“MAISHA YA MJINI”-FRESH JUMBE

fresh-jumbeBila shaka tunakubaliana kwamba ukiongelea historia ya muziki wa dansi wa Tanzania,basi jina la Fresh Jumbe lina sehemu yake ya kipekee. Huyu ni miongoni mwa wanamuziki ambao sio tu walitamba bali pia walijizolea mashabiki wa kutosha katika sanaa ya muziki wa dansi.

Kwa bahati nzuri, Fresh Jumbe hatumuongelei tu katika tungo zilizopita bali pia tungo zilizopo kwani bado anafanya muziki,bado anatikisa majukwaa na bado anaiwakilisha Tanzania. Hivi sasa anafanyia shughuli zake za kimuziki huko nchini Japan akiwa na makao yake makuu katika jiji la Tokyo.

Mahojiano niliyofanya naye mwaka juzi ni miongoni mwa mahojiano muhimu sana kwa upande wa sanaa ya muziki niliyowahi kufanya. Pale Fresh alielekeza, kuweka wazi historia ambazo pengine hapo awali zilipindishwa au kutokueleweka vizuri.

Pia Fresh aliniambia jinsi ambavyo anataka kubadili mirindimo au mtindo wa muziki anaofanya ili kukabiliana na changamoto za masoko,wapenzi wa muziki wanaobadilika kila kukicha na ili kujiweka katika ramani ya kimataifa zaidi linapokuja suala zima la burudani na muziki.

Albamu yake mpya ilikuwa itoke mapema zaidi. Mpaka hivi sasa ilikuwa iwe mitaani,madukani na mtandaoni lakini kwa sababu ambazo mwenyewe anasema zilikuwa nje ya uwezo wake, itachelewa kidogo mpaka hapo mwishoni mwa mwaka huu. Sasa wakati tukisubiri, Fresh ameachia kibao kimoja miongoni mwa vibao vinavyounda albamu hiyo. Wimbo unaitwa Maisha ya Mjini. Usikilize kwa kubonyeza player hapo chini. Nini maoni yako kwa Fresh?

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

 1. duu., 12 August, 2009

  the one and only FRESH JUMBE will buy ur work,unaimba safi sana ,hivi HUSEN jumbe wa bongo aliyeimba ule wimbo wa penzi la siri ni ndugu yako?Naye ana kipaji sana.

  Keep it up

 2. hombiz, 15 August, 2009

  mpangilio mzuri wa mashairi fresh! Milindimo ya ala nayo ni fresh-Fresh!
  mau-jumbe pia ni fresh-Fresh Jumbe!
  Keep up the good work!

 3. Salma, 17 August, 2009

  Fresh Uko juu kaka na utaendelea kuwa juu.
  Ukija bongo tutembelee tena Mwanza.

Copyright © Bongo Celebrity