siscobc

Unapotaja jina la Balozi Cisco Mtiro bila shaka watu tisa kati ya kumi wanamtambua vyema. Hivi karibuni(kama inavyoonekana pichani) aliwakilisha hati zake za utambulisho wa kibalozi kwa Rais Gloria Aroyo wa Phillipines huko katika ikulu ya Phillipines jijini Manila.

Balozi Cisco Mtiro ndio mwakilishi(balozi) wetu katika nchi za Malaysia, Phillipines, Cambodia,Singapore na Laos.

Picha na habari kwa hisani ya Pius Mikongoti.

Feedback / Comments

9 Responses to “SIKU BALOZI CISCO MTIRO ALIPOWAKILISHA HATI ZAKE”

  1. Comment by Mickey Jones - Denmark on June 16th, 2009 12:36 pm

    “MHESHIMIWA ANAYESTAHIRI SIFA ZOTE”

    Ni kweli kabisa kama yaliyosemwa na BC mheshimiwa Cisco Mtiro kati ya watu kumi tisa watakuwa wanamjuwa.

    Hii inaonyesha aina ya uongozi tunaoutaka kwa viongozi wengine Tanzania,kuwa karibu na wananchi katika kufahamu haswa matatizo ya kila siku yanayotukabili na kutafuta uvumbuzi wa njia gani zitumike kutatua matatizo mbali mbali ya maisha magumu ya Watanzania.

    Mheshimiwa Cisco Mtiro analitumikia Taifa bila ya kujali maslahi ya kibinafsi,wala
    kutobadilika katika kuwa mtu wa watu wote toka nilipokuwa na umri wa miaka mitano katika makuzi yangu.

    Mheshimiwa Cisco Mtiro ni mheshimiwa kiongozi wa kuigwa asiyechoka kulitumikia Taifa kwa manufaa ya watanzania wote.

    Denmark

  2. Comment by mr degree on June 17th, 2009 5:20 am

    siku hizi havai hereni? kweli kabadilika!

  3. Comment by kanyelamomo on June 18th, 2009 1:04 pm

    mimi naona mnampa sifa asizostahili!

  4. Comment by Christabell on June 20th, 2009 2:54 pm

    sifa zake tumpe jamani. Anastahili sifa. Habari ya hereni na nyinginezo ni personal issues. Hakuna mkamilifu, Mimi na wewe pia tuna mapungufu yetu.

  5. Comment by xxx on June 21st, 2009 9:10 am

    Bongo jamani NO COMMENT ON THIS ONE..kasheshe

  6. Comment by mtimkavubongo on June 23rd, 2009 5:30 pm

    isipokuwa mama xxx, wengine ninaomba kutofautiana nanyi hasa hasa huyo jamaa anajihita, mickey jones wewe haujui kwa nini Sisco anajulikana ngoja tukueleze tunaojua sio kwa sababu ya uongozi-
    1)Historia inatukumbusha huyu jamaa aligombea ubunge wa Temeke mwaka 1995 dhidi ya Kiongozi anayestahili sifa alizopewa Sisco ndugu Agustino Mrema-,Sisco alikuwa mtoto wa mjini muuni tu, anavaa ereni masikioni, hata wakati wa kampeni serikali yote ilihamia Temeke ikiongozwa na Rais Mkapa, Mwinyi, katibu wakati ule Mangula lakini Bwana Mrema alimbwaga chini sasa kutokana na vituko vya marehemu Ditopile kipindi hicho alikuwa mkuu wa mkoa wa DSM alikuwa anasema Hallo Hallo ya Sisco?? magazeti yalimchoro hivyo sisco amevaa ereni huku dito ananyosha kidole juu akisema halo halo ya Sisco-huyu jamaa mkapa alimpa cheo kama fadhila tu ila sio kiongozi wala hajafanya lolote ni mtu wa mademu na starehe kwa sanaaaaaaaaaaaa, kama na huyu ni kiongozi ndiyo maana hatuendelei kabisa, huyu ni mtu kapewa ulaji tu

  7. Comment by jakize on June 26th, 2009 4:44 am

    kwani sisco pia si alishakuwa,mkuu wa walinzi wa mkuu wa nchi,yule aliyekuwa akionekana na Mkapa siku zote si yeye?

  8. Comment by xxx on June 30th, 2009 9:04 am

    Mtikavubongo naona mdogo wangu umefanya home work yako. Mie toka mwanzo nasema NO COMMENT KABISA JAMANI kweli bongo yetu kuna kazi..nadhani you all can read btn the lines why i say NO COMMENTS ON THIS ONE

  9. Comment by Bongo on September 12th, 2009 1:04 am

    kwa kweli insikitisha pale watu wanaporopoka kuhusu vitu wasivyo jua. Mh. Cisco ametumikia nchi yake zaidia ya miaka 20 katika kuwakilisha nchi yake nchi mbali mbali. Hizo habari za kuva hereni ni uzushi mtupu. Fanye uchunguzi halisi kabala ya kubwata ovyo.

Leave a Reply