TAKING SOME RISKS

q

Success belongs to risk takers.Wanaosema hivyo wanajua kwanini wanasema hivyo. Kwa Q-Chillah ambaye hapo zamani tulimuita Q-Chief, inaonekana ukweli huo unakwenda sambamba na mienendo yake kwa sasa.

Hivi majuzi alibadilisha muonekano. Kutoka Q-Chillah mwenye rasta(rasta za fasheni lakini na sio zile za imani) mpaka Q-Chillah unayemuona kwenyepicha hapo juu.Kutegemea na utashi binafsi wa mtu wapo wanaosema kapendeza kwa sababu sura imeonekana vyema nk na kuna wanaosema hapana…bora alipokuwa na rasta. Maneno ya mtaani pia yapo kama kawaida; Q-Chillah “kafulia” na hivyo faranga za kutunzia rasta zimeingia mitini.Yote hayo ni maneno tu au vijimambo.Muhimu ni jinsi yeye mwenyewe anavyojisikia.Uhuru binafsi alionao mtu inabidi upewe nafasi jamani.

Yote tisa,kumi katika kuthubutu kwa Q-Chillah ni kubadilika katika aina ya muziki anaopiga.Mwenyewe anasema anabadilika kama utabiri wa hali ya hewa. Q-Chillah sasa ameingia kwenye mnanda au mchiriku kama unavyojulikana kwa wengine. Miziki ya Pwani hii.Kumbuka Q ameshajaribu pia taarab katika siku za hivi karibuni. Sikiliza kitu alichokuja nacho Q-Chillah hivi karibuni hapo chini.Wimbo unaitwa Zaka Zaka.Je huku ni kuonyesha kipaji alichonacho,kubahatisha au kuthubutu kupita kiasi? Can we still call this “Bongo Fleva”?

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Page 1 of 3 | Next page