
Barack Hussein Obama ametimiza siku 100 leo tangu aapishwe kuwa Rais wa Marekani. Wamarekani wana utaratibu wao wa kijadi wa kupima uwezo wa kiuongozi wa viongozi wao wakianza na siku 100 za kwanza. Ni utaratibu wa kihistoria ambao kwa mujibu wao,huwa unaonyesha dalili za jinsi uongozi wa Rais mpya utakavyokuwa. Misingi,misimamo na hulka ya kiongozi wao huonekana ndani ya siku 100! Obama anazidi kujijengea umaarufu na pia kukijengea chama chake cha Democrat umaarufu.Republican wanazidi kubomoka na kuonekana kushindwa katika nguvu za hoja.
Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali,Barack Obama anazidi kukubalika. Wamarekani wengi wanakiri kwamba anafanya kazi nzuri,ni muwazi na hana zile hulka za kigomvi ambazo marais wengine waliomtangulia walikuwa nazo. Kitendo chake cha kusalimiana na Rais wa Venezuela,Hugo Chavez, hotuba aliyoitoa kule Uturuki,jinsi ambavyo ameanzisha mijadala ya kidiplomasia na nchi kama Iran nk ni baadhi tu ya mifano michache kati ya mingi inayoonyesha Obama ni mtu wa aina gani.Lakini wapo ambao wanasema haeleweki na wala hatabiriki. Bado wafuatiliaji na wakosoaji wa masuala ya kisiasa nchini Marekani wanakuna vichwa vyao kujaribu kumsoma zaidi.
Wakati anaingia madarakani niliwahi kuandika kuhusu tofauti mbalimbali za matarajio ya ulimwengu kwa Obama. Kila mtu alikuwa na bado ana lake.Weusi wengi duniani tunamuona kama kioo au ushahidi kwamba inawezekana na yaliyopita si ndwele bali tugange yajayo.Mashariki ya mbali wanachoomba ni amani.Akiweza kuwaletea amani ya kudumu ni mafanikio ya kutosha.Afrika tunachoomba ni misaada zaidi,kusaidiwa.Tunaamini kwa sababu ni Obama ni “mwanakwetu” basi ni lazima akumbuke alikotoka.
Sasa kama umemfuatilia vizuri Rais Obama utagundua kwamba hajaitamka tamka sana Afrika ndani ya siku 100.Amekuwa akizungumzia zaidi nchi za ulimwengu wa tatu na sio Afrika pekee ingawa nyingi ya nchi hizo zipo barani Afrika.Zaidi aliongelea habari hizi katika mkutano wa G20 huko Uingereza ambapo uwepo wake tu katika mkutano ule ulikuwa ni ishara ya kutosha kwamba huenda yale mabadiliko aliyokuwa anayanadi wakati wa kampeni zake ndio yamewadia. Obama anaonekana kuiangalia dunia kwa mapana zaidi kuliko wengi walivyotarajia.Je hiyo ni kumaanisha kwamba Afrika haipo katika nafasi za juu katika ajenda ya Rais Obama? Sina uhakika.Nampa muda zaidi.Yawezekana ni kutokana na changamoto za hali mbaya ya uchumi wa dunia zinazomkabili. Angalau tunajua hajaacha kumpigia simu “nyanya” ake aliyeko kijijini Kogelo.
Mwisho ni kumpongeza na kumtakia kila la kheri.Akifanya vyema Obama atazidi kuandaa njia ya vizazi vya sasa na vijavyo hususani vya watu weusi.Akichemsha tutaambiwa si mnaona? Tuliwaambia…..
Feedback / Comments
26 Responses to “SIKU 100 ZA BARACK OBAMA”
Leave a Reply


sending...
akili ni nywele bwana kila mtu anazake ,i wish viongozi wetu wa africa wangekua kama obama,ila viongozi wetu TZ wabinafsi,wanajilimbikizia mali kama hawana akili nzuri.hiv ukiapa kuwa kiongozi unaapa kuwa mwizi ama??????!!
obama siku 100tu mambo mswano,si TZ yetu had mwaka unaisha raisi wetu alikuwa anatumia pesa ya mwenzie aliyomwachia,alikuwa hajaanza kutengeneza yake.sasa baba huo muda wa mwaka mmoja unafanya nn madarakani kama umeshindwa ku make ur own money??unafanya nini shoping ama??kazi kuzunguka kama TAIRI LA GARI LEO HUKU ,KESHO KULE,HUTULII??!!
haya vitu vimepanda bei kama nn??unajua si walala hoi tunaumia sanaa.uhalifu vibanda vyetu na sehemu zetu za biashara mmetubomolea kisa kusafisha jiji sasa mlivyokuwa mnasafisha hilo jiji sisi mmetufikiria mtatuweka wapi??toka lini unafanya usafi wa nyumba hujui uchafu utakapouweka???
tunamaliza vyuo,hatujui tutaenda wapi sehemu nyingi wameshikilia wageni kwanini lakini??kisa hatujui kingeredha ama??
china ilitoa bilioni 100 kwenye mwaka 2005 hivi kwaajili ya ujenzi wa shule za misingi zilizoko vijijini TANZANIA,pesa zikaliwa had leo hii watotowetu wanasoma kwenye madarasa ya mbavu za mbwa na kukalia mawe hii haki!!??hatakama unaiba kuiba gani huku jamani??tunataka kusaidiwa kilakitu na ngozi nyeupe??MWANZA NDEGE ZINAKUJA KUBEBA MCHANGA NA KUSAFIRISHWA NCHI ZA NJE kutokea shinyanga,MCHANGA HUO UNASADIKIKA KUWA NI MADINI watanzania na viongozi tupo kimyaa.
shinyanga watu wanapikia kinyesi cha ng’ombe sehemu zingine TZ watu wanakufa na njaa,au sababu hawatangazi na vyombo vya habarii??mahospitalini madawa hakuna,mmeenda kuomba pesa za kujenga uwanja wapili AFRICA wakati hautuingizii chochote badala ya kuongeza vyuo vikuu TZ.wakati viongozi wetu wanatembelea MASHANGINGI chuo kikuu DRS WATU WANASOMA HUKU WAMESIMAMA,kwanini tusigome??ni aibu kabisa nikiongelea TZ hakuna vita ila watu ni wabinafsi sana hatuangalii wenzetu why??kwann??
First of all I wounder why do we have to blame Obama for not doing anything or mentioning Africa.
A man with one head like me and you with huge responsibility worldwide do we real need to blame him? Why should we be behind Obamas life either he is intouch with is family in Kenya or not? Is that our bussiness? May be I am wrong somewhere some how.
I don’t know if Obama
Was nominated as an African Continents President? or worldwide president? or he is a USA president? it could be simply because he is a Black American first president does that mean we got rights to blame him if we feel doing so? Do will real feel sorry for that man the challenges faced by him global?
Each and African Country has its own president who was nominated to be fully responsible for its employers “VOTERS” in his/her respective country. no need to wait for Obama to bring everything on our plate. They should do their homework if they are not willing and awaiting for someone else to do their job then they shouldn’t be paid. Why getting fully salary for doing nothing? alternatively they are welcomed to step down.
In Africa we got a massive of resource if corruption from so called government were not existing I assure you could be no time to care for what Obama did and didn’t for Africa in case that resources would be proper utilized for the benefit of the indigenous “MAJORITY not MINORITY” which is not the case at the moment.
I see that’s why most of African countries are in the same stream so called “POOR” simply because we don’t want to be usefully for ourselves for the benefit of our countries just waiting people from abroad to come do what we could have done ourselve. I don’t know if we are lazy, lack of knowledge, have more money to waste or?
Good news that Obama has people in heart
he is doing his greater job to an extent now he is even trying hard to solve the war problem in Iraq, Iran, Afghanstan, Pakistan to mention few just imagine he is not waiting people from Africa, neither Middle West, Asia and so on to go do what he promised himself to do for is people but we………….? look all SADC leaders failed to remove Mugabe on power what they know its to complain and complain.
I am very much impressed with the statment that people are tring to scratch their brain and figure out what kind of person Obama could be. That’s good because a crever person does not need to tell around that I am this and that let people find out them self. Unlike those who are holding good position, well educated, rich etc go into their home village and start advertising themselves ohooo I have this, I did that and so on forgeting that they gain nothing by doing so, not everyone is happy for his/her success. I tell you it will cost people a lot of time to figure out about Obama’s.
Its also a goog Idea that in USA they have the system of Benchmarking their leaders. I am very much to know what happen after that if they find that the person in power cannot perform his duty.
1.Does he get fired
2.Given second chance
3.Called for displinary hearing or what?
I wish that system could apply worldwide
African Presidents please please do your work you have appealed to do if you can’t step down and give others a chance. If work its to much for you deligate people so that things can go smoothily and if your lack of knowledge, experience, qualification go back to school if not send your deligater to school I mean training so that they can gain more knowledge. We are sick and tired to hire people from abroad and came and do the job for us.
Mr. Kikwete hope you will make an appointment to meet Mr. Obama for relevant advice concerning how to bring back the lost economy in our country without waiting for him to come to you.
Good luck my president.
Concerned and a proud African lady!!!!!!!
Wadau kila la kheri tukutane jumanne I am on holiday. Enjoy it I will miss you
Chogo naona ndugu yangu umeyatoa yote ulikuwa nayo moyoni..pole wewe na mie pia pole zangu kwa kuwa mtanzania..kwa kweli hapa sasa viongozi wetu wanashangaa vijana wengine wapo Ulaya na hawataki kurudi bongo?? Mimi jamani wala sifagilii viongozi wetu hata siku moja actual hamna kiongozi hata mmoja wa africa nafagilia..ohh labda Mandela tu..Obama hongera sana keep it up..maana hapo Dunia nzima naangalia huyo BLACK kazi ataiweza kweli?
Presidents from African countries should just be ready to open up and learn….lakini ni vichwa ngumu saana na ninakubaliana na Chogo hap juu kuwa huenda huwa wanaapa kwa matarajio yao mengine tuuu na sio KUUTUMIKIA UMMA WA WANANCHI WALIOWACHAGUA….(Im sorry for this shouting here…ila inaumiza…)….sasa Obama ndio awape shule….kwani wao hawajaenda shule…(akili ni nywele kila mtu na za kwake ….lol…)
TUSITAFUTE source ya ku-blame kwa ajili ya matatizo tunayoyaunda sie wenyewe….Hivi Obama alishaawaambia kuwa wawe wanatoa TAX holidays kwa hao foreign investors…ama???
Si ni maammuzi ya hao viongozo wetu….(i am sure wanajuwa kwa nini wantoa tax holidays….hivi miye nikitaka kwenda ku-invest huko wanakotoka hao ma-foreign investors hivi kweli watanipa TAX holidays….nitapewa miye kweeli….kama sio kupekuliwa kama vile nimebeba virusi vya Homa ya Swine….!!!!!!!!!
HEBU viongozo wetu waacha ukilaza wafanye shughuli tulizowachagua wazifanye….hii blah blah tumechioka nayo….
….haya hizo kesi za walio-EPA….ni vipi hapa…..mboona sioni wala kusikia nini kinaendela……..(miye nilihisi (using my sixth sense)….kuwa hii ni talalila tuu nyingine in its own disguise….tulipigwa MACHANGA ya macho na mpaka sasa hivi hatuni maana mamcho yamejaa michanga….lol….sasa nisemeje…..watu wameepa….ushahidi upo….kwa nini hawaendi Segerea na kutumikia kile walichopanda……
……now…I think hii inanifanya nisikie kuumwa na nipo on the point of throwing up…nasikia kutapika sio siri….
….nawakilisha…bang bang bang….
…asiyejua maana haambiwi maana….tukae tuuu tumsubirie OBAMA aje kutuambia ama kuwaambia nini tufanye ama nini the so caleed viongozi wetu wafanye….
…nimerudi teena….BADO SIELEWI…(and I am sorry for shouting …but I am gonna shout…)….
HIVI POLITICS ni drama au DRAMA ni POLITICS….(miye fundi…hayo mambo siyaelewi saana….so come on let’s think aloud here…)
….all I can see is one of never ending dramas….nothing substancial is in the offing….WHY..??…Hivi huwa hawaoni aibu jamani…?….Kwa nini hatuna utamaduni wa-ku-deliver accordingly….??….Unawageuza wenzio kama vile hawaoni….peremende kibao kama vile tumekuwa tots…why??
….wake up you people….we need deliverance…sio maneno tuu….
Flora (hapo juu…)….thanks ever so much for such a remarkable contribution….
….u know what….no single African leader will ever step down after committing a blunder or whatever….once he is there he thinks he is the only right one to be there….(cases of Mugabe and the like…)…
wish there was a fair way of rating our African presidents and I wish they are in a position to accept and move out when they have messed about…(but this has never been the case…can’t remember it happening…)…WHY..???
Flora dada gazeti lako lina issue za msingi sana. Hata mimi nashangaa sana eti watu kulauma Obama kwamba ameisahau Africa. Charity starts at home bwana, sasa yeye kwake moto unawake, asiuzime anende kuzima moto Africa?? Sio rahisi ila mie mwenzenu i have given up on our leaders..wadau msinishangae ndio hivyo yaani kila raisi mambo yake ni hayo hayo..hamna jipya na maendeleo yana zidi kudidimia..sijua wadau mwenzenu..kuna mzee mmoja mtu mzima sana nilimuuliza vipi maendelea TZ akilinganisha na enzi zake akaniambia at times yeye anaona eti wakati wa wakoloni hospitali na huduma za jamii zilikuwa nzuri zaidi sio kama leo..yaani wadau mimi kama kijana niliona aibu sana ila that was his opinion…
mwanamke wa shoka, Flora na kwa raha zetu nimenote points zenu…etimunasema nini kiongozi wa afrika a STEP DOWM au awe na AIBU? Hivi vitu havipo ktk kichwa na kamusi ya viongozi wa kiafrika yoyote yule maana ungonjwa wa afrika nzima ni ule ule UONGOZI MBAYA NA UFISADI:..si tunaona Mugabe, Congo, Uganda ect Mugabe angekuwa mtu mwenye mshipa wa aibu angeachia ngazi ila bado na miaka yake 80 anataka madaraka na wananchi ndio wanaumia kwa njaa humo nchini mwake…kwa kweli mwenzenu AFrica yetu sijuii tutafika au la. Na mbaya zaidi watu wengi wanapenda kusifia mafisadi, maana huko mitaani wanapita na magari ya kodi zetu utasikia ´duhh check hilo shangingi ni la xxxx jamaa bwana lina akilia kweli limeiba sana huku serikalini…sasa kuiba inakuwa sifa mhhh.. Juzi nilikuwa naangali documentary ya Obama alivyoenda Kenya mara ya mwisho kabla hajawa president..yaani eti wakenya wamekaa kwenye hall na kusikiliza hotuba ambayo Obama anaongelea rushwa kuwa nyingi Kenya na ukimwi ect na wakenya wapo kibao wanasikiliza..yaani nikajiuliza do we need a foreigner to tell us kwamba Afrika ime komaa kwa rushwa?? Anyway wadau OBAMA wala sio mtu wa kuja kumaliza shida zetu serikali zetu zimalize shida zetu na Obama yeye a compliment tu if at all, maana kuna tafiti zinaonyesha sio kila msaada tunaopewa unaleta maendeleo africa..misaada mingi imetengenezwa ila Africa izidi kuwa dependant kwa hiyo nchi husika..
Naunga mkono wadau wote hapo juu. Didnt u guys know that African leaders are “Vichwa vya Wendawazimu”? Mwanamke wa Shoka, Politics is nothing but drama esp, when is used with sort of biasness/greedy eg, African Leaders. According to them politics means elevating all his friends, relatives & supporters in good positions no matter how Bogus they might be. Hebu tizama Baraza letu la Mawaziri.
Mfano; Kuna baadhi ya viongozi ambao wameonyesha kuchapa kazi na wameleta mabadiliko makubwa Kila Wizara wanapowekwa lakini sababu ya siasa/urafiki hutolewa. Magufuri alifanya kazi nzuri sana ktk Kujenga Mabarabara,na aliijua kazi yake maana kila akisimama kujibu hoja bungeni alishangiliwa kwa accuracy ya data alizotoa na almost barabara zote za nchi nzima alizijua & Wizara ya Ardhi alikwisha anza mipango ya ujenzi wa makazi bora, Fly-overs etc, Kwa vile hakuwa Kambi ya JK ndo unamuona Kazimishwa kiutendaji. Ole Njolay..amebadilisha Mwanza na kuifanya ing’ae kama unavoiona[A Cleanest city in TZ], lakini kwa vile alikuwa kambi ya Sumaye, katolewa Mwanza na kutupwa hukooo. Tukirudi U.S.A,… Hebu Tizama H. Clinton na mume wake walivokuwa wanamponda OBAMA wakati wa Kampeni, lakini OBAMA kashinda na Kampa Cheo nyeti kabisa (Secretary of State) Je Africa hiyo ingewezekana????? kweli ni vichwa vya wendawazimu….
Economic and Political transparency/Democracy in Africa havipo Sasa Jamani OBAMA Ataanzia wapi kutatua matatizo ya Africa? Pamoja na Umaskini, Njaa, Magonjwa, Ujinga na Corruption zinazotukabiri Africa, utaona nchi hizi ziko buzy kununua Siraha nzito (What for?…defending so one can stay in power). Yote haya tunamsubiri OBAMA atusaidie? ataanzia wapi?
What we need in Africa first is Moral/Social transformation…And I still believe we did wrong to adopt Capitalism at 80%, we ought to adopt Socialism at 80% and 20% be Capitalism sort of Mixed Economy. Mostly African Countries economy is weak, fragile and premature to bump directly into the current aggressive capitalism.
Narudi tena,…Sio rahisi Obama kusahau africa, kwani mikakati ya kuinusuru Africa si lazima aitangaze hadharani asijeonekana kuwa Biased President, kwani amesha-experience mwenyewe maisha ya hasa kijijini-Africa. alivokuwa Europe, alisema …We must protect underdeveloped/developing countries as they are our future markets. Tuvute subira kwa hili.
wadau wote hapo juu nawapa 5, Gervas ndugu yangu mie pia nashangaa watu wanasema eti africa tunaitaji ujuzi zaidi..kama wote tunayojua sisi waafrika mbona tunasoma unversity hizo hizo na wazungu so hiyo elimu watu wanasema na sisi pia tunapata…ila sasa hayo wasomi wetu akifika kwenye madaraka TOBAAAAAAAAAA anavyofanya kazi utadhani shule hajaenda eti kisa rushwa, ufisadi, kujilimbikizia mapesa..kwa wadau mimi sijui kama miaka 40 ajayo itakuwaje, maana hii 40 iliopita hamna kitu..
jamani wadau hapo juu nashukuru sanaa kwa hii mdahalo…inanitia moyo kuona we think in the same line….
….hivi ni lini watajufunza kuwa respoinsible na blunder zao….???
mtu anavuruga….bado anasimama tuu…tena with confidence….jamani INATIA AIBU…
….kuna kitu kimenitia hamasa….kuna huyu boss wa mambo ya ugaidi hapo kwa waliotupatia uhuru wetu….alipovuruga tuuu ni alikuwa wa kwanza KU-resign…hii ilikuwa hata kwenye the free METRO….ilinitia hamasa saana na nikaona huyo jamaa ni GENIUS…HIGHLY RESPONSIBLE….and very SENSITIVE…..
…..ninachoona miye….ni UNRESPONSIBLE LEADERS, very INSENSITIVE ONES…..
….haya huyo waziri wetu pale….na mabo ya kashfa ya vitambulisho…hivi ameshang’atuka ama bado yupo…(dont follow this much lol…)…
Hi Guys from Helsinki…Finland
Kwanza ninatoa salamu kwa wadau wote wa BC, nilikuwa Bongo toka January mpaka March,2009 mwishoni.Nimerudi kuendeleza libenenga la shule, Na mchango wangu unaanzia hapo, Bongo internet ni tatizo sana, kwanza very slow na sehemu nyingi mikoani haipatikani.Jambo hili lipo chini ya uwezo wetu wala hatumuhiji Obama, wala tatizo sio pesa, tatizo ni ubinafsi uliokidhili hata vyuo vikuu internet matatizo bongo sasa wasomi wetu watakwenda na wakati kweli karne hii ya 21st , karne ya IT, wakati huo huo Libraries zetu hazina vitabu. Jinsi ninavyozidi kufanya utafiti nazidi kuamini adui namba moja wa Mwa Africa ni yeye mwenyewe na wale wa nje wanafuatia hasa hasa kipindi hiki cha dunia huru,free world.
Kuhusu Baraka Obama, Kwali ni Ujinga kufikiri kuwa Africa inaendelea kwa kupata misaada au kutegemea wazungu,wachina au waIndi. Kwa sasa tafiti nyingi muno na vitabu pamoja na ripots kibao zinaonyesha misaada kwa Lugha ya wenzetu foreign aid haiwezi na kuleta maendeleo Africa, na ktk mizani ya faida na Hasara, Tafiti zinaonyesha Bara la Africa limepata hasara kubwa kutokana na foreign aid. Ndugu wana BC, mnajua kuwa pesa zinazotoka Africa ni nyingi mara ishirini kuliko zinazoingia Africa kwa jina la foreign aid, ngoja nitoe mifano, Benki ya dunia yaani World Bank inasema ktk ripoti yake kuwa
i .Africa kila mwaka inapoteza dollars za kimarekani billioni 80 kwa rushwa tu,
ii.Pia asilimia 40 ya utajiri unaodhalishwa kila mwaka hauwekezwi Africa yaani 40% of the wealth created in Africa every year is not reinvested in Africa
iii. Africa inatumia dola za kimarekani billion 20 kila mwaka kuagiza chakula ni bara pekee duniani ambalo haliwezi kujilisha richa ya utajiri lilonao
vi Africa inapoteza as capital flights out of Africa billioni 148 kila mwaka jumla ya hasara ni zaidi ya billioni 250 dollars za kimarekani wakati hiyo inayoitwa misaada kwa mwaka haizidi hata dollars za kimarekani billioni kumi,
ninaomba kumalizia kwa kumquote Chinue Achebe msomi wa Kinigeria, The problems of Africa is squarely, the problem of leadership, end of quote
We have leadership vaccuum in Africa, kila mtu ni mbinafsi , kelele nyingi kabla hajapewa madaraka lakini mara hakipewa madaraka wizi mtindo mmoja, sio kizazi hiki ni vizazi vijavyo hivyo Ombi langu kwa Rais Obama ni kushinikiza Africa iwepo Democrasia ya kweli ili bara lirudi mikononi mwa wananchi kama ambavyo marekani ilikuwa mikononi mwa wale Lobbysts na matajiri wa washington basi Africa itoke mikononi mwa viongozi ambao wengi wao ni mafisadi .
kila la Kheli Obama, ninajua ni kiasi gani sisi WaAfrica tunakuambishi ndiyo maana kila mtu Africa anakukumbatia na kukuita wewe mtu mweusi ingawa hilo halina ubishi,
Mwisho, African problems need an African solution by Prof George Atiye sio Obama.
This is absurd the description of the picture above was written in kiswahili how dare you turn it into english what are you trying to prove? We need to be consistent, you need to stop showing off in America they say fronting, being arrogant and inconsiderate it will never take you anywhere it will just make you look or sound like an idiot which is not good for Tanzanians we do not want to look like idiots. After all your english is not that good is broken , pidgin and awful you have got a long way to go. I can tell by the construction of your sentences it seems like you just started to learn english, you are one of those people who enjoy to be told that you are good and right you don’t like to hear that you’re wrong.
Hakuna hata mtanzania mmoja ambaye hajui kiswahili ndio maana Tanzania ni nchi moja babu kubwa sana ukienda kaskazini huna haja ya kuongea kisukuma au kihaya ukienda kusini huna haja ya kuongea kimakonde au kimakuwa popote utakapokwenda nchini wewe utaongea kiswahili bila ya ubaguzi unauona utamu wa kuwa mtanzania huo. Mkitoka nje kidogo imekuwa nongwa hatunywi maji kuna wabongo kibao walianza kusafiri tangu enzi hizo lakini ukizungumza nao hawana manjonjo na mikogo ya kijinga na katika hao wabongo kuna wanaojua kigiriki, kituruki, kijapani, kitaliani, kichina, kiarabu, kifaransa, kireno, kihisipania nk… Pia kuna watanzania ambao wamesoma kisomo cha ngumbaru na kisomo cha watu wazima watafaidika vipi na watachangia nini katika mada kama hizi ikiwa watu wengine mnataka kujionyesha na mashindano yasiyokuwa na maana kama wewe uko marekani au uingereza si ongea na hao wamarekani au waingereza ambao hiyo ndiyo lugha yao ili wakupe huo ujiko unaoutafuta au unaoutaka. Kuna watoto ambao wako shule za msingi na wazazi wao wanamiliki kompyuta pia nao wanataka kusoma mambo kama haya ili wapate kuelewa nini kinachoendelea hapa ulimwenguni wataelewa vipi. Kuna blog nyingi tu ambazo zinatumia kiingereza kitupu kwa nini huingii humo ukamwaga hayo mayai yako viza.
frateline kula tano,then big up kwa hiyo info.lete habari,lete raha watu tuelewe mambo
Hi Guys from Helsinki-Finland
Nashukuru sana kaka yangu Chogo kwa comment yako,shukrani ziwarudie uongozi wa BC kwa kutupa fursa hii
regards
Frateline
Hivi wewe unayejiita mzee wa noma, unaona sifa kuandika ki-inglish cha kwenye kamusi apo juu? unachekesha, sijui nani kakwambia sentensi ulizoandika hapo juu ni ki-english safi. Nakushangaa sijui wewe umesomea wapi, ukisahau kuwa English is a media of Instruction in Secondary schools & higher learning Institution in Tanzania. Sasa unashangaa nini watu kuchangia kwa English? Kuna watu wengi tu duniani Maarufu na hawaongei Ki-engish kizuri kama wadau tunacho ongea. Sijui kama umeona Heading zote blog hii zimeandikwa kwa lugha zote mbili..mfano “Bongo celebrity”…hivo watu wana uhuru wa kutumia lugha moja au zote kwa vile kila mtu anazielewa siku izi. Tusikulaumu sana maanake yaonekana sijui umekurupuka wapi ukaja osha kinywa lako apa room.
Frateline na wadau wote hapo juu hongereni jamani..i like the quote kwmba ´African problems need an African solution´. Frateline je wewe ulisoma IFM na ulikuwa president pale au nimekufanananisha? Na ulikuwa msastari wa mbele kwenye international student week?
Hi Guys from Helsinki,
Asante mama Liv, ni kweli mimi nilikuwa President IFM ila waweza kupitia blog yangu ili uweze kupata kuja kwa sasa niko wapi na ninafanya nini? ni muda mrefu toka 1998 ni zaidi ya miaka kumi na moja sasa. blog yangu ni http://blogs.helsinki.fi/kashaga/
Ninawashukuru BC kutuunganisha tena, mungu akubariki,
Frateline
Dear Mama Liv
Ni kweli ni mimi Frateline aliyekuwa president wa IFM mwaka 1998, ni muda sasa miaka kumi na moja, tembelea bog yangu ili ujue niko wapi sasa nashukuru BC wametukutanisha, nitumie nawe blog yako kama unayo maana mimi sikukumbuki kipindi hicho wanafunzi walikuwa wengi, ni rahisi mimi watu kunikumbuka, be blessed
Frateline
Dear Mama Liv
Ni kweli ni mimi Frateline aliyekuwa president wa IFM mwaka 1998, ni muda sasa miaka kumi na moja, tembelea bog yangu ili ujue niko wapi sasa nashukuru BC wametukutanisha, nitumie nawe blog yako kama unayo maana mimi sikukumbuki kipindi hicho wanafunzi walikuwa wengi, ni rahisi mimi watu kunikumbuka,
blog yangu ni http://blogs.helsinki.fi/kashaga/
be blessed
Frateline
Hi Guys
Samahani sana wadau wote wa BC hiyo message yangu ya Mama Liv nilituma ikawa inarudi nilifikiri haikwenda kumbe ilikwenda, siku hizi BC hakuna moderation naomba bakiza message moja comuputer yangu ilikuwa inanizengua jana ilikuwa inakata message zangu
samahani kwa usumbufu
Frateline
Hey Wadau, big up i lke al the comments.Its true that the problem of Afica should be solved by Africans.
Thx
Mzee wa noma if you don’t understand english get yourself a Dictionary in order to make things easy 4 u like you did when you wrote your 9lines comments in ENGLISH then proceeded with SWAHILI.
Do you know that english its an “INTERNATIONAL LANGUAGE”
Feel free to use the language you are confortable with and let others do the same. Since we are not in the competition after all there is no reward in return no matter what language you use.
If not then UTAJIJUA……….
wadau wote mliochangia kabla yangu comments zenu nimezikubali,nafahamu kuwa elimu tuipatayo haipishani na wenzetu shida huja juu ya mfumo wa uongozi wetu,tumekuwa tofauti na wao dus y tunarudi nyuma,mtu wa nje huwa haiibii serikali bali kama akipewa kufanya production ya idadi fulani yeye huongezea,it means hujiongezea masaa ya kufanya kazi na kutumia nguvu zake binafsi na haiibii serikali maana kazi aliyopewa huwa palepale,hivyo huicha serikali ikiendelea na yeye akijiendeleza sasa ni tofaut na sie,sisi watu wetu wakiajiriwa/wakiwa madarakani most of them huwa ni waizi nikimaanisha anakuwa mvivu mtu wa kufoj mambo na kutanguliza maslah,hapo ndipo ishu ndipo ijapo,viongozi wetu hasa hawa wanaogombea wao lengo lao ni kwenda kuponda mali za umma na kuionyesha jamii inayomzunguka kuwa yeye ni nani,wakati wenzetu huwa wanashauku ya kufanya jitihada madhubuti ili alete maendeleo/mabadiliko katika kipindi cha uongozi wake ili apate umaarufu,sasa kwa kikwete kama hatopita hiyo 2010 tutamkumbukuia nini,kipi cha maendeleo alichokifanya?ama hao mafisadi wanaofichuliwa kila kukicha kama wangefichuliwa ama wasingefichuliwa mwananchi wa kawaida asingefaidika na chochote.peace and love to all who are contributing their ideas in this site of bc.see you then.