jeffbcNaweza kusema nimeshazoea kuhoji wenzangu.Kuhoji watu ambao ndio chachu hasa ya BC bila kusahau msomaji ambaye ni wewe.Kumbe wakati nawawinda watu wa kufanya nao mahojiano,wapo wenzangu(wenzangu katika habari na mawasiliano) ambao pia huniangazia macho ili kufanya nami mahojiano.

Naomba nikiri kwamba hiyo hutokea mara chache.Naweza kukumbuka vizuri kabisa idadi ya mahojiano rasmi ambayo nimeshawahi kuyafanya.Sio kwamba sioni thamani ya mahojiano,la!Ni kwamba hupendelea tu kuwa upande mwingine wa kamera.Usinihoji sana kwanini kwa sababu sidhani kama nina jibu moja.Tutakesha.

Hivi karibuni Freddy Macha alifanya nami mahojiano ambayo yalichapishwa kwenye gazeti la Mwananchi mwishoni mwa wiki iliyopita. Kwa bahati nzuri nilishawahi kufanya mahojiano na Freddy Macha kuhusu kazi zake za uandishi,muziki na historia nzima ya maisha yake.Unaweza kusoma mahojiano yangu kwenda kwake kwa kubonyeza hapa na hapa.Kwa hiyo haikuwa kazi nzito sana aliponieleza nia yake ya kufanya nami mahojiano.Freddy ni mtu mcheshi,muungwana na mvumilivu.

Ni mahojiano mafupi lakini muhimu kiasi kwani unaweza kujua kile ninachokiwaza ninapokuwa nawaza na pia ninachofikiri kuhusu suala zima la blogs na maendeleo ya ulimwengu wa habari na mawasiliano ambapo siku hizi wewe msomaji na mchangiaji ndiye mshika tochi wa habari.Unaweza kuyasoma mahojiano hayo kwa kubonyeza hapa.

Feedback / Comments

9 Responses to “MAHOJIANO YANGU NA FREDDY MACHA”

  1. Comment by Moses Mayalla on April 16th, 2009 1:23 pm

    Big up Jeff.Uko makini mtu wangu.Keep it up!

  2. Comment by MICKEY JONES - DENMARK on April 16th, 2009 2:07 pm

    “COMRADE FREDDY MACHA NI MWANA MAPINDUZI”

    Mahojiano ya BC na Freddy Macha yametupa kumbukumbu ya watanzania wapi “tunatoka” na wapi “tunakoenda”.

    Kama asemavyo “comrade Freddy” miaka hiyo imetofautiana saana na miaka ya sasa kwa wana habari,wanamziki na hata wanamichezo.

    Tumefahamiana na comrade Feddy katika ujana wetu tokea mwaka 1976 akiwa mwanahabari wa mapinduzi ya maendeleo,namimi nikiwa mmoja
    wa mwanamziki “Bitoz” kijana,tukakutana tena nikikumbuka 1986 hapa Denmark akiwa kama mwanamuziki anayeheshimiwa saana.

    Ulimwengu umebadilika “mtandao wa habari” umeingia na kuyaendeleza yale tunayoyaita
    “uhuru wa wanahabari” na kuongezeka kwa magazeti mengi ni mojawapo ya maendeleo kuhakikisha kila mwananchi ana uhuru wa kupata habari mbalimbali,huko nyuma tuliyasoma yale tumepangiwa na “ma-comrade” ndiyo maana wengi tukajiweka mstari wa mbele kusoma vitabu mbalimbali kupata yanayotendeka nje ya nchi.

    Sitomaliza maoni yangu bila ya kumtaja mwana habari maarufu kwa wakati huu ndani na nje ya nchi mwenyekiti “MAJJID MJENGWA” ni mwandishi anayetukumbusha “tunakotoka na tuendako” kipaji chake si cha kawaida labda ni cha kuzaliwa au kurithi, mara nyingi humfananishana na “comrade Freddy” kama mwanakijiji wa mapinduzi katika mazingara yetu tofauti ya vijijini na mijini.

    mickey@mail-online.dk
    DENMARK

  3. Comment by Tram Almasi on April 17th, 2009 1:27 am

    Habari ndugu yangu,
    Ni kweli naomba nikiri kwamba tupo wengi ambao tumekuwa tukifuatilia wakubwa zetu na kazi zao kama Bro Freddy bila wao kujua. Naomba nikiri kwamba Bro Freddy alibadilisha mtazamo wangu kimaisha alipokuwa anaandika makala katika gazeti la Sunday News kama kumbukumbu zangu ni sahihi bado. Nakumbuka picha aliyokuwa ameiweka katika makala hizo ilikuwa amevaa shati la rangi rangi na kitu kama ushanga shingoni. tukiwa wadogo, tulivutiwa sana na hilo(I think u get my point)na tukasema ni lazima tujifunze lugha ili tuweze kuandika kama yeye na kuwa kama yeye-including his dressing style.
    Kwa wazazi wetu ilituletea shida kidogo, kwa sababu ilibidi tubadilishe combination,kutoka zile za sayansi(walizotaka wazee) na kusoma ‘HGL’ ili “tuwe kama Freddy Macha”. Maana tuliambiwa ukitaka kuwa mwandishi hiyo ndio ‘combi’ muafaka.
    Nashukuru tulifanya vizuri sana mimi na mwenzangu(Another Freddy fan japo he ended up doing Laws na hayupo katika fani ya habari.
    Na nilipofika high school, nilikutana na fan mwingine wa Bro Freddy anaitwa Albert Memba(Alikuwa mwandishi wa IPP Media)na tukaendeleza ushabiki wetu kwa Freddy!
    Miaka ya 90, tulikuwa a bit dissapointed kwa sababu alipotea katika anga za uandishi Tanzania,lakini baadaye tukaanza kumuona tena katika makala akiandika kutoka Brazil. You can imagine how happy I was!
    Nasikitika sijapata kukutana au kumwandikia Freddy juu ya haya.
    Baada ya Bro Freddy kupotea, mimi binafsi nikaanza kufuatilia kazi za Da’ Chemi che Mponda, nakumbuka sana makala yake juu ya maswahibu yaliyompata alipokwenda kufanya mahojiano ubalozi wa (nafikiri atakuwa anakumbuka vema juu ya hilo).
    Kwa ufupi nataka kuwajuza akina Jeff(BC),Bro Freddy, Da’Chemi, na wengine wengi, kwa kupitia kazi zenu kuna watu wanawafuatilia na wanabadili maisha yao (ili kuwa kama wao-”role models”) japo wao hawajui,kwa maana hiyo wakienda kombo na hao pia wanaenda kombo.
    Kwa kumalizia, napenda kumpa ujumbe Bro Freddy kwamba, namheshimu, naheshimu kazi zake na sijajuta kamwe”kutaka kuwa kama yeye”. Makala zake toka Brazil zilinifanya nitake kujua zaidi kuhusu Brazil na kuipenda Brazil, japo sijapata bahati ya kufika huko kama yeye!(Kicheko!!!!).
    BC keep up the good work, Bro Freddy Big up sana.AM OUT.
    TRam
    Bongo DArisalama,Daslam(whatever!)

  4. Comment by mr degree on April 17th, 2009 4:34 am

    Nimependa pale uliposema hali ni mbaya zaidi kwa Watanzania kwani imefika mahali tunazidi kuwa masikini hata wa kufikiri,kwa kweli tunahitaji kubadilika na kuacha ushabiki huu wa siasa kama tunataka mabadiliko ya kweli yatakayotuletea maendeleo. tupo pamoja!

  5. Comment by Dinah on April 17th, 2009 8:28 am

    Hongera Jeff kwa kuwa selebu kwenye BC :-)

    Mahojiano mazuri sana, Nimependa wazo lako la kuandika mazuri ya Celebs wetu kuliko mabaya ambayo yameegemea zaidi kwenye uongo/uzushi ili kuuza clicks au magazeti.

    Kungekuwa na bloggers wengine 9 kama wewe, tungekuwa mbaali ktk kupasha jamii habari chanya in terms of bloggers na sio Journalists sio kwa maendeleo ya jamii tu bali hata mtu moja moja as an individual.

    BC iendelee kuwepo mpaka mwisho wa kuhesabu Miaka.

  6. Comment by Flora on April 17th, 2009 11:27 am

    Macha U r a super star “*”

    Thanx 4 keeping us well informed though its hard to satisfy each and every individual actually you are doing your best.

    Take it easy and keep it up!

  7. Comment by Simon Kitururu on April 17th, 2009 11:35 pm

    Hii kitu bomba uliyofanya JEFF na isinuniwe.

  8. Comment by Kibarati on April 20th, 2009 8:09 am

    Binafsi napenda Mahojiano ya Jeff kwa Macha kuliko ya Macha kwa Jeff hayana lolote, Namkubali sana Macha ila naona kama alikurupuka kwenye inawezekana kwa sababu anamfahamu sana Jeff hivyo kila alichopata kuuliza aliona kina jibu.
    Nawakubali sana, Macha, Jeff, Michuzi, Pius, Full Shangwe na wengineo mnanipa kilema cha kupitia Blog zenu kila uchao. Jeff jamaa wa Spoti na Starehe nadhani mlikuwaga pamoja marafiki sana kama sikosei je bado mko pamoja? mnawasiliana?
    Shabiki wenu wa Upanga.
    Kila la heri.

  9. Comment by Freddy Macha on April 22nd, 2009 8:49 pm

    Maoni ya wasomaji wa blogu zetu ni muhimu sana kuchangia fikra na changamoto. Sema ningependa kufafanua maoni ya Kibarati aliyesema “nilikurupuka” kufanya mahojiano na Jeff Msangi yaliyotoka Mwananchi; ukilinganisha na yale aliyonifanyia bradha Jeff katika blogu ya Bongo Celebrity; ambayo bila shaka yalikuwa marefu zaidi. Ni kweli kuwa mahojiano yangu kwa Jeff Msangi gazeti la Mwananchi yalikuwa mafupi. Ipo tofauti kubwa kati ya uandishi ya magazeti na ule wa mablogu. Magazeti huendeshwa na wahariri na kanuni nyingi; mojawapo ikiwa idadi ya maneno na kiasi cha picha kutumika. Pia wahariri huamua nini kitoke na nini kisitoke; ilhali katika mablogu kuna uhuru wa kuandika chochote kiwe kirefu au kifupi; hata picha na taswira.
    Zingatia pia tofauti ya uzito wa vyombo hivi viwili vya habari. Wananchi weengi bado hawasomi fasihi za mtandao aghalabu mablogu. Kwa hiyo magazeti kwao chai na mandazi na maparachichi. La kuzingatia ni je tunayoandika yanaleta uzito gani katika kuwajenga wahusika? Mablogu yanasambaa na kutandazwa mtandaoni kwa miaka ilhali gazeti likashasomwa linawekwa kando kufungia michicha sokoni. Ndiyo maana wahariri wa magazeti husisitiza makala ziwe fupi.
    Lakini iko siku kazi za watu kama akina Jeff zitapewa uzito katika fani nzito zaidi ya vyombo vya habari: yaani kutolewa katika vitabu, televisheni na sinema, we ngoja tu: Inshallah.

Leave a Reply