
Katika maisha ya kawaida utakuwa hujakosea kabisa ukiwaita “vijana”.Lakini katika game la muziki ambao leo hii tunauita wa kizazi kipya,unaweza kabisa kuwaitwa “wakongwe”.Wamekuwepo toka enzi zileee…na bado wapo.
Si unakumbuka enzi zile Mr.II alipoanza muziki? Nina maana enzi zile alipokuwa akiitwa 2 Proud kabla hajawa Mr.II mpaka kufikia hapa alipo hivi leo ambapo tunamuita Sugu. Si unakumbuka enzi za Nigga Jay ambaye leo hii tunamuita Prof.Jay? Enzi zile akiwa na washikaji zake ndani ya Hard Blasterz. Na si unakumbuka alipoanzia MwanaFalsafa ambaye leo ukisema Binamu kila mtu anakuelewa unamuongelea nani?
Naam vichwa hivyo ndio vilivyoshirikiana katika wimbo huu uitwa Nazeeka Sasa. Wimbo umetengenezwa na Producer Hermy B. Sikiliza ujumbe uliomo kisha utoe maoni yako.Pata burudani.
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.
Feedback / Comments
28 Responses to ““NAZEEKA SASA”-MwanaFA ft SUGU & PROF.JAY”
Leave a Reply


sending...
eeeeeehhh,haka kanyimbo ni balaa ndugu wananchi. hawa ni legends kweli sababu hata mashairi yao yamepangwa yakapangika,sio kama mashairi ya vijana wa siku hizi,unaweza ukasikia mtu anasema “baby” karibu nusu ya wimbo wote. Mwanafa kazi nzuri sana kaka pamoja na wenzako. na haka kakijana kalipewa tuzo ya uproducer bora tukahisi amependelewa lakini kusema ukweli hermy b is so talented and very creative. nafurahi kwa kazi zako nzuri sababu haujirudii kama wengine na karibu kila wimbo uliotoa unashika namba moja au kuwa gumzo miongoni mwetu. kazi nzuri hermy b tunategemea mengi zaidi kwako.
sasa kama kuna m2 anabisha kuhusu ivi vichwa!!! basi anachuki binafsi awa ni wakali wabongo jamani!!!!! nani anabisha?????¿¿¿¿¿¿
Duh hawa jamaa walikua wanasubiri nini siku zote???Maana hivi vichwa ni noma vyote!!!Ebwana bonge la colabo si la kitoto!!
imekaa poa hiyo
Tune limetulia sema inaonekana kama ni Diss kiaina….na Colabo limetulia kwani wote wakali, Ila naona jimbo liko kimaugomvi ugomvi tu
Ebwana nimelisikiliza tena ili tune, ucpme kwenye mziki mnee ni full Bang ebwana yani ivi vichwa vitatu vime smash mazima
(3HEADS SMASHER)
Duh Sugu jamaa walikua wanadhani umezeeka!!!Kumbe mzee bado unaongeza mzuka.Bado unakula kuku na M kwako kama book!!!Hahaha waambie mkuu!!!
Uwiii…FA ni zaidi ya mtambo!!!Huyu ni kaka mkubwa bwana msibishane wadogo zake!!!Kusoma hawajui basi hata picha jamani hawaoni??Nashangaa!!!Wanavaa saa na hajui kuisoma…Ni wa pumbavu haswaaa!!!Achana na Makenge kama kina Inspectar…Waone wajinga tu waliokubali kua nguruwe then wanaomba mabawa!!!Hhehee!!!Prof,mzee wa mitulinga;Mkali wa rymes!!!Walisahau kua uzi unafuata sindano hawo!!!Wakitaka kujua umuhimu wa matako na wajaribu kukalia kichwa tuwaone!!!
Hili fataki ni noma wazazi!!!Asiekubali akapimwe akili!!
Ni kweli hawa jamaa wanazeeka sasa,hawatanii..
hili dude ni la kisawasawa sana.watu wazima wameamua kufanya kweli naona,hongereni sana
duuuuuuuuuuuuuuuuuuuu,yani jamani wengine mlikaaa redioni mkawa mnabishana kua uyu dogo Hame B wamempendelea? we marco wewe, mi naona ubishi unaoleta ni kama unataka ngono gesti afu umesahau uume home. we lamar ndo ukacheze marede na makahaba wa kino. Bitz zako zinajirudia kila kukichaa. Dnt hate jamani,diz guyz wanafanya kazi. Ivi F.A c yupo nje amerekodi vp? teknolojia bwana. Jize umeipa nyimbo maisha kiukweli na supu yako ya dafu. F.A naona wimbo umehakikisha ni wako, u murdered the minits u got.BY th way kuna m2 anaitwa manecky anajiita produza, hebu nenda kaombe lebo kwa hame B kama msanii labda atakufundisha production. co mnakaa na mapimbi wenzako kina pingu na desso mnarekodi utumbo afu mnakibilia kushoot video mjilambe midomo kama warembo wa kike wakati ni pumba tupu.Kama mmeshindwa kufanya hii ki2, tengezeni vigari mtembeze tepu na cd. Shwine Nyie
Mimi sio mpinzani wala hater ila kawa wanajiona wanazeeka wakae pembeni au watafute shughuli nyingine ,kwa mfano producer sugu sikaoa marekani mwan fa vipi masomo jay kwanini usimpe nafasi black chata ,anyway nimesikiliza nyimbo yakawaida sana wanajisifia sijasikia ujumbe wa maana mafumbo ndio mengi ikuwapi watetezi wa wanyonge mimi nafikiri hiphop ni watetezi wa wanyonge na maisha thug ya mtaani sio mill kama buku nguruwe mabawa au matako kichwa ,my opinion i ddnt feelng this trak lakini labda ni mimi,mdau wa wanyonge
Whoever is the producer ni nomaaaaa. siamini mziki wa kibongo ukawa na quality hivi. i am so amazed. again whoever produced it amefanya kazi nzuri. I am going to put this in my playlist for a very longtime. Natamani sana kurudi nyumbani kwa kweli. I love this song.
E bwana uCPME M2 WNG C MCHEZO TRAK LIMESTAND
KINOMA FATHER ANGU! c UNAJUA SUGU HATA ASIPOIMBA DILI ZAKE NI MILLION NDO MAANA ANKWAMBIA MILLION KWAKE NI KAMA BUKU! C MCHEZO BABA! FA-BINAMU-B:UNATISHA BRO KAMUA
TU KAMA M2 ANAWEZA AKUDISS KAMA INSPECTOR NDO ATAJUA WHO IS THE DON? HEAVY WEIGHT MC
UNATISHA BABA! KWELI NI MA-LEGENDS KATIKA FANI….NA WEWE JONGO WANAVYOKWAMBIA WAMEZEEKA WANAMAANISHA WAMEKOMAA KTK FANI!
IT’S ME BOB SAMBEKE-YOUNG MILLIONAIRE
Safi watu wazima kazi nzuri sana, inapendeza kuteam up ili kuongeza ladha kwenye game wazee keep it up guyz
Eee bwana sasa mziki wa bongo unaelekea kwenye level nyingine, Hermy B hapo kichwa umekitumia haswaa ipasavyo, na hii colabo kweli si ya kitoto, FA, Jize na Sugu!!anaebisha lazima ni hater, nafikiri Mark hapo juu is one of them, if not basi hauelewi wimbo wenyewe, lakini kama kusoma huwezi hata picha huioni? Big up sana FA, they should hate you more cause unazidi kuwaacha mbali katika kila nyanja…..”pumbavu haswaaaaaaaa”
All has been said. Track imesimama yaani Hermy kanyonga Beat mbaya halafu hawa three legends wakakandamiza kiukweli. Mark u need to understand hip hop kabla ya kutoa such lame comments! Unaongelea RHYO na Jizze ni sawa na mtu una watoto darasa la tano na la saba na just coz wa la saba got brains unataka amuachie mwenzake? Sugu kuoa na habari hapa hazihusiani na this track.
Hip ni majigambo na mafumbo. Unatakiwa uwe mwerevu kuyafumbua maama hufumbiwa wajinga. Jicheki Mark uone kama u mjinga ama mwerevu. This z my fav track yaani been at it toka juzi..! Big up Homiez.
kibokooo
uuuuuuuuuuuuuuuuuwi! Vijana mmedinda!Hamjapotelea hewani kama dege la ufaransa!
duh!
hawa jamaa wametulia sana..ujumbe unaeleweka kabisaa kuwa wapo juu,wengine wanafuata..ninapoongelea wengine nina maana wote wasiokuwepo kwenye nyimbo hii! wao sio tu kwa kuimba bali pia ni wakongwe kabisa..anayebisha basi aangalie hata picha ,sio kwa kubadilisha majina tu bali picha pia zinasomeka vyema…for haters..keep on hating,once u hate,u make them think different way to change ur opinion so we will still have more good to come..aight!
Nawapa hongera wote Sugu, Mwana FA, Prof. J, na Hermy B kazi ni nzuri.
Muziki ni mchanganyiko wa ujumbe na melody. Haijalishi kama ni mafumbo,sifa au utetezi wa wanyonge vyote ni kheri mradi ujumbe unafika, unaeleweka na umepangangiliwa vizuri bila kashfa au matusi. Mimi sioni tatizo kuhusu wimbo huu, mashairi ni mazuri, vina vinamiminika na melody haichushi. Big up!
kwa nini hamkumshirikisha sister P??
ucpime kama unabisha kalia kichwa ndio utaona umuhimu wa makalio hahahhahahahaahha
mko juuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu
Hii ni fulanaz ya Michuzi.
da mzuka sana,track imesimmama sana…..!!ujumbe nmeukubali,ni wa wazee kimuzik ila bado wanashaini kwenye game.FA umepatia sana kuwapa shavu jizze for prof na sugu
wasanii wachanga mliheshimu game ‘hao ndo waliwashawishi baba zenu ili nanyi muimbe’
angalieni hamuwezi mkakwea mnazi ili mgeme SUPU,hahaa ni noma..!!
acyeipenda hii bila shaka naye ni mabana pua,hip 2 hipohop daima
download hii nyimbo bure http://www.shwari.com ,halafu
nenda ktk link ya download
ebwana cyo mchezo m kuwa bok.mr 2?
ivi prof jay ulikuwa unawajibu kikosi au?
KWELI MMEZEEKA, LAKINI BADO MPO. LOVE THE SONG.