Mwimbaji maarufu wa muziki wa mwambao(taarab) nchini Tanzania,Bi.Nasma Khamis Kidogo,amefariki dunia. Kwa mujibu wa gazeti la Habari Leo,Bi.Nasma alifariki dunia usiku wa kuamkia juzi kutokana na ugonjwa wa malaria. Vyombo vingine mbalimbali vya habari vimeripoti kwamba Bi.Nasma ameiaga dunia kutokana na ugonjwa wa moyo ambao umekuwa ukimsumbua kwa muda mrefu.
Kifo cha Nasma ni pigo kubwa kwa ulimwengu wa taarab.Ilikuwa ni Bi.Nasma na shoga yake Khadija Omar Kopa ambao waliifanya taarab kupendwa zaidi hususani walipoanzisha style iliyokuja kujulikana kote Afrika Mashariki kama “mipasho”. Hapo ndipo nyimbo zake kama Taarab Iko Huku na Salamu la Michelini zilipokuwa gumzo na kivutio cha kila sikio.
Mojawapo ya nyimbo zake ambazo pia zilipendwa ni ule ulioitwa Mwanamke Mazingira. Usikilize hapo chini..Pole kwa ndugu,jamaa,marafiki na wapenzi wote wa sanaa na muziki popote pale ulimwenguni.Pumzika Kwa Amani Bi.Nasma Khamis Kidogo!
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.
Page 1 of 3 | Next page