
Leo ni siku ya furaha. Ni siku ya kufurahi na kutafakari. BC imetimiza miaka miwili hivi leo tangu ianzishwe! Ni vigumu kuamini kwamba siku na miaka zinakwenda kwa kasi ya namna hii.
Hatuna mengi ya kusema hivi leo zaidi ya kukushukuru wewe mtembeleaji na mchangiaji wa BC. Mtandaoni zipo blogs nyingi sana na katika lugha mbalimbali ikiwemo hii yetu ya Kiswahili. Lakini kwa sababu umechagua kila mara kututembelea na kuchangia mawazo na mtizamo wako hapa, hatuna budi kukushukuru sana sana.Tunaamini kwamba hiyo ni kwa sababu unaipenda BC na unathamini mchango wake katika ulimwengu wa habari na mawasiliano. Asante sana. Shukrani nyingi pia ziwaendee ninyi nyote ambao mara kwa mara mmekuwa aidha vyanzo vya habari zetu,burudani zetu. Pia shukrani kwa wale ambao wamekuwa wakitukosoa pale tunapoteleza. Tungependa kukuhakikishia kwamba tunathamini sana michango hiyo ikiwemo kukosolewa.
Pamoja na hilo, BC kama mojawapo ya vyanzo vya habari au kisima cha kusambaza habari, si kitu bila ushirikiano wa vyombo vingine vya habari na mawasiliano. Kwa hali hiyo ni lazima na sharti tuseme shukrani nyingi sana kwa vyombo vyote vya habari nchini Tanzania zikiwemo radio,magazeti na hata luninga.
Juu ya yote shukrani sana kwa bloggers wenzetu.Bila ninyi kazi ingekuwa ngumu maradufu.Asante sana.
Tunauanza mwaka mwingine. Kama ambavyo umeshuhudia katika kipindi kilichopita, kikubwa ambacho tunajaribu kujitahidi nacho ni kuboresha kazi zetu. Ni kazi kubwa na yenye gharama zake lakini tumedhamiria kuifanya kwa sababu tunathamini na kuamini katika ulimwengu huru wa habari na mawasiliano. Asanteni.
Feedback / Comments
18 Responses to “BC IS TWO YEARS OLD TODAY!”
Leave a Reply


sending...
HONGERA SANA BC
Nawapongezeni kwa kuwa hewani kwa umakini kabisa kwa miaka hii miwili.Kwa mtu ukiangalia tu kwa kuhesabu siku, unaweza kusema ni chache, ila kwa kazi ya kuongoza site kama hii BC ni kubwa mno.Mmefanya mambo makubwa mno kuhabarisha watu, na kizuri zaidi ni kufanya mahojiano na watu wengi ambao kwa namna moja au nyingine tunapata ukweli wa maisha yao, na nzuri zaidi ni kupata changamoto zipi walizozipitia kutupa morali nasi tujue tunapita wapi au tufanye nini kujiboresha zaidi.
Mungu awape nguvu zaidi na zaidi.
Naamnini tafakuri mliyoifanya kwa kuangalia hii miaka 2 mmejua nini muongeze kuboresha hili.Na ninaamini mambo mazuri zaidi mtaongeza.
Pamoja daima
MAKULILO, Jr.
http://www.makulilo.blogspot.com
West Virginia, USA
Happy Birth Day BC!
Kwa Kutimiza miaka mi2..Tupo Pamoko Sana! Yani BC Mnatisha Mnavyo hata vipindi vya Club Raha Leo Show! Duu! Nimekisikiliza chote hicho ni kizuri kimenikumbusha mbali sana!
Ni Hayo Tu!
Its Me BOb Sambeke!
Hi Guys kutoka Helsinki-Finland
Kwa kweli kwanza tunakila sababu ya kumshukuru mungu na pili kuwashukuru na kuwapongeza uongozi mzima wa BC, Viongozi na waandaji wa BC happy birth day and congrants!
Kwa kweli BC ni moja ya chombo muhimu ktk kutoa Elimu, burudani na kutoa hamasa ya watu kujifunza kutoka na makosa au mafanikio ya wengine, kazi hii umeifanya vizuri kwa kipindi cha miaka miwili hivyo mnastahili pongezi sana na tena sana,
Mwisho, mimi nitaendea kuwapa support na kuendelea kuwa Mdau wa BC kwa kufuata kanuni na desturi ya BC ktk kukubali na kuheshimu maoni ya wengine bila kutumia lugha chafu.
Asante sana
Be blessed and happy birth day
Frateline
Hongera sana Jeff na BC! It’s been a good two years, tunashukuru and keep up the good work!
Major COngrts i love this website its the best website, clear and fresh but it should updated ea time
Nawapongezeni sana hasa kwa kutoa burudani ya miziki mbalimbali wakati wa weekend hii inawafanya muwe unique na blog nyingine, pia nafurahi zaidi kuwa mmeangukia katika birthday yangu hivyo kila mnavyoadhimisha miaka nami nakuwa natimiza miaka kadhaa. Hongereni sana na kazi njema
Hongera BC!
BONGOCELEBRITY,
Hongera zenu nyingi sana kwa kutimiza miaka miwili tangu kuzaliwa.
Katika kipindi chenu cha miaka miwili ya uhai wenu, mmefanya mambo mengi makubwa katika jamii ya Kitanzania ndani na nje ya Tanzania, kuliko Blogi zingine, tukiwatoa “Michuzi” na “JamboNetwork”. Kila mtu analijua hilo.
Watanzania duniani kote mmetukutanisha hapa, na kutufanya kuwa kitu kimoja kama familia moja, katika kujadili mambo yetu mbalimbali ya starehe, siasa na mambo mengine mengi ya kijamii.
Katika mchango wa historia ya demokrasia yetu ya Kitanzania, katika uanzio wa utandawazi Tanzania, BC itakuwa ni mojawapo ya Blogi ya kukumbukwa. Kwa kuheshimu haki za binadamu na mipaka ya uhuru wa mtu katika kutoa maoni yake.
BC, kutokana na desturi yenu hiyo niliyoitaja hapo juu, kama mtaendeleza utamaduni wenu huo, mtaendelea kuheshimiwa na kutembelewa na watu wa rika zote, matajiri na maskini, kwa muda wote. Kumbukeni kuwa, hata viongozi wa juu wa nchi, huingia hapa BC, na kusoma yasemwayo hapa, “Believe Me”.
Wachangiaji, tujitahidi kuchangia vitu vya kuendelezana, badala ya kujikita kupondana, hali ambayo haitatuendeleza kimawazo wala kiuchumi.
It’s Great To Be Black=Blackmannen
BigUp wakubwa, much respect to u.
nawapongeza sana kwa kutimiza aka mbili, sio mchezo. Msiishie hapo endelezeni gurudumu ili la habari za ukweli zenye uadilifu, nawaombea Mungu msikwame!
Burudani zaidi
Happy birhtday wishes!
Thank a lot 4 coming up with such website I have learned a lot on the topic u always bring up. From other contributors with diferent back ground, skills, knowledge, experience and so on in this website its real a greater ideal. But please try to keep your wesite UP 2 DATE.
Looking forward to gain more knowledge through your web.
Wishing you more 20 years to come as your site to grow mature
Well done BC!
Happy birthday BC. Keep it up! Tuko pamoja.
Hongera sana Twin!
Asante kwa kutuweka karibu na celebs wetu.
Wewe unayejiita Flora,
Jipende mwenyewe na jivunie kuwa Mtanzania, ringia lugha yako ya Kiswahili.
Flora, unatutia aibu sana kwa kukumbatia na kuthamini lugha za wenzio. Wewe kama ni mweupe mwenye kujianika juani kama “mjusi”, juani, tuambie kuwa wewe ni “Mzungu” ili tukuelekeze kwenye tovuti za walugaluga wenzako.
Tovuti zetu hizi, ni za lugha ya kiswahili. Wewe Flora, naamini kuwa Bibi yako Mzaa Baba au Mzaa Mama, unapoongea nao katika simu huko Tanzania, unaongea nao kwa kiswahili. Lakini wewe hapa unatuambia kuwa unajisikia vizuri unapoongea Kiingereza. Ni aibu tupu!!!
Kuna wenzangu hapa walishakwambia kuhusu kutumia lugha yako hapa na tabia yako ya kung’ang’ani na kuitetea lugha ya kiingereza, na ulijitetea kwa nguvu zote. Tumekuwa tukikumezea kwa kipindi kirefu, sasa nimeamua kukutolea uvivu mimi na nitakuvaa kila sehemu utakapotuletea uozo wako huo.
Habari ndiyo hiyo, na ninakusubiri unijibu kwa hamu.
It’s Great To Be Black=Blackmannen
Hongera sana timu nzima ya BC Kazi nzuri na muendelee na moto huo huo.
Amani, Heshima na Upendo kwenu.
BC unajua ulivyo msaada katika kuunganisha na kuongeza habari na ufahamu kwa wengi. Binafsi na “timu” nzima ya barazani kwetu twakushukuru na kuykutakia kazi njema na kila lililo jema katika kila zuri mtendalo.
Pamoja Daima
Blackmanen kaka nilikumiss kishenz naona umerudi nanguvu mpya.
Hali ya hewa naona inakaribia kuchafuka mhhh ngoja tuone
Blackmannen you can dig in and out you will never and never change me I am proud of whom I am. Mind your issue and make contribution according to the topic provided by BC if you have no point of view you better remain silence.
I am not after anyone you don’t know me like wise and I am not even interested for that I have never attacked anybody I am just responding accordingly.
Take you time and mind your own issues + business. Leave me alone i don`t have time for urgument I have so many important issues to sort out
This Blog its not mine nor yours
I stick on freedom of expression
That is me
Dada halima,
Usikonde, mimi nipo, isipokuwa mtikisiko wa hali ya hewa ya uchumi duniani, unanipeleka puta. Maana mtikisiko wake ni mkubwa kiasi kwamba, umeanza kusikika kwa mbali katika mifuko ya suruali zangu.
Dada halima, kuhusu kuchafuka hali ya hewa hapa kijiweni, inategemea na ule upande wa pili utakuja vipi. Lakini kaa mkao wa burudani. Nakuhakikishia kupata burudani la nguvu.
Dada halima, hakikisha utakapokuwa ukiingia hapa BC, njoo na “Popcorn” zako pamoja na “Kinywaji” baridi.
Maana “bishororo” wa aina hiyo, kama huyo hapo, mimi hula sahani moja nao hadi kinaeleweka.
Dada halima, wadau wenzetu wa siku nyingi hapa BC wamejificha wapi? Au wamebadili majina baada ya kuolewa au kuoa? Mimi pia nimewamiss sana sana.
It’s Great To Be Black=Blackmannen