Kama lipo jambo ambalo liliamsha hisia tofauti kwenye ulingo wa siasa,basi ni tamko au kitendo cha mwanasiasa kijana,Zitto Kabwe,kutangaza nia ya kugombea uenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA)
Zitto Kabwe ambaye hivi sasa anashikilia nafasi ya Naibu Katibu Mkuu katika chama hicho,anasema pamoja na kwamba anaamini na kuafiki kwamba Mwenyekiti wa sasa wa chama hicho,Freeman Mbowe,ni kiongozi mzuri na kwamba amekitoa mbali chama hicho,wakati umefika wa kuwa na mabadiliko.Zitto anasema chama kimetawaliwa na “kufukuzana” uanachama. Jambo hilo lazima lifikie kikomo,anasema Zitto.
Kisha anasema lazima CHADEMA kijiandae kuchukua dola. Kwa maana hiyo labda tunaweza kusema Zitto anamaanisha kwamba CHADEMA ilivyo hivi sasa,hakiwezi au hakistahili kushika dola.Kinahitaji maandalizi!Hapa ni muhimu kukumbuka kwamba uchaguzi mkuu ni 2010 na sio 2011 au 2012.
Kama utakumbuka,miezi kadhaa iliyopita Zitto Kabwe alitangaza nia yake ya kutogombea tena nafasi ya Ubunge wa Kigoma Kaskazini anayoishikilia.Alisema anataka kujikita zaidi kwenye taaluma yake na hivyo kuachana kidogo na mambo ya siasa.Sasa tunajua kwamba hakuwa akimaanisha alichokuwa anakisema.Alijivika uhalisi wa siasa.
Je unasemaje kuhusiana na uamuzi wa Zitto Kabwe kutaka kugombea nafasi ya Uenyekiti wa CHADEMA?Unadhani atakuwa ni nahodha bora wa chama hicho cha upinzani zaidi ya Mwenyekiti aliyepo madarakani hivi sasa?
***Niliwahi kufanya mahojiano na Zitto Kabwe takribani miaka miwili iliyopita.Bonyeza hapa usome mahojiano yale ili pengine upate picha zaidi juu ya Zitto Kabwe.
Feedback / Comments
17 Responses to “MWANASIASA WA WIKI:ZITTO KABWE”
Leave a Reply


sending...
kaisha chukuliwa na ccm kabwe hana lolote wanasiasa wa bongo bwana njaa tupu kaisha pewa chake na ccm sasa naletamaneno ya kukiunda chama tena!!!!!!!!!!!!!!!!!! tutafika wabongo?
Nachelea kusema Kabwe ni mwanasiasa mzuri,lakini bado hajaiva kisiasa vya kutosha, bado hajajua vizuri ni wakati gani aseme nini?na wakati gani hatakiwi kusema nini?hata kama dhamila yake inamlazimisha kusema.Kauli ya mtu haifutiki,inasuta vibaya sana.
Nimesoma majibu yake kwa kina kwenye mahojiano na wewe Jeff.Kwanza nakupa pongezi kwa maswali mazuri na ya kina.
Majibu yanamfunga Kabwe, majibu yake na baadhi ya matendo yake ya sasa yanaonyesha si mtu shupavu,si mvumilivu,hana subira,bado ana mapungufu makubwa kusoma nyakati za kisiasa,na mbaya zaidi ni ndumilakuwili,leo anasema hivi kesho anasema na kutenda vingine.
Kuanzia alivyoboronga mitambo ya RICHMOND,sasa anavyoonyesha tamaa ya fisi kabla meza yake haijawa tayari,vyote vinaonyesha picha halisi ya Kabwe,si mpiganaji tena tunayemfahamu.
Huyu si mwanasiasa hodari,hana tofauti na wanasiasa wengine wa mlango wa kifisadi.Si mwanasiasa tuliyekuwa tukimzania.Ni vigumu na inachukuwa muda kupandisha chati yako na kuaminiwa na wananchi,lakini ni rahisi na haraka sana kuishusha chati hiyo, na uaminifu huo kupotea kama barafu iyeyukavyo baharini.
“Mbowe ni kama mental wangu”, “Niliona CHADEMA ndicho chama kitakacholeta mabadiliko”,”sitegemei kugombea tena ubunge 2010″,”nitashiriki kuhakikisha wapinzani wanachukua viti vingi vya ubunge”,”Nitajikita kufundisha kwenye local University, napenda sana kufundisha”.Hizo ni baadhi tu ya kauli zake alizotamka kwa nafasi tele, tena kwa dhamila yake ya ndani kabisa.
Leo hii anaposema chama bado hakijawa tayari kuchukua nchi,chama kilicho chini ya mental wake,je yeye mwanafunzi wake itakuwaje.Anaposema anaondoa jina na kumlazimisha na mbowe,mental wake aondoe jina anamaanisha nini.Kwani ulikuwa ni mchezo wa ukuti.
Subira huvuta heri,Kabwe wakati wake bado,bado anahitaji kuwa mentalled zaidi na zaidi,narudia tena, hakika ameshindwa kusoma nyakati za kisiasa.Kuna Demkrasia nje ya chama na kuna demokrasia ya ndani ya chama.Kabwe alitakiwa ajue kwamba kwa kugombea na mental wake,atakuwa anaitumia demokrasia ya ndani ya chama vibaya,atakuwa anajitengenezea anguko lake,na la chama chake pia.Atakuwa anatengeneza mgongano ndani ya chama.atakuwa anasimika BOMU ili chama kilipuke.Mtu anayekipenda chama hawezi kuwa chanzo cha anguko la chama chake,chama ambacho amekwishasema ndicho kitaleta mapinduzi ya kuchukua nchi kwa demokrasia ya kura, hawezi kuwa BOMU.
Nakuwa na wasiwasi na chadema sasa.Ukiona ndani ya nyumba Baba,Mama na watoto wanashindwa kuelewana na kufanya maamuzi ya pamoja, lazima ujue hawataweza kuelewana na watu wa nje,Ukiona Viongozi wa chama wanashindwa kukubaliana na kutoa maamuzi makubwa kwa pamoja mpaka watu wa nje wanagundua kuna mgogoro,lazima ujue kuongoza nchi itakuwa balaa,kwani wameshindwa kujiongoza wao, hawataweza kamwe kuongoza nchi.
Kufanya kosa si kosa, kurudia kosa ni kosa lisilosameheka.Kabwe asirudie kosa, na Mbowe pamoja na uongozi wa ndani wa chadema chake wasiruhusu hali ya mtafaruko kama hii kutoke a tena,wanatoa kengere ya tahadhari kwa wananchi kwamba hawawezi,bado ni wachanga,wameshindwa.Tunataka chadema iliyo imara,chadema inayorekebisha mambo yao ya ndani kwa busara bila kumruhusu ADUI ajue mapungufu yao.
Mungu ibariki chadema na uipe nguvu ya kuongeza viti vya wabunge mwaka 2010.Kwa sasa kuchukua nchi itakuwa vigumu labda 2015 kama tu watajirekebisha na kuonyesha utayari wa kuchukua dola.
zito ndo nini mbona sielewi????
Mara zote nimesema wasiasa sio wa kuamini. Huyu dogo watu wamemkuza mpaka akaonekana wa maana lakini bure. Anacheza kwenye chaki na CCM chama changu kama kawaida. Kuanzia kuwepo kwenye kamati ya Kikwete, kutetea ununuzi wa Richmond au vipi nikikumbushia mahusiano yake na marehemu Chifupa (kumradhi wafiwa)? Huyu ni wale wale. Atapaparika itafika wakati tutamsahau kama wengine na kibaya zaidi ameanza mapema mno. Walikuwepo akina Lamwai, Marando, Tambwe Hizza, Mrema na wengine wengi waliopotezea watu muda lakini leo wapo wapi? Mimi nishasema tunachoweza watanzania ni Taarabu mambo ya maaana kama siasa, uchumi na maendeleo kwa ujumla hatuyawezi tuwaachie wengine. Ila kwakuwa sisi ni kichwa cha wendawazimu, tutaendelea kuruhusu kila mtu atunyoe kila uchaguzi unapowadia kama unabisha subiri mwakani uone. Nasema tena TANZANIA TANZANIA NAKUPENDA KWA MOYO WOTE
Kila mpinzani atarudi nyumbani CCM!mnaoshangazwa na jambo hilo hamjui siasa. na kwa taarifa tuu mtu mwenye imani za kijamaa kama zito na slaa hawezi kudumu chadema kwa sababu kile ni chama cha matajiri( capitalists)! karibu nyumbani ZITO! najua slaa naye yupo njiani kumfuata mkewe CCM! teh! teh!
Sasa utabiri wangu umetimia,Zitto kajitoa kwenye kugombea uenyekiti wa CHADEMA.Lakini kwa kujitoa ndio anaendelea kutudhihirishia kwamba si mtu makini,si mchambuzi wa mambo mzuri kabla ya maamuzi,NI KIGEUGEU.Mwanasiasa shupavu kamwe hatakiwi kuwa kigeugeu.
“Najitoa ili kulinda maslahi ya CHAMA” Hiyo ndiyo kauli yake Zitto.Kama mimi mtu baki niligundua hatari ya kugombea kwake ndani ya chama,inakuwaje yeye hakuweza kugundua hilo kabla?Je ni nani aliyemfahamisha na kumuelimisha sasa?Kwa maslahi ya nani?Je sababu zake za kugombea zilionekana hazifahi tena baada ya ushauri huo?
Anguko la kisiasa huja haraka kama theruji iyeyukavyo baharini.Mpaka hapo CREDIBILITY ya Zitto kama kijana shupavu,mwelevu,ngangali imeshuka kwa kiasi kikubwa.Kama aliingizwa mkenge na wana chama tawala,lengo lao lilikuwa ni kummaliza yeye,kumkaanga kwa mafuta yake mwenyewe(SELF SUICIDAL).
Halafu,hivi mbona CHADEMA wanaendelea kutuchanganya sisi wafuatiliaji wake wazuri.Inaonyesha kuwa hawa viongozi wakuu hawakubaliani mambo ya msingi na ya wazi kabla ya matamko yao.Dr slaa kasema”Baada ya Mbowe na Zitto kuwakilisha fomu za kugombea uenyekiti,palitokea makundi” Mbowe akasema kwa kupinga”Hapakuwepo na makundi na CHADEMA haina makundi”.Nachelea kuendelea kusifia ufahamu na umakini wa mwenyekiti(CRITICAL THINKING).Hakutakiwa kamwe kumpinga Dr Slaa aliyetangulia kusema ukweli ulio wazi, yeye angesema “kama makundi yalikuwepo basi, kuanzia sasa hayapo tena na tumekuwa kitu kimoja”.
Unapoona mwenyekiti anachapia jambo zito namna hii,inabidi ashauriwe apatiwe mshauri wa karibu(Personal political analyst).
Kama angekuwepo personal political analyst angemwambia asiikane kauli hiyo ya Dr Slaa bali aizunguke na kujifanya alikuwa hajui na angemshauri kusema ifuatavyo “KAMA PALITOKEA MAKUNDI, BASI MAKUNDI HAYO HAYAPO TENA, CHADEMA NI CHAMA KIMOJA NA KITABAKI KIMOJA, KWA LENGO MOJA LA KUCHUKUA UONGOZI WA NCHI KWA UMOJA, NDANI YA KAULI MOJA YA DEMOKRASIA YA KURA MOJA KWA KILA MWANANCHI MMOJA KUKIPA CHAMA CHA UMOJA, CHAMA CHA CHADEMA ILIYO MOJA.
Kuna siasa na si-hasa!
BONGO imeangukia wapi!?
Huyu jamaaa namchukia kama ukimwi. Nilisoma naye enzi hizo ni bonge la tapeli la maneno, halafu ni muongo wa kufa mtu. niliposikia ameingia kwenye siasa nilisikitikia nchi yangu sana, na hapo ndipo nilipogundua kuwa wananchi tunadanywa sana. sasa imagine mtu kama huyo anafluck mpaka anapata uwaziri si tutalia????????? wananchi wa kigoma hawamjui masikini, laiti wangejua!!!! wamepigwa maneno ya uongo wakaingia line. kuprove hili angalia alivyohandle issue ya dowans!!!
Ebana nashukuru kwa mwanasiasa kijana mwenye
nguvu katika chama hiki cha demokrasia na maenndeleo(chadema)kujitoa kuwania nafasi ya uenyekiti wa chama sio siri wezee wa chama nao nawashukuru sana kumsii kijana wao kutoa jina lake kugombea ni jambo jema sana.Siku za nyuma nilivosikia zito anataka kugombea nafasi hiyo nilijusikia vibaya sana kwan brother huyu ajakomaa kivile kisiasa hivyo n vema atulie na kumuachia tajir mbowe aendelee kulisongesha gurudumu.Kwa zito ni badooo sana kuchukua nafasi hiyo.Inshallah tufikapo mwaka 2015 nashaur ndo jina la zito lionekana hapo itakua mzuka saaaaaaaaana.n hayo tu
Tatizo lililopo CHADEMA ni kuwa, kile ni chama cha ukoo na kuna watu ambao ukijitokeza hadharani kuwapinga basi wewe umetumwa na CCM. Kwa nini isiwe mtu mwingine ikawa CCM? Watanzania imefika wakati tuanze kukubali ukweli kuwa wanasiasa wanatujaza upuuzi ndani ya vichwa vyetu,tuamini kuwa akina fulani tu ndio ‘wateule’ na hawapaswi kupingwa. Mimi ninaamini kuwa Mh. Zitto Kabwe ni mpiganaji halisi ndani ya nchi hii na kamwe hawezi kuisaliti. Hivi hamshtuki, jana ilikuwa Chacha Wangwe,leo Zito Kabwe, kesho nani? Hivi ni kweli wale woto ambao wanaonekana dhahili kuwapinga ‘wateule’ hadharani ndio huwa wametumwa na CCM? Na wote wanaoitwa wasaliti ndani ya chama hiki wanatoka nje ya kanda ya kaskazini,why? Sasa ni wakati wa Mbowe kutuambia ni nani msaliti,nani sio msaliti na ni kwa vigezo gani? Napenda kumalizia kwa kuwaambia Watanzania wenzangu kuwa tusipende kuwatukuza sana baadhi ya viongozi na kuwapa wao tu hakimiliki ya kuipigania nchi yetu,tutambue kuwa hilo ni jukumu letu sote na tuna haki sawa,iwe ya kugombea nafasi yeyote ile ya kiutawala au kuchagua kwa hiyari yako mwenyewe. Nchi hii itajengwa kwa UMOJA WETU NA SIO UTENGANO WETU, TUJENGE UMOJA NA KILA MTU ATIMIZE WAJIBU WAKE IPASAVYO. Kwa umoja wetu, Tanzania yenye neema inawezekana.
JAMANI NILINI HAWA WANASERIKALI WATAKUBALI KUTUPATIA DUAL CITIZENSHIP,INASIKITISHA KUONA KISINGIZIO NI WAHINDI.WANANCHI WAKO MBALI UKILINGANISHA NA SERIKALI,NADHANI LA MUHIMU TUJIFUNZE LILILO BORA ,MWAKA 2007-2008 WANANCHI TULIO NJE TUMECHANGIA ZIDI YA MILION 14 DOLLAR KATIKA UCHUMI WA BONGO BADO TUNAONEKANA HATUNA MAANA KILA WAKIJA NCHI TUNAWAULIZA SWALI LILE LILE TOKA MKAPA HADI KIKWETE,JE HAWAONI UMUHIMU WA DUAL CITIIZEN
JAMANI NILINI HAWA WANASERIKALI WATAKUBALI KUTUPATIA DUAL CITIZENSHIP,INASIKITISHA KUONA KISINGIZIO NI WAHINDI.WANANCHI WAKO MBALI UKILINGANISHA NA SERIKALI,NADHANI LA MUHIMU TUJIFUNZE LILILO BORA ,MWAKA 2007-2008 WANANCHI TULIO NJE TUMECHANGIA ZAIDI YA MILION 14 DOLLAR KATIKA UCHUMI WA BONGO BADO TUNAONEKANA HATUNA MAANA KILA WAKIJA ULAYA TUNAWAULIZA SWALI LILE LILE TOKA MKAPA HADI KIKWETE,JE HAWAONI UMUHIMU WA DUAL CITIIZEN.PIA NADHANI KUNA UMUHIMU WA SERIKALI KUWAELIMISHA WANANCHI WA NDANI JUU YA UMUHIMU WA DUALCITIZENSHIP.INA MAANA WATOTO TULIOZAA HUKU ULAYA SERIKALI HAIWATAKI AU ,MASHAMBA YA BABU ZAO AFRICA HAWATORITHI,INFACT HAWA NDIO AKINA BARAKA OBAMA UKIWA NA NAFASI WANAKUTAKA,NADHANI HASHIMU ATANIELWA ZAID….KAENDA KUPOKELEWA UWANJA WA NDEGE NA NAIBU WAZIRI WA MICHEZO LAKINI ALIVYOJIHANGAIKIA HAWAPO HASHIMU ATACHUKUA URAIA WA MAREKANI KAMA HANA NA KAMA ANAO JE SERIKALI INAMKUBALI AWE NA DUUAL JE NASISI WENGINE……
DUALCITIZENSHIP INA UMUHIMU BONGO..WANAOGOPA WALIO NJE WATAINGIA ULINGO WASIASA
JAMANI NILINI HAWA WANASERIKALI WATAKUBALI KUTUPATIA DUAL CITIZENSHIP,INASIKITISHA KUONA KISINGIZIO NI WAHINDI.WANANCHI WAKO MBALI UKILINGANISHA NA SERIKALI,NADHANI LA MUHIMU TUJIFUNZE LILILO BORA ,MWAKA 2007-2008 WANANCHI TULIO NJE TUMECHANGIA ZAIDI YA MILION 14 DOLLAR KATIKA UCHUMI WA BONGO BADO TUNAONEKANA HATUNA MAANA KILA WAKIJA ULAYA TUNAWAULIZA SWALI LILE LILE TOKA MKAPA HADI KIKWETE,JE HAWAONI UMUHIMU WA DUAL CITIIZEN.PIA NADHANI KUNA UMUHIMU WA SERIKALI KUWAELIMISHA WANANCHI WA NDANI JUU YA UMUHIMU WA DUALCITIZENSHIP.INA MAANA WATOTO TULIOZAA HUKU ULAYA SERIKALI HAIWATAKI AU ,MASHAMBA YA BABU ZAO AFRICA HAWATORITHI,INFACT HAWA NDIO AKINA BARAKA OBAMA UKIWA NA NAFASI WANAKUTAKA,NADHANI HASHIMU ATANIELWA ZAID….KAENDA KUPOKELEWA UWANJA WA NDEGE NA NAIBU WAZIRI WA MICHEZO LAKINI ALIVYOJIHANGAIKIA HAWAPO HASHIMU ATACHUKUA URAIA WA MAREKANI KAMA HANA NA KAMA ANAO JE SERIKALI INAMKUBALI AWE NA DUUAL JE NASISI WENGINE……
Duh! Kaaaaazi kweli kweli!!!!!
“micharuko”, kacharuka, kaja na lake, hajui hili wala lile na “mtzd” naye kaibuka kutoka usingizini nalake.
Ni mambo patashika nguo kuchanika, ili mradi mtu atoe “pumba” zake zisikike. BC kazi mnayo.
Dada “micharuko”, Zitto ni pandikizi la dume, linaloogopewa na kila mtu kwa ajili ya U-Zitto wake. Freeman Mbowe, analijua, sio sawa na “Chaha”!!!!. Mwulize, akufahamishe zaidi.
“mtzd”, subira yavuta heri. Serikali ya Tanzania haimbagui mtu, hata kama wewe ni mhindi. “Dual Citizenship” iko mezani inashughulikiwa. Subiri tu, poza munkari wako.
It’s Great To Be Black=Blackmannen
………sio “Chaha”, nilimaanisha, mtu “Chacha”!!!!
Mtu aliye-”Chacha Kwake = Chacha Wangwe”.
This Is Black=Blackmannen
Katumia haki yake ya Msingi kugombea uenyekiti nashangaa watoa comment hapo wanadai ni mara katumwa na CCM, Mara pandikizi, Mara mwongo.Kijana kazi yake tumeiona na anafnaya kazi nzuri ameibua hoja zilizo na mantiki amepinga kwa nguvu zote ufisadi na ubabe wa ccm bungeni napenda alipokataa kufuta kauli yake kwa kile kilchodaiwa kamkosea nidhamu waziri. ZITO USIRUDI NYUMA VIJANA TUKO NYUMA YAKO!
ZITTO FOR PRESIDENCY 2015!!!!!!!!!!!!
Huyu kijana zito ni political opportunist tu sioni kama ni mtu makini kihivyo
kwanza chama chake chenye mizizi ya ukabila hakina sera isipokuwa wanayo political strategy ambayo ni kusema CCM ni wezi au wala rushwa.
mimi ninawashangaa chadema , zitto na wapinzani kwa ujumla, wao wameshindwa kunadi sera zao maana operation Sangara sio sera ni political gimmicks or strategy maana historia inaonyesha hakuna msafi hata kwa wapinzani, ni watu wanapigania masilahi yao, Zitto bwana mdogo anapenda cheap politics, lakini katika kuendeleza kwa undani ni nini wanataka kuifanyia nchi yetu bado sijaona,
mimi ninamjua sana Zito tulikuwa pamoja chuo kikuu katika serikali ya wanafunzi , mimi nilikuwa mbunge na Zitto alikuwa secretary General wa Daruso, huwezo wa zito naujua kabisa, hawezi kuleta mabadiliko ni mtu wa kutaka kuonyesha misimamo bubu, wakati alijimaliza pale alipoanza kutetea wala rushwa wa Tanesco mpaka mwakyembe akasema huyu ni zito au mwingine, lakini sisi tunaomjua zito ni political opportnist and risk taker kwa misimamo ya kubahatisha kama ule msimamo wa bungeni,
Mwisho mimi nitabaki kuwa Kada wa chama cha mapinduzi chama kikubwa ingawa kina watu wengi wanatiliwa shaka, namalizia kwa kizungu, If you have two evils to choose, choose less evil and the evil you know. This means between CCM and opposition party including Chadema, I still see, CCM as a less evil and the evil I know better than chadema, I am not ready to risk my country to a bunch of people who call themselves opposition leaders. They want state powers to enrich themselves and their cronies.