
Uliwahi kuimba,kucheza au kuhudhuria shughuli ambapo miziki ya Mr.Nice ilichezwa na kupokelewa na kwa shangwe? Nikiuliza namna hiyo bila shaka nitapata majibu ya ndio kuliko yale ya hapana. Kama ingelikuwa ni uchaguzi basi huenda nami ningekuwemo kwenye ‘askari wa miamvuli”
Ukinihoji zaidi nitakwambia ninakumbuka bayana jinsi wimbo wake wa Fagilia ulivyotamba.Umesahau jinsi wimbo huo ulivyopigwa na kupigwa na kupigwa tena pindi mtanzania Mwisho Mwampamba alipochukua nafasi ya pili katika shindano la Big Brother? Fagilia, Fagilia Bongo ikawa ndio wimbo wa taifa. Kila Tanzania ilipoibuka kidedea kwenye chochote kile,wimbo wa kusindikiza shamrashamra ulikuwa ni Fagilia. Sifa yoyote ilikwenda na maneno wawaaaaa…
Mafanikio aliyokuwa nayo Mr.Nice yalifungua njia katika mengi.Kwanza ilikuwa ni yeye kupata show nyingi nje ya Tanzania na kuwa msanii anayelipwa zaidi Afrika Mashariki. Hii ni kwa mujibu wake yeye mwenyewe nilipofanya naye mahojiano takribani miaka miwili iliyopita. Kama ambavyo ungetarajia,umaarufu na fedha huja na mambo yake. Mengine mazuri mengine mabaya. Unaweza kuyasoma yaliyojiri katika mahojiano hayo hayo niliyofanya naye.
Lakini wapo wanaosema kwamba once a rock-star always a rock- star.Hajapotea katika anga za muziki.Siku hizi ana bendi yake inayokwenda kwa jina Bush Band. Hivi karibuni amefyatua kibao kinachokwenda kwa jina Kidonda. Kisikilize hapo chini.Je unadhani Mr.Nice anaweza kurudia tena umaarufu aliokuwa nao hapo mwanzo?
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.
Feedback / Comments
3 Responses to ““KIDONDA”-MR.NICE”
Leave a Reply


mr nice ni mkali kuliko wasanii wote bongo!
nimemkubali mr.nice na hii track yake..keep it up bro..
sa ndo kaimba nini!