MY TANZANIA   |   PLACES TO GO   |   MEDIA   |   ONLINE ENTERTAINMENT    

kikwete-libya

Hivyo ndivyo anavyoelekea kusema First Lady wa Tanzania,Mama Salma Kikwete alipokuwa akisalimiana na Rais wa Libya,Muamar Gaddafi hivi karibuni. Anayeshuhudia ni Rais wa Tanzania,Jakaya Mrisho Kikwete.

Rais Kikwete alikuwa nchini Libya kuhudhuria Mkutano wa 13 wa wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika.Rais Gaddafi ndiye Mwenyekiti wa umoja huo hivi sasa.

Share and Enjoy:
  • Digg
  • Sphinn
  • del.icio.us
  • Facebook
  • Mixx
  • Google Bookmarks
  • email
  • LinkedIn
  • Live
  • Spurl
  • Technorati
  • Yahoo! Buzz
  • YahooMyWeb

Feedback / Comments

10 Responses to “HELLO MR.GADDAFI”

  1. Comment by Gervas on July 3rd, 2009 4:06 pm

    Hapa huwa sielewi hasa hii mikutano ya Kilimo na chakula huwa wanajadili nini Maraisi hawa? jinsi ya kuomba misaada au? Maana kwa sasa Kilimo kiko mahututi Tanzania, vijana wachapakazi vijijini wameishia mjini kuwa “Machinga” sababu Mvua haziwasaidii, soko la mazao ya biashara bovu/halipo, wakibakia vijijini wanaishia kuwa walevi wa common, ulanzi, gongo, pingu nk. Je nani akalime kijijini? vikongwe? Sijui hata hayo Mabilioni ya kikwete au zile bilioni za EPA zilizowekwa ktk Benki ya wakulima zimesaidia lolote.

    Na hapo tunasema zaidi ya asilimia 70% ya uchumi wetu unategemea Kilimo. Viko wapi vyama vya Ushirika vilivoachwa na Nyerere? Viwanda vya Nguo km, Mwatex, Mutex nk vilivyonunua pamba na kutengeneza “Kaunguza” au Kaki zile tulishonea uniform za primary, Khanga, vimebaki magofu na wadau wanauza vyuma chakavu kwa sasa. Viwanda vya Ngozi vilitengeneza viatu mikoba nk. Kama vingekuwepo basi Tanzania ingetegemea soko la ndani kwa asilimia kubwa kulikoni kutegemea soko la nje ambalo saizi limeingiliwa virus.

    Fungu linalotengwa ktk bajeti kwa ajili ya wizara ya Kilimo sijui huwa nini hasa kinafanyika maana sioni kama wakulima kule vijijini wanapata msaada wowote toka wizarani. Utasikia misamiati mingi tu, bilioni kadhaa zilinunua pembejeo. Wachina wameichukua UFI- Ubungo, badala angalau watengeneze vitrekta simple vya kishikaji kwa ajili ya kilimo, wanazidi kuchonga majembe ya mkono, mapanga na mafyekeo. Gari moja analotumia JK au Pinda linaweza nunua msafara wa magari 12 mzima wa Waziri Mkuu wa India ambaye ndiye mkuu wa serikali. Sioni bado kama kuna dalili za Tanzania kujinasua hapa tulipo, ama ndo kauli ya Mramba kwamba hata kama wananchi watakula majani Jet ya raisi itanunualiwa? Na sasa Bajeti ya Safari za JK nje imeongezwa tokea Bilioni 80 hadi 115 …sijui hizi ndio priorities ???

  2. Comment by BLACKMANNEN on July 4th, 2009 10:06 pm

    Hali yako Mr. Gaddafi?

    Hiyo ni salaam ya kweli, kutoka kwa Mama Kikwete. Afrika, imebaki na viongozi wachachache sana wa kuheshimiwa na kuenziwa kama Gaddafi, Robet Mugabe na wengine wachache kutoka Kusini mwa Afrika na sehemu zingine chache za Afrika.

    Kwa miaka nenda rudi, wazungu wamekuwa na siasa za kuwaendesha viongozi wa Afrika kama kinyesi cha uharo, katika mambo mengi yahusyo nchi zao. Lakini Gaddafi na Mugabe, wameonyesha kuikaidi tabia ya aina hiyo na kwa namna fulani, wamefaulu kuwaadabisha wazungu, kwa tabia zao hizo.

    Kikwete ni mtu wa kuuma na kupuliza kama panya. Yumo na hayumo, hasa ukiangalia swala zima, la Bashir wa Sudan. Kikwete alipokuwa Mwenyekiti wa AU. Alilikwepa sana.

    Kikwete hakutaka kuendelea kuwa Mwenyekiti wa AU, kwa kipindi kirefu, kwa sababu hakutaka aeleweke kuwa ni mtu wa kuuma na kupuliza.

    Alimtwisha Gaddafi, kwa vile nchi yake ni tajiri na ina uwezo wa kuhimili mikikimikiki ya uchumi ya adhabu itolewayo na nchi za Magharibi kama mtu ama nchi, itakaidi matakwa ya wakubwa hao wa nchi za Wakubwa. Tanzania tumbo lake ni dogo.

    Gaddafi kafanya mambo mengi Afrika. Sasa katika hatua yake ya mwisho, kama kiongozi wa Libya na Mwenyekiti wa AU, anataka ni kuiona Afrika ikiwa nchi moja. Tumwone na tumwombee kwa Mwenyezi Mungu Ndoto yake hiyo ifanikiwe na sisi wale wote tunaotaka hilo, tushirikiane naye kwa hali na mali. Ili kufanikisha ndoto yake hiyo.

    Maana kuunganisha Black Africans kusini na kati ya Afrika, na Waarabu Kaskazini mwa Afrika sio swala la utani, ni kazi hasa.

    Hapo hapo nchi za Magharibi zikibeza Mwungano wa Afrika, kwa kutumia propaganda zao kupitia network zao za vyombo vya habari barani Afrika.

    Sio jambo rahisi, ni gumu sana. Ndiyo maana watu wengi wanamtukana Robert Mugabe, bila kuelewa sababu. Wengi wanadhani ni mlafi wa madaraka, kumbe sio hivyo, anatetea watu wake, na haki itendeke katika nchi yake katika mgawanyo wa ardhi kati ya Wazimbabwe wazungu na Wazimbabwe weusi.

    Vyombo vya habari vya wakubwa, vinapotosha ukweli, na kuelekeza kumkashifu, ili achukiwe na jamii yote ya Afrika na duniani kote. Wewe unayesoma habari hizi, najua, humpendi Robert Mugabe, bila wewe kujijua ni kwa nini?

    It’s Great To Be Black=Blackmannen

  3. Comment by mr degree on July 8th, 2009 4:35 am

    teh! teh!It’s Great To Be Black! haya chukua tano!

  4. Comment by Mwanamke wa Shoka (UK) on July 8th, 2009 5:22 am

    Gervas na Blackmannen nawapa tano….put ypur feet up and chill-out….lol

  5. Comment by rasto on July 8th, 2009 6:06 pm

    mr BLACKMANNEN:utaunga mkono vipi hawa marais.hawa ni madikteta tu wanaoendesha siasa mbovu isiyowafaidi wananchi wake.nchi zetu za kiafrika ni baadhi tu ya nchi zinazoendelea.tunahitaji msaada wa hali na mali kutoka kwa hao wazungu unaowaponda.tazama zimbabwe kwa sasa inavyoangamia.shida chungu tele.na huyo gadafi je kama angekuwa mzalendo mbona kaficha mamilioni ya dola katika benki za uswisi.ah.. ndugu yangu inauma sana hali kama hii huku afrika wau wanafariki kwa kukosa chakula

  6. Comment by Amina on July 9th, 2009 11:05 am

    Hivi hizi safari za JK za kila kukicha zina faida kwa watanzania au ndo kuhakikisha anaimaliza dunia kabla hajastaafu? Mana baba huyu, hatulii nyumbani, (zipo safari zenye faida hilo nalielewa) ila nadhani nyingine ni kuzurura tu! Na watanzania hatuna desturi ya kuhoji kama wenzetu, kwamba safari flani ina umuhimu wa kwenda? na je tutegemee nini? nini matunda yake? otherwise ni kupoteza kodi za wananchi…

  7. Comment by Gervas on July 9th, 2009 1:25 pm

    Mwanamke wa Shoka Asante,Mimi huwa najiuliza maswali mengi, kwanini nchi za Afrika nyingi ni maskini na nchi nyingi za bara la Asia zinauaga umaskini?…Bajeti za Afika zinatumia pesa nyingi kununua siraha,mabomu (yaliyolipuka mbagala) nk, na wazungu wanawekeza viwanda vingi vya pombe Afrika. Kuna nini hapa? Swala la Rada nk.
    Amina…Jk kala miguu ya kuku na muda wake unaisha bila bila. Nafikiri wakati umefika watanzania tuachane na maswala ya kuchagua chama, bali tuchague sera, mgombea yupi ana sera tamu, lakini ili kufika huko bado elimu inahitajika. Kwanini ada za vyuo vikuu (vya serikali) iko juu namna hii? Pesa za mikopo zitolewazo kwanini zisitumike kupunguza ada ili kila mtoto wa masikini afike huko? wingi wa vyuo vikuu hauna maana km bei zake ziko juu.

  8. Comment by mtimkavubongo on July 9th, 2009 6:11 pm

    ninakubaliana na hoja za wengi hapo juu, lakini mimi bado nazidi kuamini kuwa sisi ktk bara la Africa tuna bahati mbaya hatuna viongozi wa kweli wengi wao bado wameshindwa kutusaidia. natumia english kuonyesha msisitizo, the vast majority of Africa leaders have failed us,do not expect anything from the current African leaders,may be the next generation, ndiyo maana JK kaamua yeye kula miguu ya jogoo kila kukicha ratiba yake ni safari, akienda kwenye halmashauri mbili ujue kesho yake ni safari.

    Mimi swala la kukaa kulaumu wazungu, wakoloni, benki ya dunia na media ya nje, nalo ninaliona sasa limepitwa na wakati nimesikia wimbo huu tokea primary enzi hizo 1980s mpaka leo ninawatoto wanakaribia kuingia university wimbo ni ule ule. Ukweli ni kwamba karibia viongozi wote wa Africa wamesoma sana na wanaelimu ya chuo kikuu na wengine wamesoma vyuo vikuu vikubwa duniani wanajua madhara ya ubepari lakini mbona hao hao viongozi ndiyo wezi, wala rushwa na hawataki democrasia ya kweli, kiini cha matatizo ya Africa hakuna viongozi wa kweli tofauti na viongozi wa nchi nyingine kama China, India, America na Europe. sisi sanaa nyingi tu kazi kulaumu wazungu tuu.

    Mugabe na Gadafi mimi ninawakubali maana Africa kote hakuna Demokrasia ya kweli hata Tanzania hakuna maana ripoti kibao zinaonyesha CUF wanashinda zanzibar na hawapewi uongozi, halafu wizi wa kura wakati wa uchaguzi ni kitu cha kawaida bongo, Kheli ya huyo mnaye muita dikteita Ghadafi kwa kuwa wazungu wamekukaririsha hivyo lakini ukweli ni kwamba maisha ya watu Libya ni mazuri sana kuliko bongo wakati Libya haipokei misaada kama Tz ambayo ni Darling wa Donors.

    JK punguza safari waziri wako wa mambo ya nje kazi yake nini? JK punguza mashangingi na magari ya serikali? Jk acha kuimba kilimo kama sera ya kutokea uchaguzi mwakani bali tekeleza kwa vitendo pesa za safari zako na mashangingi nunua matrekta na pembe jeo halafu jenga viwanda vya kusindika nafaka na matunda.
    Africa ni kaziiiiiiiiiiiiiii

  9. Comment by BLACKMANNEN on July 10th, 2009 7:02 pm

    Ndugu zanguni jipendeni na kujithamini wenyewe, msisubiri kupendwa au kuthaminiwa na watu wengine.

    Wafrika wengi wanapenda sana kupenda na kuthamini mambo ya wazungu na kuyadharau ya kwao na kuyaona ya kishenzi.

    Ian Smith (Rhodesia=Zimbabwe), John Foster (South Africa), Pinochet (Chile) na Margareth Thatcher (UK) na hata George Bush (USA), wamefanya mambo mengi ya kishenzi, kuliko ushenzi wetu sisi.

    Viongozi hawa, wameua watu wengi wasiokuwa na hatia, na hakuna hata mmoja kati yao, aliyetakiwa kukamatwa na kupelekwa mbele ya sheria ya Kimataifa kujibu mashitaka ya mauaji ya watu katika Mahakama ya Kimataifa.

    Hawa wakubwa wanapoua watu maskini, Afrika na kwingineko, hawaonekani kuwa wanafanya makosa ya jinai, kwao wanaonekana ni sawa kama sisi tunavyoua panya waharibifu, wasiotetewa hata na Wanaharakati wa Kutetea Haki za Wanyama. Inaonekana kuwa ni sawa tu.

    Mahakama hizi zinazoitwa za Kimataifa kiukweli ni kwa ajili yetu sisi wanyonge. Lakini kwa vile sisi tunapenda sana vya wenzetu (Wazungu), wala hatufikirii kuhoji kuwepo kwake na mwenendo wa kesi zinazoendeshwa huko The Hague.

    Katika kuthibitisha usemi wangu kuwa sisi tunathamini vya wazungu kuliko vyetu. Mimi mwenyewe nimeona jinsi watu wanavyojidharaulisha, kwa mtu kukubali kupewa kazi ya kumhudumia mzee wa kizungu kumbadilisha nguo zake za ndani akijisaidia, na mengine mengi.

    Wakati mtu wetu huyu huyu, akipewa kazi ya aina hiyo Tanzania na mshahara ulio sawa na anaopewa na wazungu, hatakubali kufanya kazi hiyo. Tena atakuona umemdharau sana na kumdhalilisha.

    Watu na elimu zao za Vyuo Vikuu, wanafanyakazi za aina hizo na zingine zisivyofanana na viwango vyao vya elimu, ilimradi kapata kazi Ughaibuni.

    Kama kazi ni kazi, mbona sisi hatujaona mzungu akifagia barabara zetu? Mbona sijaona mzungu kaajiriwa na msukuma kuchunga ng’ombe?

    Vichwa vyetu hivi, tumepewa kutumia kufikiria, sio kubeba nywele na kuonyesha mitindo mbalimbali ya kusuka au kunyoa. Tutumie vichwa vyetu hivi, kufikiria mambo ya maana, badala kupoteza wakati mwingi kwa kudodosa safari za Kikwete nchi za nje.

    Wewe mwenyewe kwanza, jiulize hapo ulipo unafanya nini kwa faida ya Watanzania?

    This Is Black=Blackmannen

  10. Comment by kilo on July 12th, 2009 12:59 am

    Hapo umeongea !! nakubaliana nawe kabisa .

Leave a Reply