Sheria ina kitu kinasema Every man is innocent until proven guilty. Pengine huo ndio ukweli kwani leo aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Jeshi la Polisi mkoa wa Dar-es-salaam,Abdallah Zombe(pichani) pamoja na wenzake 9 wameonekana hawana hatia katika kesi ya mauaji iliyokuwa inawakabili.
Kwa maana hiyo, Zombe na wenzake leo ni watu huru.Wanarejea makwao kwa familia zao.
Kwa vyovyote vile, kesi hii na uamuzi huu wa Mahakama Kuu, umegusa au utagusa hisia za wengi. Ni wakati mzuri wa kutizama mienendo ya sheria zetu,mahakama zetu na pia ubinadamu wetu. Kwa upande wa kesi yenyewe, je tupo makini katika kukusanya vielelezo au ushahidi wa tukio lenyewe? Tupo namna gani katika suala zima la masuala ya Forensic Investigation? Je jina maarufu(kama la Zombe) linapoingia kwenye vitabu vya mahakama weledi(professionalism) unakuwa ule ule au kidogo panakuwa na mchecheto? Ni maswali ambayo lazima tuyapatie majibu.
Pia lipo swali ambalo Pius Mikongoti ameniuliza hapa muda mfupi uliopita, Unadhani sasa atarejeshwa kazini? Sina uhakika lakini kwa kuzingatia “haki na sheria”, ndio; anastahili.
Feedback / Comments
23 Responses to “ZOMBE IS A FREE MAN!”
Leave a Reply


sending...
Haki ya Mungu Tanzania tumekwisha. Jamani kweli Zombe pamoja na ushaidi wote kumuelekea yeye bado ameachwa yuko huru? sitaki kuamini mimi. Mimi nadhani itabidi tuandamane kupinga hili, hii ni uonevu wa hali ya juu, hata Mungu atamuhukumu ZOMBE KWA HAKI, maana kama mahakama imwamua kuwa hana hatia, basi naomba MUngu amshughulikie maana yeye ni Mungu wa wanyonge.Unajua serikali inatuletea laana nchii hii. tumevumilia EPA, RICHMOND, BOT na mengineyo nadhnai wanafukiri wanamchi mafala, sasa nadhani lazima kitu kifanyike.
Mh. Jakaya Mrisho KIkwete. Kama CCM itaanguka katika uchaguzi wa mwaka 2010.
Itakuwa imeangushwa na wewe mwenyewe kwa kujitia kukaa mbali na matatizo yanayotokea, na kujiepusha kuwawajibisha viongozi wenzako walio chini yako.
Kitendo cha Mahakimu hawa kumwachia huru Zombe na wenzake, ni kitendo cha kuudhi na kuhuzunisha sana kwa mtu yeyote aliyekuwa akiifuatilia kesi hii, tangu kutoka Tume ya Kipenka.
Mh. Rais hutaweza kumweleza mtu yeyote akakuelewa kwa hili.
Mh. Rais, unao uwezo wa kuigeuza hali hii ukitaka kufanya kazi yako na Madaraka yako uliyopewa kufuatana na Katiba ya Nchi inavyosema.
Kitendo cha Mahakama kumwona Zombe hana hatia, kwa maoni ya wengi pamoja na mimi, tunaona kuwa sheria imepindishwa wazi wazi kwa manufaa ya viongozi wengine wanaosubiri hatima zao, wasijikute wakihukumiwa.
Mheshimiwa Kikwete, unamvunja moyo DPP, ambaye tumemwona kama ndiye “Mwokozi” wa wanyonge na ,akiwa ni “Mwiba” mkali wa viongozi.
DPP, anajikuta akijitengenezea maadui katika kutimiza wajibu wake kwa kazi uliyompa.
Mh. Kikwete kwa kweli nina hasira sana. Heri niishie hapa kwa sasa, ili kuona maoni ya wenzangu pengine nitapata kuelewa vizuri kilichotokea leo katika Mahakama Kuu Yetu Ya Tanzania.
This Is Black=Blackmannen
kidogo nile baada ya kusoma HUKUMU iliyotoka! lakini yana mwisho wake haya nadhani hauko mbali huo mwisho.
Kila kitu ktk mwenendo wa kesi kilijieleza wazi wazi hali ilivyokuwa na jinsi wahusika walivyofanya! Hukumu kutoka hawana HATIA!!! Sawa bwana sie tunaiachia Hukumu ya Mungu itakavyofanya kazi
Wewe unafikiri Africa kuna leadership, hakuna ndiyo maana Rais kila kukicha kusulula tu, kuomba pesa wakati msafara wake unatumia pesa kibao za wananchi, Tanzania hakuna mahakama wala hakuna haki, ushahidi uliotolewa mtu hawezi kupona Zombe ni muuaji. Rahana ya zombe na damu ya marehemu watakurudia wewe jaji mla rushwa, na viongozi wote wa chama cha majambazi-yaani C-chama, C- Cha Majambazi-CCM.
Huitaji kuwa mwanasheria kuona haki inanyongwa, wamezoea maana wanajua mwakani watatumia polisi hao hao kuiba kura, wao ni wezi wa kura sasa unategemea nini? Kwa muda mrefu sasa CCM huwa hawashindi kihalali ni wezi wa kura ndiyo jeuri yao, sasa hili la Zombe litawalipukia ngonja hasira za umma,
Viongozi wa CCM mimi ninawashangaa sanaaaaa na tena sanaaa, wanapora mali ya umma, wanatumia vibaya madaraka ya umma, Mali ya umma inakuwa mali ya familia za viongozi wa CCM, mifano mingi madini, Ubungo bus terminal, mabenki na vitu kibao
Zombe ni kaburi la CCM hata mkiiba kura lazima damu imwagike, ndiyo maana Africa vita tupu kwa sababu mnyonge hana haki, sasa ni kumalizana tu ndiyo dawa.
mungu naomba uwaweke watanzania walio soma na ambao awajasoma mwoyo wa ujasili wasipige kura mwakani waweke mgomo.mimi hasila zinanipanda tanzania tanzania….. kwanini………..
Sina budi kutowa pngezi zangu za hati kwako mheshimiwa ZOMBE.
Kwa niaba ya watanzania tunakutakia mapumziko mema wewe a familia yako.
Pili ni lazima nishukuru serikali ya CCM kwa msimamo wao usiozumba wa kutokutupana mkono kwa raha ama hida miongoni mwa viongozi wake.
Tatu napenda kuwafahamisha watanzania wote ambao hawakupendelea jinsi hukumu ya Zombe ilivyotolewa na mahakama yetu tukufu watanzania ambao waeshaanza kuzungumzia kutoipigia kura Chama chetu cha ccm hapo mwakani.
Ningependa watanzania hawa wafahamu kuwa ushindi wetu wa ccm hautokani na kura zenu mnazopiga wakati wa uchaguzi.ila maarifa tuliyokuwa nayo ndio yanayotuwezesha kukaa madarakani milele
kesi ya nyani hakimu chui! Kweli duwa la kuku halimpati mwewe!
However, what goes around comes around!
Duh!inasikitisha sana hatujui ni wapi tuegemee!kama serikali inahalalisha wauaji tena kwa kupitia mgongo wake!watu wasio na hatia wamepelekwa msitu wa pande na kuishilia huko huko!kweli?!!!!serikali imeshindwa kutumia nafasi yake katika kukomesha uovu kama huu?!nashindwa kuamini kabisa!!!mimi nilikuwa kati ya watu waliiokuwa wakiitetea sana serikali ya ccm wakati wote!but now Im fed up!wengi wetu hatuna uwezo wa kuwanyoshea kidole moja kwa moja!hasira zangu zote nilizozikusanya zitaishia kwenye uchaguzi!haijalishi ni nani atakayesimamishwa kama mgombea!kamwe hawatopata kura yangu!kizuri uchaguzi uko mlangoni na kura ziko mikononi mwetu!tumechoka!
Money talk what else?
No wonder same cluer people will be given post again in CCM, The Party of Corrupted People (PCP)and continue sucking the Nation
I wish I was a Politics funny but……….?
sijafurahishwa nauhuru wa ZOMBI,WATANZANI WENZANGU TULIFIIKILIE HILI.
Watanzania wanahuzunika bure kuhusu hukumu ya Zombe. Nawahakikishieni haya yana mwisho kama alivyoandika Adam Shafi katika kitabu chake cha Kuli. Ni kutokuwa na kumbukumbu tu lakini kama utakumbuka kesi ya marehemu Dito, walitaka kuigushi hivi hivi matokeo yake Mungu akatoa hukumu yake Dito leo hatunae. Nasema wote wanaonyonya watanzania, wote wanaofaidika, wote wanaoshiriki, wote wanaofumbia macho na wote wanaouchekelea ufisadi HAKIMU WAO NI MUNGU ALIYE JUU. Sifurahii kusema hivi ila nakuhakikishieni kuwa TUTAWAZIKA MMOJA MMOJA tena kwa VIFO VISIVYO NA THAMANI. Kamanzi nikitamka hua inakuwa mtakuja kuniambia muda si mrefu. Nasema tena kwa uchungu, TANZANIA TANZANIA, NAKUPENDA KWA MOYO WOTE!!!
Nch inanuka rushwa, inanuka dhulma, Lakini ipo siku haki ita simama tu,
Mungu hapewe rushwa wala huwa hadhulumu nafsi yeyote kama umeshinda duniani bas mbinguni unasubiriwa na zile roho za wale watu wasio na hati,
Zombe shangilia na hao wauwaji wenzako lakini kuna siku isiyo na jina mtajuta,
Kumbuka Ditopile alishangilia sana siku aliyoachiwa lakini arobaini yake ilipofika ilikuwa haina mjadala na sasa amekutana na yule aliyemuua huko ahera anamsubiria kwa hamu na wewe get ready.
Ngoja niishie hapa nasikia kichefu chefu nikiingalia hilo juso lake hapo juu. OVYOOOOO
kwa kweli ccm mmejichinjia baharini wenyewe mi nawapendaga sana pamoja na visa vyenu kila kukicha jipya mara epa mara richmond tukala ganzi kwa kuwa tumewaona wawakilishi wetu kama akina slaa,kilango wakitusaidia….
lakina sasa kwa hili la huyu osama wa tz (ZOMBE)mmeharibu kbsaaaa,ewe KIKWETE kama utayapata haya ndugu yangu plz do something la svyo yaani hamna rangi mtaacha ona safari hii,….. ILA MUNGU ATATENDA KULINGANA NA MATENDO YENU,2010 MTAIPATA
jamani! jamani! mambo haya hadi lini wapendwa, wamevutavuta muda ili watu wapunguze jaziba, sasa wamewasha moto wenyewe, halafu jiulize wazania wote wakuchukieee wewe kwani wewe ni nani basi kuna tatizo tena kubwa sana. siasa na uai wa maisha ya watu nini wapi na wapi…aaaah! jamani tunafanywa kama mijitaiira.. kumbe watanzania wasasa wote wasomi na waelewa…poa mkuu
mpwaaa hapa!
mmmh! mmm! jamaa wa basi kasababisha ajali kwa siku chache mvua kibao kapigwa, tena mahakamani akiwa na pingu, sasa watz wanapata picha hata kwa kesi zilizopo mbele yetu kwamba mahamuzi yatakuwa hayo hayo
mpwaa!
hee Mungu Tunusuru hivi sidhani ninakwenda kusimamisha miguu yangu kupanga foleni ya kupiga kura Mwakani Mwenyezi Mungu akitujaalia uhai… Ila Mwenyezi Mungu ndie anehukumu walimuachia Dito roho na za watu ona sasa yuko wapi. Haifai hivi Mh. rais Mtu wa dini kama wewe kuyatizama haya kama huyaoni… kilio cha wengi si kizuri ujue!!! mtajifanya hamsikii ila siku ya siku ikifika haya! kila la kheri Mwenyezi Mungu atulinde Watanzania Inshaallah.
Ndugu zangu hii mnaionaje kweli kweli jitu kama hili limehuwa watu bila hatia leohii anaachiwa hivi ama kweli Tanzania imelaaniwa tutabaki ndugu ndugu, amani amani ya mdomoni lakini mambo yanayotendeka humu nchini ni blaa blaa na rushwa inayonuka, sasa wewe ndugu Rais Kikwete hiliunlionaje? kweli unategemea kugombea tena kama rais wa Tanzania tena katika nchi inayonuka damu,rushwa, na blaa blaa, haya bwana
Sheria ya DUNIA daima haipo kamili.
Sheria ya DUNIA inatungwa na ipo kwa ajili ya maslahi ya wachache.
Sheria ya DUNIA ndugu zangu haina HAKI.
Sheria ya DUNIA imezama katika kutafuta UWIANO baina ya KOSA na JINSI mkosa alivyokosa.Kama hakuna USHAHIDI wa kuonyesha UWIANO unaousapoti jinsi KOSA lilivyokoswa basi MKOSAJI si MKOSA katika anga za kisheria za DUNIA .
HAKIMU WA KWELI NI MUUMBA WA WANADAMU NA VYOTE VILIVYOMO DUNIANI.
Najua mna uchungu ndugu zangu,sababu wengi wetu ni waathirika wakubwa wa SHERIA HIZI ZA DUNIA.
USHAURI wangu kwenu ndugu zangu JAMBO HILI MWACHIENI MUUMBA.HAKIKA YEYE NI MJUZI WA DHAHIRI NA SIRI,NAYE NDIYE MWAMUZI WA YOTE. NA HAKIKA YEYE ANA FAHAMU NA KUONA YOTE YATOKEAYO.KWAKE BINADAMU WOTE NI SAWA.MBELE YA MUUMBA THAMANI TOFAUTI YA WANADAMU NI KUTOKANA NA MATENDO YAO.
ASANTENI.
Binafsi nililiona hili tokea mwanzon mwa kesi that’s why ckushtuka hata kidogo!!!Nakumbuka usem usemao kuwa SHERIA IMEWEKWA ILI IVUNJWE!! kilichotekea wala c kgen ktk nchi cha muhim ndg watanzania na wanandugu wote wa marehem tumwachie MUNGU!!ila tuulize yu wapi DITOPILE?
lakn pia nas waTZ tuamke kutoka ucngzn 2seme yatosha sasa kuwapa wa2 hatam kwa ajr ya kanga,T~shirt n.k
Ewe mungu baba uliye mbinguni,endelea kuwajalia watu wako wa serikali na mahakama wafanye hivi hivi ,ili watu tuendelee kuona ubabe wao.Wape usahaulifu kuwa tunaona haya yote yanayotokea.Utujalie kumbukumbu za haya yote wakati wa uchaguzi.Tupe machungu zaidi,kwa ajili ya haki kukosekana.Amen
hivi ni mahakama imemwachia zombe ingali ushahidi ulitosheleza? au au serikali ilishindwa kuithibitishia mahakama bila ya mashaka yoyote kwamba zombe anayohatia?
Hivi ili haki itendeke ni kila anayeshitakiwa ni lazima afungwe pindi inapoonekana ama kwa mujibu wa wanahabari au mawazo binafsi kwamba ametenda hilo kosa ama inapaswa ithibitishwe kwamba hakuna mashaka yoyote mtuhumiwa ni ametenda kosa alililo shtakiwa nalo?
Leo ni zombe, kesh inaweza ikawa ni paskazia,blackmannen,kitaja,muhogo mchungu ama wengineo
Mfumo wa utendaji haki tumuhukumu mtu pale tu inapothibitishwa bila ya mashaka yoyote kwamba mtuhumiwa ametenda kosa aliloshtakiwa nalo.
eeemUNGU WETU!naomba zombe asilipe kisasi kwa mashahidi maana amechomoka kizali
I feel like throwing up….(honestly)…
…anyway….Wa-TZ tutaja amka tu pale tutakapoambiwa kuwa…”tumeshauzwa”….lakini sio vinginevyo….tupo tume-relax…tunakula kuku kwa mrija….(he he he heeeeeeee MUNGU atupe nini…??