“MSISIMKO WA DISCO UMEPUNGUA”-DEEJAY JD

dilingabc

Muziki ni lugha ya ulimwengu(universal language). Bila shaka umeshawahi kusikia msemo huo. Mimi binafsi nakubaliana kabisa na msemo huo. Kuna nyakati nimewahi hata kujiuliza,hivi dunia ingekuwaje kama kusingekuwa na muziki? Tunapokutana na kusheherekea tukio fulani,vigelegele na mayowe vingetosha?

Wakati kazi ya kubwa ya kutuletea burudani ya muziki inaanzia kwa msanii mwenyewe,pembeni yake, kwa miaka nenda rudi, amekuwepo mtu muhimu katika kukamilisha safari hiyo. Mtu huyo ni DJ au Deejay au Disco Jokey kwa wale wenzangu na mie tuliokula chumvi kidogo!

Mwanamuziki/Msanii anapomaliza kazi yake kwa kushirikiana na producer wake, hukimbilia kwa DJ kwani anatambua kabisa kwamba huyo ndiye kiungo kikuu kati yake na mashabiki au wapenzi wa muziki kwa ujumla.

Miongoni mwa DJs ambao sio tu wameifanya kazi yao kwa ustadi mkubwa bali pia waliowahi kujizolea sifa na mashabiki wa kutosha ni DJ John Dillinga Matlou au maarufu kama DJ JD. John ana historia ndefu katika muziki. Mwenyewe anasema,aliianza safari yake tangu akiwa mtoto kabisa. Mpaka hivi leo bado anaendelea kuwapa watu burudani. Hivi sasa anaendesha kampuni ya JD Entertainment ambayo inashughulika na masuala yote ya burudani,promotions na kadhalika.

Nilipofanya naye mahojiano  ambayo utayasoma hivi punde,niligundua mambo kadhaa muhimu;DJ JD ni mbunifu wa aina yake. Aina za vipindi alivyovianzisha na kuviendesha(hususani redioni) ndivyo pengine vilivyochangia mafanikio ya baadhi ya vituo vya redio vya FM tunayoyaona hivi sasa.Pia niligundua kwamba huyu ni miongoni mwa wale DJs ambao wanaifanya kazi yao sio kwa ajili ya kutafuta pesa peke yake bali kwa sababu anaupenda muziki na yote yale yatokanayo na muziki mzuri wenye kuleta burudani na starehe.

Fuatana nami katika mahojiano haya ambapo,pamoja na mambo mengine,DJ JD anaelezea hisia zake kuhusu ulimwengu wa muziki na burudani hivi sasa. Pia anajibu swali ambalo wapenzi wengi wa muziki wamekuwa wakitaka kumsikia akijibu; Je yeye na DJ Bonny Luv ni mahasimu au ni watu wawili wanaoipenda kazi yao na pia kushirikiana kwa karibu? Je unajua kwamba baba mzazi wa DJ JD sio mtanzania bali raia wa…? Endelea kusoma

BC: Karibu sana ndani ya BC. Tunafurahi kupata fursa hii ya kufanya nawe mahojiano haya.Mambo vipi?

JD: Mambo sio mabaya kusema ukweli.Namshukuru Mungu.

BC: Kwa sababu hii ni mara yetu ya kwanza kufanya nawe mahojiano na kwa sababu tunatambua kiu ya wengi(hususani mashabiki wako) labda ungeanza kwa kutueleza kwa kifupi historia ya maisha yako.Ulizaliwa wapi,ukakulia wapi na mambo kama hayo.

JD: Mimi nimezaliwa Morogoro tarehe 17/03/1973 nikiwa mtoto wa kwanza kwa upande wa baba na wa mwisho kwa upande wa mama.Mama yangu ni mtanzania wakati baba anatokea Orlando,magharibi mwa Johanesburg nchini Afrika Kusini.

BC: Mara nyingi tunapokuwa wadogo huwa tunakuwa na ndoto nyingi sana za kutaka kuwa kama fulani au kufanya kazi fulani.Mara nyingi huwa hatuna uhakika.Kwa upande wako unadhani ni lini hasa ulipotambua kwamba unataka kuwa DJ? Na kabla ya hapo ulikuwa na ndoto za kuwa nani au kufanya kazi gani?

JD: Ninachokumbuka ni kwamba wakati nikikua nilikuwa napenda sana muziki na mambo kama kuimba na kucheza kiasi kwamba mama yangu siku zote alidhani kwamba nitakuwa mwanamuziki. Tulikuwa tukigombana na mama kila mara juu ya radio cassette yake kwamba nitaiharibu kutokana na jinsi nilivyokuwa naitumia.Kwa kifupi nafiriki nimezaliwa na damu ya sanaa(artistic blood) kwa sababu najifunza vitu kirahisi sana kuliko unavyoweza kutegemea.

Mtu ambaye ameni-influence sana back in the days ni DJ DPP John Peter Pantalakis ambaye mchango wake ni mkubwa sana kwangu.

BC: Unakumbuka ilikuwa lini na wapi ulipoingia mitamboni rasmi kama DJ huku hadhira(audience) ikisubiri kupata burudani kutoka kwako? Ulikuwa na wasiwasi wowote?

JD: Nafikiri itakuwa miaka ya 1989-90s Morogoro Hotel.Kulikuwa na disco linaitwa Sunset Disco.Owner alikuwa jamaa mmoja aliyekuwa anaitwa Kasim Manga. Huyu jamaa zamani alikuwa mcheza mpira.Kwa bahati mbaya hivi sasa ni marehemu.

Wasiwasi ulikuwepo lakini sio sana kwa sababu moyoni mwangu niliamini kuwa naweza kabla hata sijapewa nafasi ya kukamata mashine.Baada ya muda mchache sana nyota ikaanza ku-shine zaidi na zaidi.

BC: Ni aina gani ya miziki unakumbuka ulikuwa unapiga ulipoanza kazi ya u-DJ? Unaweza kutukumbusha majina ya wasanii na vibao vyao ulivyopenda kuvipiga?

JD: Nyimbo ziko nyingi sana ila just to name a few kama Do you reall want my love by Moeba Mo, Slow Change, Too blind to see by K Sims, I need your answer by Joela kama nakumbuka vizuri…Change on me by Cynthia, Should I say Yes,Should I say No by Nushooz, Got to have your love by Mentronics, Back to Life by Soul 2 Soul,Is me that you want…zipo nyingi sana aisee na kila nikiandika zinakuja tu.

BC: Asante…ni kweli kabisa vibao hivyo vilikuna watu wengi enzi hizo na nadhani mpaka hivi leo. Sasa tangu uanze kazi ya u-DJ mpaka leo kumekuwepo na mabadiliko makubwa sana katika aina ya vifaa vinavyotumika katika kazi ya u-DJ.Leo hii kuna computers,ipod,MP3,MP4 na takataka kibao. Unadhani vifaa hivi vya kisasa vinachangia kwa namna gani kuendeleza burudani au kudumaza(kama unadhani vinadumaza) kazi ya DJs?

JD: Kuna some old stuff ambazo zimeboreshwa ili kwenda na wakati bila ya kupoteza taste ile ile ya turn table.Vifaa kama technics,CDX etc.

Lakini hivi vingine ni vya watoto kwa sababu hawajawahi kuvitumia na hivyo sio rahisi kwao kujua umuhimu wake kwenye industry.Lakini ndio hivyo kwamba muda unakwenda na watu wanabuni vitu vipya kila siku na wanahitaji kuuza. Lakini all in all, msisimko haswa wa clubbing unapungua kwa sababu watu siku zote wanapenda kumuona DJ akihangaika kuwafanyia kazi. Hapo na wao mzuka unapanda zaidi.

BC: Na enzi zile mlikuwa mnapata wapi miziki mipya?

JD: Kwa kweli ilikuwa issue,long story.Tutakesha hapa nikianza kukuelezea.

BC: Wakati unaanza kazi ya u-DJ ni  wazi kwamba walikuwepo DJs wengine enzi hizo ambao walikuwa wanatamba.Unaweza kututajia DJs waliokuwa wanatamba enzi hizo na walichangia vipi katika kuinua au kunoa ujuzi wako katika medani ya burudani?

JD: DJs walikuwepo wengi kwa kweli. Na wengi walikuwa wanafanya vizuri.Mimi nilikuwa nawazimia zaidi waliokuwa wanaweza kupiga na kuongea. Watu kama vile John Peter Pantalakis JPP,Rich Dilon,mambo ya mixing Lucas Joe etc.

BC: Tangu mabadiliko ya sera za kiuchumi yaingie Tanzania na kushuhudia mfumuko wa vituo mbalimbali vya radio hususani vya FM,Djs wengi mliokuwa mmezoeleka kuchezesha ndani ya clubs pekee,mliingia kwenye radio. Unaweza kutuambia ulifanya kazi katika vituo gani vya radio na uliendesha vipindi gani? Hii ni kwa faida ya wale ambao hawakuwahi kupata nafasi ya kukusikiliza enzi hizo.

JD: Kwanza nafikiri kama mimi sio wa kwanza kufanya kazi club ba radio kwa wakati mmoja basi ni kati ya wachache sana Tanzania.Nilikuwa sauti ya kwanza kusikika 101.4FM nikaanzisha kipindi kilichokuwa kinaitwa “Love and Dedication” ambacho kilikuwa cha slows Mondays to Thursday. On Fridays and Saturday nilianzisha kipindi kilichokuwa kinaitwa “Weekend Party Show” pale Radio One. Then I started another shows called “The Heat”, “Flavour 120″ whereby 120 stands for 120 minutes(masaa mawili ya Flavour).

Kulikuwa na “Love Stories” every Thursday night, “Mtaa wa Mangoma” every saturday morning. Vipindi vyote hivyo nilivibuni mimi.Pia kuna “The Rock” on ITV 2 ambayo sasa ni EATV, The Cruise on EA Radio na pale Radio Uhuru nilianzisha John 1416 etc.

BC: Tukiwa bado kwenye suala hilo hilo la DJs na vituo vya FM. Kwa mtizamo wako unadhani ujio wa vituo hivyo vilileta mabadiliko au changamoto gani kwenye ulimwengu wa burudani nchini Tanzania?

JD: Kwa kweli mimi nadhani vimeleta changamoto kubwa.Kwanza kabisa ni ajira. Kwa watu wengi ambao walikuwa na ndoto za kuwa watangazaji hapo siku za nyuma walikuwa hawajui wazipeleke wapi ndoto hizo. Lakini baada ya mfumuko wa radio stations opportunity zimekuwa nyingi. Kingine ni kwamba information zinawafikia watu haraka wanaelimika haraka na maendeleo nayo yanakuja haraka.

BC: Kama ilivyo kwa kazi zingine mbalimbali za sanaa,jamii zetu zimekuwa zikihusisha kazi hizo na uhuni au mambo mengine yasiyopendeza masikioni au machoni mwa watu.Unadhani hilo limekuwa likitokana na nini? Na wewe ukiwa miongoni mwa DJs ambao leo hii tunaweza kuwaita “wakongwe” mmechangia vipi kurekebisha fikra kama hizo?

Page 1 of 4 | Next page