MY TANZANIA   |   PLACES TO GO   |   MEDIA   |   ONLINE ENTERTAINMENT    

muuminbc

Kunako miaka ya 90,pengine hakuna mwanamuziki wa muziki wa dansi aliyekuwa na jina kumshinda Muumin Mwinjuma(pichani).Hizo ndizo enzi zile ambapo nyimbo zake kama vile Tunda zilipogeuka kuwa “wimbo wa taifa” kwa maana ya kwamba ulitawala vinywa vya watu wakubwa kwa wadogo.Jamani tunda,nitalipata wapi tunda, ilikuwa ndio mbiu ya mitaani hususani kwetu uswahilini ambako hakuna sheria ya kumzuia mtu asiweke radio lake barazani na kuburudisha mtaa mzima,utake usitake.

Hapo katikati Muumin akapotea.Wengine wakatabiri kuwa huo ndio mwisho wa Muumini.Tabia ya kuhama hama waliyonayo wanamuziki kwa sababu za kutafuta maslahi ikawa imechangia ama kupoteza umaarufu aliokuwa nao au kusababisha apoteze washabiki aliokuwa nao.Yote maisha.

Hapo mwaka jana alipotangaza kwamba anarejea kwa kishindo kwenye anga za muziki huku akiwa amekua kimuziki na kimaadili na kwamba anakuja na bendi mpya itakayokwenda kwa jina la Bwagamoyo Sound,wapo tuliodhani anatania.Haikuwa hivyo.Ni kweli alikuwa amedhamiria.

Matunda ya Bwagamoyo Sound yameanza kuonekana.Mojawapo ya nyimbo mpya kutoka kwao ni huu unaokwenda kwa jina Natafuta Mume. Wimbo huu ni utunzi wake Muumini Mwinjuma mwenyewe. Usikilize hapo.Pata burudani.BC inamtakia Muumini na Bwagamoyo Sound kila la kheri katika ushindani mpya na harakati za kutoa burudani.

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Share and Enjoy:
  • Digg
  • Sphinn
  • del.icio.us
  • Facebook
  • Mixx
  • Google Bookmarks
  • email
  • LinkedIn
  • Live
  • Spurl
  • Technorati
  • Yahoo! Buzz
  • YahooMyWeb

Feedback / Comments

4 Responses to ““NATAFUTA MUME”-BWAGAMOYO SOUND”

  1. Comment by mwaipopo on July 13th, 2009 5:59 am

    Unapomuongelea mumin mwinjuma rudi nyuma zaidi ya ‘tunda’ fika mpaka vijana jazi, sililiza ‘baba jeni’ kwenye mistari ‘aliponipita kituo cha basi mimi na watoto wakeee, jamani baba jenii’

  2. Comment by mtimkavubongo on July 13th, 2009 4:18 pm

    Hongera mumin kipaji unacho wewe haujavamia fani.wengine wanafikiri muziki ni ajira hivyo kila mtu anaweza kuwa mwanamuziki.

  3. Comment by Gervas on July 13th, 2009 4:30 pm

    Mwaipopo…ni “sikiriza” na sio “sililiza” ni mimi kifimbo cheza.

  4. Comment by mwaipopo on July 15th, 2009 8:56 am

    sahihi zaidi ni ‘SIKILIZA’, hakuna ‘R’

Leave a Reply