MAMA ANAPOLIA NA MAFISADI

mariabcUkimuuliza mtanzania yeyote wa kawaida kuhusu tatizo kubwa linaloikabili nchi hivi sasa,jibu utakalopewa ni “ufisadi”. Hili ni tatizo ambalo mpaka hivi sasa linaelekea kuzidi tu kuota mizizi. Viongozi wetu nao wanawanyooshea wengine vidole. Wale wa chama tawala nao wananyoosheana vidole. Wanasema ndani ya chama chao kuna mafisadi wanne tu!Ni kina nani hao?Kama wanajulikana inakuwaje bado wapo?

Hivi ni nani atamfunga paka kengele? Tatizo tumeshalijua. Ni ufisadi. Ni kuporomoka kwa maadili ya ki-uongozi. Kujilimbikizia mali ndio ujanja kwa mujibu wa wale walio kwenye nafasi za kufanya hivyo. Uzalendo leo hii unaishia kwenye bendera na lugha tu. Ukiwaona wanavyokenua utadhani wanakujali. Kumbe wanajiuliza una shilingi ngapi mfukoni ili wazichukue.

Mama Maria Nyerere,mjane wa Baba wa Taifa, hivi majuzi ameuliza maswali ya msingi na kukemea kwa jinsi anavyoweza. Alikuwa huko Hai mkoani Kilimanjaro. Bonyeza hapa usome alichokisema na kuonya. Bidii hizi hazina budi kuungwa mkono. Isitoshe uchaguzi umekaribia.Huu ni wakati wa kusema Imetosha Sasa. Amka na mwamshe mwenzio.

Page 1 of 3 | Next page