Huwezi kuthubutu kuzungumzia muziki wa kizazi kipya au Bongo Flava kama unavyojulikana kote ulimwenguni bila kumzungumzia na kumuhusisha moja kwa moja na muziki huo,Joseph Mbilinyi(pichani) ambaye kisanii tulianza kwa kumjua kama 2 Proud kabla hatujamuita Mr.II na baadaye Sugu.
Sugu sio tu alichangia kuipa Bongo Fleva utambulisho rasmi katika jamii,bali pia ni miongoni mwa wasanii “waasisi” walioamua kwa makusudi kuanza kutumia lugha ya Kiswahili katika kughani(rap) huku wakiwa na ujumbe ambao uligusa jamii inayowazunguka badala ya ile ya kusimuliwa au kuona katika luninga.Ukipenda unaweza kumwita “mwanamapinduzi”.
Hivi karibuni tulipata nafasi ya kufanya naye mahojiano.Katika mahojiano haya Sugu anabainisha mambo kibao yakiwemo masuala kama vile alipo na anachokifanya ,ushauri wake kwa wasanii wenzake katika masuala ya haki zao nk.Pia Sugu anajibu swali ambalo wengi wanaliogopa;je muziki wa bongo fleva uko katika njia sahihi?Kuna tofauti gani katika muziki huu tangu walipoanza na walipo hivi sasa?
Kubwa ya yote ni kwamba Sugu ameamua kuwapa zawadi maalumu mashabiki wake. Anakuja na albamu mpya! Ukisoma mahojiano haya mpaka mwisho utaweza kusikiliza single mpya kutoka kwake inayokwenda kwa jina Kambarage.
BC: Sugu, Karibu sana ndani ya BC.Mambo vipi?
SUGU: Asante sana mkuu.Nimeshakaribia kaka.
BC: Kwanza kabisa wapenzi wengi wa muziki wamekuwa wakituandikia wakitaka kujua ulipo na unachokifanya hivi sasa.
SUGU: Asante. Mimi kwa sasa nipo nchini Marekani. Naendelea na mitikasi ya maisha kama kawaida zikiwemo harakati zangu za muziki.
BC: Unaheshimika miongoni mwa wengi kama miongoni mwa “waasisi” wa muziki ambao leo unaitwa Bongo Fleva au muziki wa kizazi kipya.Wewe pia ni miongoni mwa wasanii wa mwanzo kabisa kuamua kurap kwa kutumia lugha ya Kiswahili moja kwa moja. Nini unadhani kilichangia uamuzi kama huo? Na je leo hii unadhani Bongo Fleva bado ipo katika muelekeo ule ule mliokuwa nao mlipoanza au kumekuwepo na muelekeo tofauti?
SUGU: Mimi nadhani sisi tuliamua kurap kwa Kiswahili ili kuweza kuwasiliana na mashabiki moja kwa moja kwa kutumia lugha ambayo wanaielewa. Nia yetu ilikuwa kufikisha ujumbe kwa watu na jamii yetu ambayo Kiswahili ndio lugha yake ya msingi.
Baada ya uamuzi ule kwa kweli hata sapoti iliongezeka sana na hivyo muziki wetu ukazidi kukua.Hiyo inatokana na ukweli kwamba watu sasa wakawa wana-sapoti kitu ambacho wakikielewa moja kwa moja tofauti na pale tulipokuwa tukitumia lugha za kigeni kama vile kiingereza.
Kuhusu kipande cha pili cha swali kwamba naonaje game kwa sasa; Nilikuwa Bongo hivi karibuni na ndio kwanza nimerejea kutoka huko.Kwa kweli muziki wetu unahitaji “overhaul” kubwa hasa kwa upande wa kibiashara. Bado kuna vilio vilio kutoka kwa wasanii. Wasanii wote niliokutana nao kilio chao kilikuwa ni hicho. Na hapa naweza kusema nilikutana kwa asilimia kubwa na wasanii wote muhimu na wanaotamba.
Na kwa upande wa sanaa yenyewe pia kunahitajika mabadiliko makubwa.Wasanii wengi wamesahau au pengine hawajui misingi iliyoujenga muziki huu. Misingi ya muziki huu ilikuwa ni kuwakilisha maisha ya jamii kwa kupitia kwenye muziki. Huu muziki ulikuwa ni kama Bunge la kitaa ambalo liliwakilisha sauti za umma. Lakini hapa katikati naona tulipotea kidogo. Wasanii wengi wanarap au kuimba vitu ambavyo hata wao wenyewe hawavijui. Sasa hapo kidogo pana tatizo. Nadhani tulifikia mahali ambapo,kama wasanii, tumefanya kosa la kuuutenganisha muziki na jamii wakati muziki wetu msingi wake ni jamii.Hilo ni kosa ambalo ni lazima lirekebishwe mara moja ili muziki huu uendelee kutamba.
BC: Nakubaliana kabisa na wewe. Sasa tukiwa bado kwenye suala hilo hilo la uhusiano wa jamii na muziki; Kwa wengi unafahamika kama “sauti ya watu” wakimaanisha kwamba umekuwa,kwa kupitia nyimbo zako,ukisema unachojisikia kusema au kuwasemea wale ambao pengine wasingeweza kusema. Ujasiri huo unaupata wapi au ni kitu gani kinakusukuma?
SUGU: Kwanza kabisa asante sana kwa compliment ya kuniita “sauti ya watu” kwani naamini kabisa kwamba hiyo ni sifa nzuri. Ujasiri wa kusema ninachojisikia unatokana na kuamini kwenye ukweli. Ukisimama na ukweli daima utadumu na ndio maana bado tupo bila kujalisha kama tuna track mpya hewani au hatuna. Hatutoki masikioni,midomoni na kwenye vichwa vya watu. Watu wote wanapenda na kuheshimu ukweli.
BC: Kwa muda sasa umekuwa kimya kwa upande wa kufyatua albamu na mambo kama hayo. Pamoja na hayo umekuwa ukiendeleza(kwa kupitia kampuni yako ya Deiwaka Entertainment) harakati mbalimbali za kuwasaidia wasanii wenzako hususani wale chipukizi katika kuhakikisha kwamba wanapata haki ya jasho lao na pia wanaendelea kufanya muziki ambao utadumisha heshima ya Bongo Fleva. Harakati hizo zinakwendaje? Nini mipango iliyopo hivi sasa katika kuendeleza harakati hizo?
SUGU: Ni kweli kwamba nimekuwa kimya kwa muda mrefu kiasi. Albamu yangu ya mwisho “Ujio wa Umri” niliitoa miaka mitatu iliyopita yaani mwaka 2006. Hii imetokana na majukumu kuongezeka hasa baada ya kuamua kuhamishia harakati zangu hapa Marekani. Pamoja na hayo,kama ulivyogusia, harakati za kupigania maendeleo ya huu muziki zinaendelea tena kwa ari mpya na nguvu mpya kuliko ile ya JK na maendeleo ya Bongo!
Katika mipango iliyopo mezani kwa sasa ni pamoja na kufungua radio station pale Dar-es-salaam ambayo itakuwa inapiga muziki wa rap/bongo flava pekee. Tumeshaanza kufukuzia taratibu za kibali kwa hili.Mimi naamini bongo fleva ina ufuasi mkubwa kwenye jamii ya watanzania na hivyo inastahili kabisa kuwa na radio yake. Hoja yangu hapa ni kwamba jamii ya chuo kikuu Mlimani ina radio yake,hata jamii ya kanisa la Mama Lwakatare na kanisa lake ina radio yake…sasa kwanini Bongo Fleva ambayo mimi naamini ina kundi kubwa tu la wafuasi kuliko hawa wengine wote isiwe na redio yake ambayo itasaidia kuongeza nguvu za maendeleo yake? Naamini pia kwamba kituo cha redio kama hicho kitasaidia kuongeza nguvu na mapambano dhidi ya ukosefu wa ajira hususani miongoni mwa vijana aidha directly or indirectly.
BC: Tukiwa bado kwenye suala hilo hilo la haki ya msanii na ingawa kwa kiasi fulani umeshazungumzia suala hili hapo juu, bado ningependa kukuuliza; wewe mwenyewe ulipitia changamoto gani wakati ulipoanza muziki? Na je leo hii unadhani mambo ni mazuri kidogo katika kuhakikisha kwamba msanii analipwa vizuri kutokana na kazi yake?
SUGU: Matatizo na changamoto nilizopitia mimi na wasanii wengine wa zamani ni nyingi mno ukilinganisha na sasa. Hapo katikati mambo yalianza kuwa poa mpaka tukaanza kujisahau. Lakini kama nilivyoeleza hapo juu, kwa sasa hali imekuwa ngumu tena na ndio maana kuna vilio vingi kutoka kwa wasanii kuhusu suala hili hili. Hali kibiashara imekuwa ngumu. Leo tunasoma mitandaoni kwamba hata wasanii wenye majina makubwa kama vile TID anapata tatizo la kuingiza albamu yake mpya sokoni! Na sio yeye tu,kuna wasanii kibao ninaowajua wana albamu ambazo zimeshakamilika lakini wanabaki nazo gheto tu wakizisikiliza na washkaji zao!
Na hata upande wa maonyesho nako pia kuna tatizo. Nilisikitika kuwa Bongo wakati wa sikukuu ya Pasaka hakukuwa na show yoyote ya maana ya Bongo Fleva mahali kama jijini Dar jambo ambalo ni tofauti na hapo miaka ya katikati kidogo. Ukiangalia kwa makini mambo kama hayo ndio utajua kwamba game lina tatizo na inahitajika mikakati ya haraka na makusudi ili kurudisha mzuka uliopotea.
BC:Kama zilivyo aina zingine za sanaa,muziki wa Bongo Flava umekuwa ukipitia vipindi mbalimbali.Kuna wakati huwa kama unataka kupotea vile na kisha ghafla unarejea tena.Unaposhuka lawama mbalimbali huelekezwa kwa watu mbalimbali wakiwemo DJs wanaochukua “kitu kidogo” na kupiga hewani wimbo wowote,Producers wanaokubali kumuingiza mtu studio hata kama anaonekana wazi kwamba hana kipaji,promoters uchwara nk.Kwa mtizamo na uzoefu wako, unadhani nani miongoni mwa watu niliowataja hapo juu anastahili lawama zaidi linapokuja suala zima la kushuka kwa muziki kwa ujumla?
SUGU: Mimi naona wote uliowataja hapo juu wanastahili lawama. Na pia lawama za ziada zinakwenda kwa watu wa idara za masoko kwenye makampuni yanayotoa udhamini kwa shughuli au matukio mbalimbali pale bongo. Hawa wangekuwa na moyo wa ku-sapoti projects za baadhi ya wasanii wenye “akili” na ubunifu moja kwa moja ingesaidia sana kuliko wao wanavyofanya hivi sasa yaani kutoa udhamini kwa makampuni hayo hayo kila wakati bila kuzingatia kwamba makampuni hayo yanaishiwa au kupungukiwa ubunifu kwa kiasi gani.
Isitoshe haya makampuni wanayoyapa udhamini kila siku ni ya wafanyabiashara wanaoangalia faida zaidi kuliko sanaa.
BC: Sugu wewe umesafiri sana katika sehemu mbalimbali za ulimwengu kutokana na kazi zako za muziki.Ni wazi kwamba katika safari zako umekutana na wanamuziki wengine wengi.Umejifunza mambo gani ya msingi ambayo ungependa labda ku-share na wanamuziki wanaochipukia hivi leo?
SUGU: La msingi nililojifunza ni kuwa katika lolote unalolifanya kwanza weka mapenzi ndani yake.Ukishaweka mapenzi ndani ya sanaa,utaifanya kwa dhati na vizuri.Matokeo yake ni kwamba hela itakuja tu maana kizuri chajiuza…
BC: Umekuwa mstari wa mbele kupinga kitu kinachoitwa “beef” miongoni mwa wasanii.Unadhani nini chanzo cha beef na unadhani zinachangia kwa kiasi gani kushusha thamani ya muziki au kubadili mtazamo wa wanajamii kwa muziki wa Bongo Fleva? Unatoa ushauri gani?
SUGU: Kweli mimi sipendi beef baina ya wasanii kwani naamini beef zinachangia kupoteza malengo ya wasanii na kuwaondolea uwezo wa kuungana na kupambana na adui zao wa kweli wanaosababisha muziki usizidi kusonga mbele.
Nadhani chanzo cha beef ni wivu tu wa maendeleo baina ya wasanii.Hamna cha zaidi.Hapo ndipo tunaposema usimchukie mchezaji bali chukia mchezo wenyewe ulivyo kama vipi!
BC: Najua kwamba ulipoanza muziki ulikuwa unavutiwa na wasanii wa kimataifa kama vile Ice Cube,NWA,2Pac Shakur na wengine.Leo hii ni wanamuziki gani wanaokuvutia zaidi?
SUGU: Kweli unanijua kaka!…anyway mpaka leo Pac anabaki kuwa juu kabisa kwenye list.Lakini pia kwa sasa mimi ni mshabiki na mfuasi mkubwa wa Jigga.Alichokifanya Hova ndani ya muziki huu na hata nje ya muziki ni soo kwa kweli.Wewe unajua kuhusu hili.
Kwa nyumbani nakubali harakati za washkaji kadhaa akiwemo Ngwea,Professor Jay,Joh Makini na FA.
BC: Najua kwamba ulishatangaza kustaafu.Pamoja na hayo,nijuavyo mimi msanii huwa hastaafu bali anapumzika tu.Sasa je nini mipango yako kisanii hivi sasa? Je mashabiki wako wategemee kitu kama albamu nyingine kutoka kwako?
SUGU: Yeah nilitangaza kustaafu mwaka 2002 na nikarudi kwa kishindo mwaka 2004.Hii ni miaka mitano sasa iliyopita! Ni kweli ni vigumu sana kwa msanii kuacha game hasa kwenye game la hip hop ambalo utamu wake uko kwenye wasanii kupeana “challenges’ kimistari na vitu kama hivyo.
Lakini hakuna kitu kisichokuwa na mwisho.Kadri majukumu ya maisha yanavyoongezeka iko siku itabidi niweke mic chini.Najua maisha yangu yote nitajihusisha na harakati za huu muziki na utamaduni wake kwani haya ndio maisha yangu na sitaweza kuyakwepa.
Na kwa mashabiki wangu,taarifa nzuri kwao ni kwamba hivi sasa niko studio mjini New York nakamilisha albamu yangu ya kumi(10) ambayo itaitwa VETO. Albamu hii ni kwa ajili yao exclusively!
BC: Una lolote ambalo ungependa kuongeza au una ujumbe wowote maalumu kwa mashabiki wako?
SUGU: Kwa mashabiki wangu popote pale walipo duniani,napenda wajue kwamba nawazimia na kuwajali kama wanavyonizimia na kunikubali toka siku ya kwanza. Chochote ninachokifanya kwenye huu muziki toka mwanzo mpaka sasa kisingewezekana bila wao.It’s has always been for love.Nawaomba waendelee kusapoti harakati zangu za mbele iwe kwenye muziki au pilika nyingine za mbeleni baada ya kuweka mic chini.
BC: Asante sana kwa muda wako Sugu
SUGU: Asante na wewe kwa kunipa nafasi mzee.
Asante kwa kufika hapa.Hii hapa ni zawadi kutoka kwa Sugu.Wimbo unaitwa Kambarage.
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.
Feedback / Comments
20 Responses to “TULIPOTETA KWA KINA NA “SUGU””
Leave a Reply


sending...
Here we go again. Mr 2, a.k.a Sugu!
Kwanza kabisa hongera kwa kufanya interview nzuri na Bongo celebrity na kutanabaisha wazi juu ya mambo mbalimbali yahusuyo sanaa ya “muziki wa kizazi kipya. Natumaini wasanii wengi wa muziki huu watajifunza kutoka kwenye interview hii. Big up BC kwa kumhoji sugu!
Sugu ni mmoja wa wasanii wa kweli “wa muziki wa kizazi kipya” ambao nimekuwa nikiwakubali siku zote ndani ya Bongo. Mashairi ya msanii huyu yanaigusa jamii moja kwa moja na yanaongelea hali halisi ya maisha wanayokabiliana nayo raia wengi wa Tanzania ambao wengi wanaishi maisha magumu sana. Hata kama ana nyimbo nyingine anazojipigia mapande yeye mwenyewe, lakini nyingi zimelenga kufunza, kuelimisha, kukosoa, na kuonya jamii mithili ya Professa Jay. Huu ndio usanii wa kweli wa “bongo flava!”
Lakini wasanii wengi wa bongo flava , “hasa wanaoibuka hivi sasa na kuiga umarekani zaidi”, ni kweli wanaghani vitu ambavyo hata wao wenyewe hawavielewi-kama asemavyo Sugu! Hao ndio wamejikita ktk kusifia ulevi, uvutaji bangi, uzinzi na uozo mwingine usiofaa ktk jamii. Hali hii ikiachwa iendelee, sina shaka bongo flava itaelekea pabaya!
Na pia ma-promoter uchwara nao (wa juu suti chini ndala) wakiachiwa waendelea kufanya kazi zao za kuunga-unga, wataharibu muelekeo wa sanaa hii. Ma-promoter wanaotakiwa kujitokeza na kuuendeleza muziki huu ni wale wanye upendo na bongo flava na nia maridhawa ya kuuvusha mipaka muziki huu ili uendelee kimataifa, na sio wale wa kuganga njaa kwa kupitia mgongo wa wasanii.
Radio DJz na producers vivyo hivyo! Hawa nao hawastahili kuzalisha na kutangaza kazi za wasanii vimeo ambao wanaiwekea giza bongo flava. Ni vema wajikite zaidi ktk kuzalisha na kutangaza kazi bora na sio bora kazi.
Naamini kila mtu akifanya kazi yake kwa moyo mmoja na kwa kujali ubora wa kazi, basi Bongo flava itafika mbali sana. Vinginevyo, sitashangaa sikumoja nikisikia bongo flava imekufa kifo cha mende.
Kila la kheri Mr Gufu ktk harakati zako za muziki na burudani na mkakati wa kufungua radio ya Bongo flava. Hopefully uta-revolutionize Bongo flava na kuipeleka ktk next level.
Stay blessed!
Katika watu nisiowazimia SUGU ni mmojawapo..am sorry for this..kwangu mimi naona hana jipya.ashachoka..afanye mambo mengine haya ya mic yashamshinda mana bongo kuna wasanii wapya wanawika kishenzi atawaweza wapi!
mchonga meno alikuwa bora kama si yeye,singekwenda sekondari skulii.mungu wamweke peponi mchonga meno.mark salamba australia.
Hi
BC,E bwana nashukuru kwa kumuweka Mtu mzima
2 Proud,mr 2,sugu kwenye BC,Big Up Sugu nakukubari sana uyumbishi na Kenge wanaochafua maji,Na Ndo Maana Walivyogoma kuzindua album yako we ulienda kuzindua Magic!
Hawajui Kwamba we Ulianza Kuimba Kabla Ya FM?
Kipindi Hicho David WAkati Ni Director RTD,Watu Walikufahamu na hata wasipopiga Nyimbo Zako Mjengoni Haina Maneno We tafuta Cheddar Baba Watakupigia nyimbo zako Wenyewe hao Kenge wananiuzi! Ni Hayo Tu,Huu Ni Mtazamo Wangu Msikasirike Washikaji Haya Ni mawazo tu! Ukinidiss We Ni Kenge Tu!
mimi sio mpenzi wa kihivyo wa miziki ya rap hasa hasa za huyu jamaa anajihita SUGU,
Muziki ni kama kazi nyingine za sanaa ambazo zinahitaji kipaji yaani Talent, kila ktk hii industry wapo watu wengi wameivamia ambao hawana talent kabisa-wapo too machanical ktk kuimba muziki- Ingawa ninampa big up sana huyu jamaa sugu kuwa kati ya watu wa mwanzo kuvamia industry hii na kutaka kuanza rap za kiswahili LAKINI HUYU JAMAA HANA KIPAJI HIKI, I AM SORRY TO SAY, SUGU HAS NO TALENT FOR MUSIC, ndiyo maana vijana wengi wenye talent wanakuja hivi karibuni wanamfunika kishenzi yeye anataka kung’ang’ania eti yeye ni muasisi wa bongo flava may be yes, but stay out of the game, huna kipaji hiki, ndiyo maana huyu jamaa uwa anatapa tapa, mara nastaafu, mara ninafanyacolabo,
I would like to apologize to all the fans of this bongo artist,I am terribly sorry if I have offended you.I like to speak my mind even to certain things which I am not comfortable saying.
Sugu is the man…asiyetaka aendelee kukataa tu lakini huo ndo ukweli kudadeki,na historia haiwezi kubadilika!
FOREVER SUGU!GO SUGU!
SUGU MUONGO WEWE SIO MUASISI WA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA.
MUASISI NI SALEH JABIR AKIWA NA NYIMBO KAMA ICE ICE BABY.
PIA KULIKUWA NA MUSSA SIMBA AU BLACK MOSES KAMA WACHEZA DISCO AKIWA NA KINA DIGA DIGA,OMMY SYDNEY. MFADHILI WAO ALIKUWA DJ KIM.
HIVI KARIBUNI DJ KIM KAFANYA MAHOJIANO AU KAPIGA PICHA NA ISSA MICHUZI NA AKAELEZA ALIVYOANZA KUASISI MUZIKI HUU WA KIZAZI KIPYA. KWENYE ORODHA WEWE SUGU HUKUWEPO.
LINI ULIKUWA MOTEL VILLA-MWANANYAMALA?
HISTORIA TUNAYO. ACHA UONGO NA KUDANGANYA WATU MUASISI NI SALEH JABIR.
kwani wamekataa?sugu wewe ni noma.nakukubali father
sugu babu tafuta kitu kingine cha kufanya sio mziki
He’s like a moon. A moon always shine at night,he will keep on shinin’ and nobody can stop this, so let him shine cause majority love moon-shine. Truth is like a last man standin’. In Hip Hop Sugu is a last man standin’.
Sugu unajua muziki,ni mbunifu hata katika project mbalimbali za kibiashara ya muziki,go on bro i really support you
wel done and keep on doing ur hiphop pioneer in Tanzania..
Kutoka moyoni, mi NAMKUBALI SUGU, ilembaya, watu wanaweza wakasema vyovyote bt mi nadhani hapo ndo uwezo wao wa kufikili umeishia, jama uko level zingine bro,hapa sizungumzii music pekeyake, nazungumza kuhusu HARAKATI, kaka hukamatiki.. Ila bro ulisema VETO 2takua 2naipata ht kwa machinga,mi mbona sijapata bro! naitaka kweli hii album kaka km vp nielekeze nitaipataje hapahapa DSM,na bei yake ya ukweli ni sh,ngapi nisijepigwa mwanao.
Sugu achana na wase*** watasema watachoka, kila kukicha unaendeleza bakora, wako wapi waliokucheka shuleni ulipofeli, sasa upo unachange viwanja kila unapotaka.
kaka wewe noma sana upo juuuu zaidi ya mawingu aka Clouds.
Huyo fala hapo juu hajui anasema nn? sisi tunaongelea Swahili rap miaka hiyo, Yeye anatuambia wacheza show wakina digadiga sijui amekuja lini mjini??
Unapozungumzia Sugu anamzunguzia 2Praud, kama makundi ya zamani kuna dar young mob, Dptz, Kwanza Unit, Weusi wagumu asilia. Sijui kama huyu f** anayajua hayo.
ila Sugu ankubali sana ile albamu yako ya kwanza,
“nipo kwenye microfoni hata unipe nini sitamani sioni x5. chorous
beti 1
Ni mimi nimimi kama Kingdom anakuja na hoja moja mbili kaa tayari, 3 4 5 6 saba si haba, haba na haba ujaza kibaba 8 9 10 ni mimi.
Naanza kukufunza kwa eeh bee chee
simama dede nakupa mkate nifate nikupake mate,
hapo ulipo hana hop mimi nilipo hana hiphop kwanini?
usiulize kwanini kwani uoni nikiwi cha macho!!
hicho ulichonacho kwenye macho unacho , shauri yako angalia utalia uchumi unao umeukalia,
wakati ukuta utakapo jikuta kanyanga unashindwa kutafuta,
fainali uzeeni huu…………………..
2praud jina ili nionekane baili pale demu anaponiambia,
ninunulie bia namwambia nipo tee apeche alololo sitaki blabla sitaki balaaaa,
Demu wa maggoti apige goti eti na mimi nimpe noti buuu shit,
nalinga na mbunga najikinga niwesalama salimi hadi siku naingia futi sita ardhi.
chorous
Mistari mingine ya 2praud ni hii!!!
dumu dumu vishindo ndiyo mwendo tunaokwenda dada yako ananipenda na Demu wako ananitaka,
ukikasirika kati pasuka katikati mikakati ni dhati,
kukushusha kwenye chati, sadakalawe mwenye kupata nipe kukoka ukose wewe ubaki na kiwewe kuku uite mwenye, wee nipishe niungulimishe kasheshe nikupashe upashike aaaah husinywe sumu,
life likukushinda panda kwenye kitanda zima taa funga mlango,
kuna watu wana usongo …….
Eebwana asante sana mtu mzm longtime kitambo, kwa kumaliza kila kitu, hawa maf****la wengine sijui huwa wanatokea usingizini yani pumba tupu,sasa mambo ya wacheza shoo anayaleta hapa yanini km hujui kitu piga kimya mchimba chumvi sio unaropokaropoka tu.. Kaza sugu lisongeshe twenzetu brother..
Duh! mkubwa sugu nakukubali vibaya, mwanaharakati zaidi ya Jakaya. Anayebisha kuwa wewe ni mwanzilishi wa kughani kwa kiswahili huyo ni mtoto wa juzi. nakumbuka kipindi kama cha mwaka 97 hivi wakati nipo sec pale jitegemee, tulikuita kwenye concert pale sh
To all you haters, kwa taarifa yenu sasa Sugu sio tu muasisi wa Bongo Fleva tu , bali pia ni muasisi wa wasanii wa kizazi kipya kuingia BUngeni – ni Mbunge sasa wa Mbeya Mjini
Mwanaharakati nakukubali ila kurudia kosa ni kosa usirudie tena yale uliyoyafanya ktk muziki wa kizazi kipya kushindana na wanao chipukia wewe unakua km baba kwahiyo dumisha muziki kwa kuutangaza ndani na nje ya nchii kupitia Bunge tukufu pia km wako waliokubania nafasi hii ukiwa Mh ndio nzuri kuitumia na kupatikana kwa haki ya Mtanzania Big up Sugu ila mapepe uache
go sugu goooooooo
ninavyo jua mimi hamna kufulu duniani kama mtoto kuhoji uhalali wa baba yake mbele ya mamaake mh.sugu wanaodis leo ndio hao hao walioliyumbisha dishi la mziki huu kaza buti nawadedicate na bonge la song lako MDA MREFU