
Miezi kadhaa tu imebakia kabla mrembo mpya wa Tanzania(Miss Tanzania 2009) hajapatikana. Tayari mashindano ya vitongojini yameshaanza huku matumaini yakiwa makubwa zaidi kutokana na kuongezwa kwa udhamini mzito wa kampuni ya simu za viganjani ya Vodacom.
Kwanini Hatushindi? Hilo ni swali ambalo bado litaendelea kuumiza vichwa.Lakini huenda mwaka huu tukatoka kwani habari nilizonazo ni kwamba umakini na weledi wa hali ya juu umejumuishwa katika zoezi zima la kumpata mshindi.
Pichani ni Miss Tanzania 2008,Nasreem Karim, ambaye pamoja na kuwa na viwango vya kutosha tu,hakufua dafu katika mashindano yaliyopita!
Feedback / Comments
22 Responses to “KWANINI HATUSHINDI?”
Leave a Reply


sending...
kama kweli mnataka ushindi muoneshe kile ambacho hata hao wazungu watakiona kimetokea TZ au afrika leo mnakwenda kuwaonesha wazungu yale ambayo wao ndio tamaduni zao ndani ya onesho zima huku nyinyi mkiwa watu wa kuigiza ambayo wao wanayaita urembo unaotokana na jamii zao .I m sorry but no chance no way
swali zuri tu kwanini Tanzania tunashindwa ktk hizi miss contest..binafsi nadhani 1. wasichana wanaochaguliwa sio ´beauty with brain´2. Pia maandalizi ya kwenda huko miss world ni hafifu sana mie nimesikia nchi nyingine miss anatayarishwa mwaka mzima kabla ya kwenda miss world. 3. Siasa inatumika kuchagua huyo miss TZ yaani vigezo havitumiki kikamilifu 4. Wasichana ambao wengeweza kufanya vizuri kwenye miss world wala hawajitokezi bec zoezi zima la kumtafuta miss TZ limesha tafisiriwa kwamba wote wanashiriki ni wahuni au kama sio wahuni baada ya hilo zoezi wanakuwa wahini bec mabuzi wanawafuata fuata ect binafsi wala sifagilii zoezi zima la miss Tz too much politics
sister TZ umesahau kugusia rushwa ya ngono wanayotoa washiriki kuanzia vitongoji hadi kitaifa,wasichana wenyewe wanapenda kutoa rushwa ya ngono na waandaaji nao ndo dili zao hizo, na ndio maana wasichana wenye akili zao hawawezi kushiri hata siku moja tutawapata haohao kina sepetu tu, upuuzi mtupu!
Hatushindi kwa sababu yule ambaye angeweza kutufikisha mbali katika mashindano ya miss world unakuta hachaguliwi wanajua wenyewe wanakuwa wameshampanga mtu wao, pia seriousness inakuwa haipo sana kumuandaa miss inabidi katika mavazi pia kama mwenzangu mwanzoni hapo alivyosema nguo ya usiku watanzania tunawabunifu kibao sasa hivi wa mitindo wanashindwa kudesign nguo ambayo itakuwa ya asili ya kitanzania lakini everning dress?? hata katika mavazi ya kiytamaduni tunavyo viatu ( sandals) za asili cant they wear them jamani…..mazoezi sio kuwatembeza sana tuuu kwenye mbuga au vivutio vingine, wajifunze kuwa normal wasipritend wakiwa kule waonyeshe jinsi watanzania tulivyo kuwa sio wabaguzi tunacheka na kila mtu tunaelezea nchi yetu ilivyokuwa na vivutio vingi… show them our Tanzanian Culture..
We don’t win and we will never win for unccountable reasons such as:
Bias on the selection
Lack of confidence
No motivation
Not well prepared
According to my little knowledge on beauty pageant its not about being
Tall
Thin/Slim
Talkative
Smile
Catwalk
Whatever skin color
With all the above without “BRAIN” being sharp/self representative/quick thinking capacity.I real feel pity for my country because winning its something that will never come into reality unless otherwise we make some improvement in order to pull ourselves into another level.
Best of luck to all Tanzanians Girl who wish to became our future models.
Mie nadhani tuache tu kushiriki bec hamna la maana hawa wasichana wanatuletea maana tunashuhudia wengi wao, baada ya umiss ni uhuni tu na bahati mbaya zaidi wengi wao hawajaenda shule so hata baada ya umiss kazi za maana hawapata wengi wanakuwa ´ma designer´
Mr Degree kaka yangu rushwa ya ngono kweli nilisahau hizi miss zetu zimejaa rushwa ya ngono..duhh na haya magonjwa basi sitaki wala kuongea zaidi..ila mimi binafsi nataka mfumo wote wa kuchagua hawa miss ubadilishwe na wahusika wakuu wa sasa hivi kwa kweli wabadilishwe..Flora ndugu yangu umeongea vitu vya msingi sana kuwa miss sio urefu tu ni zaidi akili, jinsi unavyojirepresent mbele za watu wa maana, maana mamiss wetu utakuta wapo na watu wa maana kazi kujichekeshacheka hawajafundishwa
kuwa just friendly and decent…
SIO TANZANIA PEKEE.
Tunapochangia hili lazima tuwe na data wandugu.Tanzania ukiachilia ile ya miaka ya 60 kufanya Miss Tanzania na kufutwa, imerudishwa tena miaka ya 90s, sina uhakika kama ile ilikua ni 1994.Cha kujiuliza, ni miaka mingapi tumeshiriki hadi sasa kwa ngazi ya Miss World?Na kushindwa ina maana waliotakiwa kushinda waliachwa bongo kwenye vitongoji?
Ni nchi nyingi ambazo zimeshiriki hiyo Miss World tangu kitambo, lakini hazijawahi kutoa Miss World.Na mara nyingi Miss World huwa anatoka huko Venezuela, India na kwingineko.Mrembo wa Nigeria alishwahi kushinda mara moja kuwa Miss World.
Kuna suala la maandalizi, vigezo, motisha nk, lakini sio kila wakati kushinda huwa ni kutokua na maandalizi.Ni lazima mshindi awe mmoja tu.Na sio lazima awe anatoka Tanzania.Maana Nanvy Sumari alishafika hadi hatua nzuri sana, tunashukuru.Miaka mingine ipo inaweza kutokea kwetu Tanzania Miss World akatoka.
Kupata washiriki wenye uwezo ni preparation nzuri kuwa siku zali ikidondoka inatukuta tupo fit.Good luck is when preparations meet opportunity.
MAKULILO, Jr.
http://www.makulilo.blogspot.com
West Virginia, Marekani
jamani nafurahi sana na kuguswa mno na stakeholders hapo juu…kwa kweli you have spoken my mind…
the so called misses are very dully…no brain power at all,…umande waliogopa…so how do they think they will compete with simmering brains…??…its utter lunacy…!!..(im sorry to say that…)
…Lundenga and his colleagues should be a little more serious…otherwise MNATUTUKANISHA huko majuu…inaudhi…kuna binti wazuri wengi na wana brains….ila kama wadau walivyosema hapo juu ni RUSHWA tupu from rushwa ya vijisent mpaka rushwa ya mwili…(im sorry again abt that…)….
They misses should try to be NOVEL…display their originality (…as Paul James put it)…mnawaonnyesha kuvaa bikini wakati wao ndio wenyewe…jamani….muwe wabunifu…(and here the BRAINS come into play….)
Naona zoezi zima la U-MISS…lichunguzwe kama kweli tuna nia ya KUPEPERUSHA BENDERA ya taifa letu huko majuu…otherwise it is crap…has to be binned… lol
well…they should try to brush them…say a year b4 they compete on the international fora…brain-improving games…a little bit of academic brush-up (viji-course vya kuwaongezea maarifa na kuongeza uwezo wao wa uelewa kwenye sensitive international issues…
…issues za mazingira: how they can help to mitigate the ongoing environmental pollution, the current global water crisis, the looming global warming, the scary HIV/AIDS pandemic, how they as MISSSES can fit-in within the society….their expected roles….role-playing among the u-miss contestants…etc, etc, etc….
…kama wameshindwa kuwa FAIR kwenye selections…basi wawa-elimishe hao wanaokuwa wameshapanga kuwa watakuwa washindi…(sasa tusemeje…)…
Hii itakuwa ni hatushindi kwa sababu hatushindi
wadau Mr Degree, SisterTz, mwanamke wa shoka mbona mmemaliza yote jamani..mimi nadhani tuache tu kwenda huko miss Miss World..maana mie enzi za Happy Magesa nilipata moyo sana nikaambulia pabaya…
hatushindi sababu,tunachagua mamiss hata backgrpund yake hairidhishi.darasani hamnazo,shule kakimbia umande au shule imempitia pembeni,kujua kingereza sio soln,soln ni AFAHMU KINGEREZA NA afahamu nini anachokiongea,ajiamini,mzuri,ANAHESHIMA.
mnanichagua mie hata kuogelea sijui,sina fani yoyote,shule nehi,jamani.
mfano kati ya wema na joketi nani aliestahili kuwa miss TZ?joket ashawahi kuwa dada mkuu wa LOYOLA,MZURI,ANAJUA ANACHOKIFANYA,ANAAKILI,ANAJIAMINI,KINGEREZA HAKIGOMBI.ANABACKGROUND NZURI,WAPUMBAVU WAKAENDA KUMCHGUA….Uozo mtupu.
CHOGO mie wataalam wa habari wameniambia kwamba Joketi ndio alikuwa anamfanyia Wema Sepetu character assassination bec yeye alishindwa kutua taji ni kweli..
wadau mwenzenu huyo miss ya last year nilivyomuona tu nilijua hamna kitu tena hapo..sijui jamani tufanyeje ili mambo yaenda salaama this time
The new miss Tanzania is beautifull but she looks old to participate in the contest…she is a beautiful girl but not for miss world…its a different story out there… Nigeria won miss world. the girl had …confidence… great personality, fluent English, smart and intelligent…plus beautfull, she looked young and fresh, she was tall…dark and slim…….see Miriam odemba…she is so similar to miss Nigeria…only if she could communicate properly, fluent English and smart… if she had all the above, 5 years ago if chosen she’d def bring the tittle home am confident about it… they are the types of girls Tanzania should search for..did you watch clips from you tube of Miss Earth!? she came 2nd…because of her looks and personality, but could answer questions cause of English and intelligence, also last years miss world…top 3 I think it was a girl from Africa too…I think she came 3rd…see her physic???? its the same as miss Nigeria and Miriam…
they are definitely the type of girls judges in miss world are looking for for Africans to win…a Naomi Campbell look…when are we going to learn…a naomi Campbell from Tanzania with brains…confidence and personality..infairness.. I have seen many contestants for miss Tanzania…very little or non to choose/qualify for the miss world tittle…its pity cause Tanzania is well known abroad for having beautifull girls in Africa… FACT!
kama hakuna changes zozote miaka nenda rudi bac hizo pesa za kufanya mashindan ya mamiss bora tufanyie mtaji wa biashara nyingine.
wasichana mnaojipeleka kushiriki mashindano tafadhalini kama hujenda shule,kingeredha nehi kaa chonjo cz mnatuharibia sana.na mnaishia kuwa wahuni cz yakukosa shughuli za kufanya so mnatake advantage ya kushiriki umiiss ndio mwanzo wa umaarufu na ndio mwanzo wa kujiingiza kwenye UHUNI.plz waachieni wenye fani,hatakama wasiposhinda wanavsomo na shughuli za kuwakeep bzy si kufanya umalaya.na nyie mamiss kuweni na akili bana umiss sio UMALAYA.mnaharibu sana ndio maana hatupati wenyesifa cz mtu na akili zake hawezi kujiunga na malaya,hata wazazi inakuwa ngumu kuwaruhusu watoto wao.
na nyie akina lundenga mbona tunasikia tetesi kuwa eti kunarushwa ya ngono mnayopewa ili mtu ashinde ni kweli??we mtu mzima na akili zako timamu hivi unasikia hizo tetesi kwenye kamati yako aahh umeridhika na umekaa kimya kama umeweka pamba masikioni?? xx@@ kabisaa ndio maana TANZANIA yetu hatupati washiriki wazuri waliokwenda shule na wanaofaa.hufanyi utafiti wowote umekaa tu?ama ndio wewe hizo rushwa za ngono unapewa??embu kua akili bac kidogo sio mwili mjomba,tumechoka kutuchagulia vituko,na kutufanya WATANZANIA wote VINYAGO VYA MPAPULE yaani tumekosa binti mzuri nchi nzima loo??nchi yenye mikoa ishirini na tano kama sijakosea na watu zaid ya milioni 30???eeh embu kuwa serious once in ur life bana.ni mtazamo tu mjomba niache njipanda hapo…
AMY you are right unajua Mariam Odemba was my favourite she is so beautiful..enzi zake i met her at Blue Palms we told her she so beautiful ect ila ndugu yangu that was it physical beauty only vitu vingine hamna kabisa akili ya kuzaliwa ni zero which is sad kwa kweli…tunahitaji a black beauty fulani hivi na sio huyo ex miss Tz mimi nilivyomuona tu nikajua ohhhhhhhhh again kusindikiza wengine…(jamani inauma bec wa afrika wenzetu mbona wanafanya vema kwa nini sisi tusiweze?)na mimi binafsi what i have seen kwa hawa ma miss wetu yaani hawajui kabisa kuji present wao wanadhani each time ni kuchekache foolish..yaani kuna mdau hapo juu amesema vizuri tu hawajua kuwa friendly and decent..maana wao wanadhani kila mtu anawataka tu ndio kazi kuchekacheka..labda ingekuwa vema kamati nzima ya Miss Tz kuangaliwa upya tena…
CHOGO mwenzio kila mwaka naangalia miss World na nikimuona miss wetu yaani anakuwa she is not standing out from the crowd si mnanielewa wadau..kwanza anakuwa kama hajiamini hivi yaani anaogopa fulani hivi..ila yule miss World m Nigeria alikuwa funga dimba, na alikuwa anajiamini maswali yote anafikiria haraka na kujibu kwa makini, na pia alikuwa anaonyesha kwamba amejianda vizuri sana…haya kazi kwetu mwaka huu Lundenga upo? BC fanyeni kuforwardia Hashim Lundenga haya maoni yetu yote ili na yeye abalidi taktics zake mwaka huu..na kama hatuwezi kujipanga basi mie nadhani tusiende huko Miss World
yeeeh!naungana na chogo,huo pia ni mfano tosha kabisa wa kuona waandaaji wanachokifanya sio,joket was perfect anakila kitu miss kama miss anatakiwa kuwa nacho,sio siri mie nimeshachoka na haya malumbano maana tulishaongea sana lakini mambo niyaleyale tu
mimi sio mtanzania lakini naunga mkono 100 percent maona ya baadhi ya washikadauu waliotoa hoja hapo juu. shida mlio nao haswa na wale judges mnaowapea hio cheo cha kuchagua nani ata-represent. kuna michezo ya ngono ya ajabu na ubadilishaji senti inayoendelea huko underground kabla maamuzi hayajafanyika. unapata kuwa wale warembo ambao wangefaa kushinda lakini walikataa kulala na majaji hawapiti. sasa hapo ndio inakuwa vigumu kushinda miss world mkiwakilishwa na malaya ambao preparation yao imekuwa ni kuangusha suruali.