b-bandbc

Subira huvuta heri.Ushaambiwa na ushasikia mtu mwingine akiambiwa. Kama hasikii huwa anaambiwa Haraka Haraka Haina…Sote tumekua tukiamini hivyo na kimsingi ni kweli kabisa kwamba subira huvuta kheri. Ndio maana kizazi hiki cha sasa kikaja na Mambo Mazuri Hayahitaji Haraka.

Lakini utajisikiaje pale unapogundua kwamba ulichokuwa ukikisubiria kumbe hakikuwa na thamani ya kusubiriwa? Utajisikiaje utakapogundua kwamba kumbe ulikuwa unachezewa shele? Wasikilize Banana Zorro na bendi yake nzima ya B-Band katika wimbo wao Zoba.

Binafsi nimeupenda wimbo huu sio tu kwa sababu ya ujumbe bali pia mapigo na mpangilio mzima wa vyombo nk.Hapa B-Band wamenikumbusha vizuri mapigo ya mwanamuziki mwingine mahiri hapa barani Afrika kutokea Zimbabwe(Oliver Mutukudzi). Loved it.

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Feedback / Comments

11 Responses to ““ZOBA”-BANANA ZORRO & B-BAND”

  1. Comment by Freddy Macha on August 1st, 2009 8:23 am

    Hebu nielezeni.
    Huyu bwa’ Banana Zorro ndiye yule aliyeimba kibao kiitwacho KIKOMBE? Kama ndiye ananisisimua kitu kimoja. Upangaji sauti. Kama siye, hamna taabu. Huu wimbo wa “Zoba”…unadinda na kuringia kitu hicho. Sauti.
    Hilo limekuwa donda kuu la muziki wetu Watanzania. Tunaweza kuhesabu katika vidole vichache vya mkono waimbaji au bendi ngapi zilizoweka mipangilio mizuri ya sauti? Waimbaji wazuri wapo. Tena wenye vipaji sana ndiyo…. Toka enzi za Frank na Dada Zake (1950′s) , Marijani, P. Balisidja, akina Shakila na Asmahani…na taarabu zao…wapo ndiyo. Lakini upangaji wa sauti nyingi (“choral harmonies” kwa kiingereza)Wanabongo hatujagusa kilele bado. Utasikia zaidi kanisani walokole wakijitahidi…lakini katika miziki ya “pop”…tunafinywa mashavu… bado.
    (Wazaire waliohamia Bongo akina King Kiki na Maquis wao wataalamu wa hilo).
    Labda ndo maana mhariri wa Bongo Celebrity ukasema Banana Zorro kakukumbusha Oliver Mutukudzi wa Zimbabwe. Maana kuanzia hapo kuelekea hadi Uswazi kwa wana Afrika Kusini…ndipo penye chimbuko la upangaji sauti. Niliwahi kufanya kazi na bwana mmoja toka Afrika Kusini…zamani kwenye 1986-7… Ronnie Mkwanazi (siku hizi bonge la actor katika runinga)…huyu bwana alikuwa akisisitiza sana kufanya “harmonies” sio kujiimbia tu.
    Kama ndivyo hivi itakavyokuwa basi tuanze kutabasamu. Hapa kwa Zorro nawaona (kwa jam) Frank Na Dada zake. Namsikia Vitali Maembe (mwana kizazi kipya mwingine) na kibao chake “Asalaam Aleikum.”
    Nakuomba Mhariri umweke Vitali siku moja…
    Nawasikia wa zamani za kale : Wana Unyanyembe, Tabora Jazz (Asha) Atomiki Jazz na Jamhuri Jazz…nasikia “Sina Makosa” ya Simba wa Nyika. EwaaH!
    Endelea kaka. Endelea kuimba na kutusaidia kunyoosha sauti za muziki wa kibongo.
    Kitu kimoja tu nikosoe. Hizi nyimbo zikiwekwa humu mitandaoni (hata miye nimepata tatizo hilo karibuni nilipoweka wimbo wangu wa “Freedom”) vigumu kusikia gitaa la besi.Wanamuziki tunaita “too much melody; too much harmony; weak rhythm section”…
    Muziki unapwaya kiasi fulani; unakuwa kama mtu mwenye nyege asiye na mpenzi; au kuku anayepiga kinanda akitafuta mahali pa kutaga mayai; huku mvua ikinyesha na vichaka hamna.

  2. Comment by Vyne on August 1st, 2009 9:43 pm

    Mh mkaka mwenye suti nyeupe na shati jekundu na stripes mh! mbona wenzio wamependeza.Hii tune kina Banana wameiba kwenye song moja la kisouth nadhani bado sijatia kidole ni song gani mh nwayssssssssss

  3. Comment by shawa metusane on August 2nd, 2009 10:04 pm

    Banana hawajaiba, kuna ubunifu wa kutosha uliofanywa na banana. Kama ilivyo kwa wanamuziki wengine wanavyoboresha nyimbo au kwaya za asili. Mnastahili pongezi.

  4. Comment by mr degree on August 3rd, 2009 3:36 am

    Vyne! hata nzela ni sample ya wimbo todi wa oliver mutukudzi,Banana anatakiwa awe mbunifu zaidi. sampling haitamtoa kimataifa!

  5. Comment by Bingo on August 4th, 2009 9:26 am

    Banana i salute you bro. This song is freaking good. The first time i heard nzela, i could feel the art in it, creativity, the melody, pitch and everything was like sooo perfect. I think you are a great artist and performer. To my opnion you are a number 1. hope your cd blows up the charts.

  6. Comment by mwageni Fred on August 6th, 2009 5:24 am

    Kwa kupitia kwako Banana zoro sasa watanzania tumepata nembo ya muziki wetu,kimsingi B band inahitaji pongezi nyingi na pia selikali yetu inapaswa kubeba jukumu la kuitangaza Tanzania kupitia B .band.

  7. Comment by MACHA Z. on August 10th, 2009 3:26 am

    we do applishet Ur work banana keep it up.Mziki now day ni kazi but angalia usifulie.

  8. Comment by kamanzi on August 10th, 2009 9:12 pm

    Wabongo mmezidi kukopi kopi nyimbo za watu. Manake nini kutuletea tyuni za wimbo wa South? Wewe banana ulikopi tyuni ya wimbo wa Nzela, wala hukutosheka ukarudi tena kukopi tyuni ya huu wimbo. Kama uanamuziki ni kukopi tyuni si kila mtu anaweza kuwa mwimbaji? Mnapigia kelele haki miliki wakati nyie wenyewe wezi wa kazi za wenzenu? Tena sio wewe peke yako, karibu wanamuziki wote ikiwa ni pamoja na ma sound engineers wa bongo wanakopi kazi za nje. Halafu tunawalalamikia mafisadi wakati kila sekta bongo imejaa ufisadi. Tanzania hauna dawa ama hakika nchi yangu ni sikio la kufa. Acha nijiimbie kwa furaha, TANZANIA TANZANIA NAKUPENDA KWA MOYO WOTE>

  9. Comment by Captain Hassan on August 12th, 2009 3:59 pm

    Kamanzi wewe mwenyewe ushakopi huo wimbo waTanzania Tanzania Nchi yangu,umeimba wimbo ambao si wako.

  10. Comment by vaileth on September 3rd, 2009 4:02 am

    Zoba nimeukubali,kwanzia songi hadi shuting.Banana we mziki umekukubali.We baba yao uko juu!!,kaza buti m2 wangu.Mi vai wa A.Town.

  11. Comment by Harrieth on September 3rd, 2009 4:12 am

    Banana,mi nakukubali nyimbo zako zote kali,lakini wimbo wa
    Zoba uko juu sana.Bigup sana mzee,we ni kichwa.

Leave a Reply