MY TANZANIA   |   PLACES TO GO   |   MEDIA   |   ONLINE ENTERTAINMENT    

Mojawapo ya mambo ambayo viongozi mbalimbali wa dunia hupenda kufanya wanapokutana ni kupiga picha.Katika nchi za magharibi kitu hicho huitwa Photo Opps au photo opportunity.Picha moja ni sawa na maneno elfu moja.Viongozi hulitambua hilo.Huwa ni nafasi ya kuwaonyesha wananchi mambo mbalimbali kwa kutumia picha.Wanaposalimiana na kujitega kwa picha huku wakiwa wanatabasamu,mwananchi wa kawaida atatafsiri kitu hicho kama amani,upendo na urafiki miongoni mwa viongozi hao na hivyo inamaanisha kwamba nchi zao zipo katika urafiki fulani ambao una manufaa kwa nchi husika.Yaweza kuwa kweli na pia yaweza kuwa sio kweli.

Photo Opps ni masuala ya kihistoria.Yamekuwepo tangu enzi na enzi.Ni masuala ya kidiplomasia.Viongozi kushikana mikono(kwa ishara ya kusalimiana),kutabasamu huku wakiwa wameelekeza nyuso zao upande walipo wapiga picha,ni mambo yaliyozoeleka.

Tangu Rais wa Marekani,Barack Obama aweke historia ya kuwa Rais wa kwanza wa Marekani mwenye asili ya Afrika au mweusi na kutokana na jinsi yeye na mkewe Michelle Obama walivyoiteka dunia,hakuna kiongozi ambaye hutaka kubakia nyuma linapokuja suala la kupiga picha nao.Bila shaka utakumbuka jinsi viongozi wa G20 walivyokuwa wanahangaika kupiga picha na Obama kule nchini Ujerumani mapema mwaka huu.

Majuzi jijini New York na kule Pittsburgh hali ilikuwa ni hiyo hiyo.Viongozi wetu wa Afrika nao hawako nyuma katika suala la picha na kina Obama.Kina Obama nao bila shaka ni wapenzi wa masuala ya picha na kwa sababu wao ndio walikuwa wenyeji kidiplomasia iliwabidi.Hizi hapa ni baadhi ya picha wakiwa na viongozi mbalimbali wa Afrika akiwemo Rais wetu,Jakaya Mrisho Kikwete.

kikwete

Rais Kikwete (katikati) akiwa na Rais Obama(kulia) na US First Lady,Michelle Obama.Bila shaka picha hii ingependeza zaidi kama Mama Salma Kikwete angekuwepo.Mtizamo binafsi.

raila

Kutoka kulia kwenda kushoto,Rais Barack Obama,Waziri Mkuu wa Kenya,Raila Odinga,US First Lady,Michelle Obama na mke wa PM Odinga,Mama Ida Raila Odinga.

kaguta

Kutoka kulia kwenda kushoto,Rais Obama,Rais wa Uganda,Yoweri Kaguta Museveni,US First Lady,Michelle Obama na Ugandan First Lady,Janet Museveni

biya

Kutoka kulia kwenda kushoto,Rais Obama,Rais Paul Biya wa Cameroon,US First Lady,Michelle Obama na First wa Cameroon,Mrs.Chantal Biya.Tayari kumeshazuka maneno katika blogs mbalimbali hususani nchini Marekani kuhusu wig alilovaa Mrs.Chantal Biya.Soma hapa.

Kwa picha zaidi bonyeza hapa

Share and Enjoy:
  • Digg
  • Sphinn
  • del.icio.us
  • Facebook
  • Mixx
  • Google Bookmarks
  • email
  • LinkedIn
  • Live
  • Spurl
  • Technorati
  • Yahoo! Buzz
  • YahooMyWeb

dullyHuwa najitahidi sana kwenda na wakati. Huwa napenda kutambua misamiati,misemo na vijineno vipya vinavyoibuka na kuanza kutumiwa mtaani.Lugha zote ulimwengu hukua kutokana na kuingia kwa misamiati na misemo mipya.Muziki,ukiwemo huu tunaouita wa “kizazi kipya” bila shaka unachangia sana katika kukua kwa lugha.Pamoja na jitihada zangu za kwenda na wakati,hutokea nikapigwa chenga.Nikawa sielewi na kubaki nikijiuliza maswali..

Leo niliposikiliza wimbo mpya kutoka kwa Dully Skyes,ghafla nikawa nimeachwa solemba.Nikatoka patupu.Wimbo unaitwa Shikide.Swali likanijia,Shikide ni nini? Kutokana na maneno yaliyomo katika wimbo wenyewe,yaelekea Shikide ni style ya kucheza.Nilipojaribu kumuuliza “mama watoto” kama yeye amelinyaka neno la Shikide au style ya Shikide alichoweza kuniambia ni kwamba labda tusubiri kuona video ya wimbo huu na ndio tutaelewa shikide ni nini.

Lakini kwa sababu BC ni uwanja mpana na penye wengi haliharibiki jambo,nimeona ni vyema kuwauliza wanaoweza kuwa wanajua zaidi.Shikide ni nini? Kwa upande wa wimbo wenyewe,Dully Sykes ambaye alipoanza muziki alikubali kuitwa “Mr.Misifa” anaonyesha tena kwamba bado yupo.

Style ya Dully Sykes haijabadilika sana tokea enzi zile alipoanza na kutamba sana na nyimbo kama vile Ladies Free,Julieta,Nyambizi(huu ulitamba na kuzua utata pia),Historia ya kweli n.k.Msikilize hapa.

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Share and Enjoy:
  • Digg
  • Sphinn
  • del.icio.us
  • Facebook
  • Mixx
  • Google Bookmarks
  • email
  • LinkedIn
  • Live
  • Spurl
  • Technorati
  • Yahoo! Buzz
  • YahooMyWeb

hafsabcKwa muda alikuwa kimya kiasi kwamba wengine wakasema huenda ameamua kujishughulisha na mambo mengine mbali na muziki.Kumbe sio kweli.Alikuwa akivizia ili anaporudi arudi na mshindo mkuu.Namzungumzia Hafsa Kazinja ambaye kama utakumbuka aliwahi kutamba vilivyo na wimbo wake wa Pressure alioshirikiana na Banana Zorro.

Bado amebakia kwenye miondoko ya zouk.Safari hii amevuka mipaka na kumshirikisha Lady Mariam kutoka nchini Uganda.Wimbo unaitwa Baleki.Usikilize.

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Share and Enjoy:
  • Digg
  • Sphinn
  • del.icio.us
  • Facebook
  • Mixx
  • Google Bookmarks
  • email
  • LinkedIn
  • Live
  • Spurl
  • Technorati
  • Yahoo! Buzz
  • YahooMyWeb

gaddafiKatika anga za siasa wiki hii tunayoimaliza,ilitawaliwa na viongozi wa dunia kupigana vijembe,kufanyiana dhihaka,kuonyesha hasira zao nk kupitia hotuba walizozitoa katika mkutano wa Baraza la Umoja wa Mataifa. Miongoni mwa wanasiasa hao,yawezekana kabisa kukawa hakuna mwanasiasa aliyeongelewa,kujadiliwa na kuzua mijadala mikali zaidi ya Rais wa Libya,Muammar Gaddafi kufuatia hotuba aliyoitoa katika mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa huko jijini New York. Ni kwa sababu hiyo ndio maana leo tunavuka mipaka katika ukurasa huu wa “Mwanasiasa wa Wiki” na kumweka Gaddafi.Rais wetu,Jakaya Mrisho Kikwete,naye alihudhuria kikao hicho na alihutubia.

Kwanini “Mwasiasa wa Wiki” hapa BC awe Kanali Gaddaffi? Sababu ni nyingi.Lakini kwa uchache,Muammar Gaddafi ni mwafrika.Hivi sasa anashikilia cheo cha Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika.Kwa hiyo,kwa mapana na marefu,alikuwa akituwakilisha waafrika.Hii ilikuwa ni mara yake ya kwanza kuhutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na mara yake ya kwanza kutembelea/kufika  Marekani.

Safari ya Gaddafi ya kuelekea New York ilikumbana na vikwazo vingi.Kwanza alikataliwa sehemu kadhaa kuweka hema lake ambalo amekuwa akisafiri nalo kila mahali anapokwenda.Huwa hafikii hotelini.Anachohitaji yeye ni sehemu ya kuwekeza hema lake.Ulinzi wake huwa ni wa ma-bodyguard wanawake watupu.Maandamano kadhaa kutoka jumuiya mbalimbali yakipinga Gaddafi kupewa ruhusa ya kuweka hema yalifanyika.”Hatumtaki katika mji wetu wala mtaa wetu” Gaddafi ni dikteta.Mabango kadhaa yaliweka wazi sababu za kumkatalia “mgeni”Ilibidi afikie katika “ofisi” ya kidiplomasia ya Libya.

Yote tisa.Kumi ni pale alipolikwaa jukwaa la Umoja wa Mataifa na kuanza kuhutubia.Gaddafi alihutubia muda mfupi tu baada ya Rais wa Marekani,Barack Obama, ambaye naye ilikuwa ni mara yake ya kwanza kuhutubia baraza hilo.Gaddafi alikuwa ametengewa dakika 15 za kuhutubia.Alihutubia kwa zaidi ya dakika 90! Wengine walidhani alikuwa akielekea kuweka rekodi ya dunia.Hakuweza kwani mpaka leo mtu ambaye anashikilia rekodi ya kuhutubia Baraza la Umoja wa Mataifa kwa muda mrefu zaidi ni aliyekuwa Rais wa Cuba,Fidel mwana wa Castro.Alihutubia kwa zaidi ya masaa manne(4).

Baada ya hotuba ya Gaddafi,swali kubwa lililobakia miongoni mwa wafuatiliaji wengi wa mambo ya siasa ni “What was he talking about?”. Wengi hawakumuelewa alipotaka,kwa mfano,uchunguzi wa kina ufanyike kutokana na vifo vya aliyekuwa Rais wa Marekani,John F.Keneddy na mwanaharakati maarufu Mchungaji Martin Luther King.Uchunguzi leo hii? Gaddafi alionekana kutokuwa na maandalizi ya kile alichotaka kukiongelea.Hili hata mimi nililiona.Alipanda na vipande chungu mbovu vya makaratasi na mara kadhaa alionekana kusahau alichotaka kusema au alikiandika kwenye kipande gani cha karatasi.Mara kadhaa alijichanganya hususani alipokuwa anaongelea homa ya mafua ya nguruwe ya Swine Flu.

Pamoja na “hitilafu” hizo,yapo mambo ya msingi ambayo Kanali Muammar Gaddafi aliyaongelea.Kwa mfano ni kweli kwamba nchi nyingi wanachama wa UN hivi leo,hazikuwa wanachama wakati umoja huo unaanzishwa.Kwa hiyo,kuna haja ya kuangalia upya muundo mzima wa umoja huo yakiwemo mambo kama vile kura ya Veto.Gaddafi pia aliongelea jinsi ambavyo madhumuni ya kuanzishwa kwa umoja huo yameshindwa.Alisema,kwa mfano,vita zaidi ya 65 vimetokea na vinaendelea kutokea huku umoja huo ambao ulianzishwa ili kuzuia kutokea kwa vitu kama vita,ukiangalia tu.Ukitaka kusoma hotuba na kusikiliza hotuba nzima ya Muammar Gaddafi,bonyeza hapa.

Je ulipata muda wa kuiangalia hotuba ya Gaddafi?Unasemaje kuhusu hotuba hiyo? Gaddafi alitoa uwakilishi ulioutegemea kwa bara la Afrika? Unakubaliana na wanaosema Gaddafi ni mzigo kwa bara la Afrika na sababu nyingine ya kudharauliwa?

Viongozi wengine waliohutubia na kuzua gumzo ni Rais wa Iran,Mahmoud Ahmadenijad ,Rais wa Zimbwabwe,Comrade Robert Gabriel Mugabe na kama kawaida Rais wa Venezuela Hugo Chavez aliyeanza kwa kuomba wasikilizaji wake wasije wakamrushia kiatu ikiwa ni dongo la moja kwa moja kwa Rais wa 43 wa Marekani,George Bush iliyembidi akwepe viatu vya mwandishi wa habari wa Iraq alipokuwa madarakani.

Share and Enjoy:
  • Digg
  • Sphinn
  • del.icio.us
  • Facebook
  • Mixx
  • Google Bookmarks
  • email
  • LinkedIn
  • Live
  • Spurl
  • Technorati
  • Yahoo! Buzz
  • YahooMyWeb

afulanibc

“Nilimuahidi mama kaburini kwake kwamba nitamtengenezea wimbo na video ikiwemo picha yake…here is my dream come true,a promise fulfilled.Hata nikifa leo nitakufa na smile kuuubwa usoni.” Albino Fulani

You need to a flashplayer enabled browser to view this YouTube video

Share and Enjoy:
  • Digg
  • Sphinn
  • del.icio.us
  • Facebook
  • Mixx
  • Google Bookmarks
  • email
  • LinkedIn
  • Live
  • Spurl
  • Technorati
  • Yahoo! Buzz
  • YahooMyWeb

Hii ni collaboration ya Kenya na Tanzania.Wimbo unaitwa Nimetoka Mbali.Ni kutoka kwa msanii Jaguar kutoka nchini Kenya akiwa amemshirikisha wa kwetu wenyewe,AY.Ni mojawapo ya track mpya mpya zinazotamba kwenye vituo vya radio,televisheni bila kusahau katika kumbi mbalimbali za raha.

You need to a flashplayer enabled browser to view this YouTube video

Share and Enjoy:
  • Digg
  • Sphinn
  • del.icio.us
  • Facebook
  • Mixx
  • Google Bookmarks
  • email
  • LinkedIn
  • Live
  • Spurl
  • Technorati
  • Yahoo! Buzz
  • YahooMyWeb

master-t3bcKwa mtu yeyote ambaye anapenda fani ya utangazaji au mtu yeyote ambaye ni msikilizaji wa radio,hakuna shaka kabisa kwamba jina la Master T sio geni. Lakini Master T sio jina lake halisi. Jina alilopewa na wazazi wake ni Taji Liundi.

Yeye ni miongoni mwa watangazaji na waongoza shughuli(MCs) ambao wamejijengea jina ,kujikusanyia idadi kubwa ya mashabiki na kujijengea heshima ya aina yake katika fani hiyo maarufu. Wiki chache zijazo ndiye atakayekuwa jukwaani kusimamia shughuli nzito ya kumtafuta mrembo mpya wa Tanzania(Miss Tanzania 2009).Atashirikiana na Nancy Sumari(Miss World Africa,2005) katika zoezi hilo.

Ukimsikiliza iwe ni redioni au akiwa msimamizi wa shughuli fulani utafurahi,utajifunza,utaburudika na kisha bila shaka utakubali kwamba jamaa ana kipaji,anaipenda kazi yake,anakuthamini wewe kama binadamu na anakupenda kama msikilizaji wake. Umakini anaouweka katika kazi yake yaweza kuwa ndio siri ya mafanikio yake.

Yeye ni miongoni mwa wale watangazaji ambao licha ya kujaaliwa kuwa na sauti inayofaa kabisa kwa masuala ya utangazaji,pia ni wenye kipaji kikubwa katika masuala ya lugha.Master T anaimudu vyema lugha ya Kiswahili na pia anakipambanua vyema Kiingereza na pia huwezi kumuweka mbali na Kifaransa.Hii inamfanya akamilishe ile preamble inayosema;ukitaka kuwa mtangazaji mzuri,sharti ujitahidi sana katika masuala ya lugha.

Hivi karibuni nilipata nafasi ya kufanya naye mahojiano ambayo utayasoma hivi punde.Katika ufupi na ufasaha wa aina yake,Master T anaweka wazi masuala mbalimbali muhimu kuhusu historia ya maisha yake,heka heka za utotoni,kazi yake kama mtangazaji,harakati zake katika mwanaharakati dhidi ya ugonjwa hatari wa ukimwi,maoni yake kwa vijana na mengineyo mengi.

Je, unajua ni mkasa gani mkubwa wa kimaisha uliowahi kumkumba Master T? Unajua wazazi wake walitaka awe nani,afanye kazi gani badala ya utangazaji?Nini mtazamo wake kuhusiana na mapambano dhidi ya gonjwa la ukimwi?Fuatana nami katika mahojiano yafuatayo na Master T;

BC: Taji,kwanza kabisa asante kwa kukubali ombi langu la kufanya nawe mahojiano haya.Pole na majukumu.Mambo yanakwendaje?

MASTER T: Vyema Kaka, nami nashukuru kwa fursa hii.

BC: Natambua kwamba wengi wana ufahamu mkubwa kuhusu historia binafsi ya maisha yako.Lakini kwa faida ya wale ambao hawana habari,unaweza kuniambia kwa kifupi tu kuhusu maisha yako ya awali;ulizaliwa wapi,ukakulia wapi,ukasoma wapi na mambo kama hayo?

MASTER T: Nimezaliwa Dar, nilisoma shule ya Msingi Kisarawe pale Kariakoo kwa muda mfupi. Nikaelekea Uswiss (Switzerland) mwisho wa miaka ya 70′ ambapo niliendelea na shule ya msingi nikijifunza Kiingereza na Kifaransa. Tukahamia Zambia na dingi, nikamalizia darasa la saba.

Ikafuata Zimbabwe niliposoma form 1-2, nikaomba kurudi Bongo, nikapangiwa Ilboru Arusha, nikapiga mpaka form 3-6, nikafurahia mafunzo ya Oljoro JKT halafu Chuo cha Diplomasia mapema miaka ya 90′. (more…)

Share and Enjoy:
  • Digg
  • Sphinn
  • del.icio.us
  • Facebook
  • Mixx
  • Google Bookmarks
  • email
  • LinkedIn
  • Live
  • Spurl
  • Technorati
  • Yahoo! Buzz
  • YahooMyWeb

maalimbcKama umewahi kusoma kitabu maarufu cha mwandishi Shafi Adam Shafi kinachoitwa Kuli, bila shaka utakuwa unakumbuka sentensi iliyofunga kitabu kile. Alisema; Yana mwisho haya.Kuli ni mojawapo ya vitabu ambavyo mpaka hivi leo namshauri mtu yeyote ambaye hajawahi kukisoma kufanya hivyo.

Kumbukumbu ya kitabu hicho ilinijia wiki hii nilipokuwa namsikiliza Katibu Mkuu wa CUF,Maalim Seif Sharif Hamad, alipokuwa akiongea na waandishi wa habari pale Buguruni ambapo aliweka wazi kwamba endapo viongozi wa chama tawala wanataka na kweli wana nia ya kuona amani inaendelea kuwepo visiwani Zanzibar,basi hawana budi kubadili mienendo yao na hususani sera na utaratibu mzima wa wananchi kujiandikisha tayari kwa kuwa wapiga kura katika uchaguzi mkuu hapo mwakani.Maalim anasema CCM inafanya njama ovu za kuwazuia wananchi kujiandikisha.

Katika kupambana na njama hizo za kiovu,Maalim anawaasa wananchi wa visiwani kusimama imara ili kutetea haki zao za msingi. Kwa msemo huu Maalim ananikumbusha yule mwanaharakati wa nchini Marekani, Malcolm X, aliyewahi  kuwaasa watu weusi kwa msemo wake maarufu wa :By any means necessary”.Tayari kumeripotiwa mapambano ya silaha za moto baina ya wananchi na vyombo vya dola.

Nakiri kwamba historia ya ndani ya visiwa hivyo imenipiga chenga.Bado naisoma. Lakini kwa juu juu inaelekea kwamba lipo kundi la watu fulani ambalo linaamini kwamba ni lazima libakie madarakani milele.Kundi hilo linaamini kwamba bila wao,hakuna uongozi.Bila wao, mambo mengi yatakwenda mrama. Hilo tumeshalishuhudia tangu mfumo wa vyama vingi ulipotinga.Kwanini kundi hilo linaamini linavyoamini? Jibu kwa sasa sina.Naendelea kufanya utafiti.Anayejua tafadhali anisaidie. Kama una pendekezo la kitabu cha kusoma, usisite.

Pamoja na hayo, kama Maalim Seif anaongelea suala la kuchukua silaha,kuweka begani na kuingia msituni na kisha kurejea juu ya vifaru,sikubaliani naye. Sijashuhudia bado mahali ambapo amani ya kweli ilipatikana kwa ubabe uliokithiri. Nafasi ya kuambiana ukweli,kuketi mezani bado ipo.Demokrasia ni suala linalochukua miaka mingi sana.Sisi bado ni wachanga sana.Tusitegemee miujiza au majibu ya siku moja au mbili.Tupande na kisha tuhakikishe mizizi imeota.Tusichoke kusema,kukosoa na kuambiana ukweli bila uoga.Kama anavyofanya Maalim Seif.Yana mwisho.

Share and Enjoy:
  • Digg
  • Sphinn
  • del.icio.us
  • Facebook
  • Mixx
  • Google Bookmarks
  • email
  • LinkedIn
  • Live
  • Spurl
  • Technorati
  • Yahoo! Buzz
  • YahooMyWeb

elizabeth_graf_lg

Yawezekana kabisa ukawa hufuatilii sana show ya Big Brother Africa ambapo watu fulani,wasichana kwa wavulana,huchaguliwa na kwenda kuishi ndani ya jumba moja(Big Brother House) kwa siku zisizopungua 90 huku kila kitu wanachokifanya ndani ya jumba hilo kikifuatiliwa,kurekodiwa na kuonekana kwa kila mwenye nia ya kuona kinachoendelea.

Sababu za kutofuatilia zinaweza kuwa nyingi.Unaweza kuwa huna muda.Unaweza kuwa huoni maana au mantiki ya kuketi mbele ya runinga yako na kutazama watu wengine huku ukitambua kwamba wanachokifanya pale ni kama mchezo wa kuigiza kitu ambacho hakibebi uhalisia.Mimi naamini kwamba wanapoanza ile show huwa wanaigiza.Lakini kadri mtu anavyozidi kukaa katika jumba lile,tabia au hulka yake ya kweli huibuka.Siamini kwamba mtu anaweza kuwa “fake” kwa siku zaidi ya 60!

Sababu za kuangalia pia zipo.Unajifunza mawili matatu.Unajifunza jinsi ya kuishi na watu,kuwasiliana na watu na pengine jinsi ambavyo mtu anaweza kunuia kufikisha ujumbe fulani kwa mwenzake au kwa jamii lakini akashindwa kueleweka au kutimiza lengo lake kutokana tu na uchaguzi mbovu wa maneno.Ukiiangalia show ile,unaweza pia kuona tofauti za kibinadamu miongoni mwa wanaume na wanawake.Sote tuna mahitaji sawa; kupenda,kupendwa,kuthaminiwa,kuheshimiwa nk lakini tuna njia tofauti tofauti za kufikia malengo yetu.

Lakini pia unaweza kujifunza kwamba unapomuona mtu kwa nje,usiwe mwepesi wa kudhani kwamba unamjua na unaelewa kila kitu alichopitia au anachopitia maishani mwake.Hili ndilo nililoliona baada ya kusikiliza ujumbe kutoka kwa binti anayeiwakilisha Tanzania(Elizabeth) katika show hiyo baada ya kutumiwa kipande cha video na msomaji mmoja wa BC.

Kwa wengi,Elizabeth ni binti mrembo mwenye kila nia ya kuendeleza sanaa ya urembo na uanamitindo.Utakumbuka kwamba aliwahi kuwania taji la Miss Tanzania bila mafanikio.Lakini je mambo ni safi au tambarare siku zote kwa Elizabeth? Anapitia au amepitia maswahibu gani maishani mwake? Msikilize Elizabeth katika kipande hiki cha video akiongea na wenzake.Bado huna sababu ya kumpigia kura za kubakia “mjengoni” Elizabeth?

Share and Enjoy:
  • Digg
  • Sphinn
  • del.icio.us
  • Facebook
  • Mixx
  • Google Bookmarks
  • email
  • LinkedIn
  • Live
  • Spurl
  • Technorati
  • Yahoo! Buzz
  • YahooMyWeb

abramomich-kilimanjararo-059

Hivi karibuni,tajiri bilionea mmiliki wa timu maarufu ya soka ya Chelsea FC ya nchini Uingereza, Roman Abramovich, alitinga nchini Tanzania na akiwa na nia ya kutalii na kuupanda mlima mrefu kupita yote barani Afrika yaani Mlima Kilimanjaro.

Safari ya Bilionea Abramovich kuja kupanda Mlima Kilimanjaro ilikuwa ni habari kubwa iliyoripotiwa na vyombo lukuki vya habari hususani nchini Tanzania na Uingereza.Kilichoifanya habari hiyo kuwa kubwa hakutokani tu na ukweli kwamba Abramovich ni miongoni mwa watu matajiri sana ulimwenguni bali pia ni ule uhusiano uliopo miongoni mwa mchezo wa soka ulimwenguni huku mashabiki wa timu ya Chelsea anayoimiliki Abramovich ya Chelsea ikiwa na mashabiki kibao ulimwenguni wakiwemo pia wale wanaoishi na kuitazama timu hiyo kutokea Tanzania.

Ingawa Roman Abramovich hakufika kileleni, ni wazi kwamba,kwa namna moja au nyingine,amesaidia kuinua soko la utalii la Tanzania na hususani upandaji wa Mlima Kilimanjaro.

Lakini ni nani aliyemuongoza njia Roman Abramovich? Kuna wadadisi wameuliza swali hili na tuna furahi kwamba jibu lake tumelipata. Aliyekuwa guide wa Roman na rafiki zake anaitwa Isaac Kitindi(pichani juu ndiye anayeonekana kushoto akiwa na Roman.

Isaac ni Mhitimu wa Advanced Diploma katika masuala ya Wildlife Management kutoka Chuo cha Elimu na Utawala wa Wanyamapori cha Mweka kilichopo Moshi,Kilimanjaro. Isaac alikuja Tanzania maalumu kwa shughuli ya kumsindikiza Roman Abramovich mlimani kwani hivi sasa anasomea masuala ya Huduma ya Kwanza (First Aid Training) katika chuo kikuu maarufu cha Havard nchini Marekani.

Isaac Kitindi ambaye wenzake hupenda kumuita Mountain Madness kutokana na umahiri wake wa kuupanda Mlima Kilimanjaro hivi sasa yupo njiani kurejea Havard huku kukiwa na habari kwamba atapitia nchini Uingereza ambapo ataonana tena na Roman Abramovich kwa mazungumzo ya kuileta Tanzania timu ya Chelsea FC hapo mwakani.

Ukitaka kujua ilikuwaje mpaka Roman Abramovich akashindwa kufika kileleni,bonyeza hapa.

Share and Enjoy:
  • Digg
  • Sphinn
  • del.icio.us
  • Facebook
  • Mixx
  • Google Bookmarks
  • email
  • LinkedIn
  • Live
  • Spurl
  • Technorati
  • Yahoo! Buzz
  • YahooMyWeb

Read the Next Page →

↑ Go Back to Top of Page