twangabc1

Wanenguaji wa kike wa Twanga Pepeta wakiwajibika wakati wa uzinduzi wa Dar-es-salaam.

twanga2bc

Safu ya wanenguaji wa kiume wakiwa kazini.

Bendi maarufu ya muziki wa dansi nchini Tanzania, African Stars au maarufu kama Twanga Pepeta, majuzi walizindua albamu nyingine ambayo ni ya kumi tangu bendi hiyo ianze kuwapa burudani wapenzi wa muziki. Albamu hii wameipa jina Mwana-Dar-es-salaam. Sijajua kwanini wameipa jina hilo lakini nahisi ni kutokana na ukweli kwamba kwa muda sasa Twanga Pepeta wamekuwa wafalme wa burudani hususani jijini Dar-es-salaam yalipo makao yao makuu.Hongera Twanga Pepeta.

Lakini wakati albamu zinazinduliwa,muziki unakonga roho,watu wanaburudika yapo maswali ambayo baadhi ya watu wamekuwa wakiuliza. Tumeona nasi tuyalete hapa ili kama kawaida kila mtu atoe maoni au mapendekezo yake; Swali la kwanza ambalo lilianzia pale kwa Michuzi JR linauliza Eti Ni Kwanini Madensa Wengi wa Kibongo Wana Vitambi? Unaweza kusoma post hiyo na maoni yaliyotolewa kwa kubonyeza hapa. Kabla mada hiyo haijatulia msomaji wetu mmoja akatutumia e-mail akihoji kwanini wanenguaji wa kike huwa wanapenda kuvaa “nusu uchi” wakati wenzao wa kiume wakiwa wameficha karibu kila sehemu ya miili yao?

Kwa sababu tunaamini kwamba sisi hapa BC hatuwezi kuwa na majibu ya kutosheleza,hatuna budi kuomba msaada kutoka kwako msomaji.Unasemaje?Eti ni kwanini? Picha za hapo juu zikusaidie katika majibu.

Picha zote kwa hisani ya Charahani.

Feedback / Comments

10 Responses to “UZINDUZI WA TWANGA PEPETA + SWALI KWA JAMII”

  1. Comment by Gervas on June 8th, 2009 2:18 pm

    Maswali Rahisi kabisa;

    1: Ktk Jamii yetu Bongo Kitambi ni dalili ya afya, Pesa, Heshima kwa watu, nirahisi hata kupewa mkopo…hata mimi ninacho

    2: Wanenguaji wasipovaa nusu uchi, watu wachache wataingia kwenye shoo, Show hazitalipa tena, hata bia hazitanyweka sawasawa.

    3. Swali juu ya Swali:…Kwa nini wanapotaka kupata “miss” katika ngazi yeyote lazima kuna hatua apite amevaa “Bikini”/chupi tu? huwa majaji wanaangalia nini hapo? inamaana akivaa nguo inayofunika mwili hawatauona uzuri wake?

  2. Comment by obasitokumbo on June 8th, 2009 5:18 pm

    Ni uzazi wa kila leo jamani, halo halo teh teh!!

  3. Comment by mr degree on June 9th, 2009 1:50 am

    BC bwana ina maana hujui kuwa biashara matangazo?

  4. Comment by Sarah on June 9th, 2009 10:35 am

    Sasa mimi nauliza swali, hiyo biashara ni kwa wanawake na matangazo ni kwa wanawake tu au vipi? manake hii imekaje, wanaume wamevaa vizuri nguo za kujisiri hata vitambi vyao wamevificha.

  5. Comment by halima on June 9th, 2009 11:05 am

    Ni aibu kubwa sana kwa hawa wadada kutokana na mavazi yao, kwa mtazamo wangu hao wanenguaji wa kike wao wenyewe wanafurahia hayo mavazi coz hapo hakuna mtoto mdogo ambaye ameshikiwa fimbo au amelazimishwa kuvaa nusu uchi.

    Cheki hapo na hivyo vitambi vyao kama vya chibuku ovyoooooooo!!!!!!!!

  6. Comment by mtimkavubongo on June 9th, 2009 3:53 pm

    semeni ukweli wanawake wanatangaza biashara ndiyo maana wanavaa nusu uchi,kama wazaramo wasemavyo “wewe binti mbona unakalia uchumi hakuna kula hapa nyumbani kama hauleti chumvi” wenye akili wameisha jua, hata kuna msemo wa kizungu unasema “women have powers between their legs” lakini wanaume wanavaa nguo zinafunika mwili mzima maana wao ndiyo wateja wanunua biashara zinazotangazwa na wanawake yaani k

  7. Comment by oyo on June 10th, 2009 4:11 am

    Wabongo Bana Kweli M`mechoka kwanini msijadiliane mambo ya maana,Hizo ni evolution tu…Je dunia ingekuwa kama zamani ungesema nini sasa..wakati babu ya Babu yako anajifunika Mbele tu na mwili wote upo wazi….Kuhusu Vitambi ni michipsi Mixer Bia wanakula mazoezi hawana

  8. Comment by kindamba on June 14th, 2009 12:07 am

    hivyo vifreza ni vya beere na miviazi na mikuku

  9. Comment by MOECASH on June 19th, 2009 1:03 pm

    I recommend this ladies do some crunches.

  10. Comment by Jaffer on June 20th, 2009 10:57 am

    nitasema wanawake wavue nguo na kucheza na bikini kwasababu inaleta jambo le ku atttract watu na kunywa pombe freshi na wazidishe kitambi kwasababu ya kuitigisha no kuleta dumu asante. i love u

Leave a Reply