
Juma Nature ni miongoni mwa wasanii wa muziki wa kizazi kipya ambao huathiri jamii moja kwa moja kila watoapo albamu au wimbo.Matumizi yake ya lugha,mtindo wake wa kughani au kurap,uhalisia wa kitu anachokiongelea nk ni miongoni mwa mambo ambayo yanamfanya atambe na akubalike zaidi.
Hivi karibuni alitoa albamu ambayo ameipa jina la “Tugawane Umasikini”. Baada ya hapo kumekuwa na tafsiri mbalimbali kuhusu “kugawana umasikini”.Bila shaka umeshasikia mtu akikuambia ah…leo ni weekend bwana…ngoja tukagawane umasikini.Starehe mbalimbali zikiwemo ngono,pombe nk zimekuwa ni “kugawana umasikini”.
Lakini yeye mwenyewe alikusudia au kumaanisha nini alipozungumzia “Kugawana Umasikini”? Ili kupata jibu kamili nilimtafuta Nature na kufanya naye mahojiano yafuatayo;
BC:Mambo vipi Nature?Umeshamaliza tour ya kuzindua albamu yako?
JN: Mambo poa kabisa ndugu yangu.Tour naweza kusema bado inaendelea ingawa baada ya kutembelea mikoa kadhaa hivi sasa nimerejea nyumbani Dar kwa ajili ya mapumziko kidogo na kuangalia masuala ya familia.
BC: Nimekutafuta kwa ajili ya kutaka kujua kitu kimoja; hivi karibuni umetoa albamu ambayo umeiita Tugawane Umasikini. Baada ya kutoka kwa albamu hiyo kumekuwepo na tafsiri mbalimbali kuhusu “kugawana umasikini”.Wengine wanasema kugawana umasikini ni pamoja na kugida maji kwa sana,ngono(zikiwemo zembe) na kwa ujumla kuamua tu kuishi bila kufanya kazi kwa juhudi kwa sababu tayari wengi wetu tu masikini na hivyo hakuna la kufanya.Je, wewe ulimaanisha nini haswa ulipotaka kuzungumzia “kugawana umasikini”?
JN: Ahahahaha, labda hapo naweza kusema hiyo ni kazi nzima ya fasihi kwamba kila mtu anaweza kuupokea ujumbe atakavyo au apendavyo na wote wakawa sahihi! Kimsingi nilichomaanisha ni kwamba kutokana na ukweli kwamba nchi yetu na wengi wa wanachi wake bado ni masikini, ni jambo muhimu sana kusaidiana.
Pamoja na umasikini tulionao,endapo tutaamua kugawana hicho hicho kidogo tulichonacho basi kwa pamoja tutaweza kuinuana.Baba wa Taifa,Mwalimu Nyerere alipenda sana kutukumbusha kuhusu “Umoja ni Nguvu”.Hapo ndipo alipoongelea sana habari za Ujamaa na Kujitegemea.Leo hii tumesahau misingi ile na ndio maana labda tunaendelea kuwa masikini.Lakini mimi nikiwa nacho kidogo na nikamsaidia mwenzangu,basi kesho si ajabu na yeye akainuka na kumsaidia yule ama yule.Kwa mwendo huo tutafika mahali pazuri zaidi.Isitoshe hatuwezi kuzungumzia utajiri wakati sisi ni masikini.
Hivyo ndivyo nilivyoomanisha na ndivyo nilivyokusudia.Wanaopotosha au kujaribu kupindisha maana halisi wanafanya hivyo kwa sababu zao wenyewe zikiwemo kujifariji nk. Lakini kama nilivyotangulia kusema hapo juu,hiyo ni kazi ya fasihi na hivyo siwezi kuwatolea macho au kuwalaumu.

Nature akifanya vitu vyake siku ya uzinduzi wa Tugawane Umasikini
BC: Kama ulivyogusia katika jibu lako hapo juu,watanzania wengi bado ni masikini lakini pia wapo watu ambao ni matajiri wa kutupwa. Una ujumbe gani kwa matajiri hao?
JN: Ni kweli kabisa usemalo,wapo matajiri wa kutupwa.Ujumbe wangu kwao ni ule ule labda kwa mtindo tofauti kidogo tu.Badala ya kugawana umasikini wao nitawaambia wagawe utajiri walionao.Wakifanya hivyo nina uhakika wataendelea kuwa matajiri na pia kuinua hali za watu wengine.Umoja ni nguvu.
BC: Kwa mtu ambaye anataka kununua albamu ya Tugawane Umasikini anaweza kuipata wapi?
JN: Albamu hivi sasa inapatikana kote mitaani.Lakini kwa uhakika anaweza kuipata pale Mamu Store-Kariakoo.Albamu hii inasambazwa na GMC Wasanii.
Editor’s Note: Ukitaka kusoma mahojiano tuliyowahi kufanya na Juma Nature siku za nyuma bonyeza hapa.
Feedback / Comments
30 Responses to ““TUGAWANE UMASIKINI” MAANA YAKE NINI?”
Leave a Reply


sending...
Kwa mara nyingine Jeff-BC anatupa mahojiano
ya mmojawapo wa wasanii aliyefikia kilele
cha mziki wa kizazi kipya ndani na nje ya
nchi.
Maswali na majibu ni mtazamo mzuri wa kuigwa
na wengine, umasikini ulikuwepo, bado upo na utaendelea kuwepo,kama hatugawani.
kama asemavyo “Jumma Nature” kila masikini akigawana na mwengine atakuwa amepiga hatua mbele ya maendeleo na kila tajiri akiusambaza utajiri wake kwa walio masikini atakuwa ameuzalisha utajiri wake, huu ni mtazamo wa fikira za kibinadamu kwa sisi watanzania ambao wengi bado tupo masikini.
mickey@mail-online.dk
Denmark
Nature hakika umeanza kukomaa mzee, tafsiri uliyoitoa imekaa sawa na inamaanisha ulikuwa unafahamu unachokifanya wakati ukitipa albamu yako jina hilo, Big up mzee. Wasanii wengine igeni mfano huu maana imekuwa kawaida kusoma mahojiano ya wasanii na waandishi na kukuta majibu yao yanatofautiana na maswali wanayoulizwa.
I just love this guy. keep it up JN. Very proud and biggest fun…
big up J. Nature. Imetulia kama ulivyokusudia. Kaza buti
Nature mbona kakomaa toka siku nyingi. Jamaa katoka mbali bwana toka enzi za “tulianzisheni za kigeto geto Juma Nature, Piko na King Sapeto … tulianzisheni za kigeto kigeto tuyapangilie na madili yetu!”
Zikaja enzi za Mzee wa Busara na swahiba wake wa kufa na kuzikana, kunyimana na kupeana, bifu na mapatano Inspector Haroun aka Babu … ilitesa kwa sana tu … huku Inspector na yeye akikimbiza nchi nzima kwa spidi ya supersonic na kibao chake cha “Mtoto wa geti kali”
Kisha akaja kwenye mkasa wa mapenzi na usaliti wa Sinta ambapo alimwimba kwa sana tu mapa alipokuja kushushuliwa pale Landmark, Ubungo.
Then jinsi alivyochapa kazi kulijenga kundi la TMK Wanaume (lile la kwanza kabisa) ambapo aliwaibua na kuwapiga tafu masela kibao kama vile kina Temba, KR Jibaba, YP an Y-Dash, Dachi girl, na wengineo ambao baadhi yao sasa hivi wanadiriki kum-diss (binadamu bwana! kweli hatufadhiliki.)
Kisha hapo kati akavuruga vuruga kwa kufunika mbaya watu kwenye korasi, mafeaturing kibao, mpaka mzee mzima akalamba tuzo Denmark na South Afrika.
Mkubwa huyu kwa gemu yuko fiti. Ukisikia “Nature mtu wa watu” sio kwamba anafagiliwa bure ila ni kwamba jamaa kila shoo anayofanya lazima kuwe na nyomi za kufa mtu … iwe Diamond, au uwanja wa nyumbani TMK, au mkoa jamaa yuko juu.
Hey nature,
nyimbo yako ni nzuri lakini nilitegema kuwa KUGAWANA KWAKO UMASIKI UNGEWEZA KUSEMA KUWA KTK PESA NILIYOPATA KTK UZINDUZI UTASAIDI JAMBO FULANI MFANO KUPELEKA MISAADA YA CHAKULA AU VIFAA KTK SHULE ZA WALEMAVU NA MAYATIMA! HAPO INGELETA MAANA NJEMA , AGANALIA MFANO ROSE MHANDO ALIPOSEMA KUWA AKIZINDUA AMETOA MSAADA WA BASIKELI WKA WALEMAVU!! KWA VILE MUDA BADO UPO NINGEFURAI KUKUONA KTK RUNINGA YANGU YA TV UNAONYSHA KUGAWANA UMASIKINI KWA KUPELEKA MISAADA YA CHAKULA NA VIFAA KWA WALEMAVU NA WATU WASIOJIWEZA WANAOLEA MAYATIMA
ASANTE
JN hongera sana unai,ba vizuri sana ila tatizo lako ni moja unapenda sana kusifia mabo ya vyakula hiyo inaniboa sana mimi acha mambo ya watoto wa uswahilini
aaaaayaaaaa wali nazi naziii big up juma kasim nature aka kibra aka sir aka nyingi sanaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
Dah dogo naona kidogo anaanza kuelewa anachokifanya. Unajua tatizo hawa madogo wanakula sana Ndumu (Baghi) hivyo kuna kipindi kazi zinawashinda kabisa, nakumbuka huyu dogo alialikwa South Africa lkn alishindwa kuperform kwa sababu ya kilaji, alichapa sana pombe. Tatizo hapa Tanzania wasomi wanajitenga na hawa kina Juma Nature (wasiosoma), lkn kama tungekuwa makini hawa madogo wangezalisha sana pesa na watu kibao wangepata ajira kupitia kwao. Hawa wanataka management tu, hivi wewe embu angalia wale jamaa wanaocheza mieleka kule Marekani, wale ni watu walioshindikana kwa utukutu, lkn watu wamewatengenezea mchezo ambao wenyewe wana enjoy na wamemekewa mameneja, madaktari, wahasibu na system nzima imekalika na watu wanakula mingo nyuma ya migongo yao. Sasa hata hawa walevi wetu kina Nature kama watu wangekuwa makini hawa madogo wangezalisha tu kwasababu wanakubalika. Sasa we angali mtu kama Juma Nature Kiroboto leo anaendesha Benzi we hauoni kama ni maajabu hayo, kutokea anaishi Temeke sehemu duni na ngumu kabisa mpaka kuja kuendesha gari la thamani na lakuheshimika hapa Tz sio mchezo. Hawa madogo wanalipa.
Nihayo tu wakuu tusijengeane bifu ila mi najaribu kuyaweka mambo sawa kutoka na experiance yangu ndogo ya biashara.
Muddy
kama kugawana umasikini ni kugawana kile kidogo tulicho nacho (kushirikiana)basi hata kushirikiana katika mapenzi, starehe hasa kwenye kununuliana beer, vyoote kwa nia nzuri ni kugawana umasikini…
Nature mzee yuko juu na sina swali juu ya jibu lake kuhusu kugawana umasikini, jamaa anajua kuongea!!!
E BWANAEE JUMA MKALI JAMANI JUMA KICHWA JUMA BOMBASTIC JUMA FANTASTIC
Nature u are clever! Thank you, we got your message through that interview and hopefully others will get the same message by listening your music.
Muziki ni ujumbe siyo paparapapara.
Wishing u best of luck!
Yap mzeeh hii inaonyesha ni jinsi gani ulivyokamaa kwa kifikra zaidi kama ulivyo kwa game…kazi tu baba.
big up sana!
tang nikufaham nature sasa hivi ndo umeanza kuimba vitu ambavyo vinaweza kumfanya mtu akakaa na kukusikiliza kwa makini kuliko ambavyo wewe unafikiria.
ujue umeanza kuimba vitu ambavyo kila binadamu hai vinamgusa.
watanzania walio wengi ni masikini sana kiasi ambacho imefika kipindi ambacho ninyi wasanii mnapaswa kukaa chini na kutafuta namna ya kuwasaidia kimawazo.
“nafurahi umekuwa WA KWANZA”Endelea kutupa vitu mtu wetu.
EBWANA IBAKUAJE HUYU JAMAA TUNASIKIA KATOA ALBUM MBONA AMWEKI MZIKIWAKE HATA MMOJA TUUSIKIA SISI TUNAOKAA UGAIBUNI.MAANA KILA MWANA MZIKI MKITOAGA HAPA HABARI ZAKE ZAKIMZIKI MNATOA NAKIBAO CHAKE CHINI.YA JUMA MBONA AMTOI TUUSIKIE? TUNAOMBA KAMA MNAO MTUWEKEE AU JAMAA HANA CD ANA RADIO CASSETI TUU?
hahahahh ushindi sio kufosi ushindi sio kipopi popi au kipoperepa papaaa……. aisee nakufagilia sana kaka kwa kazi zako nzuri. kaza buti waonyeshe watu kuwa huwa hubahatishi.
mzee karibu tena katika fani
Ebwana Muddy apo juu, sana m2mzima, hawa wanamuziki wetu kama, watu tutakaa na kuwatengenezea, mazingira mazuri bila kuwadhulumu, wataondokana na hayo maisha mabovu fasta sana..Sema sasa nao kuna bahadhi yao wabishi wakishapata buku buku za show ngumi jiwe, dada zetu wao na tungi ndo kabisa.
Msanii kama Juma Nature aka Kibla aka kiroboto aka etc ni noma na yuko Unique sana tofauti na wasanii wengine, Inabidi watu wamuangalie ni miongoni mwa wasanii wabunifu, na mwenye kuchangia maneno kibao ktk lugha yetu ya kiswahili na yanakubalika sana tu. Kama atatengenezewa mazingira na akiwa chni ya Menejiment natumaini atafanya mambo makubwa sana,Tofauti naapo wataishia kutumiwa na wajanja hadi basi kwa vijisenti vya ngama tu. Haya bwana mi yangu ndo hayo na acha tuendelee kugawana umasikini jamani kwa njia mbali mbali tusibaniane.
Nafikiri Nature amewaimbia Mafisadi/Vigogo serikalini wanaohusika ktk kuweka mikakati ya kutumia kodi tunazokatwa wananchi, hasa hasa wabunge na Mawaziri. Kwamba Japo kuwa wao ndo tumewapa dhamana ya kupanga matumizi ya pesa za kodi/Dhahabu/almasi tulizopewa na maulana, wanapodai waongezewe posho/mishahara huku wakiendesha Ma-Benz na kuishi kwenye majumba ya kifahari huku wanachi walio wapa dhamana hiyo hawana hata mahitaji muhimu ya binadamu km, chakula, maji safi, nyumba bora n.k, hapo tunakuwa hatuugawani umasikini. “Kuugawana umaskini” Naweza kuiita hiyo ni Philosophy moja muhimu sana kwa watanzania. Big up Nature!
Hongera sana JN kwa kuja upya mara nyingine tena!
sifagilii bongo flava,lakini ikija kwa juma nature,inspector harun,profesa jay,dudu baya.mmmh huwa wananifikisha mbalii kimawazo big up nature
nafikiri katika artists wanaofanya real tanzanian music ze boy z handling a label daaah!!! big up mwna uswahilini wetu
ebwana kibla uko juu……..kama kawa 2gawane umaskini imewafikia sisi maskini na hata hao wanaojiita mapededjee!!
safi sana my people, pia http://www.mtayarishaji.blogspot.com itakuwa hewani hivi karibuni.
Lovely.
ILI KUU AGA UMASIKINI.INABIDI KILA MTU AJITUME KWELI KWELI
HI
SIR
NATURE
BRO UKO JUU SANA TU SO KAZA BUTI NI KISIKILZA SONG LA MIGAMBO NABURUDIKA KWELI “TUGAWANE UMASIKINI”
HI
SIR
NATURE
BRO UKO JUU SANA TU SO KAZA BUTI NI KISIKILZA SONG LA MIGAMBO NABURUDIKA KWELI “TUGAWANE UMASIKINI”
Read more: “TUGAWANE UMASIKINI” MAANA YAKE NINI? – BongoCelebrity
nature tulia kwani upo kama vipi jipe jina la gaddafi wa bongo fleva?
Mie nakubaliana kabisa na Juma Nature kwa msemo huu alioutumia! ila kwa binaadamu wa leo kugawana utajiri ni Ndoto kwa kweli. masikini siku zote huwa na huruma na humfikiria mwenzie ambae yuko na hali kama yake. tajiri anachofikiria yeye ni kuendelea kuchuma na kujilimbikizia mahela na hakumbuki kama kuna wa2 wanashinda siku kula mara 1… serikali ye2 ndio ya kutusaidia na kutukwamua kutoka kwenye umasikini na si wao kukaa Bungeni kila siku kudai marupurupu na kula Bata, wanatuumiza sie Raia wenye uwezo wa chini!!!!!!