frankbcNiliwahi kusikia mahali fulani watu wa nchi jirani na Tanzania wakisema kwamba Tanzania huwa inachelewa kidogo kuanza mambo lakini pindi wanapoanza huwa wanakuja juu kwa kasi ya ajabu! Bila kuingilia mazungumzo yao,jamaa wakawa wanataja mifano kama vile jinsi ambavyo Tanzania imepiga hatua kwenye shughuli za kisanii kama vile muziki na hivi sasa filamu.

Kuna ukweli ndani yake; tunaweza kuanza mwisho lakini tukawa vinara. Yote inategemea jinsi ambavyo tunaamua kujiweka na kusonga mbele. Mojawapo ni kukubali kwamba kuna kukosea na pia kujirekebisha. Hivi sasa sanaa ya filamu inazidi kukua nchini Tanzania. Inatia moyo sana kuona watu wa mataifa mengine wanaangalia filamu ambazo zinaitwa “za kibongo”. 

Pamoja na hayo kazi kubwa bado ipo mbeleni.Kama alivyowahi kusema Steven Kanumba tulipohojiana naye,kuna haja ya serikali kutoa support ya kutosha ili kuzidi kuinua sanaa hiyo. Marekani ipo hapo ilipo kwa sababu ilitangaza sanaa na sera zake za mambo ya nje kupitia kwenye filamu. Ikulu ya Marekani ina kitengo cha kushughulikia masuala ya filamu.Kama filamu itaonekana haijakaa “vizuri” kwa mujibu wa taratibu zao,basi haitoki.Mradi unakufa.

Lingine ni hili ambalo muigizaji Mohamed Mwikongi(pichani) almaarufu kama Frank katika uigizaji ameliongelea majuzi alipofanya mahojiano na jamaa wa Global Publishers. Frank anasema lazima wasanii na washika dau wote katika nyanja za filamu wakubali kukosolewa. Wazungu wanaita hii constructive criticism. Unapokubali kukosolewa unajipa nafasi ya ushindi kwani maana yake ni kwamba kesho utafanya kizuri zaidi.Lakini pia ipo haja ya wakosoaji kutokuwa “wabezaji”. Unapokosoa basi useme pia sababu zako na utoe ushauri wa kujenga kwamba nini kifanyike.Kwa mwendo huo filamu za kibongo zitazidi kupata jina na sio ajabu kabisa siku moja nasi tukaona Slumdog Millionare za kikwetu.

Feedback / Comments

12 Responses to “BONGO NA SANAA YA FILAMU”

  1. Comment by leah on April 28th, 2009 8:34 am

    sure watanzania tunatakiwa kuwapa tafu wenzetu si kukubaliana nao katika uzembe na mabaya kama wanafanya but kuwa tayari kuwapongeza na kuwapa moyo pindi wajitahidipo na kuwakosoa pindi wakoseapo.

  2. Comment by Pandu on April 28th, 2009 8:51 am

    Filamu za Kibongo ni kama magazeti ya udaku.Hawa jamaa so called mastaa wa filamu badala ya kutumia muda kuboresha fani wao wameamua kutengeneza filamu zisizo na ubora kila mwezi na cha kusikitisha zaidi wanakopi Naigeria, ni kweli wanapata hela coz ni wakati wao wa kufanya ivyo coz wadau wanawakubali lkn wanaboa kwa watu wanaofatilia michezo hii kwa umakini. Mchango mdogo niwasaidie, filamu ikipewa jina la kiingereza wakati mnatumia kiswahili inaboa, mnaongea kiingereza kibovu mnaboa na sidhani kama ni lazima muongee kidhungu wakati hamjui…mbona waindi wanauza? kumbukeni huu ni wakati wenu lkn kama hakutakuwa na maboresho mtaanguka vibaya. Kanumba au Ray wakipeleka filamu kwa mdosi fasta inachukuliwa lkn wasitarajie ivi kwa muda wote mfano mdogo ni Mr Nice, mdosi alikuwa hapindui kwa Nice lkn leo hii kila Mtanzania anajua yaliyomkuta huyu msanii na wadosi hawataki ata kumsikia…kudadadek

  3. Comment by Nas on April 29th, 2009 4:42 am

    Ebwana Pandu..
    Siutani hawa mastaa wa filamu za kibongo wana copy sana, Ingekuwa ni vizuri kwa wao kuwa wabunifu zaidi.Na ni vizuri wakitumia lugha yetu ya kiswahili, kwani hivi sasa watu wameelimika vya kutosha, na filamu inaweza kusetiwa kwa lugha zaidi ata ya tano na zaidi, kama unatumia sub-tito kuangalia hiyo movie, kwani hivi wanavyofanya kila siku movie za kukopy wataishia kuwa mastaa wa Tz na kushika izo buku buku daily, na maisha yasiyo na future..Tatizo hawataki kubadilika na kujifunza zaidi akishaona maeitwa staa basi anajiona ni Brad Pit wa bongo, haya bwana..twende tuishi

  4. Comment by Naima on April 29th, 2009 7:59 am

    keep it up frank

  5. Comment by RACEZNOBAR on April 29th, 2009 1:26 pm

    kwanza naomba niwapongeze wahusika ktk utengenezaji wa film hapa tanznaia .whatever is it that they are doing, they deserve my compliments.Personally,i recognise that ,dealing with film making is so tough especially in Tanznaia,where the basic resources are virtually nonexistent.
    kweli kazi ni ngumu.Pia nawapongeza si kwa sababu eti wantengeneza film nzuri ,NO,ni kwa sababu wachache waliojitokeza ktk fani hiyo wamethubutu to take initiatives and step up to the plate.At least they are involved with it .Ofcourse ,quality is out of question here ,That will come with time and the will.Am talking about the willingness of the individuals to learn.Not just learning ,but lesarning from the right sources.With the right sources ,i mean any where but Nigeria.To me Nigeria is out of the equation here.
    Ofcourse, our quality is far from being anywhre close to a real film,at least in my opinion.But this wont hold me back from recognising and appreciating the efforts ,the courage and the whatever commitmnt folks are continuing to put into film making .So, yeah my compliments go to everybody invloved with film making here in Tanznaia.
    But on the flip side ,it would be incomplete not to comment anything
    ACTING

  6. Comment by RACEZNOBAR on April 29th, 2009 2:58 pm

    CONTINUED, FROM MY PREVIOUS POST:
    ACTING
    Personally i recognise some kinda acting is obviously being performed in our films.But i wouldn’t rate it any where close to mediacre. If anything at all it fits perfectly with OK.
    Tanzanian acting is dominated with nothing but STAGING and MELODRAMATISATION. Much of it is being copied from crappy Nigerian movies(my guess)
    MY OPINION: As tough as it can be they’ve got to learn to be EMPATHETIC with the characters they are trying to potray.
    Our acting is not convincing/compelling if you will at all.Utaona mtu anacheza nafasi ya dokta lakini mtu wa nje akiangalia huwezi kuzamishwa ktk kuamini kwamba yule ni dokta badala yake tunaanza kuona (mathalani) kwamba Kanumba anacheza kama dokta .Ninavyofahamu mimi (correct me if am wrong and i guarantee u , al just be ok if you ever want to)
    Ni kwamba watazamaji hatupaswi kuona kwamba fulani anacheza kama dokta ktk movie bali tunapaswa kuvutwa,kuzamishwa na kusahaulishwa kwamba fulani ana act nafasi ya dokta bali tunapaswa kufikiri na kuona kwamba (bila hata maneno ya muigiziaji na costume) kwamba tunachoona ni daktari na siyo kanumba anajaribu kuigiza kama daktari.
    Yes there could possibly be a bunch of factors to make a movie believable or compelling. But nothing could ever surpass the power of good acting especialy CHARACTER ACTORS, unlikely the power of super star actors.
    I also noticed a serious issue with our films.Who said that a movie looks COOL or BELIEVEABLE with all the OVER BLOWN and OVERLY EXAGERATED DRAMAS.This is a typical and persistent feature of our films.You can find this in vitually every movie. To me that’s is my biggest turn off with our movies.Beacause first of all that’s not realistic any way,It does not reflect the real situations in life.Not any where close.DIALOGUE, especially any kind of heated exchange is always OVER EXAGERATED.
    My point here is that, we need to improve our acting skills. Ofcourse we may be lacking in major resources but acting i believe is so much within our capacity .One way of learning acting , i would suggest is to watch lots of Hollywood movies. One technique i saw some folks practicing is to watch a movie over and over .Scene by scene would be more efective.Alternate between having sound on and sound off/silent .Observe your chosen character closely and carefully .Also check out the character rapport.
    Hayo ndio maoni yangu , anybody is free to criticise me or even insult me if you want
    Samahani kwa maoni mareeefu kama hivi
    thanks
    Raceznobar

  7. Comment by Maggie on April 29th, 2009 5:00 pm

    Leah, tunapenda kufanya hivyo usemavyo dada yangu, lakini inakuwa vigumu, mi binafsi uzalendo unanishindaga kabisa. It’s embarassing to the real film industries in the world kwa sababu hizi sio movies jamani wala zisiitwe filamu, ila ni videos kwenye style ya soaps, hawataki kubadilika hao na hata kujifunza hawataki, wanataka kutengeneza pesa za haraka haraka tu that’s it. It took Bollywood(India)years of hard work na kukubali kuchange, waangalieni sasa hivi wako wapi hata Oscars wanashinda,South Africa waafrica wenzetu hao hapo, badala ya kuchukua mifano yao tunawaiga Wanigeria, sisi bado tunasafari ndefu, tuna watu wenye vipaji vizuri tu vya uigizaji TZ lakini kila sinema lazima awepo Kanumba sasa kama sio soaps ni nini hizo. Poor casting, poor lighting, Tittle zenyewe ndio kabisaa, directors wanafanya a very poor job! Alikuja Kibira na kujitolea kuwapa training kidogo wakamsusia wanajifanya mastaa tayari, kazi yao kuiga sinema za Kinigeria wakidhani Wanigeria wana standard nzuri ya movies kumbe nao wachovu ni kelele tu.
    Point yangu ni kuwa wanahitaji shule ya maana na wajitahidi kufanya auditions ili kupata waigizaji wazuri, kina kanumba wanaact bora liende lakini kabla hata sinema haijaisha tumeshajua mwisho wake utakuaje kwa sababu wanatuambia kila kitu kwa midomo yao. Film unatakiwa ukiangalia actions tell you a lot hata bila kuongea. Sinema gani inatolewa mpya kila baada ya wiki mbili, for a real movie it can take a year to make that movie, lakini ikitoka hapo ni bomba, sio kucharaza tu video na kuita films.
    Safari bado ndefu.

  8. Comment by Kindo on May 5th, 2009 5:21 am

    Nakubaliana na Leah na Maggie. Mimi nimekuwa nikitazama hizi movies kwenye channel ya Africa Magic Plus DSTV kwa kweli safari bado ndefu sana. Lakini kwa vile tumeanza tutakuwa wazuri tu kama tukikubli kujifunza na kukosolewa. Rome was not built in a day. Nilijaribu kujitolea binafsi kutoa comments na ku-offer kusaidia kwa kupitia website ya Kanumba lakini sikupata majibu..maanake sometimes tafsiri za kiingereza zinazotolewa kwenye movies hizi zinasikitisha/zinapotosha ukizingatia the wide range of viewers.iam still willing to assist kwa ajili ya kujenga film/entertaiment industry yetu…..

  9. Comment by khadija salum on May 19th, 2009 6:23 am

    filamu za bongo kiukweli zinakamata,ila tatizo linakuja kutokea pale filamu inatolewa part 1,baada ya muda mrefu sana part 2 or 3 ndo inatoka.hii inakuwa haijakaa vema kwani kwa mtu mwingine anakuwa amesahau kile alichokiona mwanzo.kiukweli filamu ni nzuri ila bidii iongezwe katika kufuata muda.filamu isikae sanaaaaaaa……..thank u!!!!!!!!!

  10. Comment by YASMINE on December 31st, 2009 7:07 am

    I THINK MOHAMED MWIKOGI UPO JUU NO COMMENT BUT I ADVICE ALL ACTOR/ACTRESS KAZENI BUTI

  11. Comment by Peter M.Chilumba on October 4th, 2010 6:03 am

    Helo there! Mimi ni mdau wa filamu kwa kiasi fulani japo sijaanza rasmi kuingia huko nimeshawahi kutengeneza filamu kama tatu au nne za kibongo ya kwanza ilikuwa inaitwa Neno na ndiyo filamu ya kwanza ya Kanumba na Hisani(Tino) hii iliongozwa na Vicent Kigosi(Ray)ya pili ni Riziki nayo pia ya Kanumba akicheza na Johari hii iliongozwa na chiki Mchoma ya tatu ni Mchanga wa Macho hii ilikuwa ya Thabiti Abdul hizi zote ukitazama utagundua ni za kitambo kirefu kidogo…baada ya hapo niliamua kukaa pembeni na kuamua kujipanga kwani tofauti na tunavyodhani sisi wabongo kwamba mtu akikosa cha kufanya basi anakuwa cameraman,director au editor(kosa kubwa)Utengenezaji wa filamu sio jambo jepesi nimekuwa nikifuatilia utngenezaji wa filamu wa nje (Marekani)nikilinganisha na wakwetu najisemea mwenyewe kamwe hatutakaa tufike huko kama wasanii wetu na waandaaji wa filamu zetu hawataenda darasani japo kidogo kupata mwanga wa hii tasnia….kwanini nasema hivo….namimi najiandaa kutengeneza filamu yangu ikatokea nikamtafuta dada mmoja muigizaji(maarufu) nikamuambia nataka nikupe script yangu uisome na kuikariri vizuri napenda kila kilichoandikwa humo ndio ukisome na kiwe hichohicho jibu alilonipa nikwamba yeye ataangalia muongozo tu kisha atasema maneno yake yanayoendana na kwenye script(hana muda wa kukariri script)wakati ukitazama tuzo za Oscar au MTV award kule Marekani kuna tuzo mpaka ya mkariri bora wa Script sisi TZ vp?
    Ushauri….wasanii na waandaaji tuamkeni tusome, tukipata muda tuingie net huko utaona jinsi wenzetu waanavyofanya kazi.

  12. Comment by vicky on January 10th, 2011 10:06 am

    wanajitahidi, but kuna vitu muhimu bado hawajanyoosha… i mean pale kwenye english sub tittles….

Leave a Reply