dar-explosionImekuwa ni wiki ngumu kwa watanzania hususani waishio jijini Dar-es-salaam na zaidi waishio maeneo ya Mbagala. Milipuko kadhaa ilitetemesha jiji.Hofu ikatanda. Ikawa mshikemshike Mbagala kwenyewe mpaka katikati ya jiji na maeneo mengine. Wengine wakajua vita nyingine labda ndio imeshawadia.Penye wengi pana mambo mengi. Maneno mitaani nayo yakazidi. Hofu ikawa hofu.

Wananchi kadhaa ambao walikuwa katika siku yao ya kawaida,ya mihangaiko ya kawaida ya maisha wakapoteza maisha. Ama kweli kifo kikija hakipigi hodi! Ndio maana tunaambiwa kila siku kwamba tujiandae. Wengi wengine wakajeruhiwa. Wengi bado wapo mahospitalini.

Vifo vinapotokea au maafa ya namna hii, huwa ni wakati wa simanzi kubwa. Kifo ni kitu cha mwisho ambacho binadamu yeyote anataka kukabiliana nacho.Kinaogopesha. Lakini kifo ni sehemu inayokwenda sambamba kabisa na maisha. Ni sehemu ya maisha na sote tutapitia njia hiyo hiyo.Tunachoweza kufanya ni kutoa pole tu kwa wote walioondokewa na wapendwa wao. Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi! Pole nyingi pia ziwaendee wote waliojeruhiwa.Ni matumaini yetu kwamba Mwenyezi Mungu atawaponya na kukupeni tena afya njema.

Nini kilitokea? Ni ajali au uzembe tu wa mtu au watu fulani? Kama ni uzembe je walioathirika aidha kwa kuumia au kupoteza ndugu,jamaa na marafiki watafidiwa? Je tunavyo vitendea kazi na watendaji wa kutosha kutupatia majibu ya maswali hayo? Hayo ni baadhi ya maswali ambayo serikali ni lazima iyapatie majibu yanayoeleweka,ya wazi bila kificho. Tusipofanya hivyo,kesho bado ni tete. Yanaweza kutokea tena na tena matukio kama hili la wiki hii. Kama hali ile ilitokana na uzembe wa mtu au watu,basi hatua kali zichukuliwe. Ni wakati mwingine muafaka kwa serikali kuonyesha jinsi “inavyowajibika” kwa wapiga kura,walipa kodi na wananchi wake kwa ujumla.

Naam,kwa sababu leo ni Ijumaa na kawaida ni kwamba huwa tunaburudika na zilipendwa na kutokana na hali ya majonzi tuliyonayo,kibao cha Dr.Remmy Ongala cha Kifo ndicho ambacho nadhani ni muafaka. Kimsingi kibao hiki sio cha kuburudisha bali kutusaidia kuungana na wenzetu waliopoteza ndugu,jamaa na marafiki katika maombolezo.

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Leo pia ni Mei Mosi. Ni sikukuu ya Wafanyakazi katika sehemu nyingi za ulimwenguni ikiwemo Tanzania yetu. Nachukua nafasi hii kukutakia wewe mfanyakazi na watanzania wote kwa ujumla sikukuu njema.

Feedback / Comments

5 Responses to “POLE ZA MSIBA + MEI MOSI NJEMA”

  1. Comment by Gervas on May 1st, 2009 8:14 am

    Inakuwaje siraha hatari kama mabomu yahifadhiwe kwenye Makazi ya watu? Huu ni Uzembe wa Serikali. Usalama wa Raia maana yake nini? Yawezekana Kambi hiyo ya jeshi ilijengwa kipindi hapakuwa na makazi ya watu, lakini inaonyesha ni jinsi gani Serikali inauchapa Usingizi.

    Haya ni madhara pia ya kutopanga miji yetu. Yaani Serikali inasubiri wawekezaji pia kupanga watu katika makazi. Hivi kazi ya Viongozi wetu ni nini haswa? Kudhibiti Majanga kama Moto, Maralia, Ujambazi inakuwa taabu sana. Mwaka 1974/75 watanzania walilazimishwa kukaa katika vijiji na kampeni ilifanikiwa hadi leo vijiji vipo na faida zake zinaonekana. Makazi holela yanazidi kushamili Dar, Mwanza, Arusha na miji yote ya TZ.

  2. Comment by sisterTZ on May 1st, 2009 10:18 am

    Kwa kweli poleni sana ndugu na jamaa huko Bongo. Jamani hayo mabom mbona hatari sana?? Mimi napenda kufahamu je hao watu waliopata matatizo serikali itawalipa fidia ua ndio tena hamna kitu hapo??

  3. Comment by Mwanamke wa Shoka (UK) on May 1st, 2009 10:59 am

    ….kwanza kabla sijaanza nitoe POLE NYINGI kwa wahanga wa afa hilo. MUNGU mwenyezi mwenye heri azipumzishe roho za waliopoteza maisha yao mahala pema peponi. Amin.

    ….now back to the issues: Hata kama kambi ilijengwa kabla watu hawajasonga huko….BASI SERIKALI INGECHUKUA HATUA ZA KUZUIA WATU WASISONGE MBELE NA UJENZI KARIBU NA KITUO CHA JESHI…..ama SERIKALI INGECHUKUA HATAMU KUIHAMISHA KAMBI hiyo ya jeshi kuipeleka mbali na makzi ya binadamu….

    …..all I can see…(and to be honest have grown up used to…lol)…is the LACK OF TOWN PLAN….ujenzi holela….kukiwa na open space kwa imeachwa kwa nia nzuri tuu ya social serviceds….anatokea gabacholi anakandamiza kitu kidogo….and yes anapata hicho kiwanja….na kuporomosha kitu chake….no serivice lines are planned inline with the expansion of the city/township…..matokeo yake watu wanajenga tu bila hata kuwapo na huduma muhimu kama maji, barabara, umeme….

    ….sio kwamba TANZANIA hakuna TOWN planners….no…I dont think so….not at all…waaapo weeengi wa kumwaga….sasa…what is th problem here….(I just dont know….inasikitisha….)….

    ….angalia hali ilivyo pale Manzese….na sehemu nyinginezo…it is really no appealing to the eye…magonjwa ya mlipuko…(maana sanitation ni poor…)….siku mvua ikinyesha watu ndio wana-fungulia vyoo vyao…inaitwa kutapisha choo….(lahaula…Mungu atuafu na magonjwa….

    …..angalia issue ya Soko la Kariakoo…hakuna expansion wala nini….hakuna sanitation….watu wanapanga biashara zao chini….((katu siwalaumu maana nao wapo katika kuhangaikia maisha yao….we all do from alll walks of life))…NAILAUMU “sirikali”….ina maana hawaoni…ina maana hata Rais mwenyewe hajawahi fika maeneo ya Kariakoo hata akiwa katika UOMBAJI WAKE WA KURA….???…Hivi kweli Mheshimiwa Rais Kikwete haoni ama inakuwaje….(to be precise here…WATENDAJI wa Rais nao hawaoni tuu….mama unaweza kusema Rais yupo busy….sasa na watendaji wake nao wanalipwa TAX-payers money kwa kazi ipi yarabi…??….

    ….AMA ndio tunamsubiri OBAMA aje ku-OBAMA-lize…lol….

    …inasikitisha….hivi kweli Rais bado atasimama kifua mbele (with all his confidence kutuomba kura na kutuambia kuwa aliyotuahidi wakati akiombakura pale nyuma ameyatimiza….??…Hivi kweli atasimama aseme..??….

    ….au ni kwa vile nchi za Africa (na Tanznaia ikiwemo)…hazina mtindo wa kuchekecha utendaji wa viongozi wao in a very transparent way….??….Kumekuwa na slogan ya UWAZI na UKWELI….lakini sikuuona huo uwazi na UKWELI wenyewe…(ndio sikuuona…ama nyie mliuona huo UWAZI NA UKWELI…..ama ndio nisema ni ndoto za Alnacha…and it will never come to pass…??…

    Jamani naomba hawa viongozi wetu waelewe kubeba responsibilities zao in a manner which can alleviate the sufferings of their VOTERS….na sio tuu kutufanya kama vile mazobe mazobe….

    usipojua maana huambiwi maana…lol

  4. Comment by Ma'reen on May 2nd, 2009 4:06 am

    I was watching ITV news jana usiku saa mbili…can’t explain hasira na maumivu niliyohisi.Eti jamani jana siku ya tatu watu walikuwa bado wanalala nje, hawana msaada wowote.No food, no shelter NOTHING!Hapo ni Mbagala tu je athari ingeenea mbali zaidi ingekuwaje?Hawa watu wanajisaidia wapi?Kipindupindu kikitokea tutasema bahati mbaya?Hao wajeshi ambao ni chanzo cha tatizo mbona wana mahema ya kutosha (ninavyochukulia) si ingewachukua chini ya masaa kadhaa kuhakikisha watu wamejisitiri?Leave aside kuhusu chanzo cha tatizo, tuna tatizo mbele yetu watu wanahitaji msaada wa haraka, serikali iko busy na Mei mosi. To be frank I almost felt ashamed of being a Tanzanian!

    To make it worse, eti mbunge wao anahojiwa anadai “hili ni janga la kitaifa, tumeshtuka sana, tumesikitika sana ndo sababu hata mh Rais alitembelea vituo kuwapa pole wahanga bla bla blah…kwa sasa hata sisi bado tumechanganyikiwa!”

    OMG!Sasa wao waliobeba dhamana ya kulinda na kuhakikisha usalama wa raia wakichanganyikiwa, mfiwa na wahanga wote wasemeje?Anachanganyikiwa nini, kuna ndugu yake kafa?Nyumba yake imebomoka?Hamuoni mwanae?Yaani nasikia hasira mpaka siwezi kuendelea!

    Mimi hili sioni kama ni ajali…ni uzembe wa hali ya juu.Ni dhahiri kuwa tumezungukwa na hatari nyingi tu ila tunasonga tu mbele kwa uwezo wa Mungu ila ndo hivyo siku moja moja yatakuwa yanatulipukia ‘bahati mbaya’ basi!Kinachofuata?Wale tunaoshinda tunawapigia makelele ooh mafisadi oooh wahujumu uchumi, ndo wanakuja kutu-rescue…fulani katoka milioni kadha, mwenzie naye kamuunga mkono…life goes on. Si bora waibe tu ila majanga yakitokea watukumbuke…who cares?

  5. Comment by Flora on May 6th, 2009 4:05 am

    Message of condolence for the all families that lost their belove one. I am so sad to read such just imagine people to die just like that we are not ready to accept these behaviour.

    What is our government doing real to protect people? where is the human rights here?

    Do the following experties real exist in Tanzania.
    1. Land use planners
    2. Engeneers
    3. surveyors
    4. valuers etc

    If so do they do their job in fully manners? in order to identify area/location suitable for residential,business, industry and educational purposes or things are done traditional that cost peoples life just like that.

    Human rights organization should stand for the families who lost their relatives + those who get injured even if its minor so that government can learn and be serious not letting people to die just like that becasue of their laziness we dont allow that.

    I think government has an issue obviously they should know the cause of that incident.

    Mwanamke wa shoka, thanx a lot for your contribution, all in all I dont think in Tanzania we have Town Planners if they are there then they are not doing enough, By the way do you see how Dar Jiji was planned? The streets are just like was drawn by a kindergaten kid who was learning how to draw. Buildings are to old without space, no public open space/park, I am not sure about street + traffic lights. We need proper answer please please from the government

    Mr. Kikwete and your people should tell us what happen and what is coming next and which areas? and how are you planning to protect the innocent civilian.

    May God in Heavens rest them in “PEACE” and wishing those who are hospitalized to get well soon.

    AMEN

Leave a Reply