“MARIAMU WANGU”-REMMY ONGALA & SUPER MATIMILA

drremmyKwanza kabisa naomba msamaha kwa kutobandika “burudani yetu” ya zilipendwa kila ijumaa kwa takribani wiki mbili mfululizo.Nilikuwa nikibadilisha makazi kidogo.Ule mtaa niliokuwa nikikaa zamani nimehama! Ingawa haukuwa na mapaka yasiyoisha kulia lia kama alivyoimba Mwaruka katika wimbo wake Mtaa wa Saba, kuhama ilibidi.

Ni ijumaa tena.Kwa wale wanaoishi katika zile nchi zinazokuwa na majira maarufu ya “summer”, ni wakati mwingine wa kutoka nje,kuota jua na pia kutizama miili! Huu huwa ni wakati wa wazimu hususani kwa wenzetu wanaoitwa “weupe”(kuna mtu mweupe duniani?). Ukiwa na mambo ya mfadhaiko basi jikalie tu nyumbani mtu wangu.

Lakini hata sisi bongo tunayo majira yetu ya summer ingawa badala ya joto kali sisi huwa tuna kijiubaridi fulani hususani ile mikoa ya kaskazini na nyanda za juu kusini.Unajua tena,sisi tunachojali ni jina tu na wala sio hali halisi.Ukisema summer time tu kwetu inatosha.Usilete za kuleta.

Maneno pembeni,nyanyuka tucheze. Nani mwingine wa kutunyanyua vitini kucheza zaidi ya Dr.Remmy Ongala na Orchestra Matimila? Msikilize hapa akimlilia Mariamu wake katika wimbo Mariamu Wangu.Pata burudani.Wikiendi Njema.

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Page 1 of 3 | Next page