
Nimeshawahi kusema na leo nitarudia tena; Kama umekosa kabisa jambo au mambo yanayokufanya ujisikie furaha kuwa Mtanzania,basi angalau unaweza kupata ahueni unapoangalia jinsi ambavyo “demokrasia” ya nchi yetu imekuwa mfano wa kuigwa barani Afrika na hata sehemu mbalimbali za ulimwengu.Of course demokrasia yetu ina mapungufu mengi bado lakini ipi ambayo haina?Marekani au?
Mpaka leo,tangu Nyerere ang’atuke,hajatokea mtu akasema anataka kubadili katiba ili aendelee kutawala.Muda ukiisha mtu anaachia madaraka. Lakini kuachia madaraka haitoshi.Lipo suala zima la kuachia madaraka na pia kuendelea kushiriki katika shughuli mbalimbali za kitaifa na hata kimataifa kwa jina la Tanzania. Hali hii ni lazima ilindwe kwani ni wazi kwamba haitokei kama ajali.
Pichani ni Marais wetu,wastaafu Ally Hassan Mwinyi(mwisho kulia),Benjamini William Mkapa(mwisho kushoto) na Rais aliyepo madarakani hivi sasa,Jakaya Mrisho Kikwete(katikati). Kama unavyoona pichani wapo na wake zao au kina mama zetu wa kwanza waliostaafu na aliyepo kwenye uskani hivi sasa.
Sijui kama ni mimi tu ndio nimeona hili au vipi lakini nadhani mpangilio kidogo wa picha hii ulikwenda kombo.Sijui kwanini Mama Anna Mkapa ilibidi awe mbali vile na Mzee na pia Mama Sitti Mwinyi.Sijui.
Picha kwa hisani ya Bodi ya Utalii Tanzania
Feedback / Comments
31 Responses to “TANZANIA TANZANIA…NAKUPENDA”
Leave a Reply


“DEMOKRASIA YA UMOJA NA AMANI”
Misingi ya demokrasia yetu,iliwekwa na babu na bibi zetu kwa mtazamo wa kizazi cha mbali,
viongozi wamechaguliwa na kututumikia katika vipindi na kuachilia madaraka ingawaje bado wana uwezo wa kutuendeleza hii inaonyesha siasa ya umoja na amani kwa taifa letu.
Katika uongozi wa nchi yenye matatizo mengi kiuchumi na maendeleo ya wananchi,kutakuwepo na upinzani ndani na nje ya nchi, hayo yanakubalika katika kila nchi iliyochaguwa demokrasia ya umoja na amani.
Marumbano na upinzani hayatoweza kubadilisha mawazo na fikara za watanzania katika kuendeleza kudumisha misingi ya amani na umoja iliyowekwa na babu/bibi zetu kabla ya viongozi wetu waliopita na sasa, hii ni mojawapo ya sifa za wazi za watanzania zinavyoonekana na majirani zetu katika bara zima la Afrika.
Kinachotakiwa viongozi wetu kuwasikiliza wananchi wanasema nini katika kutatua matatizo ya maisha ya kila siku.
Kilio cha wananchi ni sawa na cha njiwa “Dove`s Cry” anayekisikia ni njiwa mwengine wa karibu, viongozi na sisi wananchi tuwe kama kundi moja la njiwa kwa kilio cha umoja tutasikika kimataifa.
Denmark
Sio Demokrasia tu bali na Uhuru wa Mahakama ambacho ndio chombo pekee cha kutoa haki vimedumu nchini. Hii nafikiri ni kwa sababu ya msingi uliowekwa na viongozi wa awali (Mwalimu) na hilo hatuwezi kulipinga na nikweli inatia raha kuona viongozi wastaafu namna hii. Lakini demokrasia/Amani hii isiishie kwa hawa viongozi tu bali hadi kwa “Wanchali na Waryanchoka” huko Tarime, Wamasai na wakulima huko Morogoro nk. Japo Tanzania hatupo juu sana kwenye demokrasia, tunachohitaji saizi ni kama Obama alivosema, strong institutions, ambapo katiba inatakiwa iwe na vifungu vya kuwabana viongozi/raisi kutokuwa na nguvu holela, Bunge lenye uwiano imara lisilo la chama kimoja,Uhuru wa Mahakama, Kamati huru ya Uchaguzi nk. Vitu hivi vitajenga sio tu demokrasia safi bali utawala bora na washeria.
Pia serikali inapaswa kuondoa hali ya umaskini wa kupindukia ya wananchi wake,Kupunguza gap kati ya maskini na matajiri kwa kutoa nafasi za kutosha kwa mtoto wa masikini kupata elimu sio tu ya msingi hadi ya juu bure kama akiri wanazo.
watanzania wanapenda sifa za kitoto kweli,
mimi sioni mnachotaka kusema
yaani amani na njaa wapi na wapi??
au mkapa alivyotoa mashamba ya watu na kuwapa kaburu wachimbe madini na wenye mashamba kubaki bila kitu ndiyo sifa hiyo au mnakejeri watu??
hapo kusingekuwa na mkapa huenda ningewaelewa ila kwasasa mmenichefua kwelikweli!!
Dada Rita…Huwezi kupata utawala ulio safi/perfect duniani yaani 100% safi haupo. Hata nyerere kuna mambo mengine aliyofanya ya ajabu mfano Kulikua na kesi ya ardhi Arusha kati ya Tajiri mmoja na mahakama kuu Arusha ilimbana tajiri huyo lakini walitumwa ma-shushushu tokea ikulu wakavamia Mahakama kuu wakachukua faili la hiyo kesi na Jaji wa Mahakama kuu Arusha akaamua Kujihudhuru madaraka. Vilevile Mwinyi Aliuzia Mbuga ya Loliondo kwa Waarabu hata viwanda vyote alivyoviacha nyerere vilikufa wakati wa mwinyi na pesa/uchumi ulishuka sana.
Hivo Demokrasia iliyopo sio mbaya ukilinganisha na wenzetu majirani japo hiyo haitoshi Mambo mengi yanatakiwa yafanyike tokea kwenye Uchumi,siasa, nk
hivyo walivyajipanga ni sawa kabisa cos ni protocol ndio inawaruhusu kujipanga hvyo mimi ndio ninavyojua hvyo km nilivyosomea protocol.
mashuka begani hoyeeeeeeeee!!!!!!!!!!!
Kweli itakapo dhihiri Uongo utajitenga.
Democracy exist to those WHO were and who are on power today not to the civilian.
Can sameone give me a concrete example where there is SOCIAL EQUALITY in Tanzania. Except citizen having rights to “VOTE”
Please I am hungry to know that and your answer will be very much appreciated.
Thank you!
hmmm!!…Mickey JOnes kidogo unanichanganya….Gervas na Ritta nimewapata.
…the ten year’s harm is unspeakable….just like the way it is….chukua chako mapema…lol.
It is disgusting…..very painful….dissapointing….
….well….hii sijui eti kwa nini wake zao wamekaa mbali nao…(alivyosema blogmaster…)…ni wao pekee wanayajua majibu
….I think it is personal….na sioni nini kinatusaidia sie watanzania….wawe karibu ama mbaali na waume zao!!!
….zaidi saana ni kukumbushiana maumivu na makovu ambayo hata baado hayaonyeshi kupona…lol
MABINGWA NA NAHAU NA METHARI KITALANI..KILA KUKICHA AFADHALI YA JANA, WANGEFANYA NINI IKIWA HAJUI KESHO YAO?????
Hivi majina ya wake zao wanaitwa nani na nani?
Manakekulikuwa na kauvumi, eti eeeh, mke kakimbilia Uarabuni, huyu ni nani? Watu bwana wakikosa kosa huvumbua kasa!
Hi Guys
I have no substantive comment, but may be, let me give what I consider a less substantive comment, We owe them a debt of gratitude for honouring our constitution not to remove term limits like their counterpart in Uganda and other African leaders. Enjoy your retirement and pension,
May almight God grant them long life.
cheers frateline
Demokrasia? Wote hawa ni CCM
mhhh sina cha kusema!
“CONSTITUTION MUST BE RESPECTED”
Nakubaliana na mtazamo wa Frateline nikiwa kama mmojawapo nayeheshimu “constitution” ya nchi kabla ya yote,inatuletea demokrasia ya umoja na amani.
Hawa viongozi hawakujaribu kuibadilisha kwa
kujiendeleza kutawala,walistahafu ingawaje bado wana uwezo mkubwa wa kuliongoza Taifa
katika shughuri mbali mbali za taifa na kimataifa.
Malalamiko ya DaRitta ingawaje kimtazamo
yapo “personal” lakini tunayaheshimu.
Hakuna viongozi wa nchi ambao hawajafanya makosa ya aina fulani katika nchi wanazowakilisha,kama wapo basi watakuwa viongozi wenye kasoro fulani ya “mental-disturb” kama ujuwavyo mwendawazimu ndiye anayejiona kila wakati yupo sawa.
Mvurugano wa kisiasa na vita za kumwaga damu kama jirani zetu Kenya na Uganda,ndiyo zimetufanya watanzania kuwa wavumilivu na “kiongozi au viongozi” wachache ambao si DaRitta asiyekuwa pekee anayechafuliwa kimawazo.
Tanzania tunakwenda taratibu kimaendeleo na uchumi wa wananchi lakini tutafika katika malengo ya maisha bora kwa kila mtanzania,ingawaje yatachukuwa mda mrefu kukamilika,mwanzo wake tunauona na mwisho wake utaonekana na kizazi kipya.
MUNGU IBARIKI TANZANIA,MUNGU IBARIKI AFRICA
mi wanasiasa kila siku wananitia hasira,tena hapa wamekusanywa wote wakapigwa picha ikawekwa hapa.bora niondoke hapa nisije kubomoa computer yangu
tabia ni kama ngozi ya mwili huwezi kuibadili na mtoto wa nyoka hafundishwi kuuma…mchelea haki hatendi ukweli.
na huo ndiyo ukweli
Chapombe ndugu yangu i feel the same..kwa upande wangu NO COMMENT..
wadau mimi mwenzenu viongozi wetu wananiboa ile kichizi..nipo ugaibuni na naona mambo mengi ya kimaendeleo yanafanyika huku, kinachoitajika ni political will tu..na sioni kwanini TZ yasifanyike pia so i have mixed feelings kuhusu viongozi wetu na maswala ya siasa kiujumla..
Teh-teh-teh!
Chapombe na Mlo Mmoja bora mtoe dukuduku lenu! Langu bado linavimba!
i like this picture, it seems like the president and former presidents are getting along well. BUT we need to see more than just getting together; we need to see the moon shine signaling the rest to the poor and middle class of this contry who have been suffering for too long, we need to see tanzania becoming a great land where all good dreams can become a reality and not only for few fat cats, we need to see the respect and patience of our fore fathers who fought for this contry paying off. underneath and above all we need a corruption free country where all of us can stand for our rights and can dream for a better tomorrow. We all need that…
Maoni ya Mickey Jones na Gervas, ni mazito na ni ya watu wanaofahamu wakiongeacho. Chukueni TANO kutoka kwangu.
Demokrasia ya kweli, Amani na Utulivu, tulionao katika Tanzania yetu leo hii, vinatokana na hekima na busara za viongozi wetu hawa wapendwa, waliosimama katika picha hii na wake zao.
Ukweli wa wazi katika hayo (Demokrasia, Maendeleo ya Amamni na Utulivu) haviwezi kupingwa na Mtanzania wa kweli mwenye kuithamini nchi yake ya Tanzania (Mzalendo).
Nchi zote duniani, haziongozwi na “Mitume”, bali zinaongozwa na binadamu. Kama ilivyo kawaida, binadamu hawezi kuwa msafi asilimia mia moja kama “Mitume” walivyo.
Katika uchunguzi wangu usio rasmi, nimekuja kugundua kuwa, watoa maoni kuhusu Maendeleo na Siasa za nchi yetu Tanzania. Sio wote kuwa ni Watanzania. Kuna Mamluki wengi sana.
Utashangaa kuona mtu anajiita Mtanzania, lakini eti hajui kuongea wala kuandika Kiswahili, isipokuwa Kiingereza tu. Mtu huyu anajikunja kutoa maoni kuhusu Siasa za Tanzania na kuwakosoa, na hata kuwatukana viongozi wetu, waliochaguliwa na Watanzania.
Je, Siasa za Kitanzania, mtu wa aina hii kazijulia wapi? Kwa sababu inaonyesha hajawahi kuishi Tanzania kwa muda mrefu, ili kuielewa jamii ya Kitanzania.
Pia nimekuja kugundua kuwa, Watanzania wengi walioko nje, wanaisemea mbovu nchi yetu na viongozi wake, kwa sababu ujio wao nchi za nje, umegubikwa na sababu nyingi.
Watanzania wako nje ya Tanzania, kimasomo, pia kuna wahalifu wa aina mbalimbali wakiwemo majambazi, waliokimbia mkono wa sheria wa Tanzania, kuna watoto wa Kitanzania waliozaliwa na kukulia nchi za nje.
Watanzania wenzetu hao juu niliowataja, kwa hali yoyote, hawawezi kuisema vizuri nchi yetu Tanzania, kutokana na historia zao za maisha. Hawaipendi na wengine hawaijui Tanzania, bali wanaisikia kupitia vyombo vya habari tu.
Watu wa aina hiyo wanapoona Watanzania tunajitahidi kufanya jambo zuri, kazi yao ni kutubeza na kukandia Maendeleo yetu, kwa kutumia mianya ya mapungufu ya kibinadamu ya Viongozi wetu wanapofanya makosa.
Watanzania wenzangu, tuwe macho na vijibwa hivyo, na hasa wale wote wanaojiita Watanzania kumbe ni maadui wa Tanzania, wanaotamani tupate matatizo ya kisiasa, kama waliyonayo wao.
MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI AFRIKA!!!
It’s Great To Be Black=Blackmannen
Blackmannen, no one is saying that Tanzania hasn’t done anything in terms of peace and stability. we are well above the bars when it comes to peace. But the need to have economic well being still remains top of our agenda. You can have peace while crippled with malnutrition, illiteracy, diseases, poverty etc etc. Thats why they say UHURU NA MAENDELEO. When you have money you increase the capacity to solve your problems. We do complain not bcoz we hate our contry, but becoz we love it, and we know it’s possible to have a rich and prosperous Tanzania. We don’t want see our children going through what we are going through right now. I salute…
ujuwe watu walioko ugaibuni ndiyo wajanja yaani waelevu,huwezi ukawaletea uongo kama mnavyoletewa ninyi mlioko tz.
wanaupeo mkubwa kuzidi hata hao viongozi wapenda rushwa hivyo tofauti hapo ni mtizamo hakuna mtu anayetaka nchi ipigane ili apate nini? ila watu wanapenda haki na si viongozi kuzurumu wananchi wavuja jasho
kunasiku hao viongozi wataletwa ugaibuni pia kujibu mashitaka ya wizi wa mali ya umma ebo wao nani kwani
mtu ye yote anaekubaliana na ccm au asio mpinzani wa ccm ndio mzalendo??? this is almost like DRC all over again!!! kama mshikaji mmoja hapo juu alivyosema amani na njaa. wazalendo wengi wana njaa!!!
jamani huko juu,punguzeni kiinglish,mi nimesahau siku hizi maanake mnanikumbusha mbali,we acha tu
watanzania nje ya nchi mma haki ya kikatiba kufichua, kukemea, na kulaani kila aina ya maovu na uozo wa mtu yeyeto anayeihujumu nchi hasa viongozi wabovu. Mpuuzi yoyote anayedhani kusifia viongozi wabovu ndio uzalendo, huyo aepukwe kama UKIMWI. Hatutaki uzalendo pumba ndani ya blog hii.
Msg sent!
tanzania ina demokrasi gana kama ina demokrasi mungalimtukana ndugu salim ahmed salim na kumwambia mwarabu huo si ubaguzi au ndio msingi wenu wa demokrasi yenu hiyo
Hongera viongozi wetu kila mmoja amejitahidi kufanya kile alichoweza, lakini…
Asiyependa kukosolewa anakasumba ya `umimi’-ubinafsi, na kinyume chake ndio demokrasia ya kweli. Sisi kama binadamu hatuwezi kufanya kila kitu safi,na atakayeona hilo ni yule aliyepembeni mwako. Wewe mwenyewe utajiona msafi hata kama ni shati jeupe lililoingia madoa ya uchafu utasema ni maua au urembo, kwasababu ya `umimi-wakupenda sifa’
Kitu kikubwa tujue mtu akikalia kiti sana mwishowe hujiona ndiye mmiliki,na hatimaye hujenga kiburi cha kuwaona wengine hawana haki ya kukikalia. Hii ndiyo demokrasia inayotakiwa kwa wabinafsi.
Nakumbuka yupo kiongozi aliwashushua wale wanaopenda kumsifiasifia, huyu amejawa na hekima ya ukweli. Sio kila anayekusifia ana nia njema, ni heri ya huyo anayekukandia ubaya kwani ameweza kukuonyesha doa lililopo kwenye shati lako, na kesho au keshokutwa utalifua liondoke.
M3