
Kila siku ya Jumanne(kama leo hivi) watanzania siku hizi hupata nafasi ya kujiongezea maarifa mbalimbali,kuburudika,kujielimisha na kujifahamisha kupitia gazeti la Kwanza Jamii kama linavyoonekana katika picha ya hapo juu.Hiyo ni taswira halisi ya gazeti la wiki hii ambalo limeshatinga mitaani.
Humo ndani utakuta makala mbalimbali kutoka kwa waandishi mbalimbali nikiwemo mimi,Jeff Msangi. Wengine niĀ kama vile Maggid Mjengwa, Freddy Macha, BAP (Born Again Pagan), Subi Sabato,Prof.Joseph Mbele, Dr.Bukaza Chachage, Joseph Mihangwa, Padri Privatus Karugendo, Eliamani Laltaika bila kusahau kona ya Aunt Subira na wengine wengi.
Lakini kama uko mbali na Tanzania au kwa sababu moja au nyingine huwezi kupata kopi halisi ya Kwanza Jamii, habari nzuri ni kwamba unaweza kuperuzi habari mbalimbali kupitia mtandaoni. Bonyeza hapa.
Page 1 of 3 | Next page