia kukijengea chama chake cha Democrat umaarufu.Republican wanazidi kubomoka na kuonekana kushindwa katika nguvu za hoja.

Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali,Barack Obama anazidi kukubalika. Wamarekani wengi wanakiri kwamba anafanya kazi nzuri,ni muwazi na hana zile hulka za kigomvi ambazo marais wengine waliomtangulia walikuwa nazo. Kitendo chake cha kusalimiana na Rais wa Venezuela,Hugo Chavez, hotuba aliyoitoa kule Uturuki,jinsi ambavyo ameanzisha mijadala ya kidiplomasia na nchi kama Iran nk ni baadhi tu ya mifano michache kati ya mingi inayoonyesha Obama ni mtu wa aina gani.Lakini wapo ambao wanasema haeleweki na wala hatabiriki. Bado wafuatiliaji na wakosoaji wa masuala ya kisiasa nchini Marekani wanakuna vichwa vyao kujaribu kumsoma zaidi.

Wakati anaingia madarakani niliwahi kuandika kuhusu tofauti mbalimbali za matarajio ya ulimwengu kwa Obama. Kila mtu alikuwa na bado ana lake.Weusi wengi duniani tunamuona kama kioo au ushahidi kwamba inawezekana na yaliyopita si ndwele bali tugange yajayo.Mashariki ya mbali wanachoomba ni amani.Akiweza kuwaletea amani ya kudumu ni mafanikio ya kutosha.Afrika tunachoomba ni misaada zaidi,kusaidiwa.Tunaamini kwa sababu ni Obama ni “mwanakwetu” basi ni lazima akumbuke alikotoka.

Sasa kama umemfuatilia vizuri Rais Obama utagundua kwamba hajaitamka tamka sana Afrika ndani ya siku 100.Amekuwa akizungumzia zaidi nchi za ulimwengu wa tatu na sio Afrika pekee ingawa nyingi ya nchi hizo zipo barani Afrika.Zaidi aliongelea habari hizi katika mkutano wa G20 huko Uingereza ambapo uwepo wake tu katika mkutano ule ulikuwa ni ishara ya kutosha kwamba huenda yale mabadiliko aliyokuwa anayanadi wakati wa kampeni zake ndio yamewadia. Obama anaonekana kuiangalia dunia kwa mapana zaidi kuliko wengi walivyotarajia.Je hiyo ni kumaanisha kwamba Afrika haipo katika nafasi za juu katika ajenda ya Rais Obama? Sina uhakika.Nampa muda zaidi.Yawezekana ni kutokana na changamoto za hali mbaya ya uchumi wa dunia zinazomkabili. Angalau tunajua hajaacha kumpigia simu “nyanya” ake aliyeko kijijini Kogelo.

Mwisho ni kumpongeza na kumtakia kila la kheri.Akifanya vyema Obama atazidi kuandaa njia ya vizazi vya sasa na vijavyo hususani vya watu weusi.Akichemsha tutaambiwa si mnaona? Tuliwaambia…..

Share and Enjoy:
  • Digg
  • Sphinn
  • del.icio.us
  • Facebook
  • Mixx
  • Google Bookmarks
  • email
  • LinkedIn
  • Live
  • Spurl
  • Technorati
  • Yahoo! Buzz
  • YahooMyWeb

blu3-new-1

Wanaitwa Blue 3.Wanatokea nchini Uganda.Ni miongoni mwa makundi ya muziki yanayofanya vizuri katika anga za burudani na muziki katika ukanda wa Afrika Mashariki.Mara nyingi wamekuwa wakitoa burudani safi katika matamasha mbalimbali yanayofanyikia Afrika Mashariki ikiwemo hivi karibuni walipoalikwa kwenye utoaji wa tuzo za Kili.Nawatafuta kujua kwanini wanajiita Blue 3. Why Blue?

Share and Enjoy:
  • Digg
  • Sphinn
  • del.icio.us
  • Facebook
  • Mixx
  • Google Bookmarks
  • email
  • LinkedIn
  • Live
  • Spurl
  • Technorati
  • Yahoo! Buzz
  • YahooMyWeb

frankbcNiliwahi kusikia mahali fulani watu wa nchi jirani na Tanzania wakisema kwamba Tanzania huwa inachelewa kidogo kuanza mambo lakini pindi wanapoanza huwa wanakuja juu kwa kasi ya ajabu! Bila kuingilia mazungumzo yao,jamaa wakawa wanataja mifano kama vile jinsi ambavyo Tanzania imepiga hatua kwenye shughuli za kisanii kama vile muziki na hivi sasa filamu.

Kuna ukweli ndani yake; tunaweza kuanza mwisho lakini tukawa vinara. Yote inategemea jinsi ambavyo tunaamua kujiweka na kusonga mbele. Mojawapo ni kukubali kwamba kuna kukosea na pia kujirekebisha. Hivi sasa sanaa ya filamu inazidi kukua nchini Tanzania. Inatia moyo sana kuona watu wa mataifa mengine wanaangalia filamu ambazo zinaitwa “za kibongo”. 

Pamoja na hayo kazi kubwa bado ipo mbeleni.Kama alivyowahi kusema Steven Kanumba tulipohojiana naye,kuna haja ya serikali kutoa support ya kutosha ili kuzidi kuinua sanaa hiyo. Marekani ipo hapo ilipo kwa sababu ilitangaza sanaa na sera zake za mambo ya nje kupitia kwenye filamu. Ikulu ya Marekani ina kitengo cha kushughulikia masuala ya filamu.Kama filamu itaonekana haijakaa “vizuri” kwa mujibu wa taratibu zao,basi haitoki.Mradi unakufa.

Lingine ni hili ambalo muigizaji Mohamed Mwikongi(pichani) almaarufu kama Frank katika uigizaji ameliongelea majuzi alipofanya mahojiano na jamaa wa Global Publishers. Frank anasema lazima wasanii na washika dau wote katika nyanja za filamu wakubali kukosolewa. Wazungu wanaita hii constructive criticism. Unapokubali kukosolewa unajipa nafasi ya ushindi kwani maana yake ni kwamba kesho utafanya kizuri zaidi.Lakini pia ipo haja ya wakosoaji kutokuwa “wabezaji”. Unapokosoa basi useme pia sababu zako na utoe ushauri wa kujenga kwamba nini kifanyike.Kwa mwendo huo filamu za kibongo zitazidi kupata jina na sio ajabu kabisa siku moja nasi tukaona Slumdog Millionare za kikwetu.

Share and Enjoy:
  • Digg
  • Sphinn
  • del.icio.us
  • Facebook
  • Mixx
  • Google Bookmarks
  • email
  • LinkedIn
  • Live
  • Spurl
  • Technorati
  • Yahoo! Buzz
  • YahooMyWeb

marlawbKama kuna mahali duniani ambapo unapotoa ahadi za kukutana ni sharti ufanye hivyo kwa uangalifu sana basi mojawapo ya sehemu hizo ni jiji letu la Dar-es-salaam.Kwanini?Kuna foleni isiyokuwa ya kawaida hususani katika ile mida inayoitwa na wenzetu wa magharibi “rush hours’.Unaweza ukakwama kwenye foleni mpaka ukashangaa.Kama ulitoa miadi ya kukutana saa fulani kwa ajili ya lunch au vinginevyo basi huna budi kuianza safari yako mapema kuliko kawaida ili yasije kukukuta yasiyotarajiwa.

Hali kama hiyo imeshawahi kumtokea mwanamuziki Marlaw(pichani) na anasema ndio sababu ya kutunga wimbo wake Pip Pip(Missing you my baby) ambao unazidi kukamata katika anga za muziki nchini Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla.Alikatiwa simu,hakueleweka.Ilibidi ajieleze kupita maelezo yenyewe.

Usikilize wimbo Pip Pip kwa kubonyeza player hapo chini kisha utueleze kero ambayo imeshawahi kukukuta kutokana na foleni za jiji letu au miji mingine ya Afrika Mashariki kwa ujumla.

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Share and Enjoy:
  • Digg
  • Sphinn
  • del.icio.us
  • Facebook
  • Mixx
  • Google Bookmarks
  • email
  • LinkedIn
  • Live
  • Spurl
  • Technorati
  • Yahoo! Buzz
  • YahooMyWeb

bc-makassyWeekend hii,watanzania sehemu mbalimbali za dunia wataungana kusheherekea Sikukuu ya Muungano.Ni miaka 45 sasa imepita tangu Tanganyika na Zanzibar zilipoamua kuungana! Kama hujaalikwa mahali kusheherekea Sikukuu ya Muungano basi tambua kwamba umejitenga sana na watanzania wenzako.Huna budi kurejea kwa wenzako kwani hata ukiendelea kukataa,wewe bado ni mtanzania.Isitoshe mkataa kwao ni….

Sasa kama ilivyo kwa miungano mingine yeyote ikiwemo hata ile ya binafsi kama vile ndoa,haikosi kasoro zake.Migogoro hutawala nyakati zingine.Kila mmoja,kwa njia moja au nyingine,huona kwamba mwenzake anampunja,anamuonea.Anadhani au kuamini kwamba angekuwa peke yake angefanya vizuri zaidi nk.Anasahau nguvu ya umoja.Anaota ndoto zake mwenyewe.Shauri yake,shauri yao.Na mara nyingi huwa tunabobea katika kutoa kasoro tu bila kuangalia yaliyo mema.Kwa vyovyote vile yapo mafanikio ya Muungano.Zipo kasoro pia.Lakini je kasoro zinazidi mema au mafanikio?Lazima tuketi chini na kujiuliza.Tukipata jibu tunaweza kuendelea na malumbano yetu ya kawaida kuhusu muungano.Tutakuwa na pa kuanzia na kuishia ikibidi.

Katika kuadhimisha sikukuu hii,nimeona nikuwekee kibao kinachoitwa Muungano. Ni kutoka kwao Orchestra Makassy.Nakutakia weekend njema na sikukuu njema ya Muungano.

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Share and Enjoy:
  • Digg
  • Sphinn
  • del.icio.us
  • Facebook
  • Mixx
  • Google Bookmarks
  • email
  • LinkedIn
  • Live
  • Spurl
  • Technorati
  • Yahoo! Buzz
  • YahooMyWeb

mama-jkbc

Wiki hii wake wa viongozi wa Afrika na kwingineko duniani wamekutana huko jijini Los Angeles jimboni California nchini Marekani  katika mkutano uliozungumzia masuala ya afya(zaidi afya mwanamke), elimu na masuala ya HIV/AIDS.Miongoni mwa wanawake hao ni Mama Salma Kikwete(pichani).

Masuala ya afya ni muhimu na yote yaliyoongelewa hapo juu ni mambo ambayo sote tunapaswa kushiriki katika kupingana nayo.Jamii isiyo na afya njema ni sawa na jamii isiyokuwepo!

Pamoja na hayo, jambo moja ambalo nimelipenda ni suala la jinsi ambavyo First Lady wetu amekuwa akiwakilisha ‘mavazi ya kwetu”.Sijui wewe unasemaje.Ukiniuliza mimi nitakwambia right on the goal Mama Salma.Endelea hivyo hivyo!!

Share and Enjoy:
  • Digg
  • Sphinn
  • del.icio.us
  • Facebook
  • Mixx
  • Google Bookmarks
  • email
  • LinkedIn
  • Live
  • Spurl
  • Technorati
  • Yahoo! Buzz
  • YahooMyWeb

nature1

Juma Nature ni miongoni mwa wasanii wa muziki wa kizazi kipya ambao huathiri jamii moja kwa moja kila watoapo albamu au wimbo.Matumizi yake ya lugha,mtindo wake wa kughani au kurap,uhalisia wa kitu anachokiongelea nk ni miongoni mwa mambo ambayo yanamfanya atambe na akubalike zaidi.

Hivi karibuni alitoa albamu ambayo ameipa jina la “Tugawane Umasikini”. Baada ya hapo kumekuwa na tafsiri mbalimbali kuhusu “kugawana umasikini”.Bila shaka umeshasikia mtu akikuambia ah…leo ni weekend bwana…ngoja tukagawane umasikini.Starehe mbalimbali zikiwemo ngono,pombe nk zimekuwa ni “kugawana umasikini”.

Lakini yeye mwenyewe alikusudia au kumaanisha nini alipozungumzia “Kugawana Umasikini”? Ili kupata jibu kamili nilimtafuta Nature na kufanya naye mahojiano yafuatayo;

BC:Mambo vipi Nature?Umeshamaliza tour ya kuzindua albamu yako?

JN: Mambo poa kabisa ndugu yangu.Tour naweza kusema bado inaendelea ingawa baada ya kutembelea mikoa kadhaa hivi sasa nimerejea nyumbani Dar kwa ajili ya mapumziko kidogo na kuangalia masuala ya familia.

BC: Nimekutafuta kwa ajili ya kutaka kujua kitu kimoja; hivi karibuni umetoa albamu ambayo umeiita Tugawane Umasikini. Baada ya kutoka kwa albamu hiyo kumekuwepo na tafsiri mbalimbali kuhusu “kugawana umasikini”.Wengine wanasema kugawana umasikini ni pamoja na kugida maji kwa sana,ngono(zikiwemo zembe) na kwa ujumla kuamua tu kuishi bila kufanya kazi kwa juhudi kwa sababu tayari wengi wetu tu masikini na hivyo hakuna la kufanya.Je, wewe ulimaanisha nini haswa ulipotaka kuzungumzia “kugawana umasikini”?

JN: Ahahahaha, labda hapo naweza kusema hiyo ni kazi nzima ya fasihi kwamba kila mtu anaweza kuupokea ujumbe atakavyo au apendavyo na wote wakawa sahihi! Kimsingi nilichomaanisha ni kwamba kutokana na ukweli kwamba nchi yetu na wengi wa wanachi wake bado ni masikini, ni jambo muhimu sana kusaidiana.

Pamoja na umasikini tulionao,endapo tutaamua kugawana hicho hicho kidogo tulichonacho basi kwa pamoja tutaweza kuinuana.Baba wa Taifa,Mwalimu Nyerere alipenda sana kutukumbusha kuhusu “Umoja ni Nguvu”.Hapo ndipo alipoongelea sana habari za Ujamaa na Kujitegemea.Leo hii tumesahau misingi ile na ndio maana labda tunaendelea kuwa masikini.Lakini mimi nikiwa nacho kidogo na nikamsaidia mwenzangu,basi kesho si ajabu na yeye akainuka na kumsaidia yule ama yule.Kwa mwendo huo tutafika mahali pazuri zaidi.Isitoshe hatuwezi kuzungumzia utajiri wakati sisi ni masikini.

Hivyo ndivyo nilivyoomanisha na ndivyo nilivyokusudia.Wanaopotosha au kujaribu kupindisha maana halisi wanafanya hivyo kwa sababu zao wenyewe zikiwemo kujifariji nk. Lakini kama nilivyotangulia kusema hapo juu,hiyo ni kazi ya fasihi na hivyo siwezi kuwatolea macho au kuwalaumu. (more…)

Share and Enjoy:
  • Digg
  • Sphinn
  • del.icio.us
  • Facebook
  • Mixx
  • Google Bookmarks
  • email
  • LinkedIn
  • Live
  • Spurl
  • Technorati
  • Yahoo! Buzz
  • YahooMyWeb

nasreembc

Miezi kadhaa tu imebakia kabla mrembo mpya wa Tanzania(Miss Tanzania 2009) hajapatikana. Tayari mashindano ya vitongojini yameshaanza huku matumaini yakiwa makubwa zaidi kutokana na kuongezwa kwa udhamini mzito wa kampuni ya simu za viganjani ya Vodacom.

Kwanini Hatushindi? Hilo ni swali ambalo bado litaendelea kuumiza vichwa.Lakini huenda mwaka huu tukatoka kwani habari nilizonazo ni kwamba umakini na weledi wa hali ya juu umejumuishwa katika zoezi zima la kumpata mshindi.

Pichani ni Miss Tanzania 2008,Nasreem Karim, ambaye pamoja na kuwa na viwango vya kutosha tu,hakufua dafu katika mashindano yaliyopita!

Share and Enjoy:
  • Digg
  • Sphinn
  • del.icio.us
  • Facebook
  • Mixx
  • Google Bookmarks
  • email
  • LinkedIn
  • Live
  • Spurl
  • Technorati
  • Yahoo! Buzz
  • YahooMyWeb

Read the Next Page →

↑ Go Back to Top of Page