MY TANZANIA   |   PLACES TO GO   |   MEDIA   |   ONLINE ENTERTAINMENT    

obama-ghanabc

Kama ulikuwa hutambui jinsi Rais wa Marekani,Barack Obama,alivyo maarufu na kipenzi cha waafrika walio wengi,basi ulichotakiwa kufanya ni kuelekeza macho na masikio jijini Accra nchini Ghana huko magharibi mwa bara la Afrika hivi leo.

Taarifa mbalimbali nilizonazo kupitia vyombo mbalimbali vya habari na pia washirika wa BC waliokuwapo jijini Accra hivi leo wanasema Ghana nzima ni kama vile ilisimama. Kila kona ilikuwa imepambwa kwa mabango,nguo nk vikimkaribisha kwa shangwe na vifijo Rais huyo wa Marekani ambaye alikuwa pia ameambatana na mkewe Michelle pamoja na mabinti zao wawili,Sasha na Malia.

Lakini tukiachana na shangwe,fujo na vigeregere vilivyojiri huko Ghana,muhimu sana ni kile alichokisema Obama wakati akihutubia Bunge la nchi hiyo. Kimsingi Obama alitumia muda huo kuongea na bara zima la Afrika.Wengi wameiita hotuba ya Obama kuwa ilikuwa ni ‘lecture” kwa viongozi wetu na vile vile wananchi.

Ukombozi wa Bara la Afrika uko mikononi mwa waafrika wenyewe. Hatuna tena sababu za kuendelea kulaumu historia ya biashara ya utumwa na ukoloni kwa mabaya yanayojiri barani mwetu hivi leo.Tuachane na vita za ukabila,udini,utaifa nk.Bado nasikia maneno hayo kutoka kwa Obama hata hivi ninavyoandika.

Ili kutunza kumbukumbu hii muhimu,hapo chini unaweza kusikiliza hotuba nzima ya Obama. Pia kama kwa sababu moja au nyingine,lugha aliyotumia Obama huielewi unaweza kubonyeza hapa ili kusoma kwa Kiswahili tafsiri ya hotuba hiyo.

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Baada ya kumaliza kumsikiliza Obama,hoja zilizonijia kichwani kwangu ni kwamba

  • Je,viongozi wetu au sisi waafrika kwa ujumla tutazinduka kidogo baada ya kusikia hoja nzito za ‘Ukombozi wa Bara la Afrika ni Jukumu Letu Sisi Wenyewe” kutoka kwa Obama?
  • Je viongozi wetu wamesikiliza kwa makini alichokisema Obama? Wapo tayari kuianza upya safari ya kulikomboa bara letu au ndio hadithi ya sikio la kufa?

Photo/Chuck Kennedy/White House

Share and Enjoy:
  • Digg
  • Sphinn
  • del.icio.us
  • Facebook
  • Mixx
  • Google Bookmarks
  • email
  • LinkedIn
  • Live
  • Spurl
  • Technorati
  • Yahoo! Buzz
  • YahooMyWeb

Feedback / Comments

4 Responses to “UJUMBE WA OBAMA KWA BARA LA AFRIKA”

  1. Comment by Gervas on July 12th, 2009 7:39 am

    BC…sio kwamba viongozi wetu hawayajui haya anayoyahutubia Obama, wanayaelewa kabisa na huwa tunawasikia wakiyaimba majukwaani hasa kampeni zikianza, ila tu ni VICHWA MAJI. Kumbukeni kuwa Hotuba moja tu haiwezi kumbadili Raisi mwenye silka ya wizi wa kura, mali za nchi, fisadi na mrafi wa madaraka. Upande mwingine tutaona Maraisi wanaotegemea misaada toka USA watajaribu kubadili mambo flani sio tu kwa sababu wamekunwa na aliyosema Obama bali wanajaribu kumtumikia kafiri ili wapate mradi wao. Katika hotuba hii phrase moja naona imebeba “theme” ya hotuba nzima ambayo nahisi ni muhimu kwa viongozi wa afrika..kwamba, “We dont need strong leaders but we need strong institutions” Obama anajaribu kumvika paka kengere sababu anaguswa na ameya-experience yanayotokea Afrika na asikomee hapo tu nafikiri kama ikishindikana tunamruhusu hata bakora awachalaze hawa!!

  2. Comment by mtimkavubongo on July 12th, 2009 5:08 pm

    Kwa kweli Obama nakupa tano, ila kama wapo watu ambao huwa wanafutilia comments zangu hapa BC tokea mwaka jana, Obama amerudia mambo ambayo nimekuwa ninayasema hapa BC.

    Ni wiki iliyopita tu, niliongelea kuwa mambo ya kusingizia ukoloni,wazungu, benki ya dunia, utumwa, ubepari, ubeberu na nchi za magharibi, yamepitwa na wakati ni wimbo nimeusikia tokea muda mrefu hautusaidii, ni uongo wezi na waporaji wa bara hili ni sisi WAAfrica.Obama karudi jambo hili kwa upana zaidi, asante sana kiongozi wa dunia huru-a great leader of a free world.

    Mimi sipendi kueleza bila mifano-twende nchi kwetu Tanzania, angalia wizi ulivyojaa kila kona na kila idara, ni aibu sana Rais wetu kuwa MATONYA kutembea kila kukicha anatembeza bakuli kumbe utajiri wa nchi yetu ni mkubwa, mali asili zinaporwa tani na tani za pembe za ndovu, wanyama na mengi haya ni mabillioni yas dollars yanapotea, madini hivyo hivyo, pesa za umma kwenye halmshauri, magari ya gharama-mashangingi, wizi wa pesa benki kuu, wizi wa pesa mashirika ya umma tenda hewa za wakubwa-Tanesco,TTCL na mifuko ya pesa,ndiyo maana nkuu wa usalama wa Taifa wa zamani alisema nchi inanuka na imeoza,na mzee Butiku ameisha sema hivyo hivyo, sasa haya mambo yote ukoloni uko wapi?marekani yuko wapi? TUNAOGOPA KUWASEMA WASOMI WETU WAAFRICA yaani elites ambao ndiyo wanapora
    nchi zetu

    Obama kasema Africa ni kwa Waafrica, hiyo ni kweli kabisa, na hasa hasa sisi vijana hawa viongozi wa sasa wameisha feli lakini Oboma umenisaidia kupaza sauti yangu maana dunia imesikia maneno yako hawatudanganyi tena

    wakati wa kuikomboa nchi na Africa ni sasa

    Hongera sana mtu wangu Obama Baraka

  3. Comment by Mzee wa Changamoto on July 12th, 2009 10:42 pm

    Kama alivyosema Gervas hapo juu. Aliyoyasema Obama si mageni kwa viongozi wetu. By the way, wanayatenda na ndio maana yapo. Hawashindwi kukomesha ukabila, hawashindwi kuweka umoja, hawashindwi kukomesha Rushwa na Ufisadi, bali wanaendeleza maana hiyo inawapa muda wa kuwagawa wananchi na kisha kuja na tule tu-ahadi twa kurekebisha mambvo ambatwo tunawapa tu-kura fulani (wakiongezea na zile za wizi) wanarejea madarakani. Ndio yale ambayo Garnet Silk kwenye wimbo wake Disadvantaged alisema “them taking advantage of the underpriviledged… they work a tricks by giving a little just to deceive you and break your little heart in two”
    Naamini viongozi wa Afrika wanajua na wapo (sitoshangaa kama watakuwa wengi wao) waliochukizwa na “kufunuliwa” kwa uzembe na uozo wao.
    Tupo tu, na siku yaja ya wenye kutenda watendayo kulipa matendo yao

  4. Comment by Mwanamke wa Shoka (UK) on July 13th, 2009 9:20 am

    Gervas na Mtimkavu nimewapata saana.

    …sijui ni lini hawa viongozi wetu wataona haja ya kuwajibika….jamaani inakatisha tamaa saana…

Leave a Reply