
Subira huvuta heri.Ushaambiwa na ushasikia mtu mwingine akiambiwa. Kama hasikii huwa anaambiwa Haraka Haraka Haina…Sote tumekua tukiamini hivyo na kimsingi ni kweli kabisa kwamba subira huvuta kheri. Ndio maana kizazi hiki cha sasa kikaja na Mambo Mazuri Hayahitaji Haraka.
Lakini utajisikiaje pale unapogundua kwamba ulichokuwa ukikisubiria kumbe hakikuwa na thamani ya kusubiriwa? Utajisikiaje utakapogundua kwamba kumbe ulikuwa unachezewa shele? Wasikilize Banana Zorro na bendi yake nzima ya B-Band katika wimbo wao Zoba.
Binafsi nimeupenda wimbo huu sio tu kwa sababu ya ujumbe bali pia mapigo na mpangilio mzima wa vyombo nk.Hapa B-Band wamenikumbusha vizuri mapigo ya mwanamuziki mwingine mahiri hapa barani Afrika kutokea Zimbabwe(Oliver Mutukudzi). Loved it.
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Bila shaka umeshasoma katika vyombo mbalimbali vya habari(magazeti/blogs) au kusikia mitaani minong’ono kuhusu “mgogoro wa afya” ya mwanamuziki/muimbaji maarufu,Banza Stone “Mwana wa Masanja”. Wengine walishasema kwamba Banza “kavuta”.
Lakini je ni kweli kwamba Banza yupo hoi kitandani na kwamba anasumbuliwa na yale maradhi sugu? Banza ameongea na tovuti/blog ya Angalia Bongo na kuweka mambo wazi.Kasemaje?Bonyeza hapa usome mwenyewe.
Photo/Abdallah Mrisho.
Je imewahi kutokea ukahisi kukata tamaa ya kuishi kutokana na sababu mbalimbali za kimaisha? Yawezekana kabisa kwani huo ndio ukweli wa maisha.Kuna nyakati za furaha na kuna nyakati za kilio.Ndio maisha.
Ingawa maisha ndivyo yalivyo,siku zote tunashauriwa kutokukata tamaa.Tunaambiwa maisha ni mapambano na hivyo tuendelee kupambana daima. Mtu mmoja ameshawahi kuniambia kwamba katika dhambi kubwa ambazo binadamu anaweza kufanya hapa duniani,hakuna iliyozidi “kukata tamaa”.
Ujumbe kama huo hapo juu ndio uliomo katika wimbo mpya kutoka kwa Flora Mbasha. Ni wimbo wa ki-injili lakini ambao hauhitaji dini yeyote ili kupata ujumbe halisi uliomo.Wimbo unaitwa Usife Moyo. Karibu.
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Muziki ni lugha ya ulimwengu(universal language). Bila shaka umeshawahi kusikia msemo huo. Mimi binafsi nakubaliana kabisa na msemo huo. Kuna nyakati nimewahi hata kujiuliza,hivi dunia ingekuwaje kama kusingekuwa na muziki? Tunapokutana na kusheherekea tukio fulani,vigelegele na mayowe vingetosha?
Wakati kazi ya kubwa ya kutuletea burudani ya muziki inaanzia kwa msanii mwenyewe,pembeni yake, kwa miaka nenda rudi, amekuwepo mtu muhimu katika kukamilisha safari hiyo. Mtu huyo ni DJ au Deejay au Disco Jokey kwa wale wenzangu na mie tuliokula chumvi kidogo!
Mwanamuziki/Msanii anapomaliza kazi yake kwa kushirikiana na producer wake, hukimbilia kwa DJ kwani anatambua kabisa kwamba huyo ndiye kiungo kikuu kati yake na mashabiki au wapenzi wa muziki kwa ujumla.
Miongoni mwa DJs ambao sio tu wameifanya kazi yao kwa ustadi mkubwa bali pia waliowahi kujizolea sifa na mashabiki wa kutosha ni DJ John Dillinga Matlou au maarufu kama DJ JD. John ana historia ndefu katika muziki. Mwenyewe anasema,aliianza safari yake tangu akiwa mtoto kabisa. Mpaka hivi leo bado anaendelea kuwapa watu burudani. Hivi sasa anaendesha kampuni ya JD Entertainment ambayo inashughulika na masuala yote ya burudani,promotions na kadhalika.
Nilipofanya naye mahojiano ambayo utayasoma hivi punde,niligundua mambo kadhaa muhimu;DJ JD ni mbunifu wa aina yake. Aina za vipindi alivyovianzisha na kuviendesha(hususani redioni) ndivyo pengine vilivyochangia mafanikio ya baadhi ya vituo vya redio vya FM tunayoyaona hivi sasa.Pia niligundua kwamba huyu ni miongoni mwa wale DJs ambao wanaifanya kazi yao sio kwa ajili ya kutafuta pesa peke yake bali kwa sababu anaupenda muziki na yote yale yatokanayo na muziki mzuri wenye kuleta burudani na starehe.
Fuatana nami katika mahojiano haya ambapo,pamoja na mambo mengine,DJ JD anaelezea hisia zake kuhusu ulimwengu wa muziki na burudani hivi sasa. Pia anajibu swali ambalo wapenzi wengi wa muziki wamekuwa wakitaka kumsikia akijibu; Je yeye na DJ Bonny Luv ni mahasimu au ni watu wawili wanaoipenda kazi yao na pia kushirikiana kwa karibu? Je unajua kwamba baba mzazi wa DJ JD sio mtanzania bali raia wa…? Endelea kusoma
BC: Karibu sana ndani ya BC. Tunafurahi kupata fursa hii ya kufanya nawe mahojiano haya.Mambo vipi?
JD: Mambo sio mabaya kusema ukweli.Namshukuru Mungu.
BC: Kwa sababu hii ni mara yetu ya kwanza kufanya nawe mahojiano na kwa sababu tunatambua kiu ya wengi(hususani mashabiki wako) labda ungeanza kwa kutueleza kwa kifupi historia ya maisha yako.Ulizaliwa wapi,ukakulia wapi na mambo kama hayo. (more…)
Swali lililopo kwenye kichwa cha habari hapo juu si langu.Ni swali kutoka kwa Mwandishi Saleh Ally wa gazeti la Mwanaspoti. Ni swali lililobeba makala nzito ambayo inahoji na hapo hapo kujaribu kupata majibu kutoka kwa wakongwe mbalimbali wa muziki wa hip hop nchini Tanzania.
Saleh anaungana na wote ambao wamekuwa wakihoji ulipopotelea miziki ya hip hop iliyokuwa imesheheni ujumbe ambao bila shaka ulipatikana baada ya msanii kuitazama jamii kwa umakini ule uliofanya akaitwa “kioo cha jamii”. Badala yake,leo hii nyimbo ni kuhusu suala moja pekee; mapenzi. Karibuni kila nyimbo inayotoka ni kuhusu mapenzi na starehe ambazo kimsingi hazisaidii sana katika kujenga jamii.Ujumbe wa leo ni nimemuona demu,kapendeza,anavutia,ana figure matata,nikamtongoza,tukaenda kwenye sita kwa sita…mtamu,kwisha kazi. Matatizo ya kijamii au hata mafanikio ya kijamii, hayamulikwi tena kupitia muziki.Kwa bahati mbaya,hata vyombo vingi vya habari navyo vinayapa kisogo mambo mazito mazito ya kijamii. Tunamuachia nani?
Pamoja hayo,Saleh Ally,anamtaja mwanamuziki/mshairi Mrisho Mpoto(pichani) kama miongoni mwa wachache waliobakia ambao wanaimba vitu vya “kueleweka”.Unakubaliana naye? Kama hukubaliani naye,nini maoni yako kuhusu muziki wa kizazi kipya?
Ili kusoma makala nzima ya Saleh,bonyeza hapa.

Obama aliposhinda katika uchaguzi wa Marekani na hivyo kuwa Rais wa kwanza mweusi,wapo waliotabiri kwamba ushindi huo ni mwanzo mpya wa watu weusi duniani.Ni tumaini jipya.
Kama wewe ni miongoni mwa waliotabiri hivyo,bado unazo sababu za kuamini kwamba ulichokitabiri ni cha kweli.Hivi majuzi,huko Uingereza,kwa mara ya kwanza katika historia ya mashindano ya urembo ya nchi hiyo,taji limekwenda kwa binti mweusi aitwaye Rachel Christie(20) kama anavyoonekana hapo pichani.
Je unakubaliana kwamba huu ni mwanzo mpya wa watu weusi duniani? Well..hata kama Rachel hasomi hizi blogs zetu za lugha ya Kiswahili,sisi tunampongeza kwa hisani ya weusi wote wanaoishi huko Uingereza.Najua ndugu zetu wabongo mpo kwa wingi tu…Reading,London,Manchester,Milton Keynes na kwingineko.Yes You Can.

You are Invited to Join us for our 2nd Annual Summer Breeze BBQ in Chicago on Sat August 8th 2009 From 2pm til 8pm.
Lets Get Together, Hang Out With Friends, Eat, Drink, Play Games, Meet New People and Have Fun
Followed By Night Of Fun With The Best DJs from The Midwest Reppin FunkHouse Entertainment and Bongo Radio DJ Dennis and DJ Nasser. Best Party in Chi-Town, Dance Party Start at 10:30pm til 4am
BBQ Location
Montrose Harbor Beach
484 W Montrose Harbor Dr
(Montrose & The Lakefront at Lakeshore Dr)
Chicago, IL
Night Party Location
Caldwell’s Kitchen & Tap
7201 N. Caldwell Avenue
(between Gross Point Rd & Harts Rd)
Niles, IL 60714
(7mins away from Downtown Chicago)
KWA HABARI ZAIDI BONYEZA HAPA

Unamjua Dina Marios kama mtangazaji maarufu wa Clouds FM kupitia kipindi chake cha Leo Tena. Ambacho unaweza kuwa hukijui kuhusu Dina ni kwamba yeye pia ni blogger. Dina ana-blog kupitia www.dinamarios.blogspot.com. Ninachopenda kuhusu blog ya Dina ni topics mbalimbali ambazo anazirusha kila mara.Mtembelee ujionee mwenyewe kwa kubonyeza hapa.

Nimeshawahi kusema na leo nitarudia tena; Kama umekosa kabisa jambo au mambo yanayokufanya ujisikie furaha kuwa Mtanzania,basi angalau unaweza kupata ahueni unapoangalia jinsi ambavyo “demokrasia” ya nchi yetu imekuwa mfano wa kuigwa barani Afrika na hata sehemu mbalimbali za ulimwengu.Of course demokrasia yetu ina mapungufu mengi bado lakini ipi ambayo haina?Marekani au?
Mpaka leo,tangu Nyerere ang’atuke,hajatokea mtu akasema anataka kubadili katiba ili aendelee kutawala.Muda ukiisha mtu anaachia madaraka. Lakini kuachia madaraka haitoshi.Lipo suala zima la kuachia madaraka na pia kuendelea kushiriki katika shughuli mbalimbali za kitaifa na hata kimataifa kwa jina la Tanzania. Hali hii ni lazima ilindwe kwani ni wazi kwamba haitokei kama ajali.
Pichani ni Marais wetu,wastaafu Ally Hassan Mwinyi(mwisho kulia),Benjamini William Mkapa(mwisho kushoto) na Rais aliyepo madarakani hivi sasa,Jakaya Mrisho Kikwete(katikati). Kama unavyoona pichani wapo na wake zao au kina mama zetu wa kwanza waliostaafu na aliyepo kwenye uskani hivi sasa.
Sijui kama ni mimi tu ndio nimeona hili au vipi lakini nadhani mpangilio kidogo wa picha hii ulikwenda kombo.Sijui kwanini Mama Anna Mkapa ilibidi awe mbali vile na Mzee na pia Mama Sitti Mwinyi.Sijui.
Picha kwa hisani ya Bodi ya Utalii Tanzania



