MY TANZANIA   |   PLACES TO GO   |   MEDIA   |   ONLINE ENTERTAINMENT    

jose_juma_naturebc

Mojawapo ya mambo ambayo yanaweza kukufurahisha kama unapenda muziki kutoka Afrika Mashariki ni pale wasanii kutoka nchi zinazounda Afrika Mashariki wanapoamua kushirikiana katika kazi zao. Mifano ipo mingi kuonyesha jinsi gani mipaka iliyowekwa na mtawala wa enzi hizo inaweza kuvukwa japo kwa kutumia muziki.

Nimewahi kuandika siku za nyuma kwamba wakati viongozi wetu wanasuasua katika kukamilisha muundo wa jumuiya ya Afrika Mashariki(ukiniuliza mimi nitakwambia ni kwa sababu kila mmoja anaweka mbele maslahi binafsi badala ya faida nyingi za muungano makini) wasanii wao wameshavuka kizingiti hicho.Wanashirikiana.

Miongoni mwa mifano ya ushirikiano huo ni huu wa Juma Nature akimshirikisha Jose Chameleon(Uganda) katika wimbo unaokwenda kwa jina Mikiki Mikiki. Kama ujuavyo hawa wote ni ‘majina makubwa” katika muziki wa ukanda wetu. Wanaposhirikiana tunategemea kitoke kitu makini.Nakuomba uwe muamuzi.Sikiliza Mikiki Mikiki hapo chini.

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Picha na Muziki kwa niaba ya GetMziki.

Share and Enjoy:
  • Digg
  • Sphinn
  • del.icio.us
  • Facebook
  • Mixx
  • Google Bookmarks
  • email
  • LinkedIn
  • Live
  • Spurl
  • Technorati
  • Yahoo! Buzz
  • YahooMyWeb

hasheem

Share and Enjoy:
  • Digg
  • Sphinn
  • del.icio.us
  • Facebook
  • Mixx
  • Google Bookmarks
  • email
  • LinkedIn
  • Live
  • Spurl
  • Technorati
  • Yahoo! Buzz
  • YahooMyWeb

hasheemt1bc

Kama uliwahi kutabiri kwamba siku moja mtanzania Hasheem Thabeet atakuja kuchezea katika ligi ya mpira wa kikapu ya NBA, unayo sababu ya kujidai kwani utabiri wako umetimia jioni hii(saa za New York).Hasheem Thabeet amechaguliwa kujiunga na timu ya Memphis Grizzlies yenye makao yake makuu huko Memphis katika jimbo la Tennessee nchini Marekani.

Hasheem anakuwa mtanzania wa kwanza kufikia hatua hiyo.Kama nchi tuna kila sababu ya kufurahia mafanikio yake na kumtakia kila la kheri. Hivi sasa anakuwa,bila shaka, “balozi” wetu katika ulimwengu wa michezo hususani mpira wa kikapu. Kila la kheri Hasheem.

Share and Enjoy:
  • Digg
  • Sphinn
  • del.icio.us
  • Facebook
  • Mixx
  • Google Bookmarks
  • email
  • LinkedIn
  • Live
  • Spurl
  • Technorati
  • Yahoo! Buzz
  • YahooMyWeb

michael-jackbc

Habari za uhakika ambazo BC imezipata zinapasha kwamba Mfalme wa muziki wa Pop,Michael Jackson,amefariki dunia huko Los Angeles nchini Marekani mchana huu.

Mfalme huyo wa Pop alikimbizwa hospitali mchana huu baada ya kuzimia akiwa nyumbani kwake maeneo ya Holmby Hills huko Los Angeles alizimia baada ya kupatwa na mshtuko wa moyo kitu ambacho kinasemekana ndicho kilichomaliza uhai wa Michael Jackson katika Kituo Cha Afya cha UCLA ilipotimia saa nane na dakika ishirini na sita (2:26pm) kwa saa za Los Angeles.

mj-jackson_1972b

Michael Jackson akiwa na umri wa miaka 13

Michael Jackson alizaliwa huko Gary,Indiana nchini Marekani tarehe 29 August mwaka 1958 akiwa ni mtoto wa saba kati ya watoto tisa wa Joseph na Katherine Jackson(wazazi wao). Alianza  kujishughulisha na masuala ya muziki akiwa na umri wa miaka minne(4) katika kundi la familia lililojulikana na kutamba kama Jackson 5(pichani).

jackson5

Kabla ya kufikwa na mauti,Michael Jackson, alikuwa anapanga kufanya show za mwisho huko London mwezi July mwaka huu.Tiketi kwa ajili ya show hizo zilikuwa zimeshakwisha(sold out)!

garyindianabc

Pichani ni nyumbani alipozaliwa Michael Jackson na ndugu zake huko Gary,Indiana nchini Marekani.Nilipiga picha hii December mwaka 2006 nilipotembelea maeneo hayo ili kujionea alipozaliwa Mfalme wa Pop.Mtaa ilipo nyumba hii unaitwa Jackson Street.

BC inapenda kutoa pole kwa wote ambao wameguswa kwa njia moja au nyingine na msiba huu.Tunaamini kwamba Michael Jackson alikuwa sio tu mwanamuziki maarufu ulimwenguni bali muziki wake uligusa wengi.Wengi walicheza,wanacheza na wataendelea kucheza miziki yake.

Hapa chini unaweza kusikiliza simu iliyopigwa kutoka nyumbani ikwake kwenda kwa watu wa huduma za dharura(Emergency)

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Share and Enjoy:
  • Digg
  • Sphinn
  • del.icio.us
  • Facebook
  • Mixx
  • Google Bookmarks
  • email
  • LinkedIn
  • Live
  • Spurl
  • Technorati
  • Yahoo! Buzz
  • YahooMyWeb

hasheem-thabeetb

Kwa mapana na marefu,jina la Hasheem Thabeet litatawala vichwa vya habari wiki hii.Swali au maswali ambayo wengi wanajiuliza ni je Hasheem Thabeet atajiunga na timu gani?

Mambo mengi yanasemwa kuhusu Hasheem.Wapo bado wanaoendelea kusema kwamba bado hayupo tayari kwa sababu alianza kucheza mpira wa kikapu “ukubwani’! Pamoja na hayo,wote wanaosema hivyo wanakubali pia kwamba Hasheem ataleta “impact” kubwa katika NBA.Wapo ambao wamefikia hata kumbeza kwamba hatoweza kutamba kama ilivyokuwa kwa Mzaire Dikembe Mutombo na badala ya yake atakuwa kama Msenegali Mouhamed Sene (Mo Sene) ambaye kimsingi hafanyi vizuri katika NBA kama alivyotarajiwa.

Waache waseme.Kwetu sisi muhimu ni kwamba kijana wetu atakuwa mtanzania wa kwanza kucheza katika NBA. Ni matumaini yetu kwamba Hasheem atafungua milango kwa wengine wengi ambao kupitia kwake wataamini kwamba “inawezekana”.Binafsi naamini Hasheem atafanya vizuri.Cha msingi ni kwamba ni lazima awe msikivu kwa makocha wake,wachezaji wenzake na daima azingatie mazoezi na kujiweka mbali kidogo na “mambo ya ujana”.

Watabiri wa mambo wanasema kuna uwezekano mkubwa  kwamba Hasheem atajiunga na Memphis Grizzlies ingawa yeye mwenyewe inasemekana hangependelea sana.Je atajiunga na timu gani basi? ESPN wataonyesha zoezi hili. Tizama ratiba ya hapo ulipo.Kwa sasa mtazame Hasheem na wenzake ambao ndio “wapo juu” katika pick ya mwaka huu.

Share and Enjoy:
  • Digg
  • Sphinn
  • del.icio.us
  • Facebook
  • Mixx
  • Google Bookmarks
  • email
  • LinkedIn
  • Live
  • Spurl
  • Technorati
  • Yahoo! Buzz
  • YahooMyWeb

shaa2bc

Kama unafuatilia Bongo Fleva kwa makini bila shaka hivi sasa umeshalisikia jina la Sarah Kaisi au Shaa (pichani) kama ambavyo anajulikana kwa mashabiki na wapenzi wa B Fleva.

Shaa ameingia kwenye game kwa kishindo.Uwezo wake wa kumiliki jukwaa,kuimba na kwa ujumla kukidhi haja ya mashabiki wa muziki huo wa kizazi kipya,ndivyo vitu ambavyo vinamfanya azidi kupanda chati na hivyo kuungana na wasanii wengine wa kike ambao wanafanya vizuri.

Hivi sasa anatamba na nyimbo zake Zamu Yangu na Pambazuko huku akiwa anapika kitu kingine studio ambacho mwenyewe anasema ni zawadi aliyopewa na Judith Wambura aka Lady Jaydee.Tunasubiri.

Leo tunao wimbo wake Pambazuko. Katika wimbo huu amemshirikisha msanii maarufu wa B Fleva,Ambwene Yessayah au AY. Usikilize. Kama kawaida maoni yanakaribishwa(ila jitahidi kutoa maoni yanayojenga badala ya kubomoa au kuonyesha chuki na dharau).Umeupenda wimbo? Unasemaje.Shaa atazidi kushika chati?Karibu.

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

shaa1bc

Shaa on stage!

Share and Enjoy:
  • Digg
  • Sphinn
  • del.icio.us
  • Facebook
  • Mixx
  • Google Bookmarks
  • email
  • LinkedIn
  • Live
  • Spurl
  • Technorati
  • Yahoo! Buzz
  • YahooMyWeb

iluminata2009bc

Kama kuna mashindano ya urembo ya kimataifa ambayo Tanzania inaweza kujivunia bila shaka ni mashindano ya Miss Universe. Bila shaka bado tunakumbuka jinsi mrembo Flaviana Matata alivyoipeperusha vyema bendera ya Tanzania huko nchini Mexico mwaka 2007. Flaviana sio tu alishika mojawapo ya nafasi za juu bali style yake ya kuwa “mrembo mwenye upara” ilikuwa gumzo la dunia nzima kitu ambacho kwa namna yake kiliitangaza sana Tanzania.Kila mtu alikuwa akitaka kujua yule mrembo mwenye upara anatokea nchini gani? Jibu walilipata.

Mashindano ya mwaka huu yanatarajiwa kufanyika tarehe 23 August huko katika visiwa vya Atlantis Paradise ndani ya Nassau,Bahamas.Jumla ya warembo 84 wanatarajiwa kushiriki mashindano ya mwaka huu.

Tumaini letu na mwakilishi wetu huko ni binti unayemuona pichani. Anaitwa Illuminata James Wize. Bila shaka tayari waandaaji wa Miss Universe Tanzania walio chini ya uongozi hodari wa Maria Sarungi tayari wameshaanza maandalizi makali ili kuhakikisha kwamba kwa mara nyingine tena Tanzania inakwenda kushindana na sio kushiriki.BC inamtakia kila la kheri Illuminata James.

Share and Enjoy:
  • Digg
  • Sphinn
  • del.icio.us
  • Facebook
  • Mixx
  • Google Bookmarks
  • email
  • LinkedIn
  • Live
  • Spurl
  • Technorati
  • Yahoo! Buzz
  • YahooMyWeb

nasma-khamisbcMwimbaji maarufu wa muziki wa mwambao(taarab) nchini Tanzania,Bi.Nasma Khamis Kidogo,amefariki dunia. Kwa mujibu wa gazeti la Habari Leo,Bi.Nasma alifariki dunia usiku wa kuamkia juzi kutokana na ugonjwa wa malaria. Vyombo vingine mbalimbali vya habari vimeripoti kwamba Bi.Nasma ameiaga dunia kutokana na ugonjwa wa moyo ambao umekuwa ukimsumbua kwa muda mrefu.

Kifo cha Nasma ni pigo kubwa kwa ulimwengu wa taarab.Ilikuwa ni Bi.Nasma na shoga yake Khadija Omar Kopa ambao waliifanya taarab kupendwa zaidi hususani walipoanzisha style iliyokuja kujulikana kote Afrika Mashariki kama “mipasho”. Hapo ndipo nyimbo zake kama Taarab Iko Huku na Salamu la Michelini zilipokuwa gumzo na kivutio cha kila sikio.

Mojawapo ya nyimbo zake ambazo pia zilipendwa ni ule ulioitwa Mwanamke Mazingira. Usikilize hapo chini..Pole kwa ndugu,jamaa,marafiki na wapenzi wote wa sanaa na muziki popote pale ulimwenguni.Pumzika Kwa Amani Bi.Nasma Khamis Kidogo!

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Share and Enjoy:
  • Digg
  • Sphinn
  • del.icio.us
  • Facebook
  • Mixx
  • Google Bookmarks
  • email
  • LinkedIn
  • Live
  • Spurl
  • Technorati
  • Yahoo! Buzz
  • YahooMyWeb

drremmyKwanza kabisa naomba msamaha kwa kutobandika “burudani yetu” ya zilipendwa kila ijumaa kwa takribani wiki mbili mfululizo.Nilikuwa nikibadilisha makazi kidogo.Ule mtaa niliokuwa nikikaa zamani nimehama! Ingawa haukuwa na mapaka yasiyoisha kulia lia kama alivyoimba Mwaruka katika wimbo wake Mtaa wa Saba, kuhama ilibidi.

Ni ijumaa tena.Kwa wale wanaoishi katika zile nchi zinazokuwa na majira maarufu ya “summer”, ni wakati mwingine wa kutoka nje,kuota jua na pia kutizama miili! Huu huwa ni wakati wa wazimu hususani kwa wenzetu wanaoitwa “weupe”(kuna mtu mweupe duniani?). Ukiwa na mambo ya mfadhaiko basi jikalie tu nyumbani mtu wangu.

Lakini hata sisi bongo tunayo majira yetu ya summer ingawa badala ya joto kali sisi huwa tuna kijiubaridi fulani hususani ile mikoa ya kaskazini na nyanda za juu kusini.Unajua tena,sisi tunachojali ni jina tu na wala sio hali halisi.Ukisema summer time tu kwetu inatosha.Usilete za kuleta.

Maneno pembeni,nyanyuka tucheze. Nani mwingine wa kutunyanyua vitini kucheza zaidi ya Dr.Remmy Ongala na Orchestra Matimila? Msikilize hapa akimlilia Mariamu wake katika wimbo Mariamu Wangu.Pata burudani.Wikiendi Njema.

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Share and Enjoy:
  • Digg
  • Sphinn
  • del.icio.us
  • Facebook
  • Mixx
  • Google Bookmarks
  • email
  • LinkedIn
  • Live
  • Spurl
  • Technorati
  • Yahoo! Buzz
  • YahooMyWeb

mandojo2

Miongoni mwa wanamuziki wa muziki wa kizazi kipya ambao wamefanikiwa kudumu na umoja wao kwa muda mrefu ni vijana wajulikanao kama Mandojo na Domokaya.Vijana hawa ambao pia wamewahi kutamba na vibao kadhaa ni mfano wa kuigwa linapokuja suala zima la “umoja wa wasanii”.

Hapa katikati walikuwa kimya kidogo kiasi kwamba baadhi ya watu,wakiwemo mashabiki na wanazi wa bongo fleva,wakatabiri kwamba huo ndio mwisho wa Mandojo na Domokaya katika anga za muziki.Walikosea.Hivi karibuni wametoa kibao kinachokwenda kwa jina la Boss/ Masimango wakiwa wamemshirikisha katika chorus mwanadada Maunda Zorro.Sikiliza kibao chao hapo chini.Bado wanaendelea kuweka mambo ya ‘banjo” katika miziki yao.

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Share and Enjoy:
  • Digg
  • Sphinn
  • del.icio.us
  • Facebook
  • Mixx
  • Google Bookmarks
  • email
  • LinkedIn
  • Live
  • Spurl
  • Technorati
  • Yahoo! Buzz
  • YahooMyWeb

Read the Next Page →

↑ Go Back to Top of Page