“NDOA YA MATESO”-MARIJANI RAJAB

weddingbcWeekend ndio imewadia tena. Kama ulidhani wiki hii ingekuwa kavu kavu nchini Tanzania bila mikikimikiki basi ulikosea.Ilikuwa ni wiki ya “mipasho”. Ilikuwa ni rusha kombora nirushe kombora au kama vile alivyowahi kuimba Prof.Jay ukimwaga ugali mimi namwaga mboga!

Bahati nzuri ni kwamba nadhani watu wazima wamejiona ovyo na kuamua kufuata njia zinazostahili. Mchezo sasa umegeuka kuwa wa kudaiana “vijisenti”. Bila shaka umesikia mmoja kadai fidia ya Tshs Bilioni 10 huku mwingine akidai fidia ya Tsh 1 tu. Kama ingewezekana huenda angedai ile ya mkoloni kabisa iliyokuwa na tundu katikati. Sijui tugange yajayo au bado tuendelee na nguvu ya hoja,uchambuzi nk.

Tuyaache hayo.Leo ni burudani ya kale.Wenyewe mnaziita Zilipendwa. Natamani tungeziita Tunazozipenda kwani ukweli ni kwamba bado nyimbo hizi zina mafundisho kemkem na ni kama zilitungwa jana. Leo tunaye Gwiji Marijan Rajab(RIP). Wimbo unaitwa Ndoa ya Mateso. Binti karudi kwao.Anasema ndoa imemshinda.Mume anamtesa.Pesa zote anamalizia kwenye makuku ya kukaanga akiwa na “vimwana’ wake huko nje wakati familia inakufa kwa njaa.Binti hana msaada wowote,hana ndugu wala jamaa hapo alipo.Kwa masikitiko anauliza kwani kuolewa ni utumwa? Binti anaomba talaka yake.Mjumbe ndie anaombwa kuwa shahidi. Kwa uchungu na aibu anasimulia yaliyokuwa yanamsibu.Anataka kurudi nyumbani kwao kwani anasema hakuzaliwa juu ya miti bali ana kwao.Ana baba na mama. Mateso.

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Pata burudani,pata ujumbe na furahia weekend yako. Maisha mafupi haya.

Page 1 of 3 | Next page