
Bila shaka tunakubaliana kwamba ukiongelea wanamuziki waliowahi kutamba barani Afrika na duniani wakiliwakilisha bara la Afrika,huwezi kumuweka pembeni mwanamama Mbilia Bel kutoka DRC(zamani Zaire).
Hivi karibuni alikuwepo nchini Tanzania ambapo alipata nafasi ya kuwaburudisha ‘waheshimiwa” pale Dodoma katika viwanja vya Bunge.Naamini waheshimiwa waliburudika zaidi kwani lets face it wengi wao walikuwa vijana zaidi enzi Mbilia Bel alipokuwa akitikisa majukwaa kwa nyimbo zake motomoto kama vile Nadina, Nairobi nk. Unaweza kujikumbukusha kidogo wimbo Nadina kwa kubonyeza player hapo chini.
Pichani ni Mbilia Bel akilisakata rumba na Mheshimiwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania,Samweli Sitta.
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.
Photo/Jube Tranquilino
Feedback / Comments
9 Responses to “A DANCE WITH MR.SPEAKER”
Leave a Reply


Jamani huyu mbona hafanani na Bi nasma?
http://habarindiohiyo.blogspot.com/2009/06/mungu-ailaze-roho-ya-marehemu-mahali.html
wamemechisha rangi za nguo zao zimeendana sana
huo mkono wa spika sasa ulikua unaelekea wapi?
Huyu nae ndio walewale wanaothamini vitu vya watu na kudharau vya kwako.
Nasikia Spika Sitta alisimamisha Bunge kwa dakika fulani ili kuomboleza Kifo cha Michel Jackson ambae hajawahi kuchangia lolote Tz (zaidi ya kuidharau na kudai inanuka later kwa aibu akadai alikuwa analinda pua yake).
Wakati Bi Nasma Khamisi ni Muimbaji achilia mbali kuwa amefariki siku chache kabla ya King of Pop na ni maarfuru hapa tZ bali pia mama huyu ni Mtanzania na hakika ktk maisha yake mafupi alichangia mishahara ya Wabunge na huyo Sitta (kulipa kodi) lakini hakukuwa na kusimama ili kuomboleza kifo cha Mama yule.
Kuna Yule Kaimu Shekhe pia ni muhimu kwa jamii yetu ya Kitanzania lakini je Bunge lilisimamishwa kuomboleza kifo chake?
Ushabiki wa Wacko uachie huko nyumbani nakumbiz a starehe sio unaupeleka mpaka kwenye shughuli za Kitaifa.
Mbilia Bell na Mr Speaker wamependeza. Unaweza kusema wanacheza “Classic Dance”.
Ni “Classic”, kwa vile hata muziki unaopigwa sio wa kileo. Hii ndiyo maana inakuwa sio rahisi kwa vijana wa kizazi kipya tunaoandika maoni yetu hapa, kuzungumzia muziki, badala yake tunajikita kuzungumzia sura na mavazi ya wanaocheza hapo.
“Nadina”, ni moja ya nyimbo kubwa (Greatest Song), alizoimba Mbilia Belle. Ukiusikiliza kwa makini, utasikia maneno ya wimbo jinsi alivyotumia nahau na misemo mbalimbali ya kiswahili na ikiwa ni pamoja na maneno kutoka katika vitabu vitakatifu.
Mbali na maneno mzuri yaliyoimbwa katika wimbo huu wa “Nadina”, mpangilio wa vyombo ni wa hali ya juu. Mtu yeyote anaweza kuinuka kitini na kucheza kwa jinsi vyombo vinavyohamasisha mwilini.
Kwa vijana wa kisiku hizi japo wanajisikia kuhamasishwa kucheza, lakini hawana maneno ya kuchangia. Kwa sababu hawaelewi kinachosemwa katika wimbo.
Vivyo hivyo, watu wenye umri mkubwa, hawaelewi au hawaoni ndani katika miziki ya Bongo Fleva au ile miziki ya kufokafoka, inayopigwa na vijana wa kisiku hizi.
Je, ni miziki gani ita dumu kati ya miziki ya akina Mbilia Belle na wenzake na akina AY na wenzake?
Jibu la swali hili, litajibiwa na “WAKATI”. Baada ya miaka kadhaa kupita tutaona miziki itakayoendelea kusikilizwa na watu wengi.
Nawaomba tuchangie vitu vya kuendelezana, badala ya kuzungumzia mtu alivyovaa, au namna anavyocheza.
It’s Great To Be Black=Blackmannen
Jamani Dinah yaani spika alisimamisha Bungu ili kumuomboleza Michael Jackson?? Aisee mbona kuna watu wengi wa maana wamefariki je alifanya hivyo..mtu kama prof Haroub Osthman jamani very humble guy..kasheshe sana tena sana
Dada yangu Dinah na SisterTZ ninakubaliana na nyinyi ni muhimu tuweze kukumbatia mambo yetu, lakini lazima tuwe watu ambao tunaangalia mambo kwa upana wake,michael Jackison ni tofauti kabisa na watu wote ambao mmewataja ambao wametangulia, mungu waweke sehemu nzuri peponi.
Kwanza kwa watu waliosoma historia ya mtu mweusi katika dunia, ubaguzi wa rangi ulikuwa ni mkubwa sana ktk nyanja zote hata muziki-michael jackison ni mmoja wa mastaa wanaotuwakilisha watu weusi ingawa mazingira ya kibaguzi yalimpotosha mpaka akatumia mkorogo naomba tusiangalie udhaifu wa jackison, naomba niquote-baada ya kifo chake BBC na CNN walisema dunia nzima ilikuwa inaomboleza vituo vya terevision walisimamisha taratibu zao za kawaida na kutangaza kifo cha machael na hii haitokei kwa kila mtu- wapo wanasayansi wakubwa sana dunia wakifa dunia haishutuki,hata ktk nchi zao, lakini kutokana na taarifa toka BBC na CNN macheal jackison alifahamika dunia nzima mpaka kijijini kwangu kule ambako hakuna umeme mimi nilimjua huyu jamaa enzi hizo bado nachunga mbuzi na ng’ombe 1980s nikiwa primary-nilikuwa mshamba kinomaaaa, hivyo sishangai kuona spika ambaye ni mwanasheria na mwanahistoria anaelewa vizuri mchango wa macheal….Michael Jackison broke all barriers and his music transcends all racial barriers, the first black musician to enjoy white TV channels,
Kwa kweli sio sahihi kwa maoni yangu kulinganisha michael jackisoni na mtu kama marehemu prof Horoub Othman huyu ni mwalimu wangu lakini huyu alipata heshimu inayomstahili, wala ni kituko kumlinganisha michael jakison na Nasima Kidoga mama Taarabu, huyu hata alipokufa hata Tanzania haijashituka lakini kifo cha michael kilishitua mpaka vijijini(rejea BBC please google) wabongo wote mazungumzo yote ya wakubwa na wadogo yalimlenga micheal jackisoni kwa nini? kwa nini tusiwalaumu wabongo kwa kukumbatia jackison?
kwa kifupi, Kifo cha michael Jackison kilikuwa na sura ya kidunia hivyo speaker hajakosea kusimamisha bunge kumuenzi mfalme wa Pop Dunia, sio yeye tu aliyefanya hivyo ni dunia nzima kuanzia,Uingereza, china, Japani, Mexico, India mpaka Africa-Marekani ndiyo usiseme-
Kuhusu Mbili Abeli na speaker, pia huyu mama miziki yake kwa sisi vijana wa zamani tunaikumbuka sanaa, enzi za taburehei, wakati huo bongo flava haijazaliwa, sasa naweza elewa speaker alipata hisia gani halafu sioni kama ni sahihi kumlaumu speaker
Shame on them leaders! Michael Jackson hata hakuwa na interest na weusi wa africa, ivo tu focus kwenye yanayotuhusu na watu wanatuhusu.
Ivi ni Mbili abel au Shalamwana anapendaga kujifunua akimaliza kucheza, ni siku nyingi naanza kusahahu.
yaani Sita kasimama apo kama statue, i dont see him dancing! sijui yuko nervous au mtoto kamchengua, body language inajionyesha