MY TANZANIA   |   PLACES TO GO   |   MEDIA   |   ONLINE ENTERTAINMENT    

who

Share and Enjoy:
  • Digg
  • Sphinn
  • del.icio.us
  • Facebook
  • Mixx
  • Google Bookmarks
  • email
  • LinkedIn
  • Live
  • Spurl
  • Technorati
  • Yahoo! Buzz
  • YahooMyWeb

elite-modelbc

INTRODUCING ELITE MODEL LOOK -TANZANIA

Compass Communications Company Limited introduces the largest and most prestigious modeling international competition in the world – Elite Model Look. Compass Communications Company Ltd is an independent TV production company that produces various TV programs and also is the organizer of Miss Universe Tanzania and other beauty pageant titles like Miss Earth, Miss International and Miss Tourism Queen International in Tanzania. The company has now branched out into a more specialized part of the industry namely professional modeling.

Elite Model Look contest was created in 1983 under the name Look of the Year. Elite Model Look competition is the largest model contest of its kind. This contest has become one of the most prestigious springboards for talents into the modeling industry. Up to now Elite Model Management is present in 5 continents and it represents more than 2,000 (Two Thousand) models internationally.

Each year, the Elite Model Look competition sees over 350,000 contestants attend regional and national castings that take place in more than 55 different countries, with at least one contestant of each country participating in the main event – the World Final..

The competition is made of several steps. Thus, through an intensive and rigorous selection process, which drives them from regional castings to national finals, at least one local contestant of each country gets a chance to participate in the World Final. Here in Tanzania Compass Communications will hold local auditions in Dar-Es-Salaam : where all applying contestants will be narrowed down to 10 to 15 semifinalists. No final event will be held this year in Tanzania and the 10 – 15 semifinalists will then be judged by a panel of judges including a representative from Elite Model Look headquarters in Paris, France, in order to find the Tanzanian model who will represent Tanzania in the World Finals in October in Sanya, China.

All girls are invited to make their dreams come true by participating in auditions of Elite Model Look Tanzania. The auditions are open to strictly girls aged 14 to 20 years, with the minimum height of 172 cm. The winner will be selected to meet the fast changing trends and needs of the fashion industry. She will be chosen based on photogenic quality, personality and natural beauty. From the approximately 70 finalists at the World Finals, 15 are chosen by an international panel of judges and they all sign an exclusive contract with Elite Model management. And out of the 15 luck ones, 3 are voted as winners. The top 3 winners will share a guaranteed remuneration of 325,000 USD in total as modeling contract.

This is the first time for Tanzania to hold the license and to select a finalist for Elite Model Look although in 1999 Miriam Odemba was selected and participated successfully in the Elite Model Look World Final in Nice, Paris through MNet Face of Africa.

For more information kindly contact Maria Sarungi Tsehai OR Mwanakombo Salim, Compass Communications, Tel: (022) 2182405, 2182596 Mob: 0784 305122


Share and Enjoy:
  • Digg
  • Sphinn
  • del.icio.us
  • Facebook
  • Mixx
  • Google Bookmarks
  • email
  • LinkedIn
  • Live
  • Spurl
  • Technorati
  • Yahoo! Buzz
  • YahooMyWeb

zitttoobKama lipo jambo ambalo liliamsha hisia tofauti kwenye ulingo wa siasa,basi ni tamko au kitendo cha mwanasiasa kijana,Zitto Kabwe,kutangaza nia ya kugombea uenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA)

Zitto Kabwe ambaye hivi sasa anashikilia nafasi ya Naibu Katibu Mkuu katika chama hicho,anasema pamoja na kwamba anaamini na kuafiki kwamba Mwenyekiti wa sasa wa chama hicho,Freeman Mbowe,ni kiongozi mzuri na kwamba amekitoa mbali chama hicho,wakati umefika wa kuwa na mabadiliko.Zitto anasema chama kimetawaliwa na “kufukuzana” uanachama. Jambo hilo lazima lifikie kikomo,anasema Zitto.

Kisha anasema lazima CHADEMA kijiandae kuchukua dola. Kwa maana hiyo labda tunaweza kusema Zitto anamaanisha kwamba CHADEMA ilivyo hivi sasa,hakiwezi au hakistahili kushika dola.Kinahitaji maandalizi!Hapa ni muhimu kukumbuka kwamba uchaguzi mkuu ni 2010 na sio 2011 au 2012.

Kama utakumbuka,miezi kadhaa iliyopita Zitto Kabwe alitangaza nia yake ya kutogombea tena nafasi ya Ubunge wa Kigoma Kaskazini anayoishikilia.Alisema anataka kujikita zaidi kwenye taaluma yake na hivyo kuachana kidogo na mambo ya siasa.Sasa tunajua kwamba hakuwa akimaanisha alichokuwa anakisema.Alijivika uhalisi wa siasa.

Je unasemaje kuhusiana na uamuzi wa Zitto Kabwe kutaka kugombea nafasi ya Uenyekiti wa CHADEMA?Unadhani atakuwa ni nahodha bora wa chama hicho cha upinzani zaidi ya Mwenyekiti aliyepo madarakani hivi sasa?

***Niliwahi kufanya mahojiano na Zitto Kabwe takribani miaka miwili iliyopita.Bonyeza hapa usome mahojiano yale ili pengine upate picha zaidi juu ya Zitto Kabwe.

Share and Enjoy:
  • Digg
  • Sphinn
  • del.icio.us
  • Facebook
  • Mixx
  • Google Bookmarks
  • email
  • LinkedIn
  • Live
  • Spurl
  • Technorati
  • Yahoo! Buzz
  • YahooMyWeb

befftabc1

Watanzania Ali Kiba, Pretty Poet( Jacqueline Kweka Kibacha) na kampuni ya Bongo UK ni miongoni mwa watu waliochaguliwa kuwania Tuzo za BEFFTA (Black Entertainment,Film,Fashion,Television and Arts Awards) zinazotarajiwa kufanyikia jijini London tarehe 17 October mwaka huu ndani ya London Hilton Metropole.

Ali Kiba amechaguliwa kuwania tuzo hizo katika kipengele cha Best International Act huku Pretty Poet akichaguliwa kuwania tuzo hizo katika kipengele cha Best Spoken Word Artist/Poets. Kampuni ya Bongo UK imechaguliwa kuwania tuzo hizo katika kipengele cha Best Event Promoters.

Kwa orodha kamili ya waliochaguliwa kuwania tuzo hizo,tafadhali bonyeza hapa. Ili kuona kazi za Jacqueline Kweka Kibacha,bonyeza hapa na hapa na hapa.

Kama ilivyo kawaida ya tuzo siku hizi,kura zinapigwa na wananchi.Wakati ukiwadia kwa zoezi hilo,BC itakujulisha.Kwa sasa tunapenda tu kuwapongeza Ali Kiba,Pretty Poet na Bongo UK for the nomination.

Share and Enjoy:
  • Digg
  • Sphinn
  • del.icio.us
  • Facebook
  • Mixx
  • Google Bookmarks
  • email
  • LinkedIn
  • Live
  • Spurl
  • Technorati
  • Yahoo! Buzz
  • YahooMyWeb

TAMKO LA MUUNGANO WA ASASI ZA KIRAIA (FemAct) NA MITANDAO YA WAFUGAJIKUHUSU KUKIUKWA KWA HAKI ZA BINADAMU NA HAKI ZA RAIA KATIKA WILAYA YA NGORONGORO KWA MASLAHI YA MWEKEZAJI; KAMPUNI YA ORTELLO BUSINESS CORPORATION (OBC)

loliondocamp06bcSisi Muungano wa Asasi za Kiraia zinazotetea Usawa wa jinsia, haki za binadamu na maendeleo na ukombozi wa wanawake kimapinduzi (FemAct) kwa pamoja na Mitandao ya Wafugaji mkoa wa Arusha tumeguswa na kusikitishwa na vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu, haki za raia na uvujaji wa sheria katika kutekeleza oparesheni ya kuhamisha wafugaji wakaazi wa jamii za Kimaasai unaoendelea katika wilaya ya Ngorongoro, Tarafa ya Loliondo inayofanywa na vyombo vya dola kwa maslahi ya mwekezaji kutoka Uarabuni, Kampuni ya Ortello Business Corporation (OBC).

Baada ya taarifa za kushitua za watendaji wa serikali kukiuka haki za binadamu dhidi ya jamii za kimasaai kutangazwa katika vyombo vya habari kadhaa ndani na nje ya nchini, FemAct na Mitandao ya Wafugaji, tuliamua kufuatilia kwa karibu ili kubaini usahihi wa taarifa hizo. Kati ya Agosti 19 na 23 2009, viongozi wa mashirika wanachama wa FemAct walifanya ziara maalum katika vijiji vya Ololosokwan, Soitsambu, Olorien – Magaiduru na Arash, pamoja na kutembelea kambi ya Oterloo Business Corporation (OBC) na uongozi wa wilaya ya Ngorongoro kwa lengo la kubaini na kuthibitisha kiwango na namna watendaji wa serikali wanavyoshirikiana na mwekezaji wa OBC kunyanyasa na kutesa raia wakaazi wa vijiji vilivyotajwa hapo juu. (more…)

Share and Enjoy:
  • Digg
  • Sphinn
  • del.icio.us
  • Facebook
  • Mixx
  • Google Bookmarks
  • email
  • LinkedIn
  • Live
  • Spurl
  • Technorati
  • Yahoo! Buzz
  • YahooMyWeb

bestabc1

Alikuwa amepotea kidogo kwenye anga za muziki.Inasemekana alikuwa nchini Uganda akimalizia masomo yake.Sina uhakika kama ndio keshamaliza au la. Nitamtafuta ili atuambie mwenyewe kwamba yupo wapi hivi sasa kimuziki,kimaisha na mambo kama hayo.

Kuna radio moja ya mbao pia iliwahi kuniambia kwamba hivi sasa anajiandaa kuitwa “mama”.Sina uhakika na na kama hayo ya hapo juu,labda tukimpata atatueleza kwa kinaga ubaga.

Wakati hayo hapo juu yote hatuna uhakika nayo(hatujamsikia mwenyewe na kawaida ya BC ni kwamba lazima mwenyewe apewe nafasi ya kuweka mambo wazi) tuna uhakika kwamba bado anafanya muziki.Hivi karibuni ameachia kibao kinachokwenda kwa jina la Tuk Pam Pam. Humo amemshirikisha msanii aitwaye Mr.Hush.Sikiliza kitu hicho kutoka kwa Besta.Welcome back Besta.I am sure lots of your fans(including us) had missed you!

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Share and Enjoy:
  • Digg
  • Sphinn
  • del.icio.us
  • Facebook
  • Mixx
  • Google Bookmarks
  • email
  • LinkedIn
  • Live
  • Spurl
  • Technorati
  • Yahoo! Buzz
  • YahooMyWeb

chrisbc

Christabel Swai(Silipa) standing on the “Roof of Africa”

Kila mwaka maelfu ya watu hutoka kila pande za dunia na kuja nchini Tanzania na hususani mkoani Kilimanjaro wakiwa na nia ya kuupanda Mlima Kilimanjaro ambao ni mlima mrefu kupita yote barani Afrika.

Pamoja na wageni wengi kuja nchini kwa lengo hilo,idadi ya watanzania ambao wameshawahi kuupanda mlima huo bado ni ndogo. Hapo ndipo suala zima la utalii wa ndani (internal tourism) linapokuja.

Lakini hivi karibuni yupo mtanzania ambaye ameonyesha mfano. Ni mtoto wa miaka 10! Anaitwa Christabel Swai. Mtoto huyo amefanikiwa kuupanda Mlima Kilimanjaro na kufika pale pale kileleni ambapo kina Kapteni Nyirenda(RIP) na wenzake waliuweka mwenge wa uhuru miaka takribani 48 sasa iliyopita.

Kwa maana hiyo,Christabel ambaye pia hujulikana kwa jina la Silipa,ameweka rekodi ya kuwa mtu mwenye umri mdogo zaidi nchini kuupanda mlima huo na kufika Uhuru Peak.

Mtoto huyo wa kike ni mwanafunzi wa darasa la nne katika shule ya Eden Garden ya mjini Moshi, alipewa cheti namba 60473 kinachoonyesha na kuthibitisha kwamba amefanikiwa kufika kilele cha mlima huo wenye urefu wa mita 5,895 kutoka usawa wa bahari.

chris-gilman

Silipa at Gilman’s Point. Wengi huishia hapa lakini ilipokuja kwa Silipa,alipumzika kama dakika 20 hivi kisha akamwambia baba yake “Dad,Lets go to Uhuru”

Christabel alifanikiwa kupanda mlima huo kupitia njia ya Rongai(miongoni mwa njia zinazosemekana kuwa ngumu zaidi) akiwa ameongozana na baba yake, Cathbert Swai ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Uwakala ya Utalii ya Ahsante Tours ya mjini Moshi.

BC inapenda kumpongeza sana Christabel a.k.a Silipa.Well done!

Share and Enjoy:
  • Digg
  • Sphinn
  • del.icio.us
  • Facebook
  • Mixx
  • Google Bookmarks
  • email
  • LinkedIn
  • Live
  • Spurl
  • Technorati
  • Yahoo! Buzz
  • YahooMyWeb

mkwabibc

Tangu ashinde katika lile shindano la Bongo Star Search, hajasikika sana katika anga za muziki kama ambavyo ilitarajiwa. Lakini pengine kimya kingi siku zote huwa na mshindo mkuu kama walivyonena wahenga. Never count someone out. Hapa tunamzungumzia Misoji Mkwabi ambaye ndiye aliibuka mshindi wa BSS mwaka jana.

Hivi karibuni Misoji Mkwabi amefyatua kibao kinachokwenda kwa jina la Sahau Shida. Misoji anasema lolote zuri linapokutokea basi hauna budi kusahau shida zako. Anasema, simama,nyanyuka,imba na ucheze na Misoji.

Msikilize Misoji kwa kubonyeza player hapo chini.

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Share and Enjoy:
  • Digg
  • Sphinn
  • del.icio.us
  • Facebook
  • Mixx
  • Google Bookmarks
  • email
  • LinkedIn
  • Live
  • Spurl
  • Technorati
  • Yahoo! Buzz
  • YahooMyWeb

majinabc

Share and Enjoy:
  • Digg
  • Sphinn
  • del.icio.us
  • Facebook
  • Mixx
  • Google Bookmarks
  • email
  • LinkedIn
  • Live
  • Spurl
  • Technorati
  • Yahoo! Buzz
  • YahooMyWeb

michael1bcTakribani mwezi mmoja sasa umetimia tangu Mfalme wa Pop,Michael Jackson, afariki dunia na kuwaacha mashabiki waliokuwa wakimsubiri awape burudani katika concerts zilizokuwa zimepewa jina la This is It. Mfululizo wa concerts hizo ulikuwa uanzie huko nchini Uingereza.

Mpaka ninavyoandika habari hii,Michael Jackson hajazikwa bado. Kulikuwa na taarifa kwamba angezikwa kesho( angekuwa hai angetimiza miaka 51) lakini mpango huo ukaahirishwa kutokana na kile ambacho kimeelezewa kuwa “kutoelewana au kukubaliana rasmi” miongoni mwa wanafamilia kuhusu wapi azikwe na kwanini azikwe siku fulani. Mpango uliopo hivi sasa ni kumzika tarehe 3 September huko Forest Lawn Memorial Park, Glendale, California.

Wakati hayo yote yakiendelea,jana imetolewa taarifa ya kushtusha. Inasemekana Michael alipewa dozi kubwa ya dawa za maumivu za Propofol(dawa hatari hizi).

Kwa maana hiyo polisi wa California wamekiita kifo chake kuwa homicide kwa maana ya kwamba alifariki dunia kufuatia kitendo cha mtu mwingine kilichosababisha mauti imfike. Anayelaumiwa au kunyooshewa kidole zaidi ni Daktari wake, Conrad Murray, ambaye ndie inasemekana alimpa hizo dawa na pia alikuwa naye mpaka dakika za mwisho.Uchunguzi bado unaendelea na polisi hawajasema rasmi ni nani wanaelekea kumfungulia mashtaka ya kuua bila kukusudia.

Je Michael Jackson aliuawa na Dr.Murray? Je hakujiua mwenyewe huyu kwa kutumia madawa ambayo bila shaka alikuwa anajua madhara yake?Nani alaumiwe?

Share and Enjoy:
  • Digg
  • Sphinn
  • del.icio.us
  • Facebook
  • Mixx
  • Google Bookmarks
  • email
  • LinkedIn
  • Live
  • Spurl
  • Technorati
  • Yahoo! Buzz
  • YahooMyWeb

Read the Next Page →

↑ Go Back to Top of Page