michael1bcTakribani mwezi mmoja sasa umetimia tangu Mfalme wa Pop,Michael Jackson, afariki dunia na kuwaacha mashabiki waliokuwa wakimsubiri awape burudani katika concerts zilizokuwa zimepewa jina la This is It. Mfululizo wa concerts hizo ulikuwa uanzie huko nchini Uingereza.

Mpaka ninavyoandika habari hii,Michael Jackson hajazikwa bado. Kulikuwa na taarifa kwamba angezikwa kesho( angekuwa hai angetimiza miaka 51) lakini mpango huo ukaahirishwa kutokana na kile ambacho kimeelezewa kuwa “kutoelewana au kukubaliana rasmi” miongoni mwa wanafamilia kuhusu wapi azikwe na kwanini azikwe siku fulani. Mpango uliopo hivi sasa ni kumzika tarehe 3 September huko Forest Lawn Memorial Park, Glendale, California.

Wakati hayo yote yakiendelea,jana imetolewa taarifa ya kushtusha. Inasemekana Michael alipewa dozi kubwa ya dawa za maumivu za Propofol(dawa hatari hizi).

Kwa maana hiyo polisi wa California wamekiita kifo chake kuwa homicide kwa maana ya kwamba alifariki dunia kufuatia kitendo cha mtu mwingine kilichosababisha mauti imfike. Anayelaumiwa au kunyooshewa kidole zaidi ni Daktari wake, Conrad Murray, ambaye ndie inasemekana alimpa hizo dawa na pia alikuwa naye mpaka dakika za mwisho.Uchunguzi bado unaendelea na polisi hawajasema rasmi ni nani wanaelekea kumfungulia mashtaka ya kuua bila kukusudia.

Je Michael Jackson aliuawa na Dr.Murray? Je hakujiua mwenyewe huyu kwa kutumia madawa ambayo bila shaka alikuwa anajua madhara yake?Nani alaumiwe?

Feedback / Comments

3 Responses to “MICHAEL JACKSON ALIUAWA?”

  1. Comment by ritta on August 25th, 2009 3:11 pm

    kifo cha michael kimeniuma sana
    ila sina cha kufanya ni kazi ya MUUMBA WETU haina makosa pumzika kipenzi chetu tutakukuta tu na sisi
    mimi machozi bado yananitoka nikimwangalia picha zake tulikuwa tunamuhitaji sema mwenyezi mungu kamuhitaji zaidi yetu bay bay DARLING

  2. Comment by princess on August 25th, 2009 3:19 pm

    michale jakson was the best man who cared about people and now he had died that it means we lost the king of pop XXX

  3. Comment by Muga Raymond Peter on August 27th, 2009 1:12 pm

    All i cn say is, i loved Michael Jackson so much, en i’l always do, may GOD rest his soul in peace, Amen.

Leave a Reply