Hapo jana Rais Jakaya Mrisho Kikwete amekuwa kiongozi wa kwanza kutoka Afrika kukutana na Rais wa Marekani,Barack H.Obama katika Ikulu ya Marekani. Hizi hapa ni baadhi ya picha za ziara hiyo. Picha zote na Freddy Maro wa Ikulu.

jk-at-wh-1bc

Rais Jakaya Kikwete akitia sahihi katika kitabu cha wageni punde tu alipowasili katika Ikulu ya Marekani maarufu kama White House.

jk-at-wh4bc

Rais wa Marekani Barack Obama(kushoto) akimkaribisha Rais Jakaya Kikwete katika ofisi yake maarufu kama Oval Office.

jk-at-wh2bc

Rais Kikwete akiwa katika mazungumzo na mwenyeji wake Rais Barack Obama ndani ya Oval Office. Marais hao waliongelea mambo mengi ikiwemo ushirikiano kati ya Tanzania na Marekani katika masuala mbalimbali.

jk-at-wh3bc

Rais Kikwete akiendelea na mazungumzo ndani ya Oval Office na wenyeji wake akiwemo Waziri anayeshughulikia masuala ya nje wa Marekani, Bi.Hillary Clinton(kulia)

Feedback / Comments

38 Responses to “WHEN JK MET OBAMA”

  1. Comment by sisterTZ on May 22nd, 2009 8:04 am

    BC JK ameongelea issue gani za maendeleo huko USA? Maana hizi picha sisi watu wa kawaida wala hazitusaidii kitu kwa kweli, twataka kusikia kitu gani kimempeke JK kwa OBAMA..

  2. Comment by Flora on May 22nd, 2009 8:11 am

    I am over joy. I will Give my full comment on Tuesday. I am on holiday.

    Thanx once BC

    Wadau have a greater w-end

  3. Comment by Jinias on May 22nd, 2009 9:36 am

    Muungwa hapo katuangusha bwana.

    DESA mpaka kwenye maongezi!

    Yaani ameshindwa kuweka kichwani points za kuongea? Khaa!

  4. Comment by Mickey Jones - Denmark on May 22nd, 2009 11:24 am

    Raisi Kikwete kuwa kiongozi wa kwanza kutoka bara la Africa kukaribishwa “white House” ni matokeo mazuri ya kazi za kiongozi wetu na wizara ya mambo ya nchi za nje.

    Nafikiri itatusaidia kwa sisi watanzania kuelewa heshima kubwa tuliyopewa kimataifa, inatokana na msimamo mzuri wa uongozi wa amani Tanzania.

    mickey@mail-online.dk
    Denmark

  5. Comment by Frateline on May 22nd, 2009 3:28 pm

    Hi guys kutoka Helsinki-Finland

    Ni hatua nzuri ya kuwa kiongozi wa kwanza kuonana na rais wa kwanza wa marekani mwenye asili ya Africa, Tatizo na wasi wasi wangu viongozi wetu wanapenda kuomba samaki badala ya kuomba ujuzi wa kuvua hao samaki sisi wenyewe,je kikwete kwenye desa lake sijui kakumbuka kilimo na kuomba jinsi ya kusaidiwa kuleta mapinduzi ya kilimo ili tuweze kujilisha, hatutaki chakula cha msaada ni sawa na mtu kupewa samaki, je kwenye desa lake sijui kakumbuka kueleza jinsi ya kusaidiwa kulinda viwanda vya wazawa ktk dunia ya ushindani wa China na wengine , je lakini desa lilikuwa la nini kwenye mazungumzo wakati issues za Africa na Tanzania wala hazihitaji hilo desa ni umasikini, rushwa, hakuna democrasia ya kweli, ukimwi, malaria, kilimo cha watu wengi kimetupwa, miundo mbinu mibovu na migogoro bara la Africa, mali asili za bara la Africa zinaporwa na mabepari wengi kutoka huko huko marekani,

    Ninapenda kuendelea kuamini na kurudia kama ambavyo nimewahi changia hapa, ni ufinyu wa mawazo kudhani kuwa Africa au Tanzania tunaweza kuendelea kwa misaada , tafiti nyingi zinaonyesha hatuwezi,hata hivyo marekani pesa nyingi wanapitisha kwenye NGOs zake kama vile USAID, PACT na nyingine ambapo zaidi ya nusu ya hizo pesa zinarudi huko marekani.

    Kwa maoni yangu, Rais Obama anaweza kutusaidia kushinikiza demokrasia ya kweli Africa na Tanzania, ili viongozi wabovu wasipate muda wa kungangania madarakani lakini sio kuleta au kutatua matatizo ya Africa, hiyo ni kazi yetu Waafrica kama kizazi cha akina kikwete kitashindwa basi kizazi kijacho, MAREKANI WANATAKA RASIMALI ZENU ZA AFRICA , NA KUMTUMIA OBAMA TUTALIWA KISAWA SAWA.

    Weekend njema wadau

    Frateline

  6. Comment by Mjanja on May 22nd, 2009 3:50 pm

    Mawazo yangu ni kama ya mdau mmoja hapo juu,kuwa,lazima tujue na kuona nini kilicho ongelewa.Picha tu hazituelezi chochote.

    Ni Rais wetu,kwa hiyo sio jambo la hajabu kwenda white house kusema hello..!!

    Mimi ningependa kuona hizo trip zina badilisha hali kule nyumbani.Kwanza walimu wetu wamepewa mishahara yao???kama bado mpaka leo kwanini hizo pesa za safari zisitumiwe kuwalipa angalau wachache??

  7. Comment by al on May 22nd, 2009 4:39 pm

    Acheni longolongo sasa si bora ameenda na desa! au mnataka aumbuke kama IMF meeting Dar alipoulizwa swali na Aisha Sese na kushindwa kujibu

  8. Comment by Gervas on May 23rd, 2009 12:26 am

    Kuimalisha urafiki na amataifa makubwa ni jambo la msingi na hapo JK nakupa tano. Tatizo si desa wala nini bali ni watanzania unanufaika vipi na huo urafiki? Kumbukeni kuwa Uchaguzi ni mwakani na kama mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Makame, J; alivosema safari hii utatugharimu Tsh. 4 Billion na selikari inataka itumie at least 60-70% ya budget hiyo toka kwenye mapato yake. je mnafikiri hizo pesa zitatoka wapi? Kuna gharama za kampeni za CCM na kama mjuavo 2005 pesa za kagoda + Ufisadi zilifanikisha uchaguzi kwa mabiioni ya pesa. Sasa mnategemea JK atatoa wapi fedha hizo? ni wazi ameshaanza tembeza bakuli kwa wakubwa huko USA na jana alikuwa anaongea na wanene wa IMF. Ingekuwa nafuu haya mapesa tunayopewa yangemwagwa kwenye Benki ya wakulima ili waanze kilimo cha umwagiliaji TZ.

    Wala hatuhitaji wawekezaji kwenye kilimo, Kila wilaya ikitengeneza mabwawa (Dams) kwa kuziba mito midogo midogo inayomwaga maji ovyo na kuleta maafa ya mafuriko, mibwawa hii ingetumiwa kwa umwagiliaji, serikali ina ma-bwana shamba waliosoma lakini ujuzi wao hautumiki maana hamna mvua. Kama kweli viongozi wetu wangekuwa wanahamasisha KILIMO kwa style ya Kampeni huko Busanda….Bongo ingekuwa Tambarare mapeeemaaa!!!!!!!.

  9. Comment by Romwald on May 23rd, 2009 2:45 am

    Awe wa Raisi wa kwanza au wa mwisho wa afrika kukutana na Obama sisi hatujali.Tunataka tujue kaongea kitu gani na sababu za yeye kukutana naye.Unajua wenzetu wana impression.Wanaweza kukubali kukutana nawe baada ya maongezi wakajiuliza “What the hell was he doing here?” kwani hawajaona contents,sababu zenye ujazo za wewe kufika pale na sio kutumia barozi au chennels nyingine za kiserikali.

    Siwezi kulaumu sasa,ila ningefurahi kuona laivu hayo maongezi.Nakumbuka ule mkutano wa IFM.kuna kipindi ilibidi nifiche suo wangu kwa mikono ili angalau nisione kinachoendelea.

    Credibility ya anayeongea,the contents na namna zinavyowakilisha zinatosha kumvutia msikilizaji na kumuhamasisha kukubali.Kinyume na hapo,tunakazi kubwa sana hasa kipindi kijacho.Kufanya kosa si kosa lakini kurudia kosa hilo si kosa tu bali ni kosa kubwa sana.

  10. Comment by any on May 23rd, 2009 10:27 am

    Kuwa wa kwanza kufika ikulu ya US au wa mwisho haijalishi, ni kafuata nini? msishangilie sana, wamarekani nao wana mahesabu yao,. so tusijione tumepataaaa na wao wanataka cha juu! mburaa.

  11. Comment by any on May 23rd, 2009 10:30 am

    Kuanzia ile siku JK ameshindwa kujieleza kwenye mkutano wa UN! sasa ivi akiwa mikutano mikubwa nakuwa nervous kwa niaba yake! yaani inatisha.

  12. Comment by kitta on May 23rd, 2009 12:58 pm

    Tumeuyazoea hayo!naunga mkono wadau walosema tujue yaliyomo desani!alikuja clinton,barabara zikapigwa deki kule arusha.akajka bush,tukaambiwa amekaa cku nyingi nongo kuliko nchi nyingine ya afrika na kuliko kiongozi yyte wa us kuwahi kija tz!hizo rekodi zina tija?au ndo zile cfa za kijinga? Kitta

  13. Comment by chogo on May 23rd, 2009 1:19 pm

    we JK WEWE,muone kwanza ,huna haya,nyau wewe,hutuliiiiiii.we kuzurula tu,kila kukicha,pesa zetu wazimalizia kwenye kuzurula tu shwain kabsaa.tulia ututengenezee pesa wewe na maendeleo ya nchi yako

  14. Comment by Pendaheli on May 23rd, 2009 5:08 pm

    JK hawezi kujieleza mimi nigeomba arudi shule anatutia haibu.

  15. Comment by Mwanamke wa Shoka (UK) on May 23rd, 2009 8:26 pm

    he he he !!!….mambo ya ud hayoooo…bila desa shule haisogei lol….inabidi kujifunza kutokutegemea desa…lol….JK senior sidhani kama alikuwa anadesa…..hata Obama mwenyewe simuoni akiwa na desa….(inatia aibu lol…)

  16. Comment by Mwanamke wa Shoka (UK) on May 23rd, 2009 8:27 pm

    nina wasiwasi na roho inauma…maana hivyo vijisenti vya misaada vyote VINAISHIA kwa WENYEWE…..waliozaliwa nazo….damn

  17. Comment by Mwanamke wa Shoka (UK) on May 23rd, 2009 8:32 pm

    african governments are corrupt because they emanate from corrupt colonials….what is happening now (the PMs scandals) just prove this….
    it is sickening

  18. Comment by sisterTZ on May 24th, 2009 7:30 am

    ANY jamani mie hiyo issue ya UN sikuwahikuiona mbali sana na nyumbani..jamani je unajua wapi naweza kupata hiyo story kwenye YOUTUBE au wapi ili nione aibu jamani..wadau tukubaliane kwamba hii elimu ya juu ni muhimu sana kwa viongozi wetu bec you learn how to handle situation kama hizo…

  19. Comment by Bingo on May 24th, 2009 12:50 pm

    Jmani mnanichekesha. Do we really need to be the first to meet Obama?? are you guys kidding or what!!! Kikwete should stop travelling and keep the promises he made when he wanted voted in back in 2005. He travels like hell but we dont see anything coming out of those trips. Watumikie watanzania at least for once kaka, we are sick and tired of empty promises, we need actions big bro. everything in TZ is shrinking, from roads construction, good governance all through to social services. Sasa kuwa wa kwanza kumuona Obama does it put bread on the table? i know the rip to the US is usual begging if not showing off, and you should understand by now that there is no free lunch. we need to work and forget about begging mr president.

  20. Comment by Mwanamke wa Shoka (UK) on May 25th, 2009 9:54 am

    Hi “ANY”….umenichekesha….at unakuwa nervous on his be-half….
    sio siri inasikitisha…lol

  21. Comment by Mwanamke wa Shoka (UK) on May 25th, 2009 9:59 am

    …sometimes uharaka wa ku-peak tactics ni muhimu….our Excellency amefanya kazi muda mrefu saana Wizara ya mambo ya nje….sasa inanishangaza saana kuona hakuweza ku-PEAK up on those tactics….like how to make a good speech…etc….I think kuna tofauti katika kutoa hotuba na “kuongea”….Obama is in conversating pose….while our JK is reading a speech….(and not conversing…)….

  22. Comment by Mwanamke wa Shoka (UK) on May 25th, 2009 4:01 pm

    Raisi wetu na first lady wake wanapenda saana mtoko nimeshawashitukia…..hamna kilichotendeka sijui hii kura zijazo wataombaje

    ….epa sioni imefikia waapi…ni machanga ya macho hayooooo

  23. Comment by Mwanamke wa Shoka (UK) on May 25th, 2009 4:04 pm

    kila leo mara Marekani mara waapi….miye sioni kama kulikuwa na ulazima wa kwenda Marikani…angetumia UBALOZI uliopo pale Darisalama mambo yangeisha na tungemuona muungwana maana angetuonyesha ana uchungu na pesa ya walala hoi ambao ni wapiga kura wake….
    ……inachekesha saaaaaaaana…”eti kuwa wa kwanza kuonana na OBAMA”…..tehe tehe tehe

  24. Comment by Flora on May 26th, 2009 9:51 am

    JK did you real consult any one b4 going to meet Obama? I don`t mean your corrupted government people, I mean people who contributed on your Ticket from TZ to America(Tax Payer)about issues to be discussed? Or you just do things on your own either people will be happy for the out come or not you just make your own decision and go?

    Who care?

    Ok it wont help. can you tell us what did you discuss and which agreement did you reach between two of you please.

    If you signed any contract or whatever

  25. Comment by obasitokumbo on May 26th, 2009 2:56 pm

    Labda kithungu kinamuona teh teh!!!!!!!!!!

  26. Comment by obasitokumbo on May 26th, 2009 2:57 pm

    Labda kithungu kinamuona teh teh!!!!!!! job true true

  27. Comment by sele on May 26th, 2009 5:37 pm

    jenataka kujua mgongano wa mafuta zanzibar umekuwaje

  28. Comment by imweimwe on May 27th, 2009 10:37 am

    Kikweteee!!!
    Ananpenda sana maujiko Mkwere huyu!!
    Kuwa wa kwanza kumuona Obama tumepata nini sasa?
    Hiyo gharama yake na msafara wake tungepata trekta ngapi?
    Hivi kwanza alikagua gwaride la heshima? Mboni picha hizo sizioni, kama wao wanavyokuja bongo?

  29. Comment by Jane on May 27th, 2009 10:37 pm

    Many of us has no clue to the necessity of our leaders going to another country. TZ for instance is in the 3rd world; Obama doesn’t need us,we need him for help. Those gwaride you’re preaching about will be done if you’re there to benefit the America and their allies. USA is thinking of using our port for drilling oil, don’t be judgemental son. Wait and see the fruits of JK.

  30. Comment by mariana on May 28th, 2009 2:48 am

    mbona hatuoni maendeleo safari kila siku,kama vp 2010 tubadili muelekeo coz maana ht language yenyewe anaboronga………..lakini washikaji tuacheni majungu put urself in hi position,wat will u do?

  31. Comment by kichwa on May 28th, 2009 10:03 pm

    vipi mnasema nini watu wa mzimuni

  32. Comment by Mwanamke wa Shoka (UK) on May 29th, 2009 6:01 am

    halafu wakisha drill oil ndio tupate madawa, solid and dependable infrastructure…or what does this mean….??…Kuna mali asili ngaapi na kwa kiasi gani zinazowapa WAGENI BILLIONS of money wakati LOACAL COMMUNITIES ambapo maliasili hizo zinatoka HAWANA HATA proper hospital…proper source of water….Take for instance Mwadui mines…and the DeBEers….pale mwadui ni kama jangwa to me….angalia hali za maeneo yoote kulipo na migodi,…kunatisha…..

    …..leo eti unasema tusubiri tuone OBAMA anataka kuchimba MAFUTA kutoka kwetu….what the hell is this again…???…Ni watu kuchukua 10% zao halafu the poor mass of innocent Tanzanian citizens kuendelea kuishi CHINI YA UMASKINI…..ni dhaidi ya umaskini…..sijui niite ni nini?…Its so painful.

    I just dont know….(i need help to really understand this….

  33. Comment by missionary on May 29th, 2009 9:13 pm

    we have to look behind what mr pre acomplished before becoming the pre.if we find something then we will be able to predict what can come out of this trip.the past can tell us how much this president will be succeseful.

  34. Comment by Bingo on May 30th, 2009 3:44 am

    Jane I dont agrre with you dear sis. do we really need em Rich Countries? i dont think so. we have been begging from them for ages, i mean since indepence, but look where we are now!! still poor burn out beggars!!! look at DRC for example… they were the dearest darling to the US, but look at what US did to them, they sucked all natural resources they ever found in the country and fled away, leaving the poor fellas even deadly poorer. DRC is now the second from last, of the 10 poorest countirs in the world.

  35. Comment by chakubanga on May 30th, 2009 5:28 pm

    Jamani kuwa na desa siyo tatizo ila twende na wakati. Desa la kwenye karatasi kubwa kama hiyo (A4)na kurasa nyingi nyingi linaahibisha (unless unatoa hotuba kwenye lectern). Hasa kwa watu wakubwa kama hao inatakiwa uandike vi-note kwenye vikaratasi vidogo vidogo (if at all)

    …anyway kuwa rais wa kwanza wa Africa kuonana na Obama siyo tatizo. Cha muhimu ni kujifunza kwake jinsi ya kuleta maendeleo ya nchi (na siyo kwenye mifuko ya watu). Obama hapendi hayo na anayapiga vita kweli kweli (kwa vitendo na siyo kwa maneno).

  36. Comment by Mwanamke wa Shoka (UK) on June 2nd, 2009 6:19 am

    Tanzania will then be next to be sucked….and they will flee…..
    inasikitisha….ila alkiyelala usimwamshe….unafikiria OBAMA atakuja kutuamsha….not at all…..

  37. Comment by KondoaIrangi on June 2nd, 2009 5:58 pm

    Ngoja mie nikae kimya.

  38. Comment by chogo on June 2nd, 2009 8:18 pm

    BINGO,MWANAMKE WASHOKA na wengine wote mliotoa point,Jinias wewe umenivunja mbavu.
    jane who told u that we can not live without depending on wazungu??wewe kua mama,unajua ni kiasi gani kinachotutoka frm our country na kiasi gani tunachogai??tunaloose sana tena sana kuliko kugain.na JK KUMSEMA mi sioni shida baba ANAZURULA huyu sijapata ona!!??hatuliiiiiiiiiii???it doesnt matter aende na desa la namna gani kinachomatter ni kitugani kiliandikwa na je sisi tutafaidikaje KAMA WATANZANIA??
    1)baba chonde chonde ENDELEZA KILIMO TANZANIA??FUFUA VIWANDA VYA USINDIKAJI MATUNDA YAANGUKA NA KUOZEANA
    2)AJIRA ZIRUDI MASHAMBANI NA WATU WAFAIDIKE WAONE UMUHIMU WA KUISHI VIJIJINI KULIKO KURUNDIKANA MIJINI WATU 10 CHUMBA KIMOJA NA HAKUNA ANAEPENDA KUVULIWA NGUO NA MGAMBO WOTE TWATAKA TUISHI KWA AMANI
    3)JIFUNZE PRIORITIES SIO UNAJIAMULIA TU KAMA WAENDA HAJA,JUA NI KITU GANI UNACHOTAKIWA KUKIFANYA CHA KWANZA NA VINGINE VINAFUATA
    3)KODI ZETU ZITUMIKE KISAWA SAWA NA SIO KUFANYIA MAMBO YAAJABU KAMA KUABUDU MWENGE,ULE NI USHWAI AM TELLIMNG U BABA,KWENYE AMRI ZA MUNGU TUNAAMBIWA USIABUDU MIUNGU MINGINE SO WHAT IS KUABUDU MWENGE??BADALA MUONGEZA MADAWA MAHOSPITALI MUONGEZE VYUO NA KUTOA ELIMU BORA NA SIO BORA ELIMU.IMPROVE SOCIAL CERVICES BABA
    4)tunataka maji safi nchi nzima,mahospitali,mashule,vyuo viwe bora sio tusome huku tumesimama, I BELIEVE U UNDERSTAND ME WELL JK,EVN IF ITS HARD TO DO ALL OF THIS I HAVE WRITTEN BT PLZ TRY EVN 2 BAC EEH!!KOMANDOO HILOO
    5)BADALA YA KUJENGA VITU VISIVYO NA KICHWA WALA MIGUU ,JENGENI BWAWA LA MAJI AMBALO KIPINDI MABWAWA YAKIFURIKA MAJI YAWEZE KUA PRESERVED ILI YATUMIKE KWENYE UKAME NA MABWA HAYO YATASAIDIA KUPRODUZE UMEME PIA NA KUPUNGUZA MGAO MKALI WAUMEME UNAOZIDI KUIPELEKA NCHI KUBAYA.NI HAYO TU KWA LEO KOMANDOO JK.XOXO

Leave a Reply