DR.IMANI KYARUZI NA MBINU ZA UJASIRIAMALI

Mwaka jana mmoja wa wataalamu na wasomi wetu mhadhiri anayeishi Uingereza Dk. Imani Silver Kyaruzi alitoa kitabu moto moto “Mbinu za Ujasiriamali” kitakachosaidia sana uchumi na akili za Mtanzania hasa yule anayependa kujiendeleza au kufanya biashara. Kitabu hiki kilichochapishwa na “Mkuki Na Nyota” mjini Dar Es Salaam ni kidogo chenye kurasa 50. Hivi karibuni alifanya mahojiano na Freddy Macha. Hii ni sehemu ya Kwanza ya mahojiano hayo.

dr-kyaruzi-na-susan-mzeebc

Dr.Kyaruzi(kulia) akiwa na Katibu Wa Chama cha Watanzania nchini Uingereza,Suzan Mzee(kushoto) wakati wa uzinduzi wa kitabu hicho Birmingham-October 2008.

FM :Muundo au fani yako ni kuuliza maswali na kupanga vichwa rahisi vya kuelewa kimaneno. (“Je wewe unauza nini?” ” Je unahitaji watu wa kushirikiana nao?”).

Twaweza kusema kazi yako ya kufundisha (Mhadhiri, Uingereza) imeathiri muundo wa kuandika kitabu hiki kizuri chenye lugha nyepesi kueleweka?

 

Dk. Imani Kyaruzi: Kweli kabisa…niliamua kutumia lugha nyepesi na yenye kueleweka baada ya kugundua kuwa watu wengi (wafanyabiashara) wanashindwa kufuatilia maelezo yaliyomo katika vitabu vya kimataifa vya ujasiriamali. Si Tanzania tu, bali hata hapa Ulaya wafanyabiashara hawana muda wa kusoma madoido ya kisomi yasiyoeleweka! Ila kwa upande mmoja haikuwa rahisi kuandika kitabu hiki kwa lugha kiswahili kwani nina muda mrefu tangu nimeondoka Tanzania na lugha imebadilika sana. Utakuta katika baadhi ya maneno nimejaribu kufikiri katika lugha zote mbili na kutafuta maneno yatakayofaa kuufikisha ujumbe bila kuupotosha.

 

FM: Mwisho kabisa (sura ya 8) unatoa muhtasari wa maudhui yako.

“…Usisahau kuwa ujasiriamali si kwa ajili ya kutengeneza faida tu! Ningependa kuwasisitiza wajasiriamali wengine waibuke wenye nia ya kugusa masikini, walemavu na wale wasiojiweza.” Unasisitiza biashara yenye wajibu sambamba na biashara ya faida. Je unakubaliana na mawazo “mapya”nchi za Magharibi karibuni kuwa na ubepari na biashara yenye hisia (compassionate capitalism au responsible capitalism) baada ya matatizo ya uchumi kutokana na mabenki kuanguka (2008-2009)?

 

Dk. Imani Kyaruzi: Ilinibidi nisisitize suala la umuhimu wa ujasiriamali-jamii (social entrepreneurship) baada ya kugundua kuwa kuna dhana potofu ya maana sahihi ya ujasiriamali. Watu wengi wanafikiria sana faida badala ya kuboresha maisha ya watu na mazingira yanayowazunguka. Si lazima kwa mfanyabiashara kutoa fungu la kumi, lakini mawazo yangu yanalenga hasa kwa Wafanyabiashara wanaotajirika sana na kusahau kuwa sehemu kubwa ya mapato yao yanatoka kwenye jamii.

Kutikisika kwa uchumi 2008/9 kunaashiria kwamba ubepari-mkomavu hauna nafasi katika kujenga uchumi na maisha bora (hasa kwa kina kabwela). Inasikitisha sana kuona kuwa Afrika na labda niongelee Tanzania yetu tunashindwa kuwa na ubepari wetu (African Capitalism) – ule usiolenga kuwajenga wachache na kuumiza walio wengi. Tutangaze rasmi kuwa ujamaa umezikwa, lakini mbadala usiwe ubepari wa magharibi. Kwanza, ubepari umejengwa na misingi au dhana potofu ya kutengeneza fedha na utajiri wa harakaharaka wenye vyanzo tata (mfano “EPA-ism”). Pili, ubepari-mkomavu umepoteza uhalisia – wachache walishachukua nafasi za peponi hivyo ukiona leo Wazungu wanalima bustani za mboga badala ya kwenda sokoni hii inaashiria kuwa tunaanza kurudi ardhini na ni jambo zuri kwa dunia ya tatu kwani mzani unalegea pande zote. Hii ndio maana yangu ya uhalisia – ya kwamba si vibaya tukitegemea sekta ya huduma, tukashinda tunalonga kwenye Tigo na Voda na matumizi ya tovuti lakini tukakumbuka kuwa kama “ukitaka mali utayapata shambani” – si vibaya kutumia mikono. Tufanye kazi kwa bidii na hakuna mbadala wa kazi na ubongo.

 

dr-imani-kyaruzibc

Dr. Kyaruzi akimkabidhi kitabu chake Balozi wa Tanzania nchini Uingereza,Mwanaidi Maajar.

FM:Je umeonaje matokeo ya G20 ambayo yameonyesha nia hiyo kupitia Rais Obama wa Marekani?

 

Dk. Imani Kyaruzi: Nina hakika G20 itakuwa na matokeo mazuri pindi maazimio yaliyofikiwa yatakapowekwa katika vitendo. Mikutano hii mikubwa huja na ahadi nyingi na tabasamu nene na picha za watu mashuhuri waliovaaa suti kali hivyo sitaliongelea sana suala hili hadi pale vitendo vitakapoanza kutendeka.

Suala moja walilolisahau kwenye G20 ni kuwahimiza watu wa Afrika kuwa wakaze uzi, waache uvivu na wapunguze utegemezi kwani jungu la wafadhili ipo siku litatakauka na watalala njaa kwa kuendekeza tabia ya kuombaomba. Siku ikifika kila mtu atajali watu wake kwanza na sio wananchi wa Mwanalugali! Tusiweke misaada ya wafadhili kama sehemu mojawapo ya miundo ya kujenga uchumi bora – hii dhana imepitwa na wakati.

 

Endelea sehemu ya pili ya Mahojiano mwezi ujao.

 

UKITAKA KUNUNUA KITABU AU KUWASILIANA NA DK. KYARUZI

 Simu : +44 -7977807295

Barua pepe: boraimani@yahoo.com

 1. Salma, 27 April, 2009

  Nimefurahi kuona jinsi gani BC inavyothamini na kuenzi,mashujaa wetu kwakujaribu kuwafichua na kuwaleta mbele ya jamii….Ijapokua kwa mda mrefu, watanzania wengi tumekua wachoyo wa kuwapongeza wale wanaojaribu kuwa mstari wa mbele nchini, katika kupambana na maadui ujinga, maradhi na umasikini, ambao Dr.Kyaruzi amejaribu kugusa mawili kati ya hayo yaani Ujinga kwa njia ya elimu kama Mhadhiri, na Umasikini kwa njia ya Uandishi kama hicho kitabu chake cha Mbinu za Ujasiriamali…Dr. Imani ameleta sura mpya kwa wasomi vijana, niwakati sasa Watanzania tuanze kuwapa moyo wasomi wetu kwakuweza kupiga hatua, na pia sisi tuweze kufata na kuyatumia mazuri yao. Hichi kitabu cha Mbinu za Ujasiriamali ni moto wa kuotea mbali, ni kitabu kilichoandikwa kwa lugha nyepesi ya kueleweka kwa watu wote wenye rika zote, kilichojaa mifano na majadweli ndani yake…nilipokisoma sikuweza kukiweka mbali…nilikua na maswali mengi kichwani kuhusu kitabu hiki,na nnaamini nisingeweza kupata majibu,ila bongo celebrity imenitatulia kwakupata nafasi ya kumhoji.
  nnahamu sana kuona sehemu ya pili ya mahojiaano haya.

 2. joseph Kulinga, 27 April, 2009

  Kwanza kabisa naipongeza kwa dhati kabisa BC kwa kazi nzuri inayoifanya ya kuwathaminisha watanzania wenzetu waliopo kote ulimwenguni kwa yale mazuri wanayoyafanya popote walipo. Pili nimefurahi mno kusikia habari za huyu ndugu niliyepotezana naye miaka mingi, enzi za Tambaza sec school na SUA, Dk.Imani Kyaruzi,nachukua nafasi hii kumsalimu, lakini pia kumpongeza kwa kazi nzuri anazozifanya huko ughaibuni, ikiwa pamoja na kuwakumbuka watanzania wenzake waliopo nyumbani kwa kuwatungia kitabu kizuri chenye nia ya kuwakomboa katika lindi la umasikini. Keep it up

 3. dan, 27 April, 2009

  Ujasiliamali, unaishi london wapi na wapi! Wizi mtupu!

 4. Frank M, 29 April, 2009

  Sasa wewe Dan unadhania kukaa London ndo kutokujua ujasilimali? Grown up man ,huyu mtu hakai London hapa ni birmigham kama ujui,usijidau kujua watu wakati wewe hata vigwaza upajui, behave man

 5. Jeylani Mkomwa, 30 August, 2009

  Kazi njema Dr. Imani,

  Sijakisoma kitabu chako, hata hivyo bila shaka ni changa moto kwa wanaojaribu kujikwamua kiuchumi. Kusoma ndio kujua, shime watanzania tukisome kitabu.

  Asante mno,

  Mkomwa

 6. Salome Charles, 23 June, 2010

  Napenda kuchukua nafasi hii kumpongeza sana Dr.Imani Kyaruzi kwa kutuwezesha sisi wajasiriamali,wajasiriamali wengi wetu Tanzania hatuna elimu ya ujasiriamali,Hivyo basi napenda kuchukua fursa hii kuhamasisha wajasiriamali wenzangu kununua kitabu hicho ili tuweze kupata hiyo elimu.
  Thanks

 7. Dr Imani Kyaruzi, 23 August, 2010

  Wapendwa wajasiriamali na marafiki,
  Asanteni sana kwa michango yenu. Ningependa kuwasiliana nanyi kwani ninapanga kufanya ziara nyingine Afrika. Mnaweza kuniandikia barua pepe: boraimani@yahoo.com
  Kwa wale walioandika tayari, tarehe za semina zitawafikia karibuni.
  Asanteni sana,
  Imani.

 8. Reginald Mponzi, 01 September, 2010

  Mi nashukuru kwa taarifa hii toka huko majuu. Je waweza angalau ukanitumia table of contents ya kitabu hicho? Tafadhali ili nijue nikitafute kwa haraka au polepole. Ninaishi mbali na DSM na huku sijakiona madukani

 9. kyejo clara w, 30 September, 2010

  TUNASHUKURU KWA KITABU SABABU ELIMU YA UJASILIAMALI TUNAIHITAJI SANA.

 10. SHAWALO, 28 January, 2011

  Nimependa kuona ni jinsi gani mko mbali nasisi huku Bongo lakini mnajali hata wale wasiojiweza kwa kubuni mbinu mbali mbali kama kutunga vitabu kama hivyo ili kuwainua wale wenye hali tofauti angalau na yeye ajihisi yupo Duniani kama walivyo wengine. Swali nikwamba mimi nakihitaji sana kukisoma hicho kitabu uwezo wa kukinunua sina na njia za kukipata sijui naomba msaada wako Dr. Imani Natanguliza shukurani za dhati kwako.

 11. Legnard, 03 February, 2011

  TAFADHALI NITUMIE TABLE OF CONTENTS NIJUE KAMA NAWEZA KUNUNUA KITABU CHAKO KWA AJILI YA KUUZIA WATANZANIA WALIO WEN GI HUKU BONGO. MIMI NI MUUZA VITABU MASHUHURI MJINI MOSHI.

  NIJIBU TAFADHALI

 12. mbaraka juma, 23 March, 2011

  dah nimefurahi kukutana na habari tamu kama hizo ingawaje nasikitika kwa kuchelewa kuzipata!nakihitaji iki kitabu haraka kwa gharama zozote ili niandae ‘future’ km kjana,mimi ni mtanzania ila nko algeria kimasomo ila dk bado kuna kazi kubwa kwa vijana waki-tz kutambua umuhimu wa ujasiriamali hivyo wanaweza kukipita madukani kitabu kama iki na kutafuta majarida ya udaku!!thanks broza kwa kutujali watanzania wenzako!

 13. bongocelebrity, 24 March, 2011

  Mbaraka
  Asante kwa kututembelea.Naomba utuandikie e-mail kupitia bongocelebrity at gmail dot com au info at bongocelebrity dot com nasi tutakuunganisha na mwandishi ili akupe maelekezo zaidi ya jinsi ya kukipata.

 14. ERIC TESHA, 21 April, 2011

  NIMEKUBALI SANA MCHANGO WA DOCTOR,LAKINI TATIZO KUBWA LA SS WATANZANIA SIO KWAMBA HATUWEZI!!!LA HASHA!!!KIKUBWA NI CONDITIONS ZINAZOTOLEWA NA BANKS N OTHERS FINANCIAL INSTITUTIONS KWA WAJASIRIAMALI WADGOWADOGO!!!HATA TUNAPOOMBA MIKOPO TUNAPEWA HIGH INTEREST RATES INSUCH A WAY M2 ANAISHIA KUTAIFISHWA NA KURUDI KATIKA HALI KAMA YA ZAMANI<SO MCHANGO WAKO NI MKUBWA DR LAKINI HALI BADO NI TATA SANA KWETU SS.MAY BE TUNASUBIRI 2015 TUTAKAPO IPIGA CCM CHINI!!!!!!

 15. AGATHA, 06 May, 2011

  Mimi nakuongeza sana kwa jitihada za kuandika hiki kitabu hakika suluhu ya maisha ya mtanzania kwa sasa ni ujasiriamali tuuu. Mungu akubariki sana na akuwezeshe uendelee kuandika vitabu vingine kwa faida ya watanzania

 16. AGATHA SHAO, 06 May, 2011

  Mimi nakupongeza sana Dokta kwa jitihada za kuandika hiki kitabu hakika suluhu ya maisha ya mtanzania kwa sasa ni ujasiriamali tuuu. Mungu akubariki sana na akuwezeshe uendelee kuandika vitabu vingine kwa faida ya watanzania

 17. LAMECK KOMBA, 11 August, 2011

  HONGERA SANA DOKTA KITABU CHAKO NIMEKISOMA/NINACHO NA NI KIZURI SANA PIA KINAMFAA MTU YEYOTE MWENYE MALENGO YA KUJIKWAMUA KIMAISHA KWA UJASIRIAMALI. USIISHIE HAPO TU,NAPENDA UENDELEE KUANDIKA ZAIDI KUHUSIANA NA UJASIRIAMALI ILI ELIMU HII ISAMBAE NA ISAIDIE KUPUNGUZA UMASKINI TANZANIA NA BARANI AFRIKA KWA UJUMLA.

 18. Godchance John Msaki, 20 October, 2011

  Am a gruduate,napenda sana kuwa msariamali na si kutazamia ajira kutoka kwa mapepari ambao hata kidogo hawalengi katika kumwinua ‘kabwela’. ningependa sana kupata makala yahusuyo ujasirialami

 19. Mpuya Sabasaba, 12 June, 2012

  Kaka Imani nakupongza sana na nimefarijika pia kwa hatua uliyopiga ukizingatia nakufahamu kwa ukaribu. Swali langu je tunawezaje pata hiyo copy hapa Dar, kuna duka au agent wako hapa DAR?
  Hongera sana Mate.

 20. IMANUEL PASCAL MWANGOMOLA, 07 August, 2013

  MIMI NI TANZANIA NAOMBA NI UWEZO WA KUKUSANYA WATU HASA WAJASILIAMALIPIA NINA LIBRARY YA KUUZA VITABU HAPA MBEYA HIVYO NAOMBA KUVINUNUA AU KUWA WAKALA NAOMBA JIBU NA NITASHUKURU SANA MY CONTACT 255755693917

 21. bongocelebrity, 07 August, 2013

  Imanuel,
  Nimempelekea Dr.Imani ujumbe wako.Asante kwa kuwasiliana na hongera sana kwa jitihada zako.

 22. DOLORES MWENDA, 18 August, 2013

  MIMI NI MJASIRIAMALI NIPO KASULU KIGOMA NAPENDA KUKUPONGEZA LAKINI HUKU KASULU HATA SERIKALI IMEPASAHAU INAFIKIRI NI SEHEMU YA BURUNDI JE WEWE UTANISAIDIAJE KUPATA HICHO KITABU?NIKIKIPATA NITAWAOKOA WAHA WENZANGU KWANI TUPO GIZANI.TENA INGEKUWA FURAHA HATA MALAIKA MBINGUNI WANGETUUNGA MKONO UKIFANYA ZIARA YA MAKUSUDI UJE KASULU UTUFUNDISHE KWANI WEWE NI MTANI WETU HUWEZI KUTUACHA TUFE KABISA.

 23. ngailo, 07 September, 2013

  KWA YEYOTE ANYETAKA KUSOMA HABARI ZA UJASIRIAMALI ANAWEZA SASA AKAPATA KITABU KINACHOITWA MJASIRIAMALI WA TANZANIA KINACHOPATIKANA MOSHI KWENYE RENNICS BOOKSHOP. BEI YAKE NI SH 15,000 TU. KITABU HIKI KITAKUWA NA TOLEO LA PILI MWEZI WA KUMI MWAKA 2013. WATU KUMI WA MWANZO KUNIANDIKIA KUPITIA mvanginyi22@yahoo.com WATAPATA KITABU HICHO KWA BEI NDOGO SANA NA WATAFURAHIA. KARIBUNI.
  L. N. NGAILO
  MUCCoBS
  BOX 7775
  MOSHI
  TANZANIA

 24. Samwel Shayo, 03 April, 2014

  jitihada na muda mwingi Dr unaoutumia kuuelimisha uma wa kitanzania na dunia kwa ujumla haulipiki kwa fedha au dhahabu bali kwa kukuombea Mungu akupemaisha marefu na amani moyoni itakayo kuongezea ubunifu na kufanya makubwa zaidi.

 25. Upendo, 21 December, 2014

  Nitapataje kitabu hiki cha ujasiriamali?

 26. sebastian kalinga, 08 April, 2015

  asante kwa wazo lako. Natamani nikisome.

 27. Thabir.S.Karwani, 06 January, 2016

  Dear Dr Imani. Nimefarajika Sana kujifumza ya kwamba wewe Ni mtunzi WA kitabu cha Mbinu za Ujasiliamali, kitabu chenye lengo la kumkomboa mtanzania kielimu kwa kutambua fursa za biashara zilizopo na mbinu za kujikwamua kwa kufanya biashara zenye lengo la kuinua kipato cha mtanzania.

  Binafsi zi zikakipata hiki kitabu na hivi sasa nakitafuta him niweze kukisoma na kunufaika na yaliuomo ndani ya ubunifu WA mtunzi Wa kitabu hiki.

  Nampongeza Dr Imani Kyaruzi kwa kuwakumbuka Watanzania kwa kuwapa dozi ya Elimu yenye manufaa kwetu sisi wote.

  Thabit.S.Karwani

Copyright © Bongo Celebrity