mrishobcSwali lililopo kwenye kichwa cha habari hapo juu si langu.Ni swali kutoka kwa Mwandishi Saleh Ally wa gazeti la Mwanaspoti. Ni swali lililobeba makala nzito ambayo inahoji na hapo hapo kujaribu kupata majibu kutoka kwa wakongwe mbalimbali wa muziki wa hip hop nchini Tanzania.

Saleh anaungana na wote ambao wamekuwa wakihoji ulipopotelea miziki ya hip hop iliyokuwa imesheheni ujumbe ambao bila shaka ulipatikana baada ya msanii kuitazama jamii kwa umakini ule uliofanya akaitwa “kioo cha jamii”. Badala yake,leo hii nyimbo ni kuhusu suala moja pekee; mapenzi. Karibuni kila nyimbo inayotoka ni kuhusu mapenzi na starehe ambazo kimsingi hazisaidii sana katika kujenga jamii.Ujumbe wa leo ni nimemuona demu,kapendeza,anavutia,ana figure matata,nikamtongoza,tukaenda kwenye sita kwa sita…mtamu,kwisha kazi. Matatizo ya kijamii au hata mafanikio ya kijamii, hayamulikwi tena kupitia muziki.Kwa bahati mbaya,hata vyombo vingi vya habari navyo vinayapa kisogo mambo mazito mazito ya kijamii. Tunamuachia nani?

Pamoja hayo,Saleh Ally,anamtaja mwanamuziki/mshairi Mrisho Mpoto(pichani) kama miongoni mwa wachache waliobakia ambao wanaimba vitu vya “kueleweka”.Unakubaliana naye? Kama hukubaliani naye,nini maoni yako kuhusu muziki wa kizazi kipya?

Ili kusoma makala nzima ya Saleh,bonyeza hapa.

Feedback / Comments

5 Responses to “TUMUACHIE “MJOMBA” AIBEBE HIP HOP YOTE?”

  1. Comment by Hombiz on July 28th, 2009 9:37 am

    Kwa mtazamo wangu mimi, naona bora nirudia yale yale niliyoyasema hapo awali mlipomleta Mr 11 katika wanja hili la bongo celebrity. Maoni yangu yalikuwa ni kama ifuatavyo:
    Wasanii wengi wa bongo flava , “hasa wanaoibuka hivi sasa na kuiga umarekani zaidi”, ni kweli wanaghani vitu ambavyo hata wao wenyewe hawavielewi-kama asemavyo Sugu! Hao ndio wamejikita ktk kusifia ulevi, uvutaji bangi, uzinzi na uozo mwingine usiofaa ktk jamii. Hali hii ikiachwa iendelee, sina shaka bongo flava itaelekea pabaya!
    Na pia ma-promoter uchwara nao (wale wa juu suti chini ndala) wakiachiwa waendelee kufanya kazi zao za kuunga-unga, wataharibu muelekeo wa sanaa hii. Ma-promoter wanaotakiwa kujitokeza na kuuendeleza muziki huu ni wale wanye upendo na bongo flava na nia maridhawa ya kuuvusha mipaka muziki huu ili uendelee kimataifa, na sio wale wa kuganga njaa kwa kupitia mgongo wa wasanii.
    Radio DJz na producers vivyo hivyo! Hawa nao hawastahili kuzalisha na kutangaza kazi za wasanii vimeo ambao wanaiwekea giza bongo flava. Ni vema wajikite zaidi ktk kuzalisha na kutangaza kazi bora na sio bora kazi.
    Naamini kila mtu akifanya kazi yake kwa moyo mmoja na kwa kujali ubora wa kazi, basi Bongo flava itafika mbali sana. Vinginevyo, sitashangaa sikumoja nikisikia bongo flava imekufa kifo cha mende.
    Wakati huo huo, mimi sidhani kama Mrisho Mpoko anaibeba hip hop ya bongo. Ni kweli yeye anaghani mambo yanayoigusa jamii moja kwa moja. Hata hivyo, mtindo wake sio wa hip hop kabisa. Yeye kajikita kweye nyimbo na ushairi wa kiasili zaidi. Hivyo kusema ati anaibeba hip hop, hilo mimi nakataa. Mrisho Mpoko, ataibeba vipi hip hop wakati fani na maudhui ya sanaa yake si hip hop!
    Mwisho namalizia kwa kusema kuwa, producers, DJ, na Promotors wa muziki huu wa hip hop ya Bongo, ni lazima wajikite kuzalisha, ku-promote, na kucheza, nyimbo bora na sio bora nyimbo. Na hili lianzie kwa producers ambao ndio wanatakiwa wafanye uhakiki wenye akili kwa wasanii hawa. Tusiwe na lundo la vijana wanaojiita wasanii, lakini viwango ni ZERO!

  2. Comment by mpole on July 29th, 2009 2:16 am

    Huyu jamaa mashairi yake yamekwenda shule,na anachozungumza ni hekima tupu kwa wenye kuelewa. Wengi wetu tunapenda kusikiliza utamu wa sauti hata kama ujumbe unakutukana. Tupende kusikiliza pia nini kinachoongelewa ili ujumbe ufike mahali pake.

  3. Comment by Dinah on July 29th, 2009 1:39 pm

    Hapana jamani! Mpoto baki hapo hapo na hip hop waachie wenyewe…..hip hop inaendana na muonekano, Mjomba huna muonekano wa hip hop thank u very much(msinidongoe kwani sijui kuwa mnafiki).

    Tatizo hao ya baadhi ya hao wanaojiita “waandishi wa habari” ni kuandika mambo kwa kuangalia upande mmoja kama sio kuandika kutokana na hisia/mawazo yao binafsi.

    Kuna uwezekano mkubwa huyu “mwandishi wa habari” wa Mwanaspoti haupendi muziki wa kizazi kipya au ule wa kughani(hip hop) kutokana na sababu zake binafsi!

    Watu/Wasanii wamechoka na kusema/kuimba ukweli bila kupata au hata kuona mabadiliko kidogo.

    Tatizo la watanzania tunapenda sana kujipa matumaini, unaimba ukweli kuhusu labda tuseme siasa…..Prof Jay Kaimba nyimbo nyingi tu kuhusu Siasa na Wanasiana bila kusahau wapiga kura (mimi na wewe) nini kimebadilika au kufanyiwa kazi ktk jamii kupitia mashairi yao?

    Hali kadhalika Sugu kasema mengi kuhusu Siasa, hali halisi ya Uchumi wa Bongo akilinganisha na wa Ulaya, Ugumu wa maisha kwa vijana…..kitu gani kimebadilika kwenye jamii yetu ya Tz since then? Tena huyu hata ukiangalia mauzo yake sio mazuri ukilinganisha na waimba Mapenzi.

    Wasanii wamechoka sio tu kwa vile hawasababishi mabadiliko bali pia hawauzi, Wanajamii wamechoshwa na Siasa za uongo.

    Kumbuka hawa vijana wako pale sio tu kuburudisha bali pia ni kujipatia kipato ili kuendesha maisha yao ya kila siku.

    Sasa mbali ya kuwa Mbunifu pia unatakiwa kujua soko liko wapi kwenye jamii inayokuzunguuka.

    Mapenzi yanamhusu au niseme yanamgusa mtu yeyote haijalishi anaishi wapi, anaelimu kiasi gani, Fukara, Masikini, Tajiri au Fisadi…..wote wanapenda na kupendwa, wanatenda na kutendwa, wanasameheana, wanaachana n.k

    Hivyo basi Wasanii hawa wanapozungumzia mapenzi (yanakwenda sambamba na starehe) iwe ni kihasi au kichanya watu wanafurahia au hata kutumia nyimbo hizo kurekebishana, kutongozeana, kujiepusha na wapenzi waovu n.k hali inayofanya kuwa na mashabiki wengi.

  4. Comment by Dinah on July 29th, 2009 1:54 pm

    Tuache kuponda kazi za wasanii wengine na kufananisha kwa vile tu tunapenda muonekano wa mtu kwa vile umefanana na wetu au tunataka kupandisha profile yake.

    Unapo jaribu kuponda hawa waimbaji wa muziki wa kizazi kipya mbele ya jamii unataka jamii hiyo ifanye nini? Iwatenge na kususa kwa kutokwenda kwenye matamasha au hata kununua cds zao?

    Unadhani wataendesha vipi maisha yao? Hebu fikiria hawa Wanabongoflava wote walipo na wanaoibuka sasa wangekuwa mtaani/vijiweni……mngeandika tena kuwa Vijana wa siku hizi kazi yao ni kukaa tu vijiweni bila shughuli, wakijipa shughuli…..mnadai wanaiga na kuimba mapenzi na starehe……

    Waandishi wa habari Cheza mbali na Bongoflava!

    Hebu tuambieni kwanini Mafisadi bado wako Mtaani? Jela kumejaa au?

  5. Comment by KBC on August 3rd, 2009 10:20 am

    Asante Sana DINAH hapo juu kwa UFAFANUZI wa kutosha..kwa kifupi “MJOMBA” MRISHO is A Good POET..Lakini sio Mwana HIPHOP..Nyimbo nyingi inazosikia redioni ni za muziki wa BONGO FLAVA..sio HIPHOP,..huyu alieanzisha SWALI hili inabidi Atembelee pale WAPI @ British Council kila mwisho wa mwezi..You have to be HIPHOP to do HIPHOP..lakini HEKO na shukrani kwa POET/MSHAIRI MRISHO..Brilliant WORK of ART..Im a BIG FAN*..www.myspace.com/mrkbc
    PAMOJA!!

Leave a Reply