romabc

Naomba nikuulize swali; Kwenye muziki unapenda zaidi ujumbe uliomo au midundo kwa maana ya beats? Kwako wewe muziki ni nini? Usiharakishe kunijibu. Fikiri kwanza.

Wakati unafikiri ngoja nikupe jibu langu.Mara nyingi huwa napenda wimbo wenye ujumbe. Midundo ikiwa imetulia huwa nazama pia.Ndio maana nampenda sana Oliver Mutukudzi(mwanamuziki kutoka Zimbabwe) wakati mara nyingi sielewi anachokiongelea mpaka pale ninapopewa tafsiri. Napenda jinsi anavyocharaza gitaa lake na kutawala jukwaa. Napenda muziki kwa sababu naamini muziki ni universal language(lugha ya dunia).

Miongoni mwa nyimbo ambazo nimezisikia hivi karibuni na kupenda ujumbe na midundo ni kutoka kwa mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania anayekwenda kwa jina Roma(pichani). Jina la wimbo wake ni Tanzania. Msikilize Roma kwa kubonyeza player hapo chini kisha uniambie kama ujumbe uliomo kwenye wimbo huu unakugusa au la.

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Feedback / Comments

24 Responses to “TANZANIA,TANZANIA,OH TANZANIA!!”

  1. Comment by shamia on May 23rd, 2009 1:27 am

    This guy is good,just like Nakaaya,he expresses what he feels and that the feelings of most Tanzanians to be honest,but he has got to be very careful with his mouth,from the bad nature of our leaders,they will want to find the way to take him down.That’s the really hip hop.Big up to this guy.

  2. Comment by miya on May 23rd, 2009 10:35 am

    ‘Take him down’ si umeskia messege ya musiki wake kuwa ameaga kwao na babu yake akamchingia ng’ombe na ile damu akambariki nayo! anyway its really high time for our leaders to realise that they need Integrity & Ethics and put it to practice to be able to led and be an example kwa sisi vijana.

  3. Comment by Nas on May 23rd, 2009 6:16 pm

    Ebwana we mchizi yaweza kuwa ndo mchizi wa kwanza kutoa kitu cha kiukweli sana katika maisha mabovu ya kibongo. Nazimika sana naulivyo Diss live.Ningekuwa Dj Bongo ili tune ningekuwa nalicheza daily yani kuna kucha linazama ni bandika bandua….Ebwana mchizinakupa big up.Yani ili tune ni maukweli matupu yani mchizi kagusa kunako.Thamani ya magari yao wanayomiliki Unajenga shule ya kijiji.
    Siutani bongo tumejaliwa vitu kibao, ila manufaa yake????????? na hatima yake???????????
    Nafikiri wadau mmenisoma, ngoja kwanza kesho tupige kura Busanda tuangalie upepo unakwendaje

  4. Comment by abdul abdul on May 24th, 2009 8:32 am

    ebwanaee si uongo thamani ya magari yao una jenga shule ya kijiji,wanyonge wanafungwa daily,vigogo hao juzi wameachiwa wakale bata

  5. Comment by Malkiory on May 24th, 2009 10:05 am

    Wanamuziki wengine wa bongo flava wanatakiwa kufuata nyayo za huyu mwanamuziki. Nampongeza kwa kuweza kufikisha ujumbe mzito kwa viongozi wala rushwa, wabadhiru na mafisadi.

  6. Comment by sixk on May 24th, 2009 12:14 pm

    kijana beats tamu, ujumbe umefika mahali pake.
    Roma…. kaza buti kaka.
    haha
    Ujumbe safi sana..
    kama Mengi alivyojitoa mhanga sembuse wewe kaka.

  7. Comment by hombiz on May 24th, 2009 9:12 pm

    sasa hizi ndio nyimbo za bongo flava niliokuwa napendelea ziimbwe! Sio freeze! Freeze 4 what!

    big up dogo Roma!
    all my blessings!

  8. Comment by CICI on May 25th, 2009 1:49 pm

    DAMN!! MUCH RESPECT .I SALUTE YOU

  9. Comment by Gwiji on May 26th, 2009 2:59 am

    Nakumbuka huyo dogo alipeform huo wimbo kwenye Fiesta ya Arusha mwaka jana sijawahi kusikia huo wimbo kwenye redio hata siku moja ,Madj wa TZ mpaka uonge ndio watapiga track yako .Message kali mno sio wasanii wakongwe kila siku wao wanaimba mapenzi wakati kuna issue za ufisadi ,maalbino lakini wao kila siku mapenzi

  10. Comment by Marce Ze D on May 26th, 2009 8:21 am

    Wanavunja amri ya sita ndani ya makanisa,
    nakuabudu miungu watu ili mradi wapate pesa.
    mbele ya madhabau ya Getrude Lowakatare,
    kwa askofu Kakobe wanadondoka mbele ya altare.WE BONGE LA MC! IBRAHIM HUSSEIN a.k.a ROMA

  11. Comment by Edwin Ndaki on May 26th, 2009 9:06 am

    aaaa..mtoto wangu nyundo mbili kisa kakutwa anavuta…kweli roma..

    tutafika tu

  12. Comment by Bob Sambeke on May 27th, 2009 2:37 pm

    Hi BC

    Ndaki Ujamalizia Hapo!

    mtoto wangu nyundo mbili kisa kakutwa anavuta

    *****Je Nani Anastahili kufungwa Mtoto wangu

    au swahiba wa K***ET*? Kaza Buti Roma!

    Utafika tu! Waumbue hao mafisi-hadi! Halafu

    Mkubwa BC weka Madude ya 2Proud Enzi Hizo

    anatoka na Album yake ya kwanza Yenye nyimbo

    kama “Nimesimama”,Za Kina Sos

    B,GWM,Mashakshuta Sauti ya Miujiza-Ubandidu!

    Mr.Four Wheel–Nimezimiss sana Enzi hizo ali

    kuwa anazitwanga Sana DJ JD!

    It’s Me Bob Sambeke-Young Millionaire

  13. Comment by mbavu on May 28th, 2009 4:12 pm

    Pamoja Bob Sambeka! Hapo umenifanya nikumbuke dude la 2Proud “NI WAPI TUNAKWENDA” Ni dude ambalo ujumbe wake unaendana na maisha ya Mtanzania mpaka ya sasa hivi..! Ni UJUMBE ambao hauchuji. Mkubwa BC tutafutie wimbo huu.. Pia itakuwa ni opportunity ya wadau wa BC kucompare maisha ya Mtanzania ya mwaka ’95 na hivi sasa 2009.
    Kuhusu huyu jamaa aliyeimba “TANZANIA”, ni ujumbe mzuri. Sema alibidi aongelee vitu positive na negative, otherwise wimbo ulitakiwa uitwe “UFISADI TANZANIA”, “LONGOLONGO TANZANIA” au kitu kingine. Kwani “TANZANIA” ni mada pana zaidi!

  14. Comment by Mtanzania on May 29th, 2009 2:01 am

    Please naomba kama kuna mtu ana Embeded code au Url ya huu wimbo anitumie jamani email yangu ni Char.lena@hotmail.com.. Please.
    That’s so creative love the Msg… Wimbo mzuri sana..

  15. Comment by kingo on May 29th, 2009 8:53 am

    hichi kitoto cha ukweli hadi kinaudhi!namna hii naweza sikiliza bongo flava.ila sasa songi za ‘kichochezi’ kama hizi hazinogi kusikiliza geto tu baada ya kununua ka-albamu kangu feki,hizi zinafaa kupigwa radio mara kwa mara(sijui ndo nina hisia za ki-gomvigomvi au vipi!).nyway,track ‘imesimama dogo.kudos

  16. Comment by mick on May 29th, 2009 4:57 pm

    nyimbo imetulia ,ujumbe wenye akili manake nilikuwa nimechoka bongo fleva kila nyimbo mambo ya mapenzii tuuu,kijana lite vitu vingine tuvisikie

  17. Comment by manyere on May 30th, 2009 6:28 am

    Sipendi sana Bongo Fleva, lakini huyu jamaa kanigusa ile mbaya. Ujumbe mkali na unagusa. Mapigo pia yameendana na ushairi. Hongera sana kijana.keep it up man!!!!

  18. Comment by s on June 2nd, 2009 10:52 am

    Huu wimbo ungekua kampeni tosha busanda.

  19. Comment by CHAPOMBE on June 2nd, 2009 11:07 am

    ur the best MC all over the TZ.kibao chako kimetukuna Mzazi dogo ni mbaya sana ” unamwaga vocal na bible mkomo wakulia” sio! doo!!

  20. Comment by ALEXANDER GEOFREY on January 12th, 2010 12:14 pm

    WIMBO WANGU WA MWAKA 2009 NI HUU. NITAMWAMBIA SAED KUBENEA AUFANYE UEW WIMBO WAKE WA MWAKA AUTOE KWENYE GAZETI LA MWANA HALISI. HAWA WOTE NI WANA MAPINDUZI

  21. Comment by Jack on February 24th, 2010 1:02 am

    Du, huwezi amini! Siko zote nilichukulia music kama uhuni maana wanaoimba wanaonekana kama wahuni, leo nilivyo sikiliza kibao hiki…nikagundua kuwa huyu dogo anaomba mbali hata kuliko mimi na watanzania wengine wengi kiasi kwamba ingekuwa TZ ni inchi ambayo watu wake wanaelimika kwa music, matangazo na taarifa za vyombo vya habari, basi hakuna hata mmoja ambaye angefaa….hebu sikia ” magari yao, moja unaweza kujenga shule ya kijiji ili wale vijanja wanauchunga ng’ombe kwa bibi wasome” unajisikiaje?
    Huu wimbo ni babu kubwa….nimechizi nao.

  22. Comment by Edwin Ndaki on September 2nd, 2010 5:39 am

    sasa mbona dogo kasahaulika kuzunguka na mh kwenye kampeni..au dogo hana kipaji au sio mlaji :D

  23. Comment by Joe NTANDU on September 23rd, 2010 5:11 pm

    ANA KIPAJI NA KILE ANACHOIMBA NI UKWELI USIOPINGIKA….

  24. Comment by TARZAN on September 25th, 2010 4:05 pm

    Ni nyimbo nzuri ambayo kila Mtanzania mpenda maendeleo ya Nchi na Mpinga Ufisadi angependa kuisikia. Tatizo tunasikiliza wachache wenye access na Internet. Labda Mzee Mengi atusaidie ili EATV, ITV izicheze nyimbo za ROMA ili watanzania wanufaike, ni sehemu ya Elimu ya Uraia. Big Up Roma

Leave a Reply