
Naam. Wikiendi tena. Wakati wa burudani. Wakati wa vikao vya kiti kirefu,familia,harusi,ubatizo,ubarikio,mwali kutolewa ndani nk.Ni muda mwingine wa kupumzisha akili.Hata kama unafanya kazi weekend hii bila shaka utakubaliana nami kwamba hata huko mabarabarani hali huwa shwari. Zile vurugu za foleni,msururu wa watu nk huwa hakuna.Ukiitazama Samora Avenue unaweza kuona kutokea Askari Monument mpaka Clock Tower.Unabisha? Hebu jaribu uone.
Kikubwa wiki hii ni kwamba tumetimiza miaka miwili. Kwa maana hiyo bado tupo kwenye mauzamauza ya kufurahi,kujipongeza na katika semina elekezi ili kuweka mstakabali wa nini kinachofuata. Kwa upande mwingine umemsikia mwenyewe mkuu wa nchi.Anasema habari za uraia wa nchi mbili hazina budi kusubiri. Anasema wasomi wamemshauri kwamba mpango wa kula huku na kule sio mzuri. Mwenyewe akasita kuleta habari za “wivu”. Wakati huo huo mkuu anasema mjenge na kuwekeza “nyumbani”. Nyumbani tena? Sijui wewe unasemaje lakini mimi naona kazi kubwa bado ipo. Washauri wasomi najua wamenielewa. Kama hawajaelewa basi tena.
Turudi kwenye burudani kwani kama ujuavyo leo ni Ijumaa. Ni mambo ya sakayonsa. Mambo ya zilipendwa. Enzi zile ambapo ugonjwa ulikuwa ni mafua tu! Wimbo unaitwa Binadamu Hatosheki kutoka kwao Orchestra Makassy. Bila shaka utakubaliana na kina Mzee Makassy.Binadamu sijui umpe nini aridhike. Hivi kwanini tupo hivyo tulivyo? Kama wanavyoimba; ukimpa jua anataka mvua. Ukimpa mvua anataka jua!Kha. Ukimpenda sana anataka kuchukiwa na ndio maana atakuletea madharau,visa,vituko na visasi.Enewei,wasikilize mwenyewe Orchestra Makassy. Pata burudani na furahia weekend yako.
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.
Subiri kidogo. Kwa sababu wikiendi hii tunaweza kusema ni wikiendi ya BC kwa maana ya kutimiza miaka miwili sidhani kama kuna ubaya kama tukiweka kibao kingine kama zawadi….sikiliza hapo chini;
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.
Feedback / Comments
6 Responses to ““BINADAMU HATOSHEKI”-ORCHESTRA MAKASSY”
Leave a Reply


[...] “BINADAMU HATOSHEKI”-ORCHESTRA MAKASSY [...]
kwa kweli bongo celebrity ni noma, nimekuwa nawafatilia sana na hasa hivi vibao mnavyotoa vya zamani vinanikumbusha sana, nyie ni noma, ningefurahi kama mnazo nyimbo za vijana jazi enzi za maneti na nyinginezo kama hizo hapo chini ningefurahi sana kupata
ni
Mfaume waniliza – DDC mlimani park
Solemba – Juwata Jazz band
Kipipa Ayubu – Dar international
Jirani – Africa International
Masikitiko – Tancut Almas
Yaliyopita – Washirika stars
Mwenyekiti mwalimu Nyerere – DDC
Usinifinyie jicho – OSS
Kimbunga kimenisonga – OSS
Asia – Bima Lee
Tulia mama – Bima Lee
Dunia Haina siri – Bima lee
Kwa mjomba – Urafiki Jazz
Tutafunga ndoa Asmaha- Urafiki Jazz
Barua nyingi nilikutumia- Western Jazz
Ewe mpenzi Christina – Western Jazz
Yamewafika wenzenu – Dar international
Maneno mengi nimesikia – KIko kids
Mimi Hanipati ng’o – Kiko kids
Mwenzeni niko taabani – Western Jazz
Mtoto wa Mjini – Masantula
Hangaika – Masantula
Gubu la mume – Vijana Jazz
Shemeji – Vijana Jazz
Bujumbura – Vijana Jazz
Magaidi wa Msumbiji- Vijana Jazz
Epuka Jambo lisilokuhusu – DDC
Jiko Limenuna – Vijana Jazz
Paulina – Dar international
Milima ya kwetu – Orchestra super rainbow
Ogopa tapeli – Vijana Jazz
Natoa Onyo – Dr. Remmy
watoto wamekuja juu – washirika stars
Nalila masumanda – washirika stars
Penzi la Ulaghai – washirika stars
Nimebaki nashangaa – Washirika stars
Kayumba- washirika stars
Kisa- washirika stars
Nyongise – Vijana Jazz
Siri ya ndani – Vijana Jazz
Heshima ya mtu – Vijana Jazz
Malaine – Vijana Jazz
Usicheze na bahari – Vijana Jazz
VIP – Vijana Jazz
Shoga – Vijana Jazz
Ni Mashaka – Patrick Balisidya
Zinduna – Zahoro Ally
kama kawaida bongo celebrity, hebu tuburudishe na vibao hivyo
mi naomba mniwekee kile kibao wanachoimba,bomu limeshapasuka wanguzi wanatapata,sijui wanaitaje ule wimbo na nisahau bendi pia,labda mnikumbushe kidogo
i mean walanguzi
CLASSIC CLASSIC CLASSIC BONGO MUSIC
Shukrani zimfikie Mzee makassy kwa miaka yoote aliyotuzawadia hii Muziki Munene..Hii SANTURI Inazunguka kila siku hapa Nyumbani Kwangu..Ilirecordiwa na Virgin records miaka ya Sabini..Maybe the 1st TZ Artist on a MAJOR LABEL??..
Wow! It has been a while since I heard “Kasongo … Mobali na Ngai”! Inanikumbusha enzi hizo na vijana wa Bwiru/Sengerema katika visiwa vya Sanane – Those were the days, life was good, and love was plenty!! No sex, BUT real innocent Love! Thanks BC-:)