Kama unaishi katika dunia hii hii tuijuayo sote,basi bila shaka umeshawahi kusikia kuhusu ugomvi kati ya mke wa kaka na dada zake kaka.Kwa maneno mengine ugomvi kati ya fulani na wifi yake au wifi yao.Mimi nimeshawahi kusikia na pia kuona mtu na wifi yake ambao hawapikiki chungu kimoja.Kila kukicha “kesi za ukoo” zilikuwa haziishi.Amani hakuna,kila mmoja anadai kuwa malikia wa boma.
Je ni kwanini huwa kunatokea ugomvi ugomvi hivi kati ya mtu na wifi yake au wifi zake?(sio wote lakini.Wapo mtu na wifi yake au zake wanaoiva kupita maelezo) Hili swali pengine limeshaulizwa mara milioni kidogo na bado majibu yasipatikane.Tunaweza kujaribu kutafuta majibu mapya kama tunataka.Mimi sitochangia.Sijui.
Pamoja na hayo, miaka kadhaa iliyopita bendi ya Vijana Jazz walijaribu kulijibu swali hilo katika kibao chao maarufu kilichoitwa Wifi Zangu. Aliyeongoza mashambulizi alikuwa mwanadada Kida Waziri.Nakumbuka kuwaona Vijana Jazz wakiuliza swali hili pale katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro enzi hizo.Kwa kweli ilikuwa ni burudani ya aina yake.
Nakuomba usikilize kibao hiki kisha,baada ya burudani, tafakari kisha jaribu kutupa majibu yako.Kwanini unadhani huwa sometimes inatokea rabsha kati ya mtu na wifi yake?Nani alaumiwe?Nakutakia weekend njema.
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.
** Wimbo huu sio original.Ni remake tu.Pata burudani.
Feedback / Comments
4 Responses to ““WIFI ZANGU”-VIJANA JAZZ(RE-MAKE)”
Leave a Reply


enzi hizo ukipigwa picha lazima uonyeshe meno! ama kweli tumetoka mbali!
Mr degree umenikumbusha mbali usisahau mpiga picha anakwambia sema NDIZI, ilimeno yaonekane vizuri. hahahahahaha
halafu namuona kitine hapo! kumbe nae kapitia vijana jazz? pia yupo na rashidi pembe wapili kutoka kulia waliosimaa.huyo mzee keshastaafu muziki tulikua tunakaae nae karibu ni kiongozi wa muda mrefu wa hiyo bendi! wengine siwajui, bc tusaidie!
sauti ya akida waziri au siyo.hii bendi ilisambaratika ama bado ipo.maana haisikiki siku hizi