
Wimbo wa weekend hii nilitakiwa na ilikuwa ni dhamira yangu kuuweka hapa wikiendi iliyopita. Sababu? Ilikuwa ni Mother’s Day kwa wengi waliopo nchi za magharibi bila kusahau kwamba siku hizi hata sisi hapa Bongo tumeshaambukizwa sijui niseme uzungu au utandawazi. Siku hizi nasi hatupitwi. Halloween tumo, Mother’s Day tumo, Father’s Day tumo,Thanksgiving tumo. Xmas na Pasaka ndio kabisa usiguse kwani hapo utachanganyikiwa nasi. Tuna barafu zetu wenyewe(pamba kwenye miti). Tuna Mbaba Xmas au ukipenda muite Father Christmas.
Sasa kwa sababu sikuuweka wikiendi iliyopita na kwa sababu kwa upande fulani naamini kwamba Mother’s Day ni kila siku, weekend hii tutajimwaya. Wimbo unaitwa Pole Mama na ni wake Mose Se Sengo “Fan Fan” (pichani) mwanamuziki mahiri kutoka DRC ambaye alizunguka nchi kadhaa za Afrika ikiwemo Tanzania(alicharaza gitaa na Makassy Orchestra). Kama ilivyo kwako wewe, katika wimbo huu Mose Se Sengo anampa pole mama yake na kumshukuru kwa yote. Nani kama mama? Pata burudani na enjoy your weekend. Kumbuka ukiamua kuiloweka,sharti uivalishe…au sio?
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.
Shukrani: Mike Mhagama…Once a DJ,forever a DJ!
Page 1 of 3 | Next page