befftabc1

Watanzania Ali Kiba, Pretty Poet( Jacqueline Kweka Kibacha) na kampuni ya Bongo UK ni miongoni mwa watu waliochaguliwa kuwania Tuzo za BEFFTA (Black Entertainment,Film,Fashion,Television and Arts Awards) zinazotarajiwa kufanyikia jijini London tarehe 17 October mwaka huu ndani ya London Hilton Metropole.

Ali Kiba amechaguliwa kuwania tuzo hizo katika kipengele cha Best International Act huku Pretty Poet akichaguliwa kuwania tuzo hizo katika kipengele cha Best Spoken Word Artist/Poets. Kampuni ya Bongo UK imechaguliwa kuwania tuzo hizo katika kipengele cha Best Event Promoters.

Kwa orodha kamili ya waliochaguliwa kuwania tuzo hizo,tafadhali bonyeza hapa. Ili kuona kazi za Jacqueline Kweka Kibacha,bonyeza hapa na hapa na hapa.

Kama ilivyo kawaida ya tuzo siku hizi,kura zinapigwa na wananchi.Wakati ukiwadia kwa zoezi hilo,BC itakujulisha.Kwa sasa tunapenda tu kuwapongeza Ali Kiba,Pretty Poet na Bongo UK for the nomination.

Feedback / Comments

5 Responses to “TANZANIANS NOMINATED FOR BEFFTA AWARDS”

  1. Comment by Rocky on August 29th, 2009 3:34 pm

    Kweli upo kimataifa Ali Kiba, maana unashundana na kina 2Face, Akon na Beyonce, kweli Ali Kiba sasa ni mwanamuziki anayetambulika kimataifa.

    Tupo pamoja Kiba

  2. Comment by BLACKMANNEN on August 30th, 2009 12:33 am

    BC, najua mambo kama haya ni makubwa, lakini kuyaleta kwetu hapa BC, pia sio rahisi.

    Mtu akiingia hapa, zaidi atasikia miziki ya akina Lauryn Hill na za wengine wakubwa. Kuangalia hapa ni kuwatangaza tu watu hawa hapa BC ili tuwaangalie.

    Mimi sijamwona Mtanzania, kama kile mlichokisema hapo juu. Yawezekana ni matatizo ya PC yangu, lakini hata hivyo, kama kweli mambo hayo yapo, basi nawapongeza sana Wabongo wenzangu.

    It’s Great To Be Black=Blackmannen

  3. Comment by micharuko on August 31st, 2009 1:40 am

    alikiba si muuza sura tu !!!!

  4. Comment by kamanzi on August 31st, 2009 3:41 am

    Ngugu watazamaji, kama ilivyo ada bado tunaendelea kutukuza wabana pua, wasuka nywele na wavaa heleni wa kiume. Bongo fleva muziki wa kike na utabaki hivyo. Wapi muziki wa kweli Tanzania siku hizi? Kila kitu sifuri bongo, kunani?

  5. Comment by nyamizi on January 15th, 2010 3:33 pm

    Mbona hamjamuweka yule dada wa Sporah Show.. ambae ndio anatamba Uingereza na TV Show yake ya Sporah Show…. Huyu dada Jina lake lilikua kwenye BEFFTA Awards… Best TV Presenter na Best TV Show… nahapa hakuna picha yake!!!!!!!!! DU.. DU.. DU.. NYIE Michemsho tu…
    Hamuendi na haki… Huyu demu anafanya mambo makubwa huko Uingereza.. amewahoji kina kikwete, Alikiba, AY, Kanumba, FA, Lady JD.. nenda YUTUBE uone mambo yake au Face Book..

    Jaribini kutanzaza watu wanaofanya vitu positive ili kuwafundisha vijana wetu wadogo.

    I like all of them.. ila nimeona tu mbona mi nilimpigia kura yule dada Sporah na mbona hapa hayupo na alikua kwenye award mbili….

    Kazi njema kaka. MKEREKETWA…

Leave a Reply