Anaitwa Hussein Rashid ingawa umaarufu wake unakuja na jina la Hussein Machozi (pichani) ambalo ndilo jina lake la kisanii. Alizaliwa mwaka 1986 katika wilaya ya Manyoni mkoani Singida. Hivi sasa Hussein Machozi ni miongoni mwa majina mapya katika anga za muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla.
Kama uliwahi kuusikia wimbo unaoitwa Kafia Ghetto unaozungumzia story ya jamaa mmoja ambaye alimfukuzia au kumtaka urafiki wa mapenzi binti mmoja kwa muda mrefu sana. Baada ya muda huo mrefu, siku moja binti huyo akaamua kwenda “ghetto” kwa ajili ya huyo jamaa ili kumpa taarifa kwamba amekubali ombi lake. Kijana akafurahi sana na kisha kumuacha binti ghetto na kuelekea dukani kumnunulia soda. Aliporejea alitahamaki kukuta binti amejilaza kitandani kwake. Alipojaribu kumgusa akagundua kwamba binti amekata roho. Jamaa akachanganyikiwa asijue la kufanya. Kwa ufupi hiyo ndiyo story iliyomo ndani ya wimbo Kafia Ghetto. Mwisho wa wimbo Hussein anauliza ungekuwa ni wewe hali hiyo imekutokea ungefanya nini? Je walimwengu watakuelewa kwamba hukumuua binti? Je ungemtoa vipi humo ndani mwako?
Hussein Machozi hakuishia hapo. Aliendelea kudhihirisha ukali wake kwa kutoa wimbo mwingine uliokwenda kwa jina Full Shangwe akimshirikisha AY. Nyimbo hizo pamoja na zingine kama vile Maji Yakimwagika, Niambie zinapatikana katika albamu yake ya kwanza inayoitwa PROMISE aliyoitoa mwaka jana 2008.
Kwa sasa Hussein Machozi anakamilisha albamu yake ya pili ambayo ameipa jina KWA AJILI YAKO katika studio za Tetemesha zilizopo jijini Mwanza. Mapema mwezi uliopita aliachia single ya kwanza kutoka katika albamu hiyo inayokwenda na kubeba jina la albamu Kwa Ajili Yako. Usikilize wimbo huo hapa.
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.
Feedback / Comments
13 Responses to ““KWA AJILI YAKO”- HUSSEIN MACHOZI”
Leave a Reply


sending...
Kazi nzuri sana kijana.Mungu akusaidie ufike mbari.ni hayo 2 kwa sasa.
mbana pua mwingine huyo!
kijana wimbo wako wa{kwa ajili yako}m2 wangu huko juu ile mbaya ucpme,kaza buti,utafika mungu yupo na we…….tk cr
Kijana amepungukiwa kitu kimoja,haana hata tumisuri akaonyesha ni mtu wa kazi.nyenyua vyuma ili uonekane ni mwanaume wa kazi ala!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
man we mkali upo juu ile mbaya ……..luv ya songz kichizi…kip t up
hahhahahahahaha mr.degree umenichekesha sana
kwa ajili yako nacheka.
kazi nzuri Hussein Machozi
e bana hussein hapo nakuaminia kwa track yako ya ukweli, alietengeneza bit pia yuko juu vibaya. e bana bone la big up keep it up.
oya kaka wapi naeza download nyimbo hii tafadhali sana naomba muniambie nyimbo hii nzuri mno.
Kila jambo lina wakati wake
i lov it big..diz is de best song dat i eva had..kip it up man husein…
i lov the song i am listening to it whenever i enter in my car good work machozi
keep it up and do not look back just keep forward and do not forget one thing: GOD
Cheers
ume imba vizuri sana uhu nyimbo utahipenda.
I am shocked to hear your very young having done a good job…i mean the way you sing make me feel good and like you more…you are gorgeous may you continue like that.