bc-makassyWeekend hii,watanzania sehemu mbalimbali za dunia wataungana kusheherekea Sikukuu ya Muungano.Ni miaka 45 sasa imepita tangu Tanganyika na Zanzibar zilipoamua kuungana! Kama hujaalikwa mahali kusheherekea Sikukuu ya Muungano basi tambua kwamba umejitenga sana na watanzania wenzako.Huna budi kurejea kwa wenzako kwani hata ukiendelea kukataa,wewe bado ni mtanzania.Isitoshe mkataa kwao ni….

Sasa kama ilivyo kwa miungano mingine yeyote ikiwemo hata ile ya binafsi kama vile ndoa,haikosi kasoro zake.Migogoro hutawala nyakati zingine.Kila mmoja,kwa njia moja au nyingine,huona kwamba mwenzake anampunja,anamuonea.Anadhani au kuamini kwamba angekuwa peke yake angefanya vizuri zaidi nk.Anasahau nguvu ya umoja.Anaota ndoto zake mwenyewe.Shauri yake,shauri yao.Na mara nyingi huwa tunabobea katika kutoa kasoro tu bila kuangalia yaliyo mema.Kwa vyovyote vile yapo mafanikio ya Muungano.Zipo kasoro pia.Lakini je kasoro zinazidi mema au mafanikio?Lazima tuketi chini na kujiuliza.Tukipata jibu tunaweza kuendelea na malumbano yetu ya kawaida kuhusu muungano.Tutakuwa na pa kuanzia na kuishia ikibidi.

Katika kuadhimisha sikukuu hii,nimeona nikuwekee kibao kinachoitwa Muungano. Ni kutoka kwao Orchestra Makassy.Nakutakia weekend njema na sikukuu njema ya Muungano.

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Feedback / Comments

8 Responses to “MUUNGANO UDUMU!”

  1. Comment by marknigga salamba on April 25th, 2009 12:18 pm

    kweli muungano ni muungano,hta viungo vya miili yetu vimeungana,baba na mama waliiungana,sisi tukazaliwa,basi wajibu,TUSALITI,na kuuthibiti muungano.nyundo yenye nguvu,naye imeungana na kijiti,kigogo,ili igonge vizuri,motokari kila chombo chake kumeungana,kitoe safari nzuri,wangonjwa uzaliwe,watu wameungana,wakupokee,na kukata kitovu,wafariki watu wamekusanyika,waihifadhi mauti wako wakuzike.mtu,watu,wanoona muungano si kitu kizuri,BASI ubongo wao una walakini,hawana safu nzuri kwa kujiuuliza.

  2. Comment by zanzibar on April 25th, 2009 6:19 pm

    MIMI NASHANGA SANA SIONI JUU YA UMUHIMU WA MUUNGANO HUU, SI VUNJA TU

  3. Comment by Flora on April 27th, 2009 9:16 am

    I don’t even know where to start? So many questions are rooming in my mind I have no where to get appropriate answers. Real my fellow citizens do we still have courage to cerebrate “UNITE” in our country? If so do we ever done research and see how much we are affected in the following statatement:

    1. Gap existing between richer and poor?
    2. Unemployment rate?
    3. Maternity death?
    4. AIDS pandemics?
    5.

  4. Comment by Flora on April 27th, 2009 9:27 am

    I don’t even know where to start? So many questions are rooming in my mind I have no where to get appropriate answers. Real my fellow citizens do we still have courage to cerebrate “UNITE” in our country? If so do we ever done research and see how much we are affected in the following statatement:

    1. Gap existing between richer and poor?
    2. Unemployment rate?
    3. Maternity death?
    4. AIDS pandemics?
    5. Basic service provided?
    6. Living conditions?
    7. Chidrens protections?
    8. Freedom of speech?
    9. Public participation in small or larger projects>
    10.Others?

    Why celebrating UNITE if the following activities still taking place into our community

    A. Leave my neighbour with hunger
    B. Girls and Women are being raped by our Grandpa,Father,Uncle, brothers etc
    C. Ministers, Directors, Managers (SUGAR DADS) are still involved in sexual activities with school girls.

    In reality those who wish to celebrate UNITE in our country I would like to let them know that they are celebrating “UNITE” VERBAL not in PRACTICAL or HUMANITY.

    Continue enjoying your UNITE day. Sorry I am out!!!!!

  5. Comment by kibunango on April 27th, 2009 9:56 am

    Shukrani sana kwa kipande hiki cha Makassy

  6. Comment by chapombe on April 28th, 2009 7:38 am

    swali,sasa muungano ukivunjwa,sisi huku wa bara,tutaita nchi yetu tanganyika,au?…wajameni,kila mtu na ubongo wake.mi hilo tu ndilo linaniumizaga kichwa.

  7. Comment by nambokola on May 5th, 2009 5:12 pm

    la kwanza watu wengi wanatizama upande mwengine kama yaaani muungano ukivunjwa itakuaje na sie tushazaana ama wengine kuhamia sehemu nyengine lakini hilo sio swali la hata kama hakuna muungano bado relation itakuwepo.
    la pili kwamba jee sisi wazanzibari tunafaidika nini ama tumefaidika nini na muungano huu ama ndio tunafaidika kwa kwenda nchi nyengine bila ya passport na wengine wanafaidika kwa kujenga nchi yao lakini sisi tunadidimia na nchi yetu kufa
    na naona imefanana na gofu sasa.
    big up dr salmin amour(command)

  8. Comment by chapombe on May 22nd, 2009 10:29 am

    sasa bwana nakombola,wewe usiseme eti kwasababu wachaga wanajenga moshi au wahaya kujenga kagera iwe sababu ya kuvunja muungano,hapo utakuwa mnaafiki mkubwa.kwani kuna wapemba au waunguja wangapi wanaojenga mahekalu mikocheni dar,kwani hawayaoni hayo magofu huko zenji.hayo ni maslahi ya mtu binafsi.vilevile usiniambie eti tanzania bara inajengwa kwako kodi za wazanzibari wakati wenyewe wanabaki nchi masikini,huo utakua uongo mkubwa,sijui kuna mzanzibari atakayeona kodi yake inachukuliwa kwenda kufungulia mradi kigoma akakubali,sana sana zanzibar inafaidi uhusiano uliokuwepo kuliko watu wa mpanda au songea.sema kuna watu wanapenda kulialia na kutia huruma kwakisingizio cha muungano bila kukaza msuli wenyewe.ona,pwani ya mashariki na kaskazini ya unguja,yote imenunuliwa na wageni na ni wenyeji wenyewe ndio wanauza kwa vijisenti.kesho hawaruhusiwi hata kusoge karibu,wenyeji wanalialia wageni wanachukua pesa taslim.kwa akili zako za mapokeo,hutaki kusonga mbele hoo muungano.we unafikiri hao viongozi wako wa kiunguja ndio wasafi kabisa,pole sana

Leave a Reply