
Kwa mapana na marefu,jina la Hasheem Thabeet litatawala vichwa vya habari wiki hii.Swali au maswali ambayo wengi wanajiuliza ni je Hasheem Thabeet atajiunga na timu gani?
Mambo mengi yanasemwa kuhusu Hasheem.Wapo bado wanaoendelea kusema kwamba bado hayupo tayari kwa sababu alianza kucheza mpira wa kikapu “ukubwani’! Pamoja na hayo,wote wanaosema hivyo wanakubali pia kwamba Hasheem ataleta “impact” kubwa katika NBA.Wapo ambao wamefikia hata kumbeza kwamba hatoweza kutamba kama ilivyokuwa kwa Mzaire Dikembe Mutombo na badala ya yake atakuwa kama Msenegali Mouhamed Sene (Mo Sene) ambaye kimsingi hafanyi vizuri katika NBA kama alivyotarajiwa.
Waache waseme.Kwetu sisi muhimu ni kwamba kijana wetu atakuwa mtanzania wa kwanza kucheza katika NBA. Ni matumaini yetu kwamba Hasheem atafungua milango kwa wengine wengi ambao kupitia kwake wataamini kwamba “inawezekana”.Binafsi naamini Hasheem atafanya vizuri.Cha msingi ni kwamba ni lazima awe msikivu kwa makocha wake,wachezaji wenzake na daima azingatie mazoezi na kujiweka mbali kidogo na “mambo ya ujana”.
Watabiri wa mambo wanasema kuna uwezekano mkubwa kwamba Hasheem atajiunga na Memphis Grizzlies ingawa yeye mwenyewe inasemekana hangependelea sana.Je atajiunga na timu gani basi? ESPN wataonyesha zoezi hili. Tizama ratiba ya hapo ulipo.Kwa sasa mtazame Hasheem na wenzake ambao ndio “wapo juu” katika pick ya mwaka huu.
Feedback / Comments
4 Responses to “HASHEEM ATAJIUNGA NA TIMU GANI?”
Leave a Reply


Everything is possible Success or Failure
Its up to him to decide which direction he want to follow? Right side or Left side
Good luck Hasheem!
You Go Bwoooooooooooooooooooooooooooooyyyyy.
THATS MY HOME BOY,PROUD OF MAN .KAZINI KWANGU NAPATA HESHIMA KUBWA KWAJILI YA WA TZ WANAOFAHYA VIZURI HAPA US.U HAVE MY FULL SUPPORT.GOD BLESS TZ.MUCH LOVE TO MY FELLOW TZ ALL AROUND THE WORLD.
N kwanini watu wafananishwe wakati wana drive tofauti za mafanikio? Plus inategemea na wana timu wenzako wanakupokea vipi.Mana unyanyapaaji uko kila kona.Ni kustay focus na kustrive to be better and make loads of friends.
Love Lady Avon